L-R - Cliff Blake, Chemi, & Jeffrey Chrispin
Bila shaka hawatakosekana watu duniani humu wanaopenda kuhadithiwa na kufahamu, "hivi kumbusu mtu inakuwaje? na, kumbusu mtu wa rangi tofauti na yako je?" haiyumkini wapo watakaofika mbali kujiuliza, "hivi kumbusu mtu wa jinsia sawa inakuwaje?" Haya, mojawapo ya maswali hayo yanasaidiwa majibu kupitia uzoefu wa Da'Chemi aliouandika kwenye blogu yake:
Wadau, katika maisha yangu sikutegemea kuwa nitakuwa na uhusiano wa kimapenzi na Mzungu. Wiki iliyopita nilimbusu Mzungu mdomoni kwa mara ya kwanza! Duh! Ajabu ilikuwa ni sawa na kumbusu mweusi, sema "lips" zao nyembamba zaidi.
Ni hivi.
Nilikuwa katika mchezo wa kuigiza, 'Can I Buy You a Drink?' ambayo ilikuwa moja wa micheo katika Six Playwrights in Search of a Stage. Ilifanyika Roxbury Community College, MainStage Ijumaa iliyopita. Katika ile rehearsal ya mwisho (yaani Dress Rehearsal) hakutokea kijana (Jeff pichani) ambaye alikuwa anaigiza kama mume wangu. Basi Cliff Blake (pichani) ambaye alikuwa anaongoza mchezo wetu, alishika nafasi yake. Ilipofika sehemu ya busu, tukapiga busu kama kawaida. Makofi!!!!! Cliff Blake ni msanii Professional hasa! Karibu ataenda Broadway.
Katika mazeozi, nilikuwa na cheka maana huyo Jeff ambaye alikuwa anaigiza kama mume alikuwa ananiogopa kwanza. Alipoambiwa anibusu kasema, 'kwa kweli hajisikii vizuri kufanya hivyo'. Mwongozaji Mkuu, Marshall Hughes, kamfokea " Kijana, wewe ni msanii hebu fanya kazi yako!" Na mimi nikamwambia Jeff, "Ushukuru hatuvuii nguo hapa!" Kacheka, kanibusu....hakuota mapemba wala kugeuka chura. Baada ya hapo kawa ananibusu kama kawaida mpaka mwisho zikawa kali. Ndo kazi ya msanii.
Mchezo, Can I Buy You A Drink, umeandikwa na Con Chapman. Katika mchezo huyo mimi na mume tumestarehe kwenye baa, anatokea jama kutusumbua (Emil Kreymer). Basi tunaamua kumkomoa kwa kujifanya sisi ni wapenda ule mchezo wa Bondage na kumwalika kujiuna na sisi, halafu jamaa anakimbia.
Ilikuwa mara yangu ya kwanza kushriki na Roxbury Repertory Theatre. Niliambiwa ni vigumu kuingia huko na watu wengi wanatokea kwenye auditions zao. Basi nilienda kwenye audition na hofu kubwa lakini siku hiyo ya kwanza nilipoenda nilipata nafasi! Mungu yu mwema!

Post your Comment