Rapa Ambwene ‘AY’ Yesaya, mmoja kati ya wasanii wa Tanzania
waliofungua milango ya soko la muziki wa Bongo Flava nje ya nchi
ameuelezea urafiki wa damu kati yake na msanii wa Uganda, Jose Chameleon
uliopelekea kupeana zawadi kubwa.
Akifunguka AY aliitaja zawadi inayoweza kuwa
aghali zaidi kuwahi kutolewa kati ya wasanii wa muziki wa nchi mbili
tofauti katika ukanda wa Afrika Mashariki na kuwekwa wazi.
Alisema Chameleon alimzawadia saa aina ya U-Boat, mwaka jana yenye thamani ya $8000 (zaidi ya shilingi milioni 16 za Tanzania) kutokana na kuguswa na urafiki wao.
“Ile
saa ni kama dola 8,000 hivi,” alisema. “Alinipatia akaniambia ‘bwana
hii ni saa ambayo nilijinunulia mwenyewe lakini kwa jinsi ambavyo mimi
na wewe tumeishi pamoja vizuri miaka mingi, naona ni vizuri kama
nikikupatia hii zawadi’. Kwa kweli nilifurahi sana,” alisema AY.
Alisema
kuwa wamekuwa marafiki kwa miaka mingi wakiheshimiana na kupeana mawazo
na kwamba msanii huyo (Chameleon) alikuwa miongoni mwa wasanii wa
kwanza kuusikia wimbo wa ‘Zigo’ hata kabla haujatoka, na alipanga
kushiriki kuifanya Remix yake.
Mbali na Chameleon, wengine waliokunwa na ‘Zigo’ na kutamani kuifanyia Remix ni pamoja na Wizkid.
Post your Comment



