Akizungumza
leo Jijini Dar es Salaam, wakati akikabidhiwa ripoti ya Uchaguzi na
Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), Dkt. Magufuli amesema kuwa atatoa
shilingi bilioni 12 kwa ajili ya ujenzi wa majengo hayo ambapo
amependekeza yajengwe Mkoani Dodoma.
Dkt. Magufuli amesema kuwa tume hiyo imefanya kazi kubwa licha ya
kuwa na upungufu wa bajeti wa kununua vifaa vya uandikishaji lakini pia
ufinyu wa maadalizi lakini waliweza kufanikisha kuandikisha kwa wakati
zoezi la upigaji zima la uchaguzi kwa nchi nzima.
Aidha rais Magufuli amesema kwa moja ya changamoto zilizomgusa ni
pamoja na Tume kukaa katika jengo la kupanga wakati kutokana na ufinyu
wa kazi zake tume haitawiki kukaa katika jengo hilo hivyo amerudisha
bakaa aliyopewa na tume ili iweze kujenga majengo ya Tume.
Aidha Rais Magufuli amesema kuwa licha ya zoezi hilo kukamilika
lakini tume inahitaji kuendelea na shughuli zake za kawaida ikiwemo
kuboresha daftari la kudumu la wipiga kura pamoja na utoaji wa elimu ya
mpiga kura na kusimamia chaguzi ndogondogo.
Post your Comment



