RAIS John Magufuli amemteua Profesa Sufian Bukurura kuwa Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania
(TPDC) kuanzia Mei 30, mwaka huu.
Profesa Bukurura anachukua nafasi ya Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Michael Mwanda.Taarifa ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Justin
Ntalikwa kwa vyombo vya habari jana ilisema kufuatia uteuzi huo, Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amewateua wajumbe sita wa
Bodi ya Wakurugenzi ya TPDC kuanzia Juni 3, mwaka huu hadi Juni 2, 2019.
Aliwataja wajumbe hao kuwa Jaji Josephat Mackanja, Balozi Ben Moses,
Profesa Abiud Kaswamila, Profesa Hussein Sosovele, Dk Shufaa Al-Beity na
Mwanamani Kidaya.
Post your Comment



