Mwezi na nusu uliopita, Wizara ya Habari,Utamaduni ,Sanaa na Michezo
iliifungia video ya wimbo huo na kumwagiza Snura awasilishe script mpya
ambayo hata hivyo baada ya kufanya hivyo nayo imekataliwa.
Snura alidai
kuwa baada ya bodi hiyo kukaa kwenye kikao iliona kuwa bado script mpya
inataka kufanana na video iliyopigwa marufuku na kumkataza kushoot.
Amedai
kuwa jibu hilo lilimchanganya na kumrudisha nyumba na kwamba video ya
pili alipanga kuwepo mwenyewe na wala hatocheza zaidi kutembea.
‘’Nilipeleka
script a video mpya ta Chura bodi ya filamu ilichukua muda kidogo
kuipitia nilifuatilia sana ndio nikapewa majibu baada ya wao kukaa kikao
na kupitia wakaniambia kuwa ile script hwajaikubali nishuti kwasababu
wanasema maudhui yake yanataka kufanana na ile video ya mwanzo.
Nilishindwa
kuelewa kwasababu kwa uelewa wangu niliona nimeandika kitu tofauti
kwasababu video ya mwanzo ilikuwa imechezwa kwenye maji na wanawake ndio
walikuwa wanacheza lakini video hiyo ambayo niliyokuwa nimeiandika
ilikuwa ni mimi mwenyewe ndio nitakuwepo kwenye hiyo video halafu
sichezi natembea huku naimba.
Halafu watu wananiona mie
natembea huku naimba na wao wananifuata kwa nyuma huku wanacheza naenda
napanda daladala na wao wanapanda nikishuka na wao wanashuka huku
wakicheza’’ Alisema Snura
Post your Comment



