Ben Pol anajipanga kufanya ziara ya ‘Moyo Mashine Tour’ itakayozunguka kwenye mikoa ya Tanzania.
Akiongea na mtangazaji Dj Magasha kwenye kipindi cha Track 2 Track
cha Fadhila FM ya Masasi, Ben Pol amesema kuwa baada ya mwezi wa
Ramadhan anatarajia kufanya ziara ya ‘Moyo Mashine’ na hana mpango wa
kuachia wimbo mpya kwa sasa.
“Kwa sasa hivi nataka kufanya ‘Moyo Mashine Tour’, nasubiri mwezi wa
Ramadhan umalizike ili niupeleke ‘Moyo Mashine’ mikoani. Bado
sijafikiria kuachia wimbo mwingine mpya kwa sasa ila nimefocus zaidi
kufanya ziara ya ‘Moyo Mashine,” alisema.
Kuhusu kufanya video Afrika Kusini, muimbaji huyo alisema, “Sababu ni
nyingi, kwa mimi binafsi nilienda kutafuta ubora wa picha kutokana na
kitu fulani hivi niliona nitakipata cha ziada. Lakini pia upatikanaji wa
vitu vyote unavyovitaka kwenye video ikiwemo magari na mazingira
tofauti.”
“Lakini kubwa kuliko vyote ni connection, kwa sababu ukiwa unafanya
kazi kila siku na watu wako wanakuwa ni wale wale unakuwa haukuwi.
Unavyoongeza watu na connection inaweza ikakusaidia na wewe ukakua
zaidi,” aliongeza.
Post your Comment



