
Gari la Fusso lililo sababisha Ajali hiyo

Namba za gari la Fusso

Toyota Rav 4 ikiwa imebamizwa vibaya na Fusso hilo

Gari la Rav 4 lilivyo haribika kwa nyuma

Namba za Gari la Rav 4

Fusso kwa nyuma

Fusso kwa Mbele
***********************************
Ajali Mbaya imetokea usiku huu iiyo husisha Gari la Fusso namba T 596 BUB pamoja na Rav 4 namba
T 675 ATK, Maeneo ya CCM Mkoani Mbeya.
Shahidi aliye kuwepo eneo la tukio amedai ya kuwa Dereva wa Gari la mizigo Fusso alikuwa mwendo kasi sana, na huku akijaribu kuyapita magari mengine matano ambayo yalikuwa mbele yake. Wakati huo anaendelea kuyapita magari hayo tayali dereva wa Rav 4 alikuwa amesha washa taa kuonesha kuwa anaelekea kulia na ndipo Dereva wa fusso akaligonga Gari la Rav 4 ambalo baada ya hapo liliseleleka kwa umbali wa Takribani mita 300 kutoka usawa wa sehemu ambapo liligongewa.
Hata hivyo dereva wa Fusso aliyesababisha Ajali hiyo amekimbia eneo hilo. Hakuna aliye umia wala kupata majeruhi.
Post your Comment


