Fikra pekee inayomsumbua Kizito
ni jinsi atakavyoweza kumwoa Nusura, binti mrembo wa mmiliki wa mabanda,
Masharubu. Mjomba Mawazo ana wakati mgumu wa kujadiliana na Masharubu
mwenye tamaa ambaye yuko tayari kumwozesha binti yake kwa mahari kubwa
mno.
Cheche bado inamuwia vigumu
kuweka uwiano kati ya biashara yake na familia, na muda wa Cheusi
unapotezwa kwa kuwaangalia watoto wake wawili watundu na mimba yake.
Cheche anapata faraja kwa Tula kwenye Kigrosari chake, huku baadae
studio yake 'ikisambaratishwa' na shangingi linalojiita Lulu linapovamia
toka kusikojulikana na kudai apatiwe huduma!
Post your Comment