ILIPOISHIA
Kila mtu moyo wake ulizidi kumuenda mbio akiwa ndani ya gari hilo. Madam Mery taratibu akajikuta akianza kusali sala yake ya mwisho kwa maana wanapo elekea kifo kipo mbele yao.
“Fanya uwashe gari”
Manka alizungumza huku machozi yakianza kumwagika, kila jinsi dereva alivyo jaribu kuwasha gari lake, halikuwaka hadi ikafika kipindi akakata tama kabisa. Matairi ya mbele tayari yalisha anza kuelea hewani kwenye korogo hilo linalo endelea kulika taratibu taratibu na matairi ya nyuma pekee ndio yapo kwenye ardhi.
“Ohoo Mungu wangu tunakufa”
Manka alizungumza huku akiyafumba macho yake, akisubiria gari hiyo kuangukia kwenye korongo hilo na huo ndio utakuwa ni mwisho wa maisha yao.
ENDELEA
Wakiwa katika hali ya sinto fahamu, gafla wakastukia watu wawili wa kiwa nyima yao wakijitahidi kulishika gari hilo kwa nyuma. Walipo geuka wakawaona Shamsa na Eddy ambaye Manka anamtambua kwa jina la Ericksom. Kwa ishara Shamsa akawa anawaomba wateremke.
Madam Mery akawajibu kwa vitendo kwamba hawawezi kushuka kutokana milango imejifunga na hakuna kitu chochote kinacho weza kufanya kazi ndani ya gari hilo.
“Tunafanyaje sasa Eddy?”
“Tafuta jiwe uvunje kioo”
“Sawa”
Shamsa akaanza kutafuta jiwe ambalo linaweza kupasua kioo cha gari hilo, kwa bajati nzuri akapata jiwe moja kubwa, kwa haraka akarudi nalo hadi sehemu ilipo gari.
“Vunja kioo kimoja wapo”
Eddy alizungumza huku jasho likimwagika, kwa maana shuhuli ya kuizuia gari hilo lisitumbukie kwenye korongo hilo ni kubwa sana kwake. Kila Shamsa alivyo jaribu kupasua kioo cha upande alio kaa madam Mery, hakikupasuka wala kuonyesha dalili ya mpasuko.
“Mungu wangu gari hii ni bullet proff na haaingia risasi, ndio maana kioo chake hakipasuki.”
Shamsa alizungumza huku machozi yakimlenga lenga, kwa maana juhudi anazo zifanya zimekuwa ni bura kabisa. Gafla taa za nyuma ya gafi hizo zikaanza kuwaka, dereva kwa haraka akajaribu kuminya kitufe cha kufungua milango hiyo akafanikiwa. Manka akajirusha nje, madam naye akafanya hiyo hivyo, shuhuli ikawa kwa dereva ambaye amekaa siti ya mbele kabisa. Uzito ulizidi kuongezeka pale alipo kuwa kwenye harakati za kutaka kuhamia siti ya nyuma ili atoke kwa maana milango yote ya mbele endapo ataifungua na kujaribu kutoka basi safari yake ni moja kwa moja hadi kwenye korongo hilo.
“Nisa…..iidi…..eeeni”
Eddy alizungumza huku akijikaza kadhi ra uwezo wake kuhakikisha kwamba analizuia gari hilo lililo anza kusogea mbele taratibu likelekea kudumbukia kwenye korongo hilo.
Wote watatu wakaanza kulishika gari hilo kwa nyuma sehemu ambapo Eddy amepashika. Dereva huyo ambaye alisha anza kukinusa kifo kwa haraka haraka akajirusha siti ya nyuma na kujirusha nje. Kitendo cha yeye kutoka Eddy na wezake wakaliachia gari hilo na likadumbukia kwenye korongo hilo refu kwenda chini.
“Ohooo honey”
Manka alizungumza huku akimkumbatia Eddy kwa nguvu. Shamsa akataka kuwaachanisha ila madam Mery akamshika mkono na kutingisha kichwa akimuashiria kwamba asifanye chochote. Askar wengine kutoka ikulu nao wakafika eneo hilo wakiwa na bunduki zao mikononi. Shamsa alipo waona askari hao akataka kuondoka ila askari mmoja akamshika bega.
“Subiri mwaya”
Kumbe sababu ya askari huyo kumshika Shamsa bega ni kutokana na Manka kumuonyeshea askari huyo kwa ishara amzuie asiondoke eneo hilo. Manka akaachiana na Eddy na kumfwata Shamsa pale alipo simama.
“Asante kwa kuyasaidia maisha yetu”
“Usijali ni kitu cha kawaida”
Manka akampa mkono Shamsa, aliye upokea taratibu. Wakaachiana mikono huku Manka akionekana kumtazama Shamsa usoni. Kumbukumbu zake zikarejea hadi pale hospitalini, alipo weza kumuona Shamsa akiwaangusha walinzi wawili walio pewa kazi ya kumlinda akiwa na Erickson ndani. Kumbukumbu zake hazikuishia hapo akakumbuka jinsi walivyo pambana ndani ya chumba hicho ili asichukuliwe Erickson ila walipo ingia Madam Mery na binti mwengine wa Kijapani hapo ndipo walipo mzidi nguvu na kuondoka naye.
“Weeee……..”
Manka hadi anastuka kutoka kwenye dimbwi la mawzo, tayari Shamsa alisha ondoka eneo hiloakijichanganya watu wanao shangaa shangaa kilicho tokea.
“Mtafuteni yule binti sasa hivi”
Manka alitoa amri kwa askari wake kutoka ikulu ambao walianza kutawanyika kumfwatilia ni wapi Shamsa alipo elekea huku wengine wanne wakibakia katika eneo hilo wakiimarisha ulinzi dhidi yake.
Eddy na Madam Mery walibaki kukonyezana kwa maana waliweza kumshuhudia Shamaa akiondoka eneo hilo baada ya Eddy kumpa ishara ya kukimbia huku akimkabidhi funguo za gari la dokta pasipo mlinzi au mtu mwengine yoyote kuweza kuona tukio hilo.
“Erickson…….!!!”
Manka alimuita Eddy huku akiwa amemkazia macho na kumtazama kwenye upande wa kushoto wa koti jeupe alilo livaa.
“Nini?”
Eddy aliuliza huku akiteremsha macho yake kuangalia ni kitu gani kinacho endelea. Eddy macho yakamtoka, wasiwasi ukamjaa mwingi, hii ni baada ya kuona damu nyingi ikiwa imelowanisha koti hilo alilo vaa ikiashiria kwamba mshono wake umepata tatizo ambalo ni kubwa sana. Kwa haraka walinzi wa Manka wakamchukua Eddy huku wakimsaidia kushika pande zote mbili za mikono yake na kuondoka naye hadi kwenye magari yao yalipo huku Manka na Madam Mery wakimfwata kwa nyuma.
“Madam tumpeleke hospitali gani?”
Dereva alizungumza huku wakiwa wote tayari wamesha ingia kwenye gari hilo.
“Wewe twende tu”
Manka alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake kila alipo mtazama Erickson wake aliye laza kichwa mapajani mwake na kujikausha kimya asizungumze chochote
***
“Mkuu hatujaweza kumpata kiongozi na hali iliyo jitokeza huku naamni kwa sama ninaamini muna ishuhudia kwneye televishion”
Mmoja wa vijana wa kikosi maalumu kutoka D.F.E walio tumwa kuweza kumuokoa mzee Godwin alizungumza na simu akiwasiliana na John ambaye yupo kwenye ukumbi wa kutano Serena Hotel akiwa na viongozi wengine wakisuribia kuweza kupata matokeo mazuri kama mzee Godwin amapatikana au laa.
“Ondokeni eneo hilo, na sura zenu zisionekane kwenye televishion”
“Sawa mkuu”
Kijana huyo akakata simu, kwa haraka akelekea kwenye uapende wa pili wa barabara, alipo waacha wezake ndani ya gari, wakiwa wamenuusurika kudumbukia kwenye korongo hilo lisa moja lililo kwisha kupita.
“Vipi wamesemaje?”
“Wamesema tuondoke sura zetu zisionekane eneo hili wala kwenye televishion”
“Poa”
Dereva akawasha gari na wakaondoka eneo hilo. Mmoja wao aliye kaa siti ya mbele pembeni ya dereva akashusha pumzi kisha akaanza kuzungumza.
“Jamani hivi munajua laiti tungesubutu kukomaa na wale makachero wa kwanza kuingia ndani mule ya msitu na sisi habari yetu ingekuwa imesha kichwa?”
“Kweli mwanagu, kwa maana tangu nizaliwe sijawahi kuona bomu la namna hii”
“Yaani muda ule nilipo anza kuuona ule mpasuko wa ardhi, akili yangu ilinituma kwa haraka kurudisha gari nyuma hadi tukafika barabarani”
“Nasikia waseng** wote walio kuwemo ndani ya msitu wamedanja”
“Weee kwa timbwili lile unahisi wasinge danja”
“Alafu kumbe mtoto wa mzee alikuwepo”
“Nani?”
“Manka, naye angeenda na maji”
“Aisee tuache utani ila lile toto ni lizuri”
“Anaye lila lile naamini kwamba ana faidi ile mbaya”
“Kweli, ukishikilia ile mitako na mihispi, mamayeee”
“Acheni ujinga nyinyi tufikirie ni jinsi gani tunaweza kumpata mzee”
Mkuu wao alizungumza na kuyakatisha mazungumzo ya vijana wake ambao wote wanamezea mate Manka mtoto wa bosi wao ambaye ni Mzee Godwin.
***
Gari zote mbili njia nzima walizisha taa japo ni mchana kweupe pee. Mwendo ambao wanatembea nao ni spidi mia na sabini, wakipunguza sana ni mia na ishirini. Kila kulipo kuwa na miji ambayo wangeweza kuwagonga wavika barabara kwa miguu, kazi ya madereva hao ikawa ni kupiga honi kuahsiria watu hao kupisha.
“Agnes upo nje kwenye kuondesha gari”
”Ina maana umesahau kipindi kile, tumetoka kupiga tukio tukawa tunaendesha zile gari ndogo, kitu tulicho watesa nacho polisi wewe mwenye si ulishuhudi mziki”
“Kweli, umenikumbusha mbali kinyama”
“Jamani hivi yule dokta aliye tupa mafunzo yupo hai?”
“Kusema kweli mimi sifahamu habari zake, kabisa”
Agnes alizungumza huku akiongoza msafara huo wa kurudi jijini Dar es Salaam. Hawakuwa na wasiwasi wowote kwa maana wote humo ni mawaziri wa wizara tofauti tofauti pasipo Rahab ambaye hapo nyuma alibahatika kuwa mke wa raisi wa awamu aliyo pita.
Kwa bahati nzuri njiani hawakuweza kusimamisha na askari. Moja kwa moja wakaelekea nyumbani kwa Agnes anaye ishi peke yake pamoja na mlinzi ambaye hamruhusu kuingia kwenye nyumba yake zaidi ya kukaa kwenye nyumba ya nje iliyopo pembezeni mwa jumba lake hilo la kifahari. Agnes akaminya honi mara moja geti hilo likafunguliwa, gari zote zikaingia ndani na kuzunguka nyuma ya nyumba hiyo ambapo kuna maegesho ya magari mengine. Wakashuka woye watano kwenye magari yao.
“Hembu ngoja nikamcheki huyu mlinzi asije akaleta ujinga”
“Poa”
Agnes alizungumza huku akiondoka eneo hilo na kuwaacha wezake wakimtazama mzee Godwin ndani ya gari, anaye watazama kwa macho ya hasira sana.
“Mzee huyu kipindi cha ujana wake anaonekana alikuwa HB wa ukweli”
Fetty alizungumza kwa utani huku akimtazama mzee Godiw kweye kioo. Wezake wote wakajikuta wakimcheka mzee Godwin, kwa maana mateso aliyo yapata basi sura yake imeweza kukunjamana kiasi kwamba hata mwananchi wa kawaida akimuona hawezi kufahamu haraka haraka labda ajitambulishe.
“Vipi kuna mtu aliye kuja kuniulizia leo?”
Agnes alizungumza huku akimtazama mlinzi wake usoni.
“Hapana bosi”
“Uliacha nyumba yangu wazi ehee?”
“Hapana bosi sihatoka kabisa leo”
“Ok ni hivi, kuanzi leo mtu yoyote atakaye kuja kuniulizia muambie kwamba mimi sipo sawa”
“Sawa mkuu”
“Na kingine, hihitaji geti dogo ulifungue fungue”
“Sawa bosi”
“Mbona unajibu kinyonge nyonge hujakula nini?”
“Ahaa bosi, mimi nimesha pata msosi”
“Ok kazi njema”
Agnesa akamaliza kuzungumza na mlinzi wake moja kwa moja akarudi walipo wezake na kuwakuta wakicheka na kufurahi.
“Jamni nimesha zungumza na huyu mlinzi wangu, sasa tunamuweka wapi huyu mzee”
“Huna stoo yoyote humu ndani?”
“Ninayo tena kubwa”
“Basi tumuingize ndani huyu tukajue ni nini cha kufanya”
“Sawa, tena kuna mlango wa huku nyuma ni vyema tuka muingiza”
Wakamshusha ndani ya gari, wakambeba kwa kushirikiana wakaingia kupitia mlango huo wa nyuma ambao sio rahisi kabisa kwa mlinzi kuweza kujua ni kitu gani ambacho kinaendelea, Wakamuingiza stoo, kitendo cha kumuweka sakafuni, Rahab akaanza kumpiga mateke ya hasira mzee Godwin hadi wezake wakamzuia
“Punguza hasira Rahab”
Fetty alizungumza huku akijitahidi kumshika Rahab.
“Mpumbavu ameniulia mume wangu huyo”
“Ni kweli, punguza hasira. Huyu tuna maswali tunahitaji kumuhoji tuweze kujua”
“Yaani eheeee haki ya Mungu, nihatakikisha ninakata kipande kimoja kimoja cha huyo mwanaharamu mpaka vyote viishe”
Rahab alizungumza huku akijiapisha. Akatoka stoo na kuwaacha wezake wakimsidikiza kwa macho.
“Utakatwa kweli mwili wako, lione”
Anna alizungumza huku akimsuta mzee Godwin kisha naye akatoka stoo humo.
***
Manka moja kwa moja na walinzi wake wakafika hospitli ya Ocean Road, wakapokelewa na madaktari kwa haraka haraka na moja kwa moja, Eddy akapakizwa kwenye kitanda cha matairi na kupelekwa katika chumba cha upasuaji. Madaktari kwa haraka haraka, wakaanza kuchana nguo zake kwa kutumia mikasi, walipo maliza kwa haraka wakaanza kumsafisha Eddy kwa dawa maalumu ya kuua bakteria kwenye vidonda. Nyuzi za kwenye mshono wa Erickson karibia zote zilifumuka, hii ni kutokana na muda ule alipo kuwa akipambana kuwaokoa Manka na wezake wasidumbukie kwenye korongo, misuli yake iliweza kutanuka na kusababisha nyuzi hizo ambazo hazina hata wiki, kuachiana kwenye kidonda hicho.
Daktari mkuu akaagiza vichukuliwe vipimo kwenye kidonda hicho ili kuona kama kutakuwa kuna tatizo jengine waweze kukabiliana nalo kwa haraka iwezekanavyo. Madaktari wasaidizi wakafanya hivyo, huku wengine wakimalizia kushona kidonda cha Eddy ambaye wamesha mchoma sindano ya usingizi, ili kuwa rahisi kwa woa kuweza kuifanya kazi hiyo.
Opareshini ikachukua masaa takribani masaa manne. Madaktari walipo maliza, wakamtoa Eddy na kumuingiza katika chumba maalumu cha uangalizi wa hali ya juu(ICU).
“Samahani nina mazungumzo na nyinyi”
Daktari mkuu alizungumza na Manka na madam Mery ambao muda wote walikuwa wakidwatilia upasuaji huo unakwendaje wakiwa nje ya chumba cha upasuaji, na hadi Eddy alipo ingizwa ICU walizuiwa kutoa kumuona na waliombwa waweze kusubiri kwa masaa kadhaa hadi aweze kuamka. Wakaongozana na daktari huyo ambaye ni mzee wa makamo, mwenye asili ya kiarabu na mfupi kidogo. Wakaingia ofisini kwa mzee huyo, ambapo akawakaribisha kwenye viti viwili vilivyopo mbele ya meza yake kisha yeye akazunguka kwenye meza yake na kukaa kwenye kiti chake.
“Vipi daktari hali ya mgonjwa?”
Manka aliuliza mara baada ya kukaa kwenye kiti, daktari huyo akavua miwani yake na kujifuta macho yake na kitambaa cheupe kisha akaivaa kwa mara nyingine.
“Hali ya mgonjwa tunashukuru Mungu kwamba tumejitahidri ya uwezo wetu na tumeweza kuyaokoa maisha yake”
“Ohoo asante Mungu”
Madam Mery alizungumza huku akishusha pumzi nyingi.
“Ila kuna kitu kinginine ambacho ni hatari tumeweza kukigundua kwenye mwili wa mgonjwa”
“Kitu gani daktari?”
Manka aliuliza huku macho yakiwa yamemtoka, daktari akamtazama jinsi alivyo pata taharuki hiyo. Akatamani kuzungumza kitu anacho taka kukizungumza. Ila akawa anafikiria kama ameanza hivyo tu je hicho atakacho kizungumza si kitaweza kumletea shida kiongozi huyu wa nchi isitoshe ana taarifa za juu ya baba yake kuweza kutekwa na watu wasio julikana. Madam Mery aliweza kuyaelewa mawazo ya daktari aliye kaa kimya kwa muda akimtazama Manka.
“Manka tulia mwanangu”
Madam Mery alizungumza huku akimshika mkono Manka aliye anza kumwagikwa na jasho ambalo dhairi limesababishwa na woga mwigi.
“Dokta zungumza jamani please”
“Sawa ila sio taarifa mbaya sana, kwa maana tunaweza kuishuhulikia kwa kadri ya uwezo wetu.”
“Zungumza sasa daktari”
“Tumeweza kuchukua vipimo kwa mgonjwa, kiujumla afya yake ipo vizuri, ila ana vimelea vya ugonjwa wa saratani, ambao imetulazimu kwamba kuanza kufanya matibabu leo hii hii, ila ninaamini kwamba kila kitu kinaweza kuwa vizuri”
Manka akajikuta akishusha pumzi nyingi huku akiwa amemtazama daktari huyo. Mlio wa simu ukawastua wote walio kaa eneo hilo, Manka akajipapasa mfukoni mwa koti lake akatoa simu yake na kufungua ujumbe huo wa meseji na kuisoma meseji hiyo iliyo mstua na kumfanya anyanyuke kwenye kiti alicho kalia huku macho yakiwa yamemtoka na kuwafanya Madam Mery na Madam Mery kumtolea macho wakitaka kufahamu ni kitu gani kilicho andikwa kwenye meseji hiyo.
SORRY MADAM (99) (Destination of my enemies)
Manka akahisi mwili mzima ukitaka kumuishia nguvu, taratibu akaka kwenye kiti huku akiwa ameishia simu yake. Ikambidi Madam Mery kuichukua kwa haraka simu hiyo na kuusoma ujumbe ambao umeandikwa.
(TUNAHITAJI KUFANYA MABADILIKO, MUACHIE ERICKSON, TUKUPATIE GODWIN. NA SWALA HILI LIFANYIKE NDANI YA MASAA 24 LEO)
Madam Mery akashusha pumzi nyingi, ukimya ukatawala ofisini humo, daktari asifahamu kinacho endelea. Ubaya wa meseji hiyo iliyo tumwa, nambaya yake ni Private, ikimaashisha kwamba haijaweza kuonekana na kufahamika mtumaji ni nani. Manka akaichukua simu yake na kupiga baadhi ya namba na kuiweka sikioni.
“Ndio muheshimiwa”
“Niandalieni kikao cha wakuu wote wa majeshi, ninakuja sasa hivi ikulu”
“Sawa muhehsimiwa”
Manka akakata simu, akanyanyuka kwenye kiti na kupiga hatua hadi mlangoni kisha akageuka na kumtazama dokta na Madam Mery aliyepo nyuma yake.
“Dokta nahitaji mgonjwa wangu mumpatie matibabu ya kutosha. Na hitaacha walinzi waweze kumlinda, yoyote ambaye hausiki na kuingia kwenye chumba hicho ninakuomba asiingie”
“Mimi nitabaki kukaa na mgonjwa”
Madam Mery alizungumza huku akimtazama Manka, ambaye naye akamtazama kwa sekunde kadhaa kisha akaitingisha kichwa cha kukubali mama yake mdogo huyo kuweza kubaki hapo hospitalini na kumlinda Erickson.
“Sawa muheshimiwa”
“Tafadhali daktari ninakuomba sana mgonjwa wangu mumtazame kwa maana yeye ndio kila kitu kwenye maisha yangu”
“Usijali hilo muheshimiwa, tutajitahidi kadri ya uwezo wetu kwa maana kazi yetu ni kuokoa maisha ya wa watu”
“Nitalishukuru daktari”
Manka na madam Mery wakatoka katika ofisi hiyo na kuanza kuelekea katika chumba alicho lazwa Erickson, ila ukweli wa kila kitu ni madam Mery pekee ndio anafahamu kwamba Erickson ndio Eddy, ambaye amefahamu kwamba pia ni mwanaye, japo amezaliwa na mwanamke mwengine ambaye si dada yake.
“Mama mdogo nakuomba uwe makini na Erickson, kwa maana sijui ni kitu gani nifanye juu ya hii meseji”
“Usiwe na shaka katika hilo, ninakuomba uende ukafanye kikao hicho, na aikiwezekana tutawageuka wote hao, watamkosa Erickson na pia tutamuokoa muhueshimiwa”
“Asante mama mdogo kwa ushauri wako”
Manka akamkumbatia madam Mery kwa nguvu, kisha wakaingia kwenye chumba alicho lazwa Erickson ambaye kwa sasa anahemea mashine yahewa safi.
“Erickson wangu ni mzuri eheee?”
Manka aliuliza huku machozi yakimlenga lenga. Madam Mery akatingisha kichwa akionekana kukubaliana na lile ambalo amelizungumza Manka.
“Mama mdogo, tafahdali mlinde sana Erickson”
“Usijali wewe niachie walinzi tu wakusaidiana nao”
“Unahitaji wangapi?”
“Wanne”
“Sawa sasa hivi ninawaacha hapo nje”
Wakatoka wote kwa pamoja ili Manka amuonyeshe madam Mery walinzi atako waacha hapo nje. Walipo maliza zoezi hilo la kutambulishana. Manka akaondoka eneo la hospitali na kuelekea ikulu na kumuacha madam Mery akiwa amekaa chumba kimoja na Erickson ambaye hadi sasa hivi hajazinduka katika usingizi mzito ulio tokana na kuchomwa sindano ya usingizi.
***
Shamsa moja kwa moja akaelekea hadi nyumbani kwa Eddy mara tu ya kutoka kwenye korongo. Kitu cha kwanza kukifanya baada ya kufika karibu kabisa na nyumba hiyo akasimamisha gari lake, kisha akashuka na kuanza kutembea kwa miguu hadi getini. Ukimya ulio tawala ndani ya nyumba hiyo dhairi kunaonyesha hakuna mtu wa aina yoyote ndani ya nyumba hiyo, ukizingatia akili ya viongozi wengi sasa hivi walipo serikalini pamoja na askari akili zao zipo katika kumtafuta raisi Godwin.
Akaingia kwenye geti, kwa umakini mkubwa, alipo hakikisha kwamba eneo la nje hapo lipo salama, moja kwa moja kwa mwendo wa kasi akaingia ndani, hali ya sebleni hapo haikuwa tofauti sana na siku ambayo waliondoka. Akalelekea kwenye chumba cha ardhini ambapo, ndipo pesa za Eddy alipo ziweka. Akaingiza namba za siri kwenye mlango wa chumba cha kwanza kisha akaitoa picha kubwa iliyopo ukutani na kukuta sehemu nyingine ya kuingiza namba za siri ili mlango wa chumba cha pili uweze kufunguka.
Akatuliza akili yake kisha akaanza kuingiza namba ambazo anakumbuka jinsi siku alivyo kuja eneo hilo na Eddy, vidole vyake vilivyo kuwa vikiminya minya hizo batani.
Haikuwa kazi ngumu kwake, mlango huo ambao ni kipande cha ukuta ukafunguka taratibu. Shamsa akaingia ndani ya chumba hicho na kukuta pesa zote walizo ziacha zikiwa humo humo. Kwa haraka akaanza kubeba vibunda vingia na kuviweka katika chumba cha kwanza, alipo hakikisha pesa ambayo ameichukua hapo inamtosha, akaufunga mlango huo, akatoka na kuelekea katika chumba chake cha kulala. Akafungua kabati lake na kutoa begi lake kubwa la mgongoni, akashuka nalo kutoka gorofani hadi kwenye chumba hicho kilichopo chini ya ardhi.
Akaanza kuziingiza pesa hizo ambazo kwa haraka haraka hakujua ni kiasi gani kwa maana zimefungwa nyingi kwenye vibunda. Alipo malinza kulijaza begi hilo akarudi nalo chumbani kwake. Akaingia bafuni na kuoga, akabadilisha nguo na kuvaa nguo nyingine ambazo zilikuwa kwenye kabati lake hilo.
‘Niende bank gani nikabadilishe hii pesa?’
Shamsa alizungumza huku akijitazama kwenye kioo, jinsi alivyo pendeza. Suruali yeusi, buti nyeusi, tisheti jeupe pamoja na kikoti cheusi, alikiri mwenyewe kwamba amependeza. Akafungua tena kabati lake na kutoa kofia nyeusi na kuivaa.
‘Hapa sio rahisi kwa mtu kuweza kunifahamu’
Shamsa alizungumza huku akiendelea kuzungumza mwenyewe. Akachukua parfum yake moja ambayo kipindi cha nyuma alikuwa anaipenda sana kujipulizia kwenye mwili wake. Akaitingisha kidogo, akafungua mfuniko wake na kuanza kujipulizia mwilini mwake, ila gafla kichefuchefu kikamkamata na kujikuta akiuziba mdomo wake an kukimbilia bafunini, akainama kwenye sink la kunawia na kuanza kutapicha.
“Ohoo Mungu wangu nini tena?”
Shamsa alijiuliza huku akijitazama kwenye kioo kilichopo kwenye sink hilo. Akafungu maji na kuanza kusukutua na kuyatema kwenye sinki huku mapigo ya moyo yakimuenda mbio.
“Nina nini tena”
Alijiuliza huku akianza kutoka bafuni huko, akaka kitandani akizidi kufikiria ni kitu gani ambacho kinamsumbua kwa wakati huo. Kidogo nguvu zikamrudia na hali ya mapigo ya moyo kumuenda kasi ikampungua. Akanyanyuka kitandani akanyanyua begi lake lililo jaa pesa, akalibeba mgongoni na kuanza kutoka ndani homo. Akajikaza na kuanza kutembea moja kwa moja hadi kwneye gari lake alipo liacha.
Akashusha pumzi nyingi, mara baada ya kukaa kwenye siti ya dereva, akafunga mlango huku begi hilo la pesa akiwa wameliweka siti ya pembeni.
Safari ikaanza kuelekea benki yoyote ambayo alihisi kwamba anaweza kupata huduma ya kubadili pesa hiyo ya kimarekani na kupewa shilingi. Akafika baki ya Bacrayse maeneo ya Posta, akasimamisha gari lake eneo la maegesho kisha akashuka na kuelekea ndani.
“Nahitaji kubadili pesa”
Alimueleza muhudumu wa mapokezi, ambaye alimuonyesha mlango wa kuingia kwenye moja ya ofisi ya wahudumu wanao shuhulika na ubadilishaji wa fedha za kigeni. Akaingia kwenye ofisi hiyo na kumkuta dada mmoja mwembamba kiasi aliye valia vizuri sara zake na kupendeza. Akalivua begi lake na kukaa kwenye kiti alicho karibishwa kukaa
“Nahitaji kubadili pesa”
“Ni kiasi gani?”
Shamsa akafungua begi lake hilo na kuanza kutoa vibunda hivyo vya pesa na kuanza kuvipanga hapo mezani. Kadri jinsi anavyo vitoa ndivyo jinsi dada huyo alivyo baki ameshangaa kwa maana katika utendaji wake wa kazi hakuwahi kukutana na mtu anabadilisha pesa kiasi hicho kikubwa.
“Inabidi tuzihesabu”
“Sawa hakuna shida”
Dada huyo akaanza kufungua rababend ya kibunda kimoja moja na kuweka noti hizi kwenye mashine maalumu ya kuhesabia pesa. Kazi ya kuzihesabu pesa hizi ikachukua dakika kumi na tano hadi wanamaliza na kiasi cha pesa ambacho kimepatikana hapo ni dola milioni mbili na laki nne, ambazo ni sawa na shilingi bilioni tano na milioni arobaini za kitanzania.
“Unaweza kubibadilishia hiyo dola laki nne?”
“Na hizi mbili”
“Nahitaji kufungua akaunti na niziweke”
“Sawa”
Wakaanza kufanya harakati za Shamsa kufungua akaunti kwa kuwahonga wahudumu wanao mshuhulikia swala la kumfungulia akaunti, haikuchukua muda kitu alicho wapatia ni picha za passport size alizo piga nje ya benk hiyo kwenye moja ya studio. Hadi lisaa moja linakatika kila kitu Shamsa akawa amemaliza hadi kadi ya benki akawa amepatiwa. Akazibeba milioni mia nane arobaini kwenye begi lake huku pesa nyingine akiziweka kwneye maboksi aliyo patiwa hapo benki, akaziingiza kwenye gari lake na kuondoka.
Kizungu zungu na kustuka mapigo ya moyo kwa mara kadhaa, kukamfanya Shamsa kuamua kupitia kwenye hospitali moyo iitwayo Bochi, maeno ya Mbezi kwa msuguri. Akachukua noti kadhaa na kushuka kwenye gari lake, akalifunga vizuri na kuingia hospitalini hapo. Akamuhonga nesi wa mapokezi ili aweze kuonana na daktari kwa haraka haraka. Kweli nesi huyo akampatia nafasi ya kipekee ya kumuingiza kwenye chumba cha daktari japo kuna foleni ya kina mama wamejipanga wakisubiri huduma.
“Unajisikiaje”
Shamsa akaelezea tatizo linalo msumbua, daktair moja kwa moja akatambua kwamba binti huyu ni mjamzito, japo hakutaka kukisia akaamua kumfanyia vipipo vya kupima mimba. Shamsa akayasubiria majibu ndani ya chumba hicho hicho cha daktari.
“Dokta nina sumbuliwa na nini?”
Daktai akatabasamu huku akiwa ameshika karatasi aliyo andika majibu hayo. Akaiweka miwani yake vizuri na kuyapitia majibu kwa mara ya pili kisha akamtazama Shamsa.
“Hongera sana binti, unaonekana una ujauzito wa mwezi moja sasa”
“Dokta What……?”(Daktari nini?)
“Vipimo vinaonyesha wewe ni mjamzito wa mwezi mmoja sana”
Shamsa akajikuta akifumba mdomo wake kwa kiganja cha mkono wa kulia, hakuamini kwamba ipo siku anaweza kupata ujauzito tena wa mwanaume anaye muheshimu kama baba yake, ambaye ni Eddy. Akaikwapua karatasi ya daktari hiuyo na kuisoma vizuri, hapakuwa na kitu kilicho badilika zaidi ya majibu konyesha yeye ni mjamzito.
“Dokta asante”
Shamsa akanyanyuka na kuondoka ofisini humo akiwa katika hali ya mshangao. Hakujua hata aanze vipi kumueleza Eddy. Akaingia kwenye gari lake na kuondoka eneo hilo, safari ya kueleka alipo waacha Phidaya na Sa Yoo ikaanza huku njia nzima kichwa chake kikiwa na mawazo mengi sana. Shamsa akafanikiwa kufika salama salami kwenye kijiji cha Wamasai hao, akakuta wakiwa kwenye mkutano huku Phidaya na Sa Yoo wakiwa wamesimama pembeni.
“Umechelewa hadi tukapatwa na wasiwasi”
Phidaya alikuwa wa kwanza kuzungumza mara baada ya Shamsa kushuka kwenye gari. Wakasalimia kwa kukumbatiana.
“Mbona umechelewa”
Shamsa akawaadisia mambo aliyo kutana nayo huko alipo toka, huku swala la yeye kuwa mjamzito akawaficha wezake.
“Wanajadili nini hao?”
“Wanajadili juu ya vifo vya vijana wao”
“Nimekuja na pesa za kutosha tunaweza kuwapatia wao, kama rambirambi yetu”
“Basi ngoja nifanye kumuita mmoja wao ili nimueleze hili swala”
Sa Yoo akamuita binti ambaye walikuwa naye akamueleza kitu wanacho taka kukifanya, binti huyo akapeleka ombi hilo kwa mwenyekiti wa mkutano huo ambaye naye aliweza kuwaeleza wanakijiji wote walio kubaliana kwa pamoja kupokea rambirambi hiyo.
“Tuwape tu sisi tuondoke zetu, nimesha choka kukaa hapa kijijini”
“Hapana mama, tuwasimamie wanaweza kudhulumiana si unafahamu hii ni pesa”
“Kweli unacho sema Shamsa”
Wakakubaliana kwa pamoja na kila familia ambayo ilipoteza kijana mmoja iliweza kupatiwa milioni kumi. Zoezi hilo likachukua masaa matatu na kumalizika pasipo kutokea vurugu ya aina yoyote. Shamsa, Sa Yoo na Phidaya wakawaaga wanakijiji hao walio ingiwa na furaha ya pesa, na kuondoka zao kijiji hapo.
***
“Hii meseji niliyo mtumia Manka ninaamini kwamba ni lazima itamchanganya”
Rahab alizungumza huku akiwatazama wezake walio kaa kwenye sofa za hapo sebleni mwa Agnes.
“Sasa itakuwaje, akikataa kumleta Erickson?”
Agnes aliuliza huku akimtazama Rahab usoni anaye onyesha kudhamiria kufanya kile ambacho amekifikiria.
“Nitamuua Godwin kwa mkono wangu”
“Ila Rahab tufanye kwanza mabadilishano ya Erickson na Godwin”
“Kisha, hata kabla hawajamchukua Godwin tunamuua”
Fetty alizungumza na kuwafanya wezake wote kulifikiria swala hilo.
“Natambua kwa sasa atakuwa amekwenda kujadiliana na viongozi juu ya meseji uliyo mtumia”
“Alafu Anna wewe si waziri wa mambo ya ndani, fanya basi uende ikulu ukajue mpango wao ni nini”
“Alafu?”
“Ukisha fahamu mimi huku nyuma nitamtumia Manka meseji nyingine ya kumambia ni wapi tuje kufanya mabadilishano”
“Sawa nitaifanya hiyo kazi”
Anna akakubaliana na wezake, akatoka nje na kuingia kwenye moja ya gari alilo kabidhiwa na Agnes, akaondoka na kuianza safari ya kwenda ikulu.
“Jamani alafu nina namba ya meja Paul Msuya”
“Wa nini tena huyo?”
“Huyu siku alisha wai kunigusia juu ya jeshi kupanga kufanya mapinduzi ya serikali ya sasa hivi, na kama tukiwahi kuungana nao basi tunaweza kuichukua hii nchi”
Wazo la Halima likawafanya wote kukubaliana nao. Halima akatoa simu yake mfukoni na kumpigia meja Paul Msuya na kuiweka loud speaker
“Ndio Meja”
“Nahitaji tuonane kwa mazungumzo yake uliyo wahi kunishirikisha”
“Ohooo safi sana waziri kwa sasa upo wapi?”
“Nipo nyumbani kwangu, sasa sijui tuonane wapi?”
Wakapanga sehemu ya kuonana, ndani ya nusu saa lijalo, Wote wanne walio salia wakaondoka huku wakiwa kwenye magari tofauti tofauti kila mmoja. Wakafika sehemu waliyo kubaliana kuweza kufika na kumkuta meja huyo akiwa na vijana wake wanao mlinda.
“Naona umekuja na timu yako”
“Ndio kwa maana tunataka kufanya kitu cha uhakika katika hili”
“Na huyo si alikuwa ni mke wa muheshimiwa Preygod”
“Ndio meja”
Meja Paul Msuya akasimama kwa haraka na kupiga saluti akiwa pamoja na vijana wake jambo lililo mshangaza sana Rahab.
“Heshima yako mkuu”
“Nashukuru”
“Ni vyema sana tumekupata kwa maana karibia asilimia sabini ya jeshi la Tanzania tulikuwa tunamuunga mkono raisi Praygod, ni wachache sana walio kuwa juu yetu wanao muunga mkono raisi Godwin”
“Sasa huyo unaye sema ni raisi Godwin mimi kwa sasa ninaye”
“Unaye sijakuelewa”
“Baada ya kifo cha mume wangu, na mimi nimeamua kulipiza kisasi kwa Godwin kwa maana yeye ndio amehusika na kifo cha raisi Praygod”
“Ina maana raisi Praygod amefariki?”
“Ndio amefariki, katika mlipuko ulio tokea pale Mlimani City mwezi ulio pita”
“Mungu wangu”
“Nahitaji unikutanishe nia viongozi wote wa jeshi, nataka kufanya mapinduzi na kuhakikisha tunaitoa mizizi yam zee Godwin yote”
“Sawa mkuu”
“Na hili sihitaji liweze kuchukua muda mrefu, leo au kesho kazi iwe imesha kamilika, sinto weza kuona nchi yangu inaendeshwa katika hali isiyo zinga haki na katiba iliyo wekwa”
Rahab alizugumza kwa machungu sana na kuwafanya wote kutulia na kumsikiliza kwa umakini na hapo ndipo ikaonyesha kwamba kuna nguvu ya utawala ambayo Rahab anayo.
“Sasa mkuu unatuhitaji sisi jeshi kuweza kufanya nini?”
“Nahitaji ikulu nzima muweze kuiweka chini ya jeshi, huku wanajeshi wote wanao onekana kuwa ndio wasaliti wa hii nchi muweze kuwatia nguvuni na mkono wa sheria unakuwa juu yao. Na kingine, kwa wale ambao watakuwa ni wakaidi, basi damu haina budi kumwagika”
“Sawa madam”
“Andaa vikosi vyote na uwajulishe juu ya ujumbe wangu na ujumbe alio nipatia mume wangu, nchi hii ni nchi ya kila mwananchi na si nchi ya familia moja wala ukoo mmoja, hatuwezi kufwata maamuzi ya kichwa kimoja ni laziama kufwata maamuzi ya pamoja. Mimi na wezangu hapa tunahitaji makombati ya kijeshi pamoja na silaha”
“Ina maana hawa mawaziri nao watavaa, mavazi hayo?”
“Ndio meja, hawa ni mahodari zaidi ya unavyo wafikiria”
Rahab alizungumza kwa kujiamini. Akatoa simu yake mfukoni na kuisoma meseji iliyo ingia kutoka kwa Anna ambaye yupo ikulu.
(NIMEFIKA NA NIPO KWENYE KIKAO TUMA UJUMBE)
Rahab kwa haraka akaandika meseji nyingine na kumtumia Manka. Alipo malinza hapo, kikao hicho cha dharura walicho kutana na meja kikavujwa rasmi huku Fetty na Anna wakiondoka na meja huyo kwenda kambini huku Agnes na Rahab wakirudi nyumbani kuendelea na mpango wao wa mapinduzi.
***
Wakiwa wanafikiria ni nini cha kufanya juu ya meseji ambayo kiongozi wao ametumiwa na mtu ambaye anaonekana ndio mtekaji, ujumbe mwengine wa meseji ukaingi kwenye simu ya Manka na kwa haraka akaufungua na kuusoma.
(LEO SAA SITA KAMILI USIKU, TUKUTANE DARAJA LA KIGAMBONI KUFANYA MABADILISHANO YA ERICKSON WETU NA RAISI GODWIN, OLE WAKO UJE NA ASKRI TUTAKUONYESHA)
Meseji hiyo ya kitisho ikamfanya Manka kushusha pumzi huku akiwatazama watu waliomo humo ndani ya kikao. Akawasha maiki yake kwa kuminya batani ya kuwashia na kuwaomba watu wote wamsikilize. Akaisoma meseji hiyo kila mtu akaonekana kuogopa kwa maana hapo ni lazima kufanywe maamuzi magumu.
“Madam miimi ninakushauri kwamba ni vyema tukamtoa huyo Erickson anaye mtaka na tena kwenye daraja la baharini, vijana wetu wanaweza hata kujificha ndani ya maji na muda ukimfika tunawaokoa wote wawili”
“Kweli muheshimiwa, ninaungana kabisa na mkuu wa jeshi la maji, mimi nipo tayari kutoa vijana wakaweza kupambana katika hili”
“Nimewaelewa je ikishindikana inakuwaje?”
“Sidhani kama hao magaidi wana uwezo wa kuweza kupambana na serikali na kuiangusha chnini. Serikali yetu ina nguvu ndio maana tukakuteua wewe kutuongoza. Muheshimiwa fanya maamuzi magumu katika hilo”
“Ila kana nilivyo waeleza hapo awali, Erickson ni mgonjwa, itakuwaje katika hili?”
“Madam kama atakuwa amezinduka, anaweza hata kukalishwa kwenye kiti cha magurudumu, na kabla hajafika kwa magaidi hao tunaweza kumchukua”
Manka akanyamaza kimya akiwaza mawazo hayo yanayo tolewa na wakuu hao wa vikosi mbali mbali vya majeshi. Hapakuwa na njia yoyote zaidi ya kuwaamini, na kufanya maamuzi hayo ambayo kwa upande wake kusema kweli ni magumu. Ujumbe ukatumwa hospitalini kwa walinzi, wakaoambiwa waweze kuwaleta ikulu Erickosn na madam Mery. Huku hekaheka za kuanza kufanya maandalizi ya tukio la saa sita usiku yakaanza, vikosi maalumu, vikaanza kuwekwa tayari kwa kazi hiyo. Hata Manka mwenyewe akajiandaa kijeshi kuhakikisha kwamba baba yake na Erickson wanarudi mikoni mwake.
Haukupita muda mrefu Erickson na madam Mery wakafikishwa Ikulu huku Erickson akiwa amesha zinduka. Wakamueleza Erickson mpango mzima ambao upo mbele yao.
“Erickson mpenzi wangu ninakuomba sana uweze kunisaidi katika hili”
Manka alizungumza kwa shauku, Eddy akamtazama Manka jinsi anavyo muomba, akaona akikataa inaweza kuleta picha mbaya, ikambidi kukubali. Madkatari wa hapo ikulu wakitwa na kuanza kumuandaa Erickson kwa kumchoma sindano ambazo walidai zinaweza kumpatia nguvu na kuondoa mamumivu yote ya kidonda anacho kisikia. Walipo maliza kufanya hicho, Erickson akavalishwa jaketi la kuzuia risasi na nguo za kawaida.
“Nitaweza kutembea mwenyewe”
“Kwa hiyo hauta kaa kwenye kiti cha matairi”
“Ndio dokta”
Vikosi vyote vilipo hakikisha vimekaa sawa, wakaanza kusubiria muda na masaa yasonge ili waweze kwenda kwenye sehemu ya tukio kwenye daraja la Kigamboni lililo jengwa juu ya bahari.
***
Mipango yote waliyo panga Manka na viongozi wengine wa kijeshi, Anna akavifikisha kwa Rahab na wezake, hawakupoteza muda wakawasiliana na meja Paul Msuya, na kumueleza kila kitu. Naye hakuta kupoteza muda akaanza kupanga vikosi vyake vya uvamizi Ikulu kwa ajili ya kuipindua nchi.
“Sisi tutadili na hao wote ambao watakuwa chini ya maji wamejificha”
Anna alizungumza huku akiwatazama wezake.
“Anna na Halina nyinyi mutakuwa chini ya daraja, Agnes utakuwa na bunduki ya kudungua kisha mimi na Fetty tutakuwa na huyu fala”
“Sawa”
“Kingine tukumbuke kwamba yote haya tunayafanya kwa ajili ya macho ya mamilioni ya watanzania wanao tarajia nchi yetu kurudi katika mfumo ambao walisha uzoea. Hili tunalo kwenda kulifanya si kwa faida ya nchi na si kwa faida ya matakwa yetu binafsi”
Maneno ya Rahab yakamgusa kila mmoja na wote wakajikuta wakikumbatiana kwa pamoja huku kila mtu akiwa amepania kazi ambayo anakwenda kuifanya kwa siku ya leo. Hawakujua kama kuna kupona au kufa, ila walicho kusudia ni kuhakikisha kwamba wanatimiza kile walicho kihitaji kukifanya. Wakavalia mavazi ya kijeshi, kial mmoja silaha yake akaiweka katika sehemu ambayo amekusudia kuiweka.
Anna na Halima, wakabeba na nguo pamoja na mitungi ya kuwasidi kukaa chini ya maji kwa muda mrefu, baada ya kila mmoja kuhakiksha maandalizi yake binafsi yamekamilika, wakatoka nje na kumchukua raisi Godwin wakaumuingia kwenye gari aina ya Range rover ambayo ni nyeusi, wakapanda Rahab na Fetty ambaye ni dereva. Anna Halima na Agnes wakaingia kwenye gari jengine ambalo ni BMW X6. Kila mmoja wao akawa na kifaa cha mawasiliano ambacho kiliweza kiwawezesha wote watano kuweza kuwasiliana kwa wakati mmoja.
“Hivi sasa ni saa mbili usiku, safari yetu moja kwa moja itakuwa hadi Kigamboni mwanzo wa daraja, na baada ya hapo tunaweza kusubiri hadi pele saa sita itakapo timu”
“Sawa”
Wakatoka kwenye jumba hilo la Agnes, aliye mpa maelezo mlinzi wake kufunga geti na kukaa ndani na asitoke. Safari ikaanza huku gari waliyo panda Agnes ikitangulia mbele na gari waliyomo Rahab ikifwatia nyuma. Hawakwenda kwa mwendo wa kasi kuhofia kustukiwa, uzuri wa gari zote zina vioo vyeusi ambavyo sio rahisi kwa mtu wa nje kuweza kuona ndani.
Wakafanikiwa kufika Kigamboni saa tatu na nusu usiku na kuwawahi hata makachero wa serikali walio fika saa nne kamili usiku.
Anna na Halima wakavaa mavazi yao ya kuzamia ndani ya maji pamoja na gesi zao kisha wakatoka na kuzama baharini pasipo mtu yoyote kuweza kuwaona zaidi ya Agnes, ambaye yeye alisalia ndani ya gari peke yake. Masaa yakazidi kwenda taratibu, kila mmoja akatamani kuweza kuona saa sita inafika kwa haraka.
Makachero kutoka ikulu pasipo kufahamu kwamba wanacho kifanya wanaonwa na maadui zao, wakaanza kuzuia magri yaliyo kuwa yanahitaji kupita katika daraja hilo na hadi inatimu saa sita kasoro tano, gari la Manka akiwa na Erikckson aliye mpakiza siti ya nyuma likafika mwanzo wa daraja kuelekea Kigamboni.
“Naona wamesha fika”
Fetty alizungumza huku akiwa analitazama gari la Manka kwakutumia darubini.
“Liweke gari barabarni”
“Poa”
Fetty akaliwasha gari na taratibu akaanza kojongea kwenye daraja hilo. Manka naye alipo weza kuiona gari hiyo akawasiliana na makachero wake walio zagaa kila mahali, na kuwaeleza kwamba wahusika wamesha fika.
”Kuweni makini na musifanye chochote pasipo mimi kuweza kuwapatia amri ya kufanya”
“Sawa mkuu”
Manka naye akalisogeza gari lake taratibu. Kisha akalisimamisha umbali mkubwa kutoka lilipo simama gari Rahab. Saa sita kamili ilipo fika, simu ya Manka ikaita, akaitoa mfukoni mwake na kukuta namba inayo piga hapo ni hiyo private namba. Kwa haraka akaipokea na kuiweka simu yake sikioni.
“Habari Manka, naamini umekuja na mtu tunaye muhitaji”
“Ndio na mimi ninaimani umekuja na baba yangu”
“Yupo, mshushe Erickson nasi tumshushe baba yako mzee Godwin”
“Sawa”
Manka akakata simu na kumgeukia Erickson aliye mpakiza siti ya nyuma.
“Honey wakati ndio huu, nakuomba ushuke, vijana wapo chini ya daraja watafanya yao”
“Sawa”
Erickson, taratibu akafungua mlango wa gari hilo, kabla hajashuka Manka akamshika mkono, wakatazamana kwa sekunde kadhaa kisha akamuachia. Eddy akapiga hatua hadi mbele ya gari la Manka linalo washa taa zenye mwanga mkali, na kwa upande wa mbele ya daraja akamuona Rahab akimshusha raisi Godwin, japo Rahab amejificha sura yake kwa kujichora na rangi nyeusi wanazo tumia wanajeshi wakiwa vitani ila aliweza kumfahamu kutokana na tembea yake. Erickson akageuka na kutazama nyuma, Manka kwa ishara akamuomba atembee.
Erickson taratibu akaanza kutembea akilifwata gari la Rahab lilipo, huku Mzee Godwin naye akianza kutembea kwa kuchechemea akionekana ni mtu mwenye majeraha makubwa sana. Wakazidi kutembea huku pande zote mbili wakiwatazama jinsi wanavyo tembea. Agnes aliye jificha sehemu akiwa na bunduki yanye lensi ya kuona mbali, akawa analifwatilia tukio hilo kwa umakini.
Ila Agnes akiwa eneo hilo akaona kuna sehemu moja ya pemeni ya bahari kukiwa na mtu ambaye ana bunduki kama yake, na ameielekeza kwa Eddy kwa haraka Agnes akanza kuimvuta mtu huyo karibu na kumkumbuka kwamba mtu huyu ni mlinzi wa John.
“Shitiii”
Agnes akaikoki bunduki yake na kumuelekezea mtu huyo na kumpima maeneo ya kichwa. Mzee Godwin hadi anakaribiana na Erickson akaweza kuona alama nyekundu ya buduki ikiwa imemlenga Erickson kifuani. Kwa haraka Mzee Godwin kwa akamuwahi Erickson ambaye anatambua ni mkwe kwa mwanaye Manka, akamsukuma na risasi ambayo ilipangwa kumpiga Erickson ikapiga mzee Godwin mgongoni na kumuangusha chini na kumfanya Eddy kushangaa na kwaharaka akaipiga magoti chini na kumgeuza Mzee Godwin na kumkuta akimwagikwa na damu mdomoni.
“BABABAAAAAAAAAA”
Eddy alipiga kelele humu machozi yakianza kumwagika usoni mwake na kumfanya Mzee Godwin kutabasamu na kumshika mkono wa kulia Eddy na kuuweka kifuani mwake.
ITAENDELEA- USIKOSE SEHEMU YA 100 NA YA MWISHO
Post your Comment