Umoja
wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) umelaani kitendo cha baadhi ya
wananchama wa vyama vya upinzani kumbeza Rais John Magufuli na kumuita
dikteta kutokana na kuendelea kutumbua majibu ndani ya Serikali yake.
Naibu
Katibu Mkuu wa Oganizasheni na Siasa ya UVCCM Taifa, Pilly Mbanga
alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akizungumza na wananchama wa CCM mjini
Morogoro wakati wa ziara yake ya kuimarisha uhai wa chama na jumuiya
zake.
Mbanga alisema UVCCM wanaunga mkono utendaji wa Rais Magufuli na hawatakubali kamwe kauli zinazotolewa na wapinzani zinazolenga kumkatisha tamaa.Alisema anafanya hivyo kwa lengo la kutetea wanyonge.
Mbanga alisema UVCCM wanaunga mkono utendaji wa Rais Magufuli na hawatakubali kamwe kauli zinazotolewa na wapinzani zinazolenga kumkatisha tamaa.Alisema anafanya hivyo kwa lengo la kutetea wanyonge.
Post your Comment