Get the latest updates from us for free

mas template
Home » » TAHADHARI: NIMETAPELIWA LAKI TANO KWA NJIA YA SIMU ( USAJIRI HAUNA TIJA YOYOTE KWA MTANZANIA )

TAHADHARI: NIMETAPELIWA LAKI TANO KWA NJIA YA SIMU ( USAJIRI HAUNA TIJA YOYOTE KWA MTANZANIA )

Written By mpekuaji on Sunday, May 6, 2012 | 3:38:00 AM


Ujumbe ufuatao umetumwa na Richard M.,
---

Wanablog,

Nawataharisha wizi wa kupitia mtandao wa kusafirisha pesa kwa simu za mkononi unaoendelea Dar es Salaam kwa kasi ya ajabu. Watu wengi wamelizwa. Na ukifika huko makao makuu mnajikuta mko wengi mnaolalamika.

Jana nimelizwa laki tano. Wezi wanatengeneza namba mbadala na kublock ya mwanzo, baadaye kuitawala na kutuma messeji ya amri/order kwa watu wako au wasaidizi ili watume pesa kwa mtu Fulani na kwamba ni haraka.

Message zinatumwa hivi; 

  1. Mwizi: Hapo kuna sh.ngapi nijibu nikuagize?. 
  2. Mwizi: Embu mtumie huyu jamaa laki 5 fanya haraka kidogo namba yake 0656685054 anaitwa Ricky halafu nijulishe. 
  3. Kama mtandao mbovu wa Tigo anasema- “Ngoja nikupe ya voda”
  4. Ya voda 0769870813
  5. Mwizi: Mbona hunijulishi chochote/ fanya haraka anasafiri.
  6. Ujumbe wa Mtandao: G42UO138 Imethibitishwa Tsh500,000 imetumwa kwa JOEL MOSHA Tarehe 3/5/12 saa 12:48 PM Salio lako la M-Pesa ni Tsh4,300. Umeingia kwenye droo!

Ukifyuatilia *Pesa unaamiwa ameshazichukua tena kwa kutumia Mawakala wawili na ni hapa Dar es Salaam.

Wengine wanajifanya wako kwenye kikao cha harusi na hivyo pesa zinahitajika haraka.

Yaelekea kuna ushirikiano kati ya wezi na vijana waliopo kwenye mtandao. Kumbe mtu anaweza jifanya ametumwa kuchonga namba ya mtu baada ya kupoteza simu. 


Eti hapo anahitaji kutaja namba tatu za watu alowasiliana nao karibuni. Sasa iweje hao 'agents' wa mitandao wasihakiki vya kutosha kabla ya kubadilisha laini ya simu?. 

Nimefika makao makuu lakini nikaambulia hadithi tu zaidi ya kurudishiwa namba yangu . Eti wizi wa mtandao uko kila mahali hata mabenki. Sielewi maana ya zoezi la kusajili simu kwa kutumia picha. 

Huu uzembe wa makampuni ya simu utatuliza wengi.

Victim

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts