ILIPOISHIA
Vyombo vyote vya habari vikarusha tukio zima, ikiwa ni habari ya dharura(breaking news). Kwa kamera moja ya muandishi wa habari aliye kuwemo ndani ya jengo hilo na kujibanza kwenye moja ya kona pasipo kuonekana, aliitegesha kuelekea moja ya tv kubwa, na mawasiliano yakaruka moja kwa moja kwenye kituao anacho kifanyia kazi, na kwakupitia video hiyo vituo vyote vya televishion nchini Tanzania vikawa vinaonyesha tukio hilo walilo liita la kigaidi, likiongozwa na waziri mstafu bwana Eddy Godwin, jambo lililo wastua wananchi wengi na kutambua maana ya waziri huyo kujiudhuru ndio hiyo.
ENDELEA
Shamsa akasimama wima pasipo kuwa na woga wowote
“Kaa chini wewe binti, kaa chini nitakupasua ubongo wako huo”
Mmoja wa watekeaji alizungumza huku bunduki yake akiwa ameielekezea kwa Shamsa, Dulla kwa haraka akamshika mkono Shamsa na kumvutia chini.
“Shamsa unataka kufanya nini, watakuua hawa watu”
“Nahitaji kuzungumza na baba yangu Eddy”
“Wasikilize watu wenyewe hawana akili kabisa hawa”
Dulla aliendelea kulalama kwa sauti ya chini, huku akiendelea kumshikilia Shamsa asiweze kunyanyuka kutoka katika sehemu aliyo lala.
“Funga mabakuli yenu wana haramu nyinyi”
Mtekaji huyo alizungumza kwa sauti ya kufoka na kuwafanya Dulla na Shamsa kunyamaza kimya.
***
“Madam”
Priscar alizungunza huku alimgeukia mdama Rahab aliye keti siti ya nyuma, akamkabidhi simu ambyo kuna ujumbe wa video uliingia. Rahab akaichukua simu hiyo na kutazama video hiyo.
“Ndugu wananchi, ninaimani kwa kufanya hivi serikali na wananchi kwa ujumla mutakuwa mumenielewa nini dhamira yangu, baada ya kujiudhuru”
Rahab akajikuta akistuka baada ya kumuona ni Eddy akizungumza kwenye video hiyo akiwa amevalia mavazi meusi pamoja.
“Eddy………!!”
Rahabu hakuamini macho yake kwani sura na sauti vya mtu anaye zungumza ni Eddy mwenyewe, ila kitu ambacho kinazidi kumshangaza zaid, Eddy amemuacha kwenye kwenye handaki mbalo kipindi walipo kuwa wakifanya kazi za ujambazi walikuwa wakijificha huko yeye na wezake.
“Serikali isipo hitaji kufwata matakwa yangu basi watu wote waliomo ndani ya jengo hili wateteketea kwa kupigwa risasi hadi kufa”
Ujumbe huo wa sauti ukaishia hapo, magari kwenye foleni yakaanza kuruhusiawa huku Rahab akiwa amepoteza amani ndani ya moyo wake. Kwani hiyo ni moja ya skendo ambayo itakuwa ni ngumu sana kuweza kujisafisha mbele ya wananchi ya Watanzania.
Raisi Praygod akaitisha kikao cha dharura kwa maofisa wote wa ngazi za juu katika jeshi. Hali ya hatari inayo endelea katika jiji la Dar es Salaam kuhusiana na kutekwa kwa jengo la kibiashara la Mlimani City, ndio mada kuu ya kuweza kuzungumziwa ni jinsi gani ya kuweza kuwaokoa mateka wote wanao sadikika kutekwa na waziri wa ulinzi, pasipo kujua kwamba mtu aliye panga mpango huo ni miongoni mwa washauri wa raisi walio panga kufanya kazi hiyo.
Vikosi vya vitengo vyote vya jeshi kuanzia polisi, jeshi, zima moto pamoja na usala wa taifa, waliweza kutumwa katika jengo la Mlimani City kuhakikisha kwamba wanaweza kuwaokoa watu wote walio weza kutekwa ndani ya jengo hilo,
Waandishi wa habari, karibia vituo vyote vya habari nchini Tanzania wakaweka kambi katika jengo la Mlimani City kuweza kurusha habari kwa mambo ambayo yanaendelea katika eneo hilo.
Sio waandhishi pekee wa Tanzania, bali hata kutoka mashirika makubwa kama BBC, Sky news pamoja na CCN, waliweza kuweka kambi ili kuitaarifu dunia juu ya kuwepo kwa tukio hilo la ugaidi ambalo limejitokeza nchini Tanzania, huku tukio hilo walikifananisha na tukio lililo tokea nchini chini Kenya miaka kadhaa iliyo pita kwa kutekwa kwa jengo la kibiashara, ambapo ni watu wengi waliweza kutekwa na wengine waliweza kupoteza maisha yao katika shambulio hilo.
Ulinzi mkali ukazidi kuimarishwa nje ya jengo la Mlimani City, barabara inayo pita kuelekea Mwenge pamoja na Ubungo zote ziliweza kufungwa, hawakuruhusiwa watu kuweza kukatiza katika maeneo hayo.
Simu ya mezani iliyopo ndani ya chumba cha kuongozea kamera zate ndani ya jengo hilo, ikaanza kuita Briton na watu wake wote wakaitazama, kila mmoja akiwa katika hali ya kujiuliza ni nani anaye ipiga simu hiyo kwani hapakuwa na mtu aliye weza kufikiria kwa muda huo kuna simu ambayo inaweza kupigwa katika eneo hilo. Briton akajikaza na kuipokea simu hiyo, ila hakuzungumza kitu chochote.
“NYOTE MUMEKUFAAAAA”
Sauti nzito inayo kwaruza kwaruza ilisikika upende wa pili wa simu hiyo, jambo lililo muogopesha Briton na kujikuta akiutoa mkonga huo wa simu sikioni mwake na kuutazama kwa macho ya mshangao.
***
“Eddy…………!!”
Manka alijikuta akishangaa huku akitazama taarifa inayo rushwa kituo cha CNN, kuhusiana na kutekwa kwa jengo la Mlimani City.
“Ndio maana nikakuambia Eddy ni mtu hatari hafai kwenye hii jamii”
Mzee Godwin alizungumza huku akimtazama Manka machoni mwake, muda wote John alikaa kimya akiitazama taarifa hiyo kwani hakujua kwamba huo ni mchezo. Kitu kinacho muumiza kichwa zaidi ni jinsi gani ambavyo Eddy anaoeneka kuwa ni mtu hatari sana kwenye mipamgo yake kwani hadi kufikia hatua ya kuweza kuteka jengo hilo kubwa la biashara nchini Tanzania, basi amekamilika katika mipango yake, ila ukweli ni kwamba mpango huo wote mzee Godwin anaufahamu, ni njia moja ambayo inaweza kumfanya adui yake huyo kukimbia kimbia ndani ya nchi yake kama aliyo kuwa akiandamwa yeye kipindi Eddy alipo kuwa madarakani.
Katika taarifa hiyo, inayo endelea kuruka, hewani kukaonyeshwa kiongozi huyo ambaye amevalia sura inayo endana na Eddy, akiwachukua wanaume wawili alio wasimamisha mbele ya kamera pasipo huruma akawatandika risasi za kichwa, jambo lililo zidi kuwastua watu wote.
***
“Eddy kuna tatizo”
Samson alimuambia Eddy aliye kuwa amesimama mbali kidogo na computer hizo mara baada ya kupiga simu ya vitisho kwa watekaji hao, kwa haraka akaelekea sehemu alipokuwa amekaa Samson, akashahudia watu wawili wakiwa wameuwa kwa kupigwa risasi kisha kiongozi wao huyo akizungumza kitu.
“Atendelea kufa mmoja baada ya mwengine”
Ujumbe huo mfupi ukazidi kuwachanganya Eddy na Samson ambao hawakujua wafanye nini kwa wakati huo, Eddy akaingia kwenye chumba alicho kuwa amelala, akachangua changua kwenye nguo zililzo wekwa bila ya mpangilio juu ya meza, akabahatika kuweka kulpata koti moja jeusi refu kuanzia chini hadi juu, ambapo lina kofia kubwa, na mtu akilivaa si rahisi kuweza kujulikana. Akalivaa, alipo ona limemtosha vizuri akatoka nje ya chumba hicho na kumuuliza Samson jinsi anavyo onekana.
“Unaonekana upo vizuri”
“Basi inatupasa kuweza kuifanya hii kazi ya kuwaokoa mamia ya watu walio weza kutekwa nyara ndani ya jengo hilo”
“Tutaifanya vipi hii kazi ikiwa, usalama umeimarishwa kila kona”
“Tutajua ni jinsi gani ya kuweza kufanya ila kwa sasa inatupasa kuweza kuondoka katika eneo hili, hakuna muda mwengine wa kuweza kupoteza”
Wakatoka na Samson na kuingia kwenye gari, safari ya kurudi jijini Dar es Salaam ikaanza, akilini mwa Eddy, akawa anafikiria ni jinsi gani anaweza kuifanya kazi hiyo ya kisiri pasipo mtu yoyote kumtambua.
Mwendo wa masaa manne wakafanikiwa kufika katika jumba lake la kifahari, ambapo hapakuwa na mlinzi wa aina yoyote anaye linda hapo, macho ya askari yote yapo kwenye jengo la Mlimani City. Wakaingia kwenye moja ya chumba cha siri cha Eddy kilichopo chini ya ardhi na chumba hicho mara nyingiu huwa anaficha silaha zake za siri za kupambana endapo kunakuwa na tatizo kubwa.
Samson akabaki akishangaa silaha nyingi za kivita zilizomo ndani ya chumba hicho, akaanza kukagua silaha moja baada ya nyingine, zote zinaonyesha zina uwezo mkubwa pale zinapo tumiwa katika mapambano ya kuzitoa roho za watu.
“Hizi silaha zote umezitolea wapi?”
“Kipindi nipo madarakani nilikuwa nikiwa namtumia dokta mmoja wa kiisrael, ndio alikuwa akinitafutia wataalamu ambao walizitengeneza hizi silaha.”
“Walizitengeneza kisiri bila ya serikali kuweza kufahamu?”
“Ndio pasipo serikali kuweza kufahamu kwani ni ulinzi wangu binafsi”
Eddy akalivua koti ambalo amelivaa na kuchukua moja ya bastola, yake na kutoa magazine akakuta risasi za kutosha, kisha akairudishia, akafungu moja ya kabati linalo funguliwa kwa namaba za siri, akatoa visu vidogo vipatavyo ishirini vilivyomo kwenye moja ya mkanda mrefu.
“Unaweza kutumia visu?”
“Ndio kama hivi”
Kwa haraka sana, Eddy alichomo moja na kukirusha kwenye moja nguzo iliyomo ndani ya chumba hicho, kuonyesh umahiri wake wa kuweza kutumia visu hivyo.Eddy akavua nguo zake zote na kuvalia nguo nyeusi tupu kisha akachukua moja ya jaketi la kuzuia risasi na kulivaa, kisha akamalizia na jaketi kubwa lenye kofia.
“Hivyo ndivyo unavyo vaa?”
“Ndio, nahitaji kuifanya hii kazi pasipo mtu mwengine kunifahamu kwani ni hatari sana”
“Unaonaje ukasubiria kuifanya kazi hii usiku?”
“Ndio mpango ni lazima kuifanya kazi hii usiku”
“Tutaongozana, nipe tano”
Eddy akagonganisha ngumi yake na ngumi ya Samson, kuashira kuungana kwao kuifanya kazi ya kuwaokoa watu wali tekwa kwenye jengo la Mlimani City
SORRY MADAM (32) (Destination of my enemies)
Hadi majira ya usiku hapakuwa na jambo lolote lililo weza kufanywa na askari katika kuwaokoa mateka katika jengo la Mlimani City, watu wenye ndugu zao wakakesha wakiomba Mungu ndugu zao waweze kutoka humo ndani, vilio vya wamama, vilizidi kutawala kila muda jinsi unavyo zidi kwenda kwani hapakuwa na jibu lolote lililo weza kutolewa na jeshi likawaridhisha.
Kitu kilicho zidi kuwaumiza zaidi vichwa serikali kwa ujumla ni kundi kubwa la watoto wadogo na wanawake waliomo ndani ya jengo hilo, hawakuhitaji kuweza kuwaona wakiendelea kuteseka, ikamlazimu raisi Praygod Makuya kuwasiliana na watekaji hao, kuwauliza ni kitu gani wanancho kihitaji zaidi ili kuweza kuwaachia baadhi ya watu watakao wahitaji.
“Muheshimiwa raisi, hakuna ambalo unaweza kulifanya juu ya hili, hatuhitaji pesa wala silaha. Tunacho hitaji ni roho za binadamu wote waliomo ndani ya jengo hili.
Simu ikakatwa, nusu raisi Praygod aangusha machozi chini, hasira kali dhidi ya Eddy ikazidi kumpanda kwani ndio mtu aliye weza kuipokea simu yake na kuzungumza ujinga wa aina hiyo.
“Muheshimiwa raisi tuna fanyaje sasa?”
“Andaeni vikosi vyote kuweza kuvamia, hatuwezi kuendelea kusubiria kuona wanawake, watoto na vijana wakiendelea kuumia na kuteseka ndani ya jengo hilo. Kama wangekuwa wanahitaji pesa nipo tayari kutoa kiasi chochote cha pesa ila hawapo tayari, wanataka roho inaniumaaa.”
Raisi Praygod alizungumza kwa uchungu huku machozi yakimlenga lenga, ofisi nzima watu wote wakabaki kimya, kwani wazo alilo litoa kiongozi wao sio wazo baya ila ni wazo ambalo roho za watu zitazidi kuteketea.
“Baby huwezi kufanya hivyo”
Sauti ikasikika ikitokea mlangoni, watu wote wakageuza macho yao kutazama ni nani aliye zungumza, wakamkuta ni mke wa raisi. Watu wote wanamfahamu Rahab uwezo wake alio weza kuuonyesha kipindi cha kuweza kumpindua makamu wa raisi aliye jaribu kumpindua mume wake kwa uroho wa madaraka. Rahaba akazidi kutembea hadi mbele kwenye televishen kubwa iliyomo ndani ya ofisi hiyo ya Ikulu, inayo onyesha matukio moja kwa moja kwenye jengo hilo la Mlimani City
“Mume wangu hapa si ishu ya kutumia nguvu, ni ishu ya kutumia akili sana, kuahkikisha watekaji wanaanguka mmoja baada ya mwengine.”
“Ukiseme nguvu itumike, tazama wamama, tazama watoto, tazama mabinti wadogo tazama watu wote kwa ujumla ndani ya jengo hilo, watakufa. Damu hiyo itakayo mwagika utailipia wapi mume wangu, fikiri kabla ya kutenda tafadhali.”
Rahab alizungumza kwa sauti ya upole na unyenyekevu, iliyo anza kutengua taratibu maamuzi ya Raisi Praygod ndani ya moyo wake. Kamanda anaye ongoza vikosi vyote vya oparesheni, ikamlazimu kusimamisha kwanaza swala zima kushambulia, kuhofia watu wengi kuendelea kufa kwa kupigwa risasi.
“Ni saa ngapi sasa hivi?”
Eddy alimuuliza Samson huku wakiwa wamesimama juu kabisa kwenye moja ya gorofa lililopo karibu na maeneo ya Mlimani City, huku wakiwa wamevalia nguo nyeusi tupu, huku Eddy sura yake akiwa ameifunika na kofia kubwa la koti alilo livaa, ambapo sio rahisi sana kwa mtu kuweza kumfahamu. Samson yeye amevalia kitambaa cheusi usoni kilicho weza kuificha sura yake na kumbakisha macho yake tu, kidogo amefanania na watekeji hao.
“Ni saa saba na robo usiku”
“Tunatakiwa kutumia dakika kumi tuwe tumesha maliza”
“Ndio muheshimiwa”
“Kuanzia sasa usiniite muheshimiwa?”
“Ila nikuite nani?”
“BLACK SHADOW”(KIVULI SHEUSI)
“Nimekupata Black Shadow”
Kwa kutumia mshale mrefu wenye kamba ngumu sana. alio urusha Samson na kwenda kukita moja ya kuta ya jengo la Mlimani City, waliweza kuitumia kamba hiyo, kupitia huku wakiburuzika kwa kutumia mikono yao hadi sehemu ya juu kabisa ya jengo la Mlimani City pasipo mtu yoyote kuweza kuwaona wala kustukila jambo lolote.
Wakaanza kutafuta sehemu ya kuweza kuingilia kupitia juu katika jengo hilo, haikuwachukua muda sana wakafanikiwa kuipata na kuzama ndani ya jengi hilo kimya kimya pasipo mtu yoyote kuweza kufahamu uwepo wao ndani ya jengo hilo.
Samson akatoa ramani ya jengo zima ambayo aliweza kutumia wa Rahabu masaa machache yaliyo pita, kupitia email, kisha wakaitoa nakala yake na ndio hiyo wanayo itumia kwa wakati huo, mpango wa kuvamia jengo hilo kisiri, anafahamu Rahab peke yake na hakuhitaji kuweza kumueleza mtu yoyote juu ya mpangui huo kwani, mtu wanaye muhisi ndio mtekaji ndio mtu anaye kwenda kuokoa mamia ya wananchi ya watu waliomo ndani ya jengo hilo, kazi kubwa ya Rahab ni kuhakikisha kwamba hakuna pua yoyote ya askari inahusika kwenye mpango wa kwenda kuwaokowa wananchi hao kwani tangu asubuhi walikuwepo nje ya jengo jilo ila walishindwa kuweza kufanya lolote dhidi ya magaidi hao.
“Hapa ndilo eneo walipo wananchi wengi, huku ndipo kwenye ofisi za mawasiliano, sasa tuanze na wapi?”
“Tugawane, nenda chumba cha mawasiliano mimi acha niende kwenye eneo la wananchi, kumbuka hakuna kutumia bunduki, nakukumbusha katika hilo”
“Sawa Mr black Shadow”
Samson akaikunja ramani hiyo na kuiruidisha mfukoni alipo itoa, na kila mtu akapita nji yake anayo iweza kupita. Kwa kutumia visu vidogo ambayo vinasumu kali, inayo ua ndani ya dakika mbili na kumkausha mtu na kuwa kama mkaa, Eddy akaanza kuvitumia kwa kukirusha kwa mmoja wa watekaji walio weza kusimama akipiga doria katia eneo ambalo ilikuwa ni bahata mbaya kwake kupita kwani ndipo alipo kuwepo bwana Black Shadow(Eddy Godwin)
Mauaji ya kimya kimya yakaendelea kufanyika ndani jengo la Mlimani City, Eddy akitumia visu vyake kuwaangusha watekaji nyara hao kisiri siri, huku Samson akitumia nguvu zake kuweza kuvunja shingo ya kila aliye weza kukutana naye kwenye kumi na nane.
“Mama”
Mtoto mmoja wa kike mwenye umri yapata miaka minne alimtingisha mama yeka, baada ya kumuona mtu aliye valia mavazi meusi akimrushia kisu cha shingo mmoja wa watekaji aliye anguka kimya kimya pasipo mwenzake kutazama.
Mama huyo alipo tupia macho yake katika eneo alilo onyeshwa na mwanaye, macho yake yakakutana na macho ya mtu huyo ambaye hawakujua ni nani, ila alicho kifanya mtu huyo ni kuweka kidole chake mdomoni kuwaashiria kwamba wasizungumze chochote, kwa haraka mama huyo akamzima mdomo mwanae, asije akamwaga mchele kwenye kuku wengi na mambo yakaharibika.
Mmoja wa watekaji katika kupita pita, akawakuta wezake wakiwa wamekufa kifo cha kuogopesha sana kwani miili yao iliweza kubadilika na kuwa myeusi tii.
“Muheshimiwa tumevamiwa”
Mtekaji huyo alizungumza na Briton, aliyemo kwenye chumba cha mawasiliano. Kwa haraka akawaamuru mafundi mitambo walio waweka chini ya ulinzi kutama kupitia kamera zote ni kitu gani ambacho kinacho endelea ndani ya jengo hilo.
“Fu***”
Briton alijikuta akitukana huku akichanganyikiwa kwani, watu wake wengi waliweza kuangushwa chini, huku mtu aliye valia koti kubwa jeusi lenye kofia ndio akiifanya kazi hiyo.
“Wote sasa jiandaeni kwa mashambulizi kuna hali ya hatari narudia, tupo kwenye hali ya hatari”
Briton alizungumza kupitia simu ya upepo huku akichukua bunduki yake, Lukuman na Briton wakatoka ndani ya chumba hicho na kuwacha vijana wawili pamoja na Brian, ili kuweza kuendelea kumtazama muuaji huyo anapita ameneo gani.
Kitendo cha Lukuman aliye jitengenezea sura kama ya Eddy pamoja na Briton kutoka na kutokomea karibu na eneo hilo lachumba cha mawasiliano ndipo Samson alipo weza kufika.
Akautazama mlango huo ulio andikwa na maandishi madogo ya rangi nyeusi
(Security control room)
Mmoja wa mafundi mitambo alipo gundua, kupitia kamera iliyopo njee ya mlango wa chumba hicho kama kuna mtu amesimama nje ya mlango kwa haraka akaweza kubadilisha video hiyo na kuihamishia kwenye kamera nyingine inayo waonyesha Briton na Lukuma sehemu wanapo pita.
“Wewe wewe hembu rudisha kwenye kamera uliyo itoa”
Brian alizungumza huku akimnyooshea bastola fundi mitambo huyo, aliye anza kutetemeka mwili mwiza, kwani miili ya watu wawili walio washuhudia wakipigwa risasi mbele yao, bado imo ndani ya chumba hicho wakiwa wamelala sakafuni na endapo atafanya kama kinyume na alicho weza kuamrishwa basi kifo kitamuhusu.
Kitendo cha fundi mitambo huyo kurudisha picha inayo onyeshwa na kamera iliyopo mlango, wote wakastukia mlango wa chumba hicho unao fungwa kwa kutumia umeme ukiangushwa chini wote kwa kuvunjwa, taa zote zilizomo ndani ya chumba hicho zikazimika gafla, jambo lililo wachanganya Brian na vijana wake wawili walio baki ndani ya chumba hichi wakimlinda yeye kama kiongozi mkubwa, japo sio yeye anaye ongoza kundi hilo.
Brina na watu wake wakaanza kupiga risasi pasipo na mpangilio wowote, mafundi mitambo wapatao sita wote kila mmoja akajitafutia sehemu yake ambayo anaweza kujificha, wengine wakaingia chini ya meza, wengine wakilala chini, mmoja kwa kiwewe alicho nacho akajikuta akijilazisha kujificha kwenye kindoo kidogo cha kuwekea mataka taka.
Brian na watu wake wakajikuta risasi zikiwaishia kwa kuweza kupiga piga ovyo pasipo kuweza kumuona mtu mwenyewe wanaye mpiga. Mngurumo mzito kama simba, ukasikika ukitokea mlangoni, Brian na watu wake wakazidi kuogopa
“Muheshimiwa kuna nini kinacho endelea”
Sauti ya Lukuman kupitia simu ya upepeo ilisikika kwenye redio moja ya upepo iliyo anguka chini, hapakuwa na mtu aliye weza kuijibu zaidi kila mmoja aliisikilizia sauti hiyo kama ya simba ikiendelea kunguruma ndani ya chumba hicho, hadi fundi mitambo aliye jificha kwenye ndoo ya taka mkojo ukamtoka pasipo kujizuia.
***
Kwa kamera ya mwandishi wa habari aliyemo ndani ya jengo aliweza kuchukua moja ya tukio la mtu anaye toa msaada ndani ya jengo hilo na kuirusha moja kwa moja hadi kwa kitu cha habari chake anacho fanyia kazi, ambapo vituo karibia vyote vilivyo kuwepo kwenye eneo la Mlimani City waliweza kurusha tukio hilo, jinsi mtu huyo mwenye ujuzi wa kurusha visu jinsi akiendelea kuwaua watekaji hao mmoja baada ya mwengine.
Taarifa hiyo ikafufua matumaini kwa viongozi walimo ndani ya ikulu ya Tanzania, raisi Praygod akajikuta akilegeza tai yake shingoni, akishuhudia mtu huyo akishusha chini watekaji hao.
“Huyu ni nani?”
Raisi aliuliza baada ya habari hiyo kuisha baada ya kurushwa kwa muda wa kama dakika tano. Hapakuwa na mtu aliye weza kutoa jibu la uhakika kwani kila mmoja ndio kwanza anamuona mtu huyo ambaye wanaamini ni mkumbozi wa watu mamia waliomo ndani ya jengo hilo. Rahab akajikuta akitabasamu usoni mwake, kwani mwanaume anaye mkubali na kumpenda ndio anaye fanya kazi hiyo iliyo washinda mamia ya askari wanaume walipo nje ya jengo la Mlimani City wakijidai wanaimarisha ulinzi usio na faida
Hasira kali ikampanda gafla mzee Gdowin baada ya kuiona taarifa hiyo, akajikuta akichomoa bastola yake na kupiga moja Tv, iliyomo kwenye ofisi yake, na kuwafanya watu wote kustuka kwa tukio hilo.
“Shitiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii………………………….!!!”
Mzee Godwin alizungumza huku akiendelea kutetemeka kwa hasira, kwani mpango wake umesha ingia doa.
“Nahitaji muniletee kichwa cha huyo mwanaharamu”
Mzee Godwin aliondoka ndani ya ofisi hiyo kwa hasira na kuwaacha John wakiwa wanashangaa, ikambidi Manka atoke na kumgwata baba yake sehemu alipo elekea.
“Baba baba”
Manka alimuita Mzee Godwin anaye tembea kwenye kordo hiyo kwa mwendo wa kasi sana huku akiwa amefura kwa hasira
“Baba sasa hicho kichwa cha huyo mwanaaramu tutakipataje?”
“Manka fanyeni kama nilivyo waambia sihitaji maswali zaidi”
“Sawa baba hauhitaji maswali ila nahitaji kujua yule mtu ni nani hadi ukasirike kiasi hicho?”
“Ni EDDYndio anaye waokoa hao watu”
Mzee Godwin akaondoka na kumuacha kwenye hali ya maswali mengi kwani, Eddy ndio mtekaji wa jengo hilo la bishara, sasa itakuwaje ni Eddy huyu huyo ndio anaye waokoa watu aliyo wateka.
Manka akageuka akiwa amechoka kwa jibu alilo pewa na baba yake, akamkuta John akiwa yupo mbali kidogo pamoja na mpambe wake huku naye akiwa amesikikia kila kitu kwamba muokoaji huyo ni Eddy Godwin, wote wakabaki wakiwa wametazamana pasipo kufahamu ni nini kinacho endelea.
***
Eddy akasimama katikati ya eneo walilo wananchi wengi chini, akatazama kila mahali akajiridhisha watu wapo salama, hata kabla hajazungumza kitu cha aina yoyote mlio wa risasi iliyo pita karibu na kifua chake ukamstua, ikawa ni kazi yake sasa kuanza kupambana na watekaji wawili hao ambao ni Briton na Lukuman.
Eddy akajaribu kurusha visu vyake vyote ila vikamuishia pasipo kuwapata watekaji hao ambao nao wanajiweza sana kwenye swala zima la kupambana. Roho ya Shamsa ikazidi kumuuma kumuona baba yake Eddy akiwa ni miongoni mwa watekaji hao walio waua watu wasio na hatia.
Lukuma na Briton wakamuweka Eddy mtu kati huku kila mmoja akiwa amechomoa panga lake refu linalo waka kwa kung’ara, kwa bahati mbaya risasi zote ambazo walizo kuwa wakimpiga Eddy aliye kuwa akifanya kazi ya kujaribu kuziweza kuzikwepa, ni moja tu iliyo weza kumpiga kwenye paja la mguu wake wa kushoto, na kumfanya Eddy asimama huku akichuchumia.
Kitendo hicho kikiwa kinaendelea Shamsa aliweza kushuhudia damu ikimtoka mtu ambaye anaamini amekuja kuwasaidia na kuwaokoa.Bila ya uwoga na wala pasipo kuhofia maisha yake, Shamsa akasimama wima na kuanza kupiga hatua za kwenda walipo simama watu hao walio muweka kati mtu aliye valia mavazi meusi tupu.
Eddy akabaki akiwa katika mshangao mkubwa, baada ya kumuona Shamsa akikaribia katika eneo hilo ambalo ni hatari kwa maisha yake. Eddy akajaribu kutingisha kichwa chake kumzuia Shamsa asiweze kusogelea eneo hilo, ila ndio kwanza Shamsa akaongeza mwendo wa kuwasogelea akiwa amejiandaa tayari kwa kupigania watu wote waliomo ndani ya jengo hilo.
==> ITAENDELEA
Usikose kufuatilia sehemu inayofuata kupitia ubuyublog.com
Post your Comment