Waziri
Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa ameagiza wakuu wa wilaya na mikoa kufanya
ziara katika maeneo yao hasa vijijini ili kujua matatizo ya wananchi wao
kwa ukaribu na kuyapatia ufumbuzi.
Mhe.Majaliwa
ameyasema hayo leo hii Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wakuu wa
wilaya na mikoa walipokuwa Ikulu wakila kiapo cha maadili ya viongozi
kabla ya kwenda kuapishwa na wakuu wa mikoa yao.
Aidha
Waziri Mkuu amesema kuwa wakuu wa mikoa na wilaya waache kukaa
maofisini mwao badala yake watembelee wananchi na hasa wale wa hali ya
chini ili kujua matatizo yao ya Ardhi na kupatia ufumbuzi migogoro ya
wafugaji na wakulima.
Pia
Mhe.Majaliwa amewasisitiza wakuu hao kutambua kwamba majukumu
waliyonayo ni makubwa na wananchi wana mategemeo makubwa juu yao na
hivyo ni budi wakatekeleza wajibu wao na kuhakikisha watanzania
wanapata huduma zote za muhimu kwa kutumia elimu, uwezo, uadilifu,
uaminifu na uwajibikaji walionao ili kufanikisha maendeleo kwa wananchi.
Aliongeza
kuwa wakuu hao wana jukumu kubwa la kusimamia pesa za serikali pesa za
miradi zinakokwenda katika halmashauri za wilaya zao na kukazia kuwa
Serikali haitasita kuchukua hatua kwa yeyote ambaye hatofanya kazi zake
kikamilifu.
Waziri
mkuu amewaagiza wakuu wa Mikoa kushirikiana kwa karibu na wakuu wa
Wilaya ili kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya maeneo yao kwani wananchi
wana kiu ya maendeleo katika maeneo yao.
Post your Comment



