Get the latest updates from us for free

mas template
Home » » WEMA SEPETU : SUPER STAR IMENIGHARIMU ZAIDI YA MIL 30

WEMA SEPETU : SUPER STAR IMENIGHARIMU ZAIDI YA MIL 30

Written By mpekuaji on Saturday, June 9, 2012 | 5:09:00 AM


The most anticipated movie of the year is finally ready to hit your shelve. 'The Superstar', filamu ya kwanza kutoka kwa muigizaji bora wa kike in Tzee mwaka 2012, Wema Sepetu na kampuni yake binafsi "Endless Fame Company"  sasa iko tayari.

Filamu hiyo  imekuwa blessed na appearance za Tzee wakiongozwa na Wema Sepetu, Hemed Suleiman, Snura Mushi, Jacquilene Wolper, Mwinyi Ahmed, Herry Sameer aka Mr.Blue, Ben Kinyaiya, Hartman Mbilinyi, Nurdin Bakary aka Shetta, Barnaba Boy and Khaleed Mohamed aka TID.

'Superstar' ni movie inayozungumzia maisha ya Wema Sepetu kwa kiasi fulani, jinsi ambavyo anaishi na maisha yake umaarufu, namna gani jamii na vyombo vya habari vinavyomchukulia pamoja na mahusiano yake ya kimapenzi yalivyo kwa ujumla.

"Kupitia hii movie watu wengi ambao wanadhani wananijua kutokana na wanayosoma kupitia magazeti ya udaku basi wataujua ukweli wa mambo ambao kwa muda mwingine unapindishwa tu kwa makusudi na baadhi ya watu ili tu kunichafua. Kwa ujumla ni filamu ambayo inazungumzia maisha yangu mimi.

"Kama ambavyo unaona casting ilivyo, nimewatumia watu ambao kiukweli ni masupastaa wa ukweli na ambao kwa namna moja au nyingine wanahusiana na maisha yangu ya ukweli nje ya movie. Imenigharimu zaidi ya millioni 30 kuweza kuikamilisha hii filamu, hivyo wahindi inabidi wajiandae kwa fedha ya kueleweka kuweza kupata haki ya kuuza hii movie."
  -Alimaliza Wema.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts