Kama ulikuwa unasubiria kuona mashindano ya Big Brother Africa basi pole sana sababu kwa mwaka huu hayatakuwepo.
Mashindano ya Big Brother yametokea kuwavutia watu wengi kutokana na
kukutanisha washiriki wanaotoka mataifa mbalimbali ya Africa, huku
Tanzania ikionekana kufanya vizuri kwenye mashindano hayo.
Taarifa zilizotolewa na waandaaji wa mashindano hayo kupitia M-Net
wamesema kwa sasa wanajiandaa kuweka mikakati ili kuboresha mashindano hayo hapo mwakani.
Mpaka sasa taji hilo la Big Brother linashikiliwa na Idris Sultani
aliyefanikiwa kushinda mwaka jana na kupata zawadi ya fedha kiasi cha
dola laki tatu
Post your Comment



