Get the latest updates from us for free

mas template
Home » , » TANGA RAHA- Sehemu ya Tisa ( 9 )

TANGA RAHA- Sehemu ya Tisa ( 9 )

Written By Bigie on Tuesday, February 20, 2018 | 10:44:00 AM

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA

Rahma akiwa anaendelea kuzungumza na simu kwa mbali nikamuona Mama Fety(Fatuma) akija katika eneo la ninapoishi huku akiwa ameongozana na mwanamke mwengine ambaye sikuweza kumtambua mara moja kwani bado wapo mbali kidogo na nilipo simama mimi
 
ENDELEA
Rahma akamaliza kuzungumza na simu akashush kiio cha gari katika upande nilio simama mimi
“Baby wala siingii ndani hapa baba amenifokea kama nini kwa jinsi nilivyo chelewa”
“Sawa tutaonana kesho shule?”
“Powa.Nakupenda Sir Eddy”
“Hata mimi ninakupenda pia”
Rahma akawasha gari na kuondoka.Nikabaki nimesimama huku nikiwaona Mama Fety na mwenzake wakija nilipo simama
“Mambo Eddy?”
“Powa vipi?”
“Safi mida ya mchana nilikuja sikukuta ulikwenda wapi?”
“Kuna sehemu nilikwenda kufwatilia mambo yangu ndio ninarudhi hivi”
 
“Ahaa vipi chai ulikunywa”
“Ohhh yaani mwanao alipokuwa anaileta yaani nilikuwa ndio naondoka ikanibidi niiweke ndani na sasa hivi kama unavyo niona ndio ninarudi”
Nikamuona rafiki wa Mama Fety akimminya Mama Fety kiunoni kama anapeana ishara ila sikujua ni ishara ya nini
“Karibuni ndani”
Tukaingia chumbani kwangu nikawakaribisha na kuwawashia video waangalie wanachopenda kuangali.
“Baby huyu ni rafiki yangu anaitwa Saumu…..Saumu huyu kama nilivyo kuadisia anaitwa Eddy ndio mahabuba wangu”
Utambulisho alio ufanya Mama Fety haukunifurahisha hata kidogo japo ninajitahidi kuweka sura ya furaha usoni kwangu
“Nashukuru kukufahamu Eddy”
 
“Na mimi pia nasg=hukuru kukufahamu”
Nikachukua Laptop yangu na kuanza kupangilia mada nitakazo fundisha shuleni siki itakayo fwata.Wakaendelea kutazama Video baada ya muda Mama Fety akanyanyuka kutoka katika sofa alilo kaa hadi kwenye sofa nililo kaa mimi.
“Baby”
“Mmmmm”
“Mbona upo kimya jamani hata huzungumzi na sisi?”
“Kuna kazi hapa nina ifanya si unajua kesho ni Jumatatu inanibidi kupangilia kila kitu cha kufundisha mapema ili kesho nisipate tabu”
“Utamaliza saa ngapi?”
“Kwani munataka kuondoka?”
“Hapana ila nilitaka kujua ni saa ngapi utamaliza kwani mimi na rafiki yangu tunataka tukupeleke ukashangae shangae mji”
 
“Kwa hili best itakuwa ngumu”
“Kwa nini jamani?”
“Hap nilipo nimechoka kiasi kwamba nikimaliza tu hii kazi nalala ili kesho nisichelewe kazini”
“Jamani Baby si tunakwenda mara moja mida ya saa tano tano tunarudi”
“Yaani kweli kwa hapo nisamehe baby hembu tufanye siku nyingie”
“Mama Fatuma kweli shemeji Eddy anaonekana amechoka muache apuumzike kwani si yupo kila siku”
“Shemeji umeona eheeee”
“Haya bwana mumeamua kunishambulia watu wawili basi sina jinsi inabindi nikubaliane na nyini”
 
Nikashukuru Mola kwa shemeji Saumu kunitetea.Mama Fety akarudi alipokuwa amekaa awali na kuendelea kutazama video,baada ya dakika kumi wakaaga na kuondoka mimi nikashukuru Mungu.Nikamaliza kufanya kazi zangu nikaingia bafuni nikaoga na kupanda kitandani na kuaanza kuulazimisha usingizi huku kumbukumbu za maisha yangu ya nyuma zikianza kunijia akilini.

Machozi yakaanza kunimwagika nilipokumbuka jinsi baba na mama walipokufa siku moja wakiwa shambani wakilima.Inasadikika kuwa radi ya kimiujiza iliwapiga na kuwaua na chakushangaza jua lilikuwa ni kali katika siku hiyo na hapakuwa na dalili yoyote ya mvua kushusha.Sura ya mdogo wangu ikaanza kunijia nikakumbuka kipindi mdogo nilipokuwa nina cheza naye hadi siku anafariki kwa kubakwa mbele ya macho yangu
 
Nikakumbuka jinsi nesi mmoja laiyejitolea katika kunisaidia akanipeleka katika kituo vha kulelea watoto yatima kilichopo Iringa ambapo nilipata fursa ya kuendelea na elimu yangu ya msingi na kufanikiwa kufaulu vizuri na kuendelea na eleimu yangu ya sekondari hada kidato cha sina na kufanikiwa kuingia chuo na kusomea ualimu.Na hapo ndipo nikaajiriwa Tanga Mjini na katika maisha yangu yote nilitokea kuwaogopa wasichana hadi Rahma aliponitoa uoga wangu siku mbili za nyuma.Kwa msongamano wa mawazo nikapitiwa na usingizi na kulala.
 
Nikastushwa nn sauti ya mlio wa saa yangu ya ukutani ikiniashiria ni asubuhu,Nikajiandaa na kwenda zangu shule kuwajibika.Nikafika shule moja kwa moja nikaongoza hadi ofisini na kuwakuta baadh ya wanafunzi waalimu wakiendele na na maandalizi ya masomo yao tukasalimiana nao na kukaa katika sehemu yangu.

Kendelea ya wanafunzi kukusanyika ikawadia kama kawaida yangu nikaenda kwenye mkusanyiko huo wa wanafunzi ambao mara nyingi waalimu tunautumia katika kutoa matangazo.Wanafunzi wakiwa wanaendelea kuwepo mstaarini nikaliona gari alilo kuja nalo Rahma jana nyumbani kwangu.

Akashuka mwana mama wa kiarabu huku wakiongozana na Rahma anayeonekana mnyonge kama mtu aliyetoka kupigwa muda mchache ulio pita.Wakapokelewa na mwalimu wa zamu na kuelekezwa katika ofisi za waalimu.Furaha yangu yote ikapotea nikajikuta nina shauku ya kutaka kujua ni kwanini Rahma ameletwa shule tena akiwa katka hali ya unyonge.Wanafunzi walipo tawanyika nikaelekea ofisini na kuwakuta Rahma na Mama aliyemleta huku wakiwa wanazungumza na mwalimu wa zamu
 
“Malimu hii toto kuwa jinga sana……yeye chelewa chelewa rudi nyumbani chelewa amka yeye leo fanya tia yeye makofi awai amka ndio lete mimi hapa shule”
Mama aliye mleta Rahma alizungumza kwa Kiswahili kibovu ila niliweza kumuelewa,Rama akawa ananitazama kwa macho ya kuuiba iba huku akiwa amenunu
 
“Sawa mama tumekuelewa ila mwanao si jeuri na tabia yake ni njema labda hiyo tabia ya kuchelewa awe ameianza siku za hivi karibuni”
“Sawa malimu ila jana yeye danganya mimi na baba yake kwamab kwenda kwa nyanya yake ila nyanya yake dai yeye akukaa hata saa moja akaondoka hata jui alikuwa wapi na yeye rudi nyumbani saa tatu usiku”
“Rahma jana ulikuwa wapi?”
Mwalimu wa zamu alimuuliza Rahma na kunifanya nianze kuogopa kwani sikujua Rahma atajibu kitu gani kwani kili nilipomtazama usoni nikahisi ataitoa siri
 
“Sir jana mimi nilikwenda kwa bibi ila nikawahi kuondoka wakati ninarudi nikakuta kuna ajali ile barabara ya Mwahako basi pale nilitumia kama masaa mawili tukisubiri wagari yaliyopata ajali yatolewe barabarani…….Baada ya hapo nikaendelea na safari yangu….Nikiwa njiani gari ikapata pancha sikuwa na jinsi zaidi ya kumpigia fundi ninayemjua atoke huku mjini hadi sehemu mimi nilipo kufika kwanza akawa hana vifaa ikamlazimu arudi tena mjini ndio aje na kifaa cha kugungulia tairi za gari nililo kuwa nalo.Mpaka tunamaliza ni saa mbili usiku”
Uongo wa Rahma ukafanania na ukweli nikajikuta nikishusha pumzi kidogo nguvu zikaanza kunirejea.
 
“Jana nimemuelewesha baba akanielewa sasa sijui kwanini mama yeye amekuwa mbishi….”
“Malimu hii toto anza tabia ya vivu leo hadi amsha na makofi si kazi ndogo”
“Sawa mama hilo tutalifanyia kazi”
“Mimi malimu taka huyu kula bakora tano za nguvu kesho yeye menyewe atakumbuka wahi shule”
“Sawa”
“Taka ona mbele yangu wewe chapa hii toto zembe”
Mwalimu wa zamu akanyanyuka na kufungua kaati ambalo tunahifadhia fimbo akatoa fimbo moja ya mti wa mpera ambayo imekaukavizuri na kukaa katika kiti chake.
 
“Rahma chukua hii fimbo nenda pale kwa Sir Eddy akakuchape mimi mkono wangu unaniuma.Sir Eddy hembu nichapie huyo mualifu kwa niaba yangu”
Mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio kwani tangu nianze kazi yangu ya uwakimu sikuwahi kumchapa mwanafunzi wa aina yoyote na mbaya zaidi mwanafunzi ninaye anza kumchapa ndio kiburudisho cha roho yangu.Rahma akanipa fimbo huku akinikonyeza
“Wewe kijana taka chapa Rahma fimo za nguvu usimlezee kabisa”
 
Mama Rahma alizungumza na kuzidi kuigopesha.Nikimtazama Rahma usoni ananiambia nimchape kidogo kidogo kwa sauti ya chini sana ambayo haikuwa rahisi kwa wengine kutusikia huku sura yake ikiwa imejaa huzuni,nikimuangalia mama Rahma ninamuona jinsi alivyo na shauku ya kuona mwanae ninamchapa
“Wee weka mkono vizuri ukikwepesha ninafuta ninaanza upya”
Nilizungumza kwa kujikaza huku Rahma akionekana kuwa muoga wa kuchapwa.Akanyoosha mkono wake,Nikashusha fimbo ya kwanza kwa nguvu kwenye kiganja chake na ku fanya Rahma kutoa kelele ya maumivu na kuanza kulia
“Weka weka vizuri mkono wako”
 
Rahma akauweka huku akinitazama kwa jicho la hasira,Nikashusha fimbo ya pili ikiwa na jazo wa nguvu kama fimbo ya kwanaza.Rahma akavivikicha viganja vyake kisha akaweka tena huku akionekana kununa na sura yake kubadilika na kujawa na hasira.

Fimbo ya tatu ikatua katika kiganjani  Rahma hakuosogeza kiganja chake,Fimbo ya nne na ya tano zote zikamwingia katika kiganja chake huku zikiwa na ujazo sawa.Akaushusha mkono wake akaniangalia kwa sekude kadhaa huku akinipandasha na kunishusha pasipo waalimu wala mama yake kuona kwani aliwapa mgongo kisha akaondoka  sehemu yangu na kurudi alipokuwa amesimama mwanzoni
 
“Nenda zako darasani”
Mwalimu wa zamu alimrihusu Rahma akaondoka na kuniacha nikiwa ninajiuliza sijui nitatumia mbinu gani kumtuliza Rahma kwani tayari nimesha jichafulia C.V.Mama Rahma akasimama na kuja nilipokuwa nimekaa na kunifanaya nistuke kidogo
“Malimu wewe onekana upo serious na kazi yako.Omba wewe fwatii nyendo zote za huyu binti na ngoja patie wewe namba yangu ya simu.Chochote mbaya anafanya julisha mimi ”
“Sawa”
 
Mama Rahma akanipa namba yake ya simu kisha akatuaga na kuondoka zake laity kama angejua ameniachia msala wala asingenipa hata hiyo nambay yake ya simu.Nikabeba vitabu vyangu na kuelekea darasani kwa kina Rahma ambapo kipondi cha somo langi la Biology ndia cha kwanza.Nikamkuta Rahma ameegemeza kichwa kwenye meza huku rafiki yake akimbembeleza.Wanafunzi wote wakasimama kunisalimia ila Rahma hakusimama zaidi ya kubaki kama nilivyo mkuta.Nikafundisha nilichopamga kukifundisha katika siku hiyo kisha nikatoka darasani huku nikumuavha Rahma akiwa katika hali yakeKabla sijafika mbali kutoka darasa la kina Rahma mwanafunzi ambaye alikuwa anambembeleza Rahma aliniita na kuja hadi nilipo simama
 
“Sir kuna mzigo wako nimepewa na Rahma nikupatie”
Akanipa kikaratasi pasipo mtu yoyote kuona.Nikaondoka na kwenda ofisini nikaweka vitabu vyangu kisha nikaelekea chooni ili niweze kukisoma kikaratasi hivyo kwa shauku.Nikafunga malango wa chooni nikakitoa kikaratasi nilicho pewa na kuanza kukisoma
 
{EDDY…..EDDY……EDDY
Nimekuita jina lako kama lilivyo ili ujue nimekasirishwa na use**e ulionifanya.Wewe si mtu wa kuninyanyulia mkono wako na kunipiga mimi kisa umemuona mama yangu na ukajaa siifa hadi hilo bichwa lako likakaribia kupasuka.Tambua nimekuokoa katika mengi nilikuwa sishindwi kuwaeleza wazazi wangu kuwa wewe ndio unaye nit***a na ndio hapo ungejua kuwa baba yangu ni mtu wa aina gani.Umeona haitoshi ukanichapa mafimbo yako hadi hapa kiganja kilipo kimevimba.SASA WEWE SI UMEIANZISHA VITA BASI UMEIPATA NITAKUFANYIA KITU KIBAYA AMBACHO HUTOKUJA KUNISAHAU KATIKA MAISHA YAKO WEWE JANA SI ULINAIMBIA MDOGO WAKO ALIBAKWA NA KUFA MBELE YAKO SASA NA MIMI NITAHAKIKISHA NINATUMIA KIASI CHOCHOTE CHA PESA ILI NA WEWE UBAKWE MBELE YA MACHO YANGU NA WANAUME WEZAKO NA MIMI HIYO NDIO ITAKUWA MALIPO YANGU
 
BY:ONE ARMY LADY(msichna wa jeshi moja)}
Hadi ninamaliza kusoma kikaratasi nikajikuta mwili mzima ukimwagikwa na jasho huku mikono ikinitetemeka kama nimepigwa na shoti ya umeme.Sikujua hata nifanyenye niaanza kumlamu mwalimu wa zamu ni kwanini hakumalizana na Rahma yeye mwenye.Nikarudi ofisini kila story iliyokuwa ikipigwa ndani ya ofisi hiyo na waalimu wengine wala sikuzielewa kabisa na nikajikuta msongamano wa mawazo ukinipelekesha puta
 
“Sir Eddy una tatizo gani?”
Madam Zena aliniuliza na kuwafanya waalimu wote kuniangalia wakisubiria jibu langu
“Ahhaa kichwa kina nisumbua kidogo nahisi ni homa”
“Fanya ukapime kwani mbu wa Tanga hawana masihara kabisa katika kunyonya damu”
“Sawa”
 “Madam nimekuelewa”
“Eddy au timu yako jana imefungwa ndio umekosa raha”
Mwalimu mwengine alinitania na kuwafanya wengine wacheke
“Wee Sir Sm hembu muache mwenzako si unaona anaumwa….Mwaya Eddy ukizidiwa sema nikupeleke kwako”
Kauli ya mwalimu Zena ikawafanya waalimu wengine kugua na kuanza kucheka na wakaendelea kutaniana.Nikapata wazo la kwenda darasani kwa kina Rahma kwani muda wa mapumziko bado haujafikia.Nikamuomba mwalimu niliye mkuta akifundisha aniitie Rahma.Jibu alili nipa likazidi kunichanganya
 
“Rahma aliniomba ruhusa kama dakika 20 zilizopita kwa jinsi anavyo onekana anaumwa sana”
“Asante mwalimu”
Nikarudi ofisini huku mawazo yakizidi kuniandama sikujua hata nifanyanye.Nikakusanya viti vyangu ambavyo ni muhimu nikaviweka kwenye begi langu na kuomba ruhusa kwa mwalimu mku.Madam Zena akaniomba anisindikize kwa kutumia gari yake ndogo.Sikuwa na kipingamizi zaidi ya kumkubalia.Nikamuelekeza hadi tukafika kwangu tukaingia ndani nikamkaribisha kinywaji Madam Zena taratibu akaanza kunywa
 
“Ehee Eddy kwako ni kuzuri mtu akiingia anaweza akasema umeanza kazi miaka mingi kumbe hata mwezi mwenyewe huna”
“Asante…”
“Unaishi na nani?”
“Peke yangu”
“Duu hongera sana ndugu yangu”
Simu yangu ikaingia meseji na namba iliyoleta meseji hito imeandikwa PRIVETE.Taratibu nikaanza kuisoma meseji hiyo
{NIPO NJE NAKUFWATILIA KILA HATUA NA HUYO MALAYA ZENA ULIYE NAYE NDANI KWAKO NITAMUUA UKISHUHUDIA}
Nikatamani ardhi ipasuke nidumbukie.Nikazidi kuchanganyikiwa pale Madam Zena aliponiaga anataka kuondoka ili akawahi kipindi chake cha kufundisha baada ya mapumziko ya saa nne asubuhi
 
  ITAENDELA

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya