Msanii wa filamu Faiza Ally amewataka wasanii wenzake wa filamu kuacha kutafuta ‘kiki’ ambazo haziwanufaishi katika kazi zao.
Faiza amesema wasanii wengi wa kike wa
filamu wanatafuta kiki za mapenzi bila kujua kiki hizo zitawasaidiaje.
“Kiki sio mbaya lakini hiyo kiki inakusaidiaje?, mimi ukiona nafanya
kiki ujue kuna kazi ambayo inakuja, sio kufanya kiki alafu unakaa kimya
ilimradi uonekana na wewe upo, kwa hiyo mimi ningewashauri wasanii
wenzangu wa filamu tufanye kazi,” alisema Faiza.
Muigizaji huyo kwa sasa anajipanga kuachia filamu yake mpya iitwayo ‘Baby Mama Drama’.
Post your Comment



