WAKATI akisafiri kuelekea nchini Marekani kwa ajili ya kushiriki utoaji
wa tuzo za BET, msanii wa kizazi kipya, Nassib Abdul ‘Diamond’,
amewataka Watanzania waendelee kumuombea ili arudi na tuzo hizo
zinazotarajiwa kutolewa Juni 26.
Diamond alichaguliwa kuwania tuzo hizo kipengele cha msanii bora wa kimataifa kutoka Afrika (Best International Act Africa).
Kupitia kwa meneja wake, Babu Tale, licha ya Diamond kuwashukuru
Watanzania kuendelea kumtia moyo kutokana na kazi zake mbalimbali
zinazoendelea kumtangaza kimataifa, ameomba maombi ya Watanzania ili
aweze kushinda tuzo hiyo.
“Mniombee ili nirudi na tuzo, naamini Watanzania wananiombea ndiyo
maana kazi zangu zinaendelea kufanya vizuri kimataifa naomba muendelee
kunitia moyo nirudi na tuzo,” alisema Diamond.
Diamond aliyeshinda tuzo mbalimbali ikiwemo Kili, Afrima na nyingine
nyingi alitarajiwa kusafiri kesho kwenda nchini Marekani kwa ajili ya
kushiriki utoaji wa tuzo hizo.
Post your Comment



