ILIPOISHIA
Ukelele wa kulia kwa uchungu ulio tokea juu kabisa ya gorofa ukawafanya wote watatu kustuka hususani Shamsa ndio alishtuka zaidi, akajitoa mikononi mwa madam Mery na kuanza kukimbilia kuelekea gorofani, huku Madam Mery na Sa Yoo wakimfwata kwa nyuma. Wote watatu wakamkuta Black Shadow akiwa amepiga magoti chini, akilia kama mtoto huku sura yake akiwa ameiinamisha kwenye mwili wa Sabogo ulio lala chini kwa kunyooka ukishiria kwamba Sabogo amepoteza maisha.
“Babyyyy……..”
Shamsa aliita huku akikimbilia sehemu alipo Black Shadow, na kuwaacha Sa Yoo na Madam Mery wakiwa wamesimama wasijue ni nini cha kufanya.
ENDELEA
Shamsa akazidi kumsogelea Black Shadow, taratibu akamgusa begani jambo lililo mfanya Black Shadow kujiifikiria kwa muda kabla hajainyanyua sura yake kwa maana anamtambua vizuri Shamsa kwamba ni mwanae wa kumlea japo Shamsa hatambui ukweli wa aina yoyote.
‘Liwalo na liwe’
Black Shadow alizungumza huku taratibu akinyanyua kichwa chake kutoka katika mwili wa Sabogo aliye iaga dunia kwa kupigwa risasi na Lee Si. Taratibu Black Shadow akaigeuza sura yake na kumtazama Shamsa aliye stuka na kuyatoa macho yake, mstuko huo haukuwa kwa Shamsa peke yake, bali Madam Mery pamoja na Sa Yoo nao wakabaki wakimkodolea macho Eddy kwani wote walili wanamtambua vizuri hususani madam Mery aliye kuwa mwalimu wa Eddy tangu akiwa kijana mdogo.
“EDDY………”
Shamsa aliita huku akiwa bado hayaamini macho yake, mwili mzima Shamsa akahisi unamuishia nguvu. Taratibu Shamsa akajikuta akianguka kwenda chini, kabla hajafika chini Eddy akamdaka, Shamsa akazimia.
“Shamsa, Shamsa, Shamsaa”
Eddy alimuita Shamsa ila hakuitika kwa haraka Eddy akamnyanyua Shamsa na kumuweka begani mwake na kuanza kutoka kushuka kwenye jengo hilo huku Madam Mery na Sa Yoo wakifwata kwa nyuma wote wakionekana kuchanganyikikwa. Wakafika chini Eddy akataka kupanda pikipiki yake, ila Sa Yoo akamuomba watumie gari ambalo walikuja nalo.
“Lete funguo”
Eddy alizungumza mara baada ya kumuingiza Shamsa ndani ya gari, Sa Yoo akamkabidhi Eddy funguo na wote wakaingia kwenye gari, wakaondoka eneo hilo. Hapalukwa na mtu aliye weza kuzungumza kitu cha aina yoyote, kila mmoja alimfikiria Shamsa aliye laza kichwa mapajani mwa Madam Mery huku Sa Yoo akiwa siti ya mbele mara kwa mara aligeuka nyuma kuwez akumuangalia Shamsa.
“Unaelekea wapi?”
Sa Yoo aliuliza baada ya kuona wanaelekea nje ya mji. Eddy hakujibu kitu chochote zaidi ya kuongeza mwendo kasi wa gari hadi wakafika kwenye msitu mmoja mkubwa. Eddy akakunja kushoto kwenye barabara ndogo iliyo jaa nyasi nyingi. Akaongeza mwendo kasi hadi wakafanikiwa kufika kwenye pango kubwa, ambapo Eddy kwa haraka akshuka kwenye gari na kumtoa Shamsa, akambeba begani, Madam Mery na Sa Yoo wakamfwata kwa nyuma pasipo kuuliza ni wapi wanapo ingizwa.
Madam Mery na Sa Yoo wakaonekana kushangaa mazingira ya ndani ya pango hilo lililo jengwa kwa ndani vizuri na kuna taa nyingi ambazo zinapendezesha mandhari ya ndnai ya pango hilo.
Eddy akamlaza Shamsa kwenye moja ya sofa, lililopo sebleni. Akamfungua kifungo cha suruali yake kisha akamvua tisheti aliyo vaa akabakiwa na sidiria.
“Mpeni muda wa kupumzika amepoteza fahamu huyo”
Eddy alizungumza huku jasho likimwagika usoni mwake, akashusha punzi na kuanza kuwatazama Madam Mery pamoja na Sa Yoo binti aliye msaidia kipindi anatafutwa na askari wa hapa nchini Japan.
“Kweli wewe ndio Black Shadow?”
Sa Yoo aliuliza huku macho yake akiwa amemtumbulia Eddy.
“Ndio mimi”
Eddy akamtazama Madam Mery ambaye anaonekana anajambo ambalo anahitaji kuzungumza ila anashindwa kulizungumza kwa wakati huo kutokana na uwepo wa Sa Yoo. Eddy baada ya kuligundua hilo akaanza kutembea kuelekea nje na Madam Mery akamfwata kwa nyuma.
“Umefikaje huku?”
Eddy alimuuliza Madam Mery kwa sauti nzito iliyo jaa hasira ndani yake, kwa maana kumbukumbu ya chanzo cha mtu aliye haribu maisha yake, ikamjia Eddy kichwani na Madam Mery ndio muhusika mkuu wa maisha ya Eddy kuharibika wakishirikiana na Mzee Godwin.
Taratibu Madam Mery akapiga magoti chini, huku machozi yakimwagika, kwani anamuelewa Eddy vizuri na anatambua hali aliyo kuwa nayo kwa sasa ni hali ya hasira na endapo atazungumza jambo baya basi maisha yake yapo hatarini kuondoka.
“Eddy, ninahaki ya kufa mikononi mwako, nipo tayari hata sasa hivi maisha yangu yatoke, ila nina kitu kimoja ninahitaji kuzungumza na wewe kabla hujaniua”
Madam mery alizungumza kwa sauti ya unyonge, machozi yakiendelea kumwagika usoni mwake. Kitendo cha sauti ya Madam Mery kupenya masikioni mwa Eddy kikazidisha hasira yake na kujikuta akikunja ngumi, mkono wa kulia huku mmkono wa kushoto ukimtetemeka sana.
“Sinto hitaji kusikia kitu chochote kutoka kwako, niliyaacha maisha yako kwa mara ya kwanza kwa kuheshimu msiba wa mke wangu, mwanangu na mama yangu. Ila kwa sasa nitakuua kisha atafwata Godwin”
Eddy alizungumza huku akimgeukia Madam Mery aliyepiga magoti pembeni yake. Akatamani alichomoe koo la Madam Mery kwa mkono wake wa kushoto unao tetemeka kwa hasira, ila akajikuta mkono huo ukiwa ni mzito sana kufanya jambo hilo. Madam Mery akatulia kimya, huku macho yake ameyafumba kwani anatambua ni nini anacho stahili kufanyiwa. Zikapita sekunde kadhaa za ukimya, Madam Mery akayafumbua macho yake na kumuona Eddy akiwa anaondoka kuingia ndani ya pango hilo na hajamfanya kitu chochote.
“Eddy tunatakliwa kumuua Godwin”
Eddy akasimama, kisha akageuka taratibu na kumtazama Madam Mery aliye piga magoti. Macho ya Eddy yaliyo jaa uwekundu wa hasira huku kwa mbali yakilengwa lengwa na machozi ya hasira, yakaanza kumpandisha na kumshusha madam Mery. Kisha sauti mbili moyoni mwake zikawa zinabishana kwenye kufanya maamuzi. Sauti yake ya kwanza inamtuma kumuua madam Mery muda huo huo, huku sauti yake ya piliikimuomba asifanye mauaji ya mwana mama huyo na amsikilize kwa kile ambacho Madam Mery anahitaji kumuambia.
“Tanzania pamoja na raisi Praygod wapo matatani, muda wowote na saa yoyote wanaweza kupoteza maisha……”
“Kutokana Godwin amekuwa……….Raisi wa nchini Tanzania”
“NINI…..?”
Eddy alistuka sana kusikia habari hiyo ambayo ni mbaya sana ndani ya masikio yake. Akamfwata Madam Mery kwa kasi hadi sehemu alipo piga magoti, jambo lililo mfanya madam Mery ajikute amekaa chini kutokana na kumuogopa Eddy.
“Umesemaje………..?”
“Ni…nini….memee..eeesema baa…ba yak…o Go…d……win amekuwa raisi wa Tanzania”
Madam Mery alizungumza huku mwili mzima ukimtetemeka, japo kuna baridi Eddy akajikuta jasho likimwagika kwa hasira. Kila alicho kifikiria juu ya Mzee Godwin kilimchanganya akilini mwake.
“Na Phid….aya bado yupo hai”
Maneno ya Madam Mery yakazidi kumumshangaza Eddy akilini mwake na kuanza kumkumbuka Nesi Phidaya ambaye alimfananisha na mke wake ila kitu kilicho mchanganya ni kwamba tayari alisha mzika mkewe Phidaya.
***
Matajario mazuri ya watanzania juu ya uongozi wa Raisi Godwin, yakaanza kupotea kadri siku zilivyo zidi kwenda. WWengi walitarajia ugumu wa maisha utapungua ila ndio kwanza ukazidi kuongezeka mara kumi ya awali walivyo kuwa.
Nchi haikuwa ya watanzania wote bali, ikageuka kuwa nchi ya watanzania wachache, wenye nguvu ya kipesa na wenye maamuzi ya kufanya chochote kwa wakati wowote na kwamtu yoyote. Uonevu ukazidi kuongezeka kwa wananchi wa hali za chini, watu wote walio msaidia mzee Godwin kuingia madarakani, walikabidhiwa madaraka makubwa ambayo, hata watu wengine walio kua katika serikali ya raisi Praygod na kumuunga mkono, waliweza kupigwa chini, huku baadhi yao wakibambikiwa kesi na kusekwa magerezani, huku wengine wakifilisiwa na kubaki kuwa masikini kabisaa.
“Mzee tunatakiwa kidogo tuwajali wananchi, hata miaka mingine mitano ukigombania uraisi wakupatie kura zao”
Mshauri wa raisi wa Mzee Godwin, alizungumza huku akimtazama raisi Godwin usoni mwake. Mzee Godwin akatabasamu kidogo kisha akaachia kicheko cha dharau na kumtazama mshauri wake bwala Mgwira
“Ni nani aliye kudanganya kwamba kutakuwa na kupiga kura tena nchini Tanzania?”
“Una maana gani muheshimiwa?”
“Maana yangu ni kwamba hakuna mtu ambaye atanitoa madarakani kwa kupiga kura. Hii nchi kwa sasa ni yangu na nitaiongoza hadi pale nitakapo fariki na endapo itatokea nitakufa basi atakaye tawala atakuwa ni Manka mwanangu kipenzi”
Bwana Mgwira akabaki amemtumbulia macho mzee Godwin, anaye zungumza kwa kujiamini sana.
“Nahitaji nchi hii nibadilishe mfumo wa utawala, uwe utawala wa kifalme na si utawala wa kiraisi”
“Muheshimiwa……………..!!!”
“Ndio, na tena wasiliana na viongozi wote kesho ninahitaji kufanya nao mkutano sawa”
“Sawa muheshimiwa”
Mzee Mgwira hakuwa na kitu cha kuzungumza zaidi ya kukubaliana na raisi Praygod ambaye siku zote akizungumza haitaji mtu yoyote aweze kukipinga. Manka akaingia kwenye sebule ya baba yake na kumkuta akiwa amekaa na Mzee Mgwira, ambaye baada ya kumuona Manka akanyanyuka na kuondoka, kuwapisha baba na mwana kuzungumza.
“Baba mbona unaonekana leo una furaha sana?”
“Ninafuraha mwanangu kwa maana nimefikiria kitu ambacho nina imani kitakuweka wewe kwenye mazingira mazuri sana”
“Kitu gani hicho baba, wakati unamiliki kila kitu kwa sasa?”
“Ninakwenda kubadilisha mfumo wa serikali kutoka katika mfumo wa serikali ya uraisi na kuingia katika serikali ya ufalme”
Mzee Godwin alizungumza huku akifurahia sana.
“Ufalme, ufalme wa aina gani?”
“Nahitaji kuwa mfalme, nitakuwa nikiongoza katika maisha yangu yote na hata mimi nikifa basi wewe mwanangu utatawala katika kiti cha ufalme na utakuwa ni malkia”
Manka naye aklajikuta akitabasamu na kufurahi sana, juu ya wazo ambalo baba yake amelifikiria. Kwa nguvu walio kuwa nayo walijiamini kwamba kila kitu ndani ya Tanzania ni chakwao.
“Wezako wanaendeleaje?”
“Wapo salama tu, kila mtu anaendelea na majukumu yake kwenye wizara ambayo umewapatia”
“Basi wasiliana nao na kesho uwaambie kwamba nina kikao ambacho kitakuwa kinakwenda kuihalalisha serikali ninayo ifikiria”
“Sawa baba”
Manka akanyanyuka kwenye sofa alilo kalia akamsogelea baba yake na kumbusu shavuni na kuondoka zake sebleni na kumuacha Mzee Godwin akifikiria mambo yake.
Siku iliyo fwata, mkutano wa viongozi wote ndani ya serikali ya Mzee Godwin wakakutana kwenye kikoa ambacho kila mmoja alishangazwa na ukubwa wa kikao hicho kwa maana tangu uongozi wa raisi Godwin uanze hajawahi kuitisha kikao kikubwa kama hicho.
“Habari za asubu”
Raisi Godwin alizungumza kupitia kipaza sauti kilichopo kwenye meza yake, kila kiongozi aliye kuwepo kwenye eneo hilo aliitikia. Raisi Godwin akawatizama viongozi walio chini yake kisha akakohoa kidogo na kuanza kuzungumza kitu ambacho alikusudia kukizungumza.
“Ninahitaji kubadilisha mfumo wa serikali”
“Serikali ambayo ninahitaji iwe kwa sasa, itakuwa ni serikali ya ufalme, na hili swala sinto hitaji mtu wa iana yoyote kuweza kulipinga hili”
Minong’ono ya chini chini ikaanza kutawala ndani ya chumba cha mkutano, kila mmoja aliweza kuzungumza chake juu ya kitu kilicho zungumza na Raisi Godwin.
“Kuna baadhi ya sekta nitazifuta rasmi kuanzia leo na sekta ya kwanza itakuwa ni Tume ya taifa ya uchaguzi”
“Eheee bwana Luka unahitaji kuzungumza nini?”
“Muheshimiwa raisi wazo lako ulilo litoa si baya, ila itakuwaje kwa hao wananchi ambao tuna waongoza, watakubaliana kweli na hili?”
“Jeshi tunalo, nguvu ya pesa tunayo ni nani anayewezakupinga kauli yangu?”
Raisi Godwin alizungumza na kuwafanya viongozi wote kuwa kimya wasizungumze neno la aina yoyote.
“Ninaagiza waziri wa mawasiliano, vijulishe vyombo vya habari namuwatangazie juu ya hili nililo zungumza sawa”
“Sawa mkuu”
“Na kitu cha mwisho ambacho labda nitawahurumia wananchi wangu, waweze ku[iga kura za ndio na hapana kupitisha serikali ninayo itaka na watakao kataa. NITAJUA NI NINI CHAKUFANYA”
Raisi Godwin alizungumza na kufunga kikao na kuondoka ukumbini na kuacha mingong’ono ikiendelea, kuna walio kubaliana naye na wapo walio pinga wazo hilo ila walizungumza chichi chini kuhofia ni kitu gani ambacho kitakwenda kutokea juu ya maisha yao.
Kama waziri wa mawasiliano, alivyo agizwa, akaitisha mkutana wa waandishi wa habari, karibia televishion zote nchini Tanzania zikawa katika ukumbi huo wa mikutano. Waziri wa mawasiliano akatoa agizo ambalo limetolewa na raisi Godwin, hadi waandishi wa habari wenyewe wakaanza kushangaa kwa taarifa hiyo kwenda kwa wananchi.
Ikawa ni taarifa mpya kwa wananchi, wapo waliohisi kuchanganyikiwa, ila uhuru wa kuwakilisha mawzo yao kwenye jamii wanashindwa kwa maana anaye kwenda kinyume na raisi Godwin kwa kuweka kitu chochote kibaya kinacho mfedhahesha raisi basi hufatiliwa na hupotea katika mazingira ya kutatanisha. Siku na tarehe ya kupiga kura za kuuweka uongozi wa ufalme madarakani ukawadia, huku vipengele vya kupiga kura vikiwa ni NDIO na HAPANA.
***
Hali ya Phidaya, ikazidi kuimarika siku hadi siku, chini ya usimamizi wa Rahab na raisi mstafu bwana Praygod aliye fukuzwa nje ya nchi ya Tanzania. Phidaya akaruhusiwa kutoka hospitali na kupeleka moja kwa moja katika nyumba ambayo raisi Praygod aliweza kuinunua kwa ajili ya maisha yake ya kudumu kwa maana hakuhitaji kurudi tena nchini Tanzania.
“Kwa nini unasema uhitaji kurudi kwa mumeo Ranjiti”
Raisi Praygod alimuuliza Phidaya wakiwa katika meza ya chakula.
“Ranjiti sio mume wangu”
Phidaya alizungumza huku akimtazama raisi Praygod usoni mwake.
“Una maana gani?”
“Ngoja nimsaidie, huyu ni mke wa waziri wako wa zamani wa ulinzi Eddy Godwin”
Raisi Praygod akajikuta akiishusha glasi ambayo alihitaji kunywa fumba la juisi ila akashindwa kabisa kufanya hivyo, hapo ndipo kumbukumbu za kumbumbuka Phidaya zikaanza kufanya kazi kichwani mwake. Kitu kilicho kuwa kikimpa uhakika kwamba huyu si mke wa Eddy ni kutokana na msiba ambao hata yeye aliweza kuhudhuria akiwa kama kiongozi.
“Haiwezekani…….Huyu binti si alisha kufa?”
“Ndio alikufa, ila si kama watu tulivyo dhania, ila Phidaya yupo hai. Na ndio huyu hapa tuliye kaa naye hapa”
“Hivi, Eddy yupo wapi kwa sasa?”
“Mara ya mwisho kumuona, alikuwa yupo Japan”
Phidaya alizungumza kwa sauti ya upole sana huku machozi yakimlenga lenga
“Itabidi nimtafute Eddy”
Raisi Praygod alizungumza huku akiwatazama Rahab na Phidaya.
***
Shamsa akakurupuka kutoka katika usingizi wa nusu kufa. Akawakuta Sa Yoo, Eddy na Madam Mery wakiwa wamekaa kimya wakimtazama. Shamsa akamtazama Eddy, kisha akamtazama Madam Mery, taratibu akaka kitako akisaidiwa na Sa Yoo ambaye wakati wote alikaa karibu yake akimkanda kanda kwa maji ya baridi.
“Umeamka”
Sa Yoo alizungumza huku akitabasamu, Shamsa sura yake haikuwa na furaha yoyote kila alipo yatazama mavazi aliyo vaa Eddy, akajikuta akimkumbuka Black Shadow wake. Ukimya ukatawala ndani ya sebule hapakuwa na mtu aliye weza kuzungumza kitu chochote. Sa Yoo, akatazama tazama ndani ya sebule hiyo akaona tv kubwa iliyo kwenye moja ya ukuta ndani ya sebule hiyo. Ili kuvunja ukimya huo akanyanyuka na kwenda ilipo Tv hiyo na kuiwasha kisha akarudi kukaa kwenye sofa. Kila mtu akayapeleka macho yake kwenye Tv hiyo, na kukuta taarifa ambayo imeishangaza ulimwengu mzima.
‘WATANZANIA WAPIGA KURA YA KUWEKA SERIKALI YA UFALME NA SI URAISI’
“What…………”
Eddy alizungumza huku akinyanyuka kwenye sofa alilo kaa na kuisogea ilipo tv hiyo kuisikiliza vizuri taarifa hiyo kwenye kituo cha televishio na CNN.
“INABIDI NIRUDI TANZANIA KUIOKOA NCHI YANGU”
Eddy alizungumza huku akiitazama picha ya Mzee Godwin, ikionyeshwa kama raisi aliye hitaji kufanya mabadiliko hadi ya kiserikali.
Mikakati ya kuanza safari ya kwenda nchini Misri, inapo sadikika yupo Phidaya ndipo alipo. Kwa msaada mkubwa wa Mzee Yo pamoja na Sa Yoo, wakamuwezesha Eddy kutengenezewa sura ya bandia ya daktari mmoja bingwa wa kutengeneza sura hizi hapo nchini Japan.
Eddy akatafutiwa hati ya kusafiria, jambo ambalo halikuwa gumu sana kwake na baada ya muda akafanikiwa kuweza kupata hati ya kusafiria. Baada ya siku mbili mbele safari ikaanza. Eddy akakaa siti moja na Madam Mery huku Shamsa akikaa na Sa Yoo aliye omba kusafiri nao. Masaa kadhaa yakakatika angani wakiwa katika ndege ya shirika ETHIAD. Wakafanikiwa kufika nchini Misri majira ya saa tisa usiku. Wakakodi vyumba kwenye moja ya hoteli ya kitalii. Gharama zote zikiwa juu ya Madam Mery.
“Sa Yoo ile namba ya mwanamke aliye kupigia siku ile si unayo?”
“Ndio niliiandika kwenye kijikitabu change”
Sa Yoo akafungua begi lake na kutoa kitabu chake cha kuhifadhia kumbukumbu na kuanza kuitafuta namba, haikuchukua hata dakika akafanikiwa kuipata namba hiyo na kumkabidhi Shamsa, aliye itazama kwa muda kisha akachukua na kuanza kuiingiza kwenye simu ya mezani iliyomo ndani ya chumba chao, hakuhitaji kusubiria kupambazuke ndio aipige namba hiyo.
“Vipi?”
Sa Yoo aliuliza huku akiwa amemtumbulia macho Shamsa aliye ushililia mkonga wa siku kwa mkono wake wa kushoto huku akiwa ameuweka karibu kabisa na sikio lake.
“Inaita”
Shamsa akaendelea kuisikilizia simu hiyo kwa muda, ikaendelea kuita hadi ikakatika. Akajaribu kwa mara mbili zaidi ila haikupokelewa akaamua kuliacha zoezi hilo.
“Labda huyo mtu atakuwa emelala, tusubiri asubuhi”
Sa Yoo alishauri, Shamsa akakubaliana na wazo hilo. Eddy akiwa chumbani kwake, akasikia mlango ukigongwa, akautazama kwa muda kisha akasimama na kwenda kuufungua, Akakamkuta madam Mery akiwa amesimama.
“Vipi hujalala bado?”
Eddy alimuuliza Madam Mery ambaye alitingisha kichwa akiashiria kwamba hajalala bado. Eddy akamkaribisha ndani Madam Mery, kila mmoja akaka kwenye sofa lake akionekana kuwa hana kitu cha kuzungumza hususani madam Mery ambaye muda wote kichwa chake alikiinamisha chini.
“Mbona kimya uzungumzi kitu?”
“Eddy kila nikikutazama nafsi yangu inanisuta sana, bado najiona ni mkosaji kwako”
“Ahaaa hayo mambo yamesha pita, tuangalie ni kitu gani ambacho tunapaswa kukifanya kwa wakati huu”
“Ni kweli ila nikiwa kama binadamu, nazidi kujiona kwamba mimi ni mkosaji, ninaamini ni mambo mengi ya kinyama ambayo nilikufanyia.”
Madam Mery alizungumza huku machozi yakimlenga lenga, Eddy akamtazama kwa muda akajikuta akiingiwa na roho ya huruma, taratibu akasimama na kwenda kukaa kwenye sofa alilo kaa madam Merry ambalo linaruhusu wakae watu wawili.
“Nitazame Mery……”
Eddy alizungumza huku akimshika kichwa Madam Mery kwa mikono yake miwili huku akimgeuzia alipo.
“Hapo mwanzo nilikuchukia sana, ila baada ya kunielezea ukweli nikajua si wewe mwenye makosa. Wewe umeshurutishwa. Ila adui yetu ni Mzee Godwin. Tunatakiwa kufanya kitu kwa ajili ya mioyo yetu. Tuhakikishe kwamba tunafanikiwa kumtokomeza na safari hii ninahitaji iwe ndio mwisho wa maadui wangu”
“Eddy nitahakikisha……ninafanya kila utakalo niambia, itakuwa ni kwaajili ya kufuta dhambi zangu nilizo kuwa nimezifanya juu yako”
Madam Mery alizungumza huku machozi yakimwagika, taratibu Eddy akajikuta akimkumbatia madam Mery aliye zidi kulia kwa uchungu
“Shh………shiiiiii nyamaza usilie”
Eddy akaendelea kumbembeleza madam Mery hadi, Madam Mery akajikuta akipitiwa na usingizi, Eddy hakuona haja ya kumsumbua zaidi ya kumuacha alalie kifua chake. Kutokana na uchovu mwingi, Eddy naye akajikuta akipitiwa na usingizi. Sa Yoo na Shamsa hawakulala hadi asubuhi kunapambazuka.
Shamsa akatoka chumbani kwao na kwenda kwenye chumba ambacho analala Eddy, alihitaji kumuelezea kuhusiana na namba ya mtu ambaye wanaamini anaweza kuwasaidia kumpata Phidaya. Shamsa akashika kitasa cha mlango wa mlango wa kuingilia ndani kwa Eddy akataka kupiga hodi ila akasita kwa muda na kukiachia. Akiawa anajifikiria cha kufanya mlango ukafunguliwa, akakutana na Madam Mery akiwa anatoka katika chumba hicho, huku nywele zake akiziweka vizuri.
“Za asubuhi”
Madam Mery akaanza kumsalimia Shamsa, jambo lililo mfanya Shamsa kutokujibu kitu chochote zaidi ya kumkodolea macho Madam Mery yaliyo jaa maswali mengi.
“Shamsa nakusalimia”
“Aha…aa salama”
Shamsa akajitahidi kuizuia asira yake isijitokeze, madam Mery hakujua chochote zaidi ya kuelekea chumbani kwake na kumuacha Shamsa akimtazama hadi anaingia chumbani kwake. Shamsa akaingia chumbani kwa Eddy bila ya kubisha hodi na kumkuta akitoka bafuni kuoga akiwa na taulo kiunoni mwake.
“Nilihisi umeacha tabia yako kumbe bado unayo tu”
Shamsa alizungumza kwa sauti ya kukasikirika. Jambo lililo mshangaza Eddy
“Tabia gani?”
“Hujui ni nini ulicho kifanya, huyu madam umelala naye usiku kucha”
Shamsa alizungumza huku machozi yakimlenga lenga hata Eddy akabaki akiwa ameduwaaa. Moyo wa Shamsa ulipata maumivu makali kiasi kwamba akahisi unataka kuchomoka. Alijitahidi kujizuia ila hisia za mapenzi zilizidi kumuumiza japo ameutambua ukweli kwa Black Shadow ni Eddy anaye muheshimu kama baba yake.
“Shamsa, sijalala na huyu madam, alikuja jana usiku chumbani kwangu kuna mambo tulikuwa tunazungumza, ndio akapitiwa na usingizi”
Eddu alizungumza huku akiwa amemtazama Shamsa, aliye jawa na hasira ya dhahiri kwamba kuna kitu kinamuumiza, moyoni mwake. Shamsa akajikuta akiachia msunyo mkali na kutoka chumbani kwa Eddy na kumuacha akiwa ameduwaa. Eddy hakuhitaji kuliwekee maanani swala hilo zaidi alicho kifanya, akajiandaa kwa haraka kisha akatoka chumbani kwake na kuelekea chumbani kwa Shamsa na Sa Yoo. Akawakuta wakiwa wamekaa kwenye sofa moja huku Shamsa akionekana kuwa mnyonge.
“Mbona umekuwa mnyonge kiasi hicho Shamsa?”
Eddy aliuliza kwa sauti ya chini kiasi huku akikaa kwenye sofa la pembeni. Sa Yoo akamtzama Eddy kisha akamtazama Shamsa.
“Naona hajisikii vizuri, labda inaweza kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa”
Sa Yoo alijibu huku naye akiwa hajui ni kitu gani ambacho kinamsumbua rafiki yake huyo, ambaye kwa sasa amekuwa kama ndugu yake. Madam Mery akiingia ndani ya chumba hicho huku akiwa amesha badilisha nguo zake tofauti na alizo kuwa amezivaa jana kwenye safari. Kabla madam Mery hajazungumza kitu chochote, mlio wa simu ya mezani ukawastusha kila mmoja na kujikuta macho yao yote wakiyageuzia kwenye simu hiyo inayo endelea kuita kwa muito wa taratibu.
***
Msisimko wa mapenzi ukaanza kumpanda Rahab aliye lala fofofo, taratibu akayafumbua macho yake yaliyo jaa uchovu wa usingizi wa usiku kucha. Akamkuta mume wake, raisi mstafu bwana Praygod akiwa anaipitisha mikono yake kwenye sehemu ya kifua chake, kilicho jazia chuchu zilizo jaa vizuri.
“Mmmm…..baby bwanaaa asubuhi yote hii unaniamsha”
Rahabu alizungumza kwa sauti iliyo jaa mapozi mengi huku macho yake yakilegea kwa msisimko huo anao patiwa na mume wake.
“Nina hamu na wewe mke wangu”
“Kweli?”
“Ndio honey”
Raisi Praygod alizungumza huku akiendelea kuyaminya minya maziwa ya Rahab, kutokana wote wawili walila usiku huo pasipo kuwa na nguo yoyote mwilini wakajikuta wakizama kwenye dimbwi zito la mapenzi. Rahab kama kawaida yake alihakikisha anampatia mume wake penzi lililo jitosheleza.
“Ohooo….ooo”
Raisi Praygod alitoa miguno huku taratibu Rahab akijilaza pembeni ya mwili wa raisi Praygod. Taratibu Rahab akaupeleka mkono wake kwenye meza ya pembeni alipo iweka simu yake ya mkononi. Akaitazama vizuri na kukuta missed call kadha zilizo ingia majira ya usiku.
“Mmmm namba ngeni”
“Jaribu kuzipiga hizo namba”
Rahab akaanza kuipiga namba ya kwanza, iliyo ita kwa muda na kupokelewa na sauti ya kike.
“Haloo, jana usiku ulinipigia, nani mwenzangu”
“Naitwa Sa Yoo, niliwahi kuzungumza na wee nikiwa Japan ukanieleza kuhusiana na swala la bosi wangu Madam Phidaya kwamba yupo nchini hapa Misri”
“Waooo, ina maana upo ndani ya Misri”
“Ndio madam, sijui wewe upo sehemu gani?”
“Ila kwa maagizo ya Phidaya aliniambia mtu ambaye anatakiwa kuonana naye ni Lee Si”
“Ah…….a.aaa..ndio ila Lee Si ameniagiza mimi kuweza kuja, ila unaweza kumuambia madam kwamba Sa Yoo nipo hapa ninamtafuta”
“Sawa hembu subiri kama dakika tano, nitakupigia tena”
Rahab akakata simu na kushuka kitandani, akavaa gauni lake jepesi na kutoka chumbani kwake na kwenda moja kwa moja hadi kwenye chumba cha Phidaya akagonga mara moja mlango ukafunguliwa, wakakutana na Phidaya ambaye alikuwa akifanya usafi.
“Za asubuhi Phidaya”
“Salama vipi mbona mapema, na unaonekana kama kuna tatizo?”
“Hapana sio tatizo, ila nina habari ambayo kidogo ni njema kwako”
“Habari gani hiyo”
Rahab akaingia ndani na moja kwa moja akaenda na kukaa kitandani mwa Phidaya ambaye naye akamfwata na wakaka kwa pamoja.
“Nimepata simu kutoka kwa binti mmoja anaitwa Sa Yoo sijui unamfahamu”
“Ndi..ndio ninamfahamu, amesemaje?”
Phidaya alizungumza huku akionekana kuwa na tabasamu pana usoni mwake.
“Ameniambia kwamba yupo hapa nchini Misri amekuja kuonana na wewe?”
“Yupo wapi?”
“Ohoo sikumuuliza ni wapi alipo, ilangoja niipige tena ile namba uzungumze naye”
***
Kadri siku zilivyo zidi kwenda ndivyo jinsi Dokta Ranjiti alivyo zidisha wingi wa vijana wanao weza kumsaidia kumtafuta Phidaya ndani ya nchi ya misri. Alikodisha vikundi vitano vinavyo jiusisha katika swala la uhalifu, na kila kikundi akawa amekiahidi donge nono la pesa, endapo tu watafanikisha kumkamata Phidaya akiwa hai. Kila kikundi kiliweza kupatiwa picha za kutosha zenye kuionyesha sura ya Phidaya. Upelelezi ulizidi kuwa mkali katika miji yote.
“Bado hamjampata?”
Dokta Ranjiti alimuuliza mmoja wa viongozi wa kikundi cha uhalifu
“Bado hatujampata, vijana wanaendelea kumtafuta kwa udi na uvumba nitahakikisha kwamba tutampata”
“Hembu harakisheni kumtafuta, au hamtaki pesa nyinyi”
“Mzee hakuna ambaye hapendi pesa ndio maana kazi yako tunaifanya usiku na mchana tutahakikisha kwamba anapatikana”
“Sawa fanyeni hivyo”
Dokta Ranjiti akakata simu, huku hasira ikiwa imempanda. Akilini mwake alihisi kuchanganyikiwa, kwani katika maisha yake anampenda mke wake Phidaya kuliko kitu cha aina yoyote ndio maana alihakikisha anafanikiwa kuwa na Phidaya katika maisha yake.
“Bosi kuna simu yako hapa”
Kijana anaye mlinda dokta Ranjiti aliingia ndani ya chumba cha dokta Ranjiti akiwa na simu mkononi mwake. Akampatia dokta Ranjiti na kuiweka sikiooni.
“Nani mwenzangu?”
“Hakuna haja ya kuweza kulifahamu jina langu, ila mwanamke ambaye unamuhitaji yupo njiani kuelekea kwenye hoteli ya AHAL, iliyopo katikati ya jiji la Cairo”
Sauti ya kike ilisikika upande wa pili wa siku, kabla dokta Ranjiti hajazungumza kitu chochote simu ikakata. Akajaribu kuitazama namba iliyo mpigia kwa bahati mbaya akakakuta ni namba private ambayo si rahisi kwa mtu yoyote kuweza kuipga, labda mwenye namba hiyo akupigie yeye mwenyewe.
“Jiandae twende hoteli ya AHAL”
Dokta Ranjiti alizungumza huku akinyanyuka kwa haraka kutoka kwenye kiti ambacho alikuwa amekalia. Wakatoka na mlinzi wake na kuingia kwenye gari lake, na safari ya kueleka katika hoteli aliyo elekezwa na msamaria mwema.
***
Simu ikaita na Sa Yoo akaipokea na kuzungumza na mtu aliye piga kwa bahati nzuri akakuta ni sauti ya Rahab
“Ehee ulisema kwamba upo wapi?”
“Nipo katika hoteli ya AHAL, gorofa ya ishirini chumba namba elfu mbili na tisa”
“Sawa tunajiandaa tunakuja hapo mulipo sasa hivi na Phidaya”
“Sawa nitawapokea”
Simu ikakatwa Sa Yoo akawageukia, Eddy na wezake huku akiwa na tabasamu pana usoni mwake.
“Wanakuja”
“Saa ngapi?”
Eddy aliuliza kwa shauku kubwa, kwa mbali machozi yakimlenga lenga.
“Ameniambia dakika chache watakuwa hapa”
Shamsa hakuonekana kuwa na furaha ya aina yoyote zaidia alicho kifanya ni kunyanyuka na kutoka nje ya chumba hicho pasipo kumuaga mtu yoyote.
“Mbona mwenzako yupo hivi?”
Eddy alimuuliza Sa Yoo baada ya Shamsa kutoka ndani ya chumba hicho.
“Sifahamu anasumbuliwa na nini, kwa maana hii hali imeanza asubuhi hii tu”
Hapakuwa na aliye weza kuliwekea maanani swala la Shamsa, kila mtu kwa wakati huo akawa anamfikiria Phidaya. Baada ya dakika tano Shamsa akaingia akiwa katika hali yake ya unyonge. Hapakuwa na mtu aliye msemesha. Baada ya dakika tano mbeleni simu ikaita, Sa Yoo kwa haraka akakimbialia hadi mezani na kuipokea simu hiyo.
“Tumesha fika kwenye hii hoteli, tupo hapa chini. Sijui unaweza kuja kutuchukua”
Sauti ya Rahab ilisikika kwenye simu hiyoi
“Sawa basi ninakuja”
Sa Yoo akakata simu na kuwataarifu wezake habari hiyo, wote kwa pamoja wakatoka kwenye lifti hiyo na kuanza kushuka kwenda chini.
Rahab na Phidaya wakiwa ndani taksi waliyo jia, wakaendelea kumsubiria mwenyeji wao kuja kuwapokea, uzuri ni kwamba Phidaya anamfahamu Sa Yoo, macho yao kwa pamoja wakawa wanatazama kwenye mlango wa kutokea kwenye hoteli hiyo kubwa ya kitalii, yenye wageni wengi wanao ingia na kutoka.
Meseji ikaingia kwenye simu ya dokta Ranjiti inayosomeka kwa maandishi makubwa (TUPO KWENYE TAKSI NYEUPE HAPA KATIKA MAEGESHO MUHESHIMIWA)
Meseji hiyo ilimtosheleza dokta Ranjiti kuyapitisha macho yake kwenye maegesho ya magari yaliyopo katika eneo hilo. Akaiona taski nyeupe iliyopo kwenye eneo hilo, dokta Ranjiti akashuka kwenye gari kwa haraka huku bastola yake ikiwa mkononi mwake. Kwa hatua za haraka anazo zitembea dokta Ranjiti, akafanikiwa kuifikia taksi hiyo kwa haraka, pasipohata kuzungumza chochote akaufungua mlango wa nyuma wa siti hiyo. Phidaya akastuka macho yakamtoka, mwili mzima akahisi umemuishia nguvu, alipo iona sura ya dokta Ranjiti iliyo jaa hasira. Rahab naye akajikuta akimeza fumba la mate asijue ni nini afanye kwa maana mdomo wa bastola ya dokta Ranjiti ukiwa umewaelekea.
“SHUKA NDANI YA GARI”
Dokta Ranjiti alizungumza kwa hasira kali, bila hata ya kubisha Phidaya akashuka ndani ya gari, huku Rahab naye akafwatia kushuka. Dokta Ranjiti kwa iashara akawaelekeze sehemu ya kuelekea kwenye gari lake. Macho ya Eddy, Sa Yoo, Shamsa na Madam Mery wakawashuhudia Phidaya na Rahab wakiingia kwenye moja ya gari la kifahari huku nyuma yao akiwepo dokta Ranjiti.
“RANJITIIIIIIIIIIIIIIIIIII…………………….”
Eddy aliita kwa sauti kubwa na kumfanya dokta Ranjiti kutazama sehemu sauti hiyo inapo tokea, kwa haraka aliweza kuotambua sauti hiyo ni ya Eddy, ila sura ni tofauti kabisa, ila macho yake yalipo muona Madam Mery akiwa nyuma ya mtu huyo akagundua kwamba kila kitu kimeharibika. Kwa kiwewe dokta Ranjiti akajikuta akifyatua risasi kadhaa kuelekea anapotokea Eddy na kusababisha watu kuanza kukimbia kimbia ovyo kuyaokoa maisha yao.
==>ITAENDELEA...
Usikose kufuatilia sehemu inayofuata kupitia ubuyublog.com
Usikose kufuatilia sehemu inayofuata kupitia ubuyublog.com
Post your Comment