Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es saalam
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam inawashikilia watu
wanane wakihusishwa na tukio la ujambazi wa kutumia silaha baada ya
mwenzao mmoja kukutwa na bastola iliyokuwa na risasi tatu.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi Kanda
Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Siro alisema Mei 13 mwaka huu saa 2:00
usiku katika eneo la Mbezi Beach njia panda ya Goba, walifanikiwa
kukamata bastola aina ya Browning namba 6.35 ambayo alikuwa nayo
mtuhumiwa Waziri Jamali (39) mkazi wa Mbezi.
“Silaha hiyo ilipatikana baada ya askari kupata taarifa kutoka kwa
msiri kuwa kuna kundi la watu wanaojihusisha na ujambazi wa kutumia
silaha katika maeneo hayo, askari walifika na kumkamata mtuhumiwa huyo,”
alisema.
Mtuhumiwa huyo katika mahojiano alikiri kuhusika katika matukio
kadhaa ya ujambazi na kuongeza kuwa upelelezi unaendelea wa tukio hilo
ili kubaini uhalali wa silaha hiyo na kujua matukio waliyowahi kufanya
na utakapokamilika atafikishwa mahakamani.
Katika tukio jingine, Kamanda Sirro alisema polisi pia inamshikilia
Wenceslaus Mtui (46) mkazi wa Makongo Juu kwa kosa la uuzaji wa madini
bandia.
Post your Comment



