Mke
wa Rais, Mama Janeth Magufuli amewataka Watanzania kuiga mfano wa
Mhubiri wa Nigeria, TB Joshua kwa kujitoa katika kuwasaidia wazee na
watu wasiojiweza.
Mama
Magufuli alisema hayo alipokuwa akitoa misaada katika Kituo cha Kaseka
cha Wazee na Walemavu wa Ukoma kilichopo wilayani Masasi Mkoa wa Mtwara.
“Niombe
viongozi waliopo hapa kuhakikisha walengwa wanafaidika na misaada
wanayopata, tayari nimepata malalamiko mengi kutoka kwa Wasukuma
wenzangu kule Mwanza, yanavunja moyo.
‘‘Naomba
watu wasiuze wala kuiba hii misaada ni dhambi kubwa ukichukua chakula
cha mtu mwenye mahitaji na asiyejiweza hiyo ni laana itakufuatilia kwa
sababu ni sadaka imeshaombewa,” alisema.
Post your Comment



