Naibu
Spika alisema amepitia picha za tukio hilo na amejiridhisha kuwa baada
ya kusomwa kwa dua siku hiyo wakati wabunge wa upinzani wakitoka nje ya
ukumbi wa Bunge, Mbunge huyo wa Chadema alipita upande ambao alikuwa
amekaa Mbunge Goodluck Mlinga na kumvua kofia na kisha kutoka nayo nje
ya ukumbi wa bunge, jambo ambalo lilimfanya kushindwa kuendelea na Bunge
kutokana na kutokuwa na vazi rasmi.
Kanuni za Bunge hazijaweka wazi mwongozo au utaratibu wa kutoa adhabu
kwa Mbunge atakayefanya kitendo kama alichofanya Mhe. Anatropia
Theonest. Hivyo kwa mamlaka niliyopewa chini ya kanuni ya tano fasiri ya
kwanza na kwa kuzingatia matakwa ya kifungu cha ishirini na nne C, D na
E cha Sheria kinga na madaraka na haki za bunge natamka kuwa kitendo
hicho kilikuwa ni cha dharau kwa kiti cha spika pia kilikuwa kitendo cha
fujo ndani ya ukumbi wa bunge.
"Nachukua hatua ya kutoa onyo kali kwa
Mhe. Anatropia Theonest kwamba kitendo alichofanya ni ukiukaji wa sheria
na uvurugaji wa shughuli za bunge, hivyo namuonya kwamba asirudie
kufanya kitendo kama hicho na endapo atarudia tena hatua kali
zitachukuliwa kwa mujibu wa sheria za kanuni za Bunge" alisisitiza Naibu
Spika
Post your Comment



