Get the latest updates from us for free

mas template
Home » » SPIKA WA BUNGE AWASILI MJINI KIGALI KUHUDHULIA MKUTANO WA SABA WA MASPIKA WA MABUNGE-AFRIKA MASHARIKI

SPIKA WA BUNGE AWASILI MJINI KIGALI KUHUDHULIA MKUTANO WA SABA WA MASPIKA WA MABUNGE-AFRIKA MASHARIKI

Written By mpekuaji on Monday, May 7, 2012 | 9:56:00 AM

Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kigali baada ya kupokelewa na Mwenyeji wake Spika wa Bunge la Rwanda Mhe. Rose Mukantabana (Kushoto). Mhe. Makinda yupo Kigali Rwanda kuhudhuria Mkutano wa Saba wa Maspika wa Mabunge wananchama wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika leo
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akizungumza na Mwenyeji wake Spika wa Bunge la Rwanda Mhe. Rose Mukantabana mara baada ya Kuwasili Mjini Kigali kuhudhuria Mkutano wa Saba wa Maspika wa Mabunge wa Nchi wananchama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika leo.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akipata maelezo ya awali kuhusu Mkutano huo kutoka kwa maafisa wa Bunge la Tanzania. Wa kwanza Kushoto ni Bi. Justina Shauri , Afisa Dawati wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Bunge la Tanzania na Ndg. Charles Mloka, Mkurugenzi wa Kamati za Bunge anayemuwakilisha Katibu wa Bunge katika Mkutano huo.
Mhe. Makinda na Mwenyeji wake wakiondoka Uwanja wa Ndege mara baada ya Kuwasili.
Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts