Get the latest updates from us for free

mas template
Home » , » AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 21 na 22)

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 21 na 22)

Written By Bigie on Sunday, March 4, 2018 | 4:37:00 PM

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA                      
ILIPOISHIA   

Nikasimamisha gari pembeni ya ukuta wa nyumbani kisha nikashuka kwa haraka na kuanza kukimbilia getini, nikafungua geti na kuingia ndani. Sikuamini macho yangu kuwakuta wale askari ambao niliwaacha muda mchache tu ulio pita. Sasa hivi wote wawili wamelala chini wakiwa wanavuja damu ikionyesha kwamba wameuwawa. Nikiwa katika kushangaa shangaa, mlango wa kuingilia sebleni ukafunguliwa, uso kwa uso nikakutana na Yudia aliye shika begi lake mkononi akionekana yupo kwenye harakati za kutoroka huku nyumbani kwetu
       
ENDELEA
Kwa haraka nikaichoma bastola yangu na kumuelekezea Yudia ambaye amebaki akiwa amesimama na kunikazia macho, akawatazama askari alio waua, kisha akayarudisha macho yangu kwangu. Akalitupa begi lake chini akiashiria kwamba yupo tayari kwa mapambano. Akaanza kunifwata kwa kasi huku akinitazama sikutaka kumpiga risasi lengo langu kubwa ni kumkamata akiwa hai. Alipo nisogelea karibu nikaruka hewani na kumtandika teke la kifua lililo mrudisha nyuma na kumuangusha chini. Nahisi Yudia hakuweza kunifahamu vizuri, alihisi mimi ni mtu wa kawaida kawaida sana lakini sivyo, kwa maana tama yangno nimesha ikweka mbeni na sasa hivi ninacho kijali ni kazi yangu ya kulitumikia taifa langu.
 
Yudia akajizoa joa chini na kunyanyuka, akajidai kukunja ngumi, nikamtazama kwa macho makali yaliyo jaa hasira, akajaribu kurusha ngumi kadhaa ila zote nikazikwepa na kumtandika ngumi ya shingo iliyo myumbisha na kumungusha chini. Kwa haraka akasiamam huku akitingisha kichwa chake akihitaki kujiweka sawa. Akarusha teke kwe mguu wa kulia, kwa kasi ya ajabu nikaupiga mguu wake wa kushotoi hata kabla mguu wake wa kulia haujafika chini. Anguko hili la sasa, likamfanya Judia kutoa kilio cha maumivu makali kwa maana amengukia mbavu zake.
Nikamsogelea kwa ukaribu huku bastola yangu ikiwa mkononi. Nikampapasa na kuitoa bastola yake aliyo ificha kwenye viatu, nikaanza kumburutu na kumuingiza hadi sebleni. Nikamburuza hadi chumbani kwake na kumtupia kitandani. Chumba chake kimechanguliwa changuliwa sana.
“Nahisi safari hii utanijibu kwamba wewe ni nani?”
 
“Fu**……..”
Sikumpa nafasi ya kumalizia tusi lake, nikamtandika kofi zito la shavu hadi akamwagikwa na damu za mdomo.
“Wewe ni nani?”   
Yudia akaka kimya huku akinitumbulia macho, hakujibu chochote. Sikujali kama ni mwanamke au ana uzuri gani, nikamtandika ngumi nzito ya uso, iliyo mfanya apige ukunga mkali sana wa maumivu.
“Wewe ni nani?”
“Niueee tuu”
“Ahaa nikuue?”
“Ndioo”
Yudia alizungumza huku akilia, nikakoki bastola yangu na kuiweka sawa, nikavuta traiga na kuiruhusu risasi kutoka ikatua kwenye paja la Yudia na kumfanya apige ulelele mkali sana.
“Nimekuuliza wewe ni nani?”
Nilizungumza huku jasho likinimwagika uso mzima, sikuhitaji kufanya upuuzi mwingine kwa binti huyo. Damu nyingi zikasambaa kwenye shuka la kitandani, Yudia akanitazama kwa uchungu sana huku dhairi akionyesha kwamba ana hasira kali sana dhidi yangu.
 
“Wewe ni nani?”
“M…..i…i…mi ni……mwan…..an….a…..mgamb….oo wa Alsahab”
Yudia alizungumza huku akilia sana tena kwa uchungu mkali sana.
“Umefwata nini nyumbani kwa mama yangu?”
“N…ii nilitumwa kuja…..a kumpe….lelezaa”
“Nani kakuagiza?”
Hapo Yudia akaka kimya, nikaisogeza bastola yangu karibu kabisa na paji la uso wake huku mwili mzima ukinitetemeka kwa hasira kali sana
“NANI KAKUTUMAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA”
Niliuzungumza kwa kufoka hadi Yudia akayafumba macho yake kwa maana sauyti yangu imetoka ikiwa na mtetemesho mzito wa hasira.
“Meya Meyaaaaa, ndio mzamini wa haya yote”
“Ahaaa lengo lake ni nini?”
 
“Kuu….kuuu muondoa raisi madarakani”
“Raisi madarakani!?”
“Ndio kuna kikundi tayari kipo nchini Tanzania, kipo tayari kujitoa muhanga kesho kutwa raisi akija hapa Tanga”
Hapo sasa ndipo nikaanza kupata picha ya haraka sana, wale watu nilio waona katika jumba lile la kifahari kumbe ndio wana mpango wa kumuua raisi.
“Dany naomba uniue kwa maana nimesha toa siri ya kundi langu ni lazima wataniua kiukatili mimi”
Yudia aliniomba huku akimwagikwa na machozi mengi usoni mwake. Sikutaka kabisa kufanya mauji ndani ya nyumba yetu. Nikampiga Yudia shingoni na kitako cha bastola yangu, kisha nikambeba begani na kutoka naye chumbani kwake. Moja kwa moja tukatoka nje, nikachukua begi lake la nguo na kuondoka eneo hilo. 

KwA umakini wa hai ya juu nikatoka nje kabisa ya geti, baada ya kuchunguza kwamba hakuna watu wanao nifwatilia. Nikasogea hadi gari shemu lilipo nikamuingiza Yudia ndani ya gari pamoja na begi lake, kisha nikazunguka upande wa pili wa dereva nikaingia na kuondoka nyumbani. Akili yangu kwa haraka ikanituma kwa daktari aliye kuja kunitibu leo. Kutokana alisha nielekeza sehemu ilipo hospitali yake moja kwa moja nikaeleka hadi kwenye hospitali yake japo ni usiku ila nimedhamiria kufika katika eneo hilo.
Nimatoa Yudia ndani ya gari na kuuingia naye ndani ya hospitali hiyo, nikakutana na nesi akiwa mapokezi ana sinzia sinzia. 
 
“Nimemkuta daktari?”
Sauti yangu ikamstua nesi huyo aliye jikuta akikurupuka na kunitazama. Akamtaza Yudia niliye mbeba begani.
“Yupo wapi daktari”   
Nilimuuliza kwa ukakali, pasipo kunijibu chochote kwa ishara akanionyesha eneo la kuingia ambapo ndipo kwa daktari. Nikaelekea katika chumba hicho cha dkatari, pasipo kubisha hodi nikaufungua mlango huo na kumkuta dokta aliye kuja kunitibu nyumbani akiwa amekaa kwenye kiti huku mbele yake kukiwa na meza kubwa. Alipo niona akavua miwani yake na kunyanyuka na kunisogele.
“Muweke hapo kwenye kitanda”   
Alizungumza huku akinionyesha kitanda ambacho kipo hapo kwenye ofisi yake huku kikiwa kimezungushiwa shuka kubwa la kijani. Nikamlaza Yudia chali na kumuweka vizuri.
 
“Amefanyaje huyu binti”   
“Tumevamiwa na majambazi nyumbani, amejeruhiwa”
“Mungu wangu, dokta huyo akaanza kumpima pima Yudia kwa kiganja cha mkono wake wa kulia maeneo ya shingo.
“Nahitaji uweze kumuhudumia hadi apone na iwe siri, kwa maana kuna watu wanaitafuta familia yetu na kuiangamiza”
“Kina nani hapo?”
“Hilo halikuhusu wewe fanya kazi yako, hakikisha hadi asubuhi anakuwa salama, nitakuja kumuona sawa?”
“Sawa, ila anaonekana kwamba ametikwa na damu nyingi, na hapa kwetu damu umetuishia”
Likawa ni jambo jengine jipya kulisikia.
“Kwa hiyo mimi nifanyaje?”
“Tunaweza kuipima damu yako na yake kama zitaendana basi unaweza kumchangia damu”
Nikafikiaria kwa dakika kama mbili huku nikimtazama Yudia aliye lala kitandani hatambui ni nini kinacho endelea.
 
“Kutoa damu itachukua muda gani?”
“Sio muda mwingi, kama dakika kumi hivi”
Nikakubali madaktari waweze kunifanyia vipimo vya kuipima damu yangu, cha kushukuru Mungu damu yangu ipo salama na inaweza kumchangia Yudia kwa maana kuni la damu yani ni O PLUS.
Nilipo maliza kutolewa damu chupa moja, daktari aka niruhusu kuondoka, nikatoa simu yangu huku nikiingia kwenye gari. Nikampiga RPC ambaye nina imani kwamba amesha patiwa taarifa na K2 juu ya watu ambao wanataka kufanya mashambulizi dhidi ya raisi.
“Halooo”
Sauti ya uchovu iliyo jaa usinhizi ilisikika upande wa pili wa simu yangu.
“Unazungumza na Dany agnet wa NSS 008. Kuna habari uliweza kupatiwa na mkuu wangu nauliza kama mumesha zitekeleza”
 
“Ahaaa, haizo habari ni uongo kabisa, nimetuma vijana hao kwenye eneo hilo wamekuta hakuna kitu”
“Mkuu unasema hakuna kitu wakati hadi ushahidi wa picha upo?”
“Nimekuambia hivii hakuna kitu, kama munaweza fwatilieni wenyewe, sisi kazi yetu ni kulinda raia na mali zao na si kumlinda raisi wala taifa”
Simu ikakatwa nikabaki nimeikodolea macho, maneno ya mkuu huyo wa polisi yakanichosha kabisa. Nikawasha gari na kuondoka katika eneo hilo huku safari hii nikiwa ninaelelkea kwenye eneo nilipo ona kikundi cha magaidi hao ambao hata Yudia mwenyewe amadhibitisha kwamba wapo kwa ajili ya kujiyoa mihanga.
 
Nikiwa njiani, nikajaribu kumpigia K2 simu yake, ikaita na kukata pasipo kupokelewa, nikajaribu zaidi ya mara tano ila haikupokelwa. Nikampigia Joseph, ambaye naye simu yake sikuipata hewani japo nikarudia mara kadhaa nikishisi kwamba ni mtatandao una sumbua. Nikafika maeneo ya karibu ya sehemu ya jengo hilo, nikazima simu yangu, bastola ya Yudia na yangu nikazitoa magazine na kukuta zikiwa na risasi za kutosha. Nikashuka kwenye gari na kaunza kutembea kwa umakini sana kuelekea kwenye jumba hilo. Uzuri kuna giza nene, na nguo nyeusi nilizo zivaa sio rahisi kabisa kwa mtu kuweza kuniona. 
 
Nilipo fika karibu na ukuta wa jumbah hilo, nikavuta kasi na kukimbia, nikauoaramia ukuta huo kwa kasi hadi juu. Nikachungulia ndani na sikuona chochote kilichopo kwenye eneo hilo. Taratibu nikashuka kwa ndani huku nikichuchumaa. Nikatazama kila kona ya jumba hilo, ukimya mwingi umetawala.
Nikatoa bastola yangu na kuiweka vizuri, taratibu nikaanza kunyata kuelekea kwenye moja ya dirisha linalo waka taa kwa ndani. Nikachungulia na kuona vijana wawili wa kiume wenye umri kati ya miaka kumi na mbili hadi kumi na tano, wakiunda mabomu juu ya meza kubwa iliyomo chumbani humo.
‘Jesus christ’(Yesu wangu)
Nilijikuta nikisema kimoyo moyo kwa maana mabomu hayo wanayo yatengeneza watoto hayo ni mabomu ambayo mtu anaweza kujifunga mwilini mwake pasipo mtu yoyote kuweza kujau. 

Watoto hao wenye asili ya kiafrika, waliendelea kufanya kazi hiyo wakiwa kimya, nikajaribu kutazama vizuri pembeni ya chumba hicho nikaona jamaa wawili walio valia vilemba wenye asili ya Kisomali, wakiwa wamesimama huku mikononi mwao wameshika bunduki aina ya AK47, wakiwa wamewalekezea watoto hao wanao onekana kufanya kazi chini ya ulinzi mkali wa watu hao. 

Nikiwa hapo nikasikia honi kwenye geti, ikanibidi nijifiche kwenye moja ya mti mkubwa ulipo ndani humu, kijana mmoja kwenye bunduki akakimbilia getini, sikujua ametokea wapi, akachungulia kwenye geti hilo kupitia kijishimo kidogo kilichopo hapo getini, kisha kwa haraka akafungua geti hilo lenye pande mbili. Gari ambayo ina namba za usajili za mkuu wa mkoa nikaliona likingia hapo. Akashuka mwanaume mmoja aliye valia suti huku akiwa na dereva wake.
 
“Meya yupo?”
“Ndio mkuu”
“Nipeleke”
 Kijanahuyo akatangulia mbele huku, mzee huyo akafwatia nyuma huku dereva wake naye akiwa anafwatia kwa nyuma. Kwa umakini mkubwa nikaanza kuwafwatilia ni wapi wanapo elekea. Wakapandisha katika ngazi zilizopo kwa nje, wakaingia kwenye moja ya mlango uliopo gorofani. Nikatazama pande zote za eneo hilo sikuona mtu na mimi kwa umakini wa hali ya juu nikaanza kupandisha kwenye ngazi hizo hadi nikafika mlangoni. Nikiwa mlangoni nikasikia sauti ya watu wakizungumza, ikanibidi kutega sikio lango katika mlango huko kusikiliza mazungumzo ya humo ndani.
“Mkuu mbona umechelewa?”
Sauti hiyo si ngeni kabisa kwangu ni sauti ya meya, kwa ujuzi wangu wa haraka haraka nikatambua kwamba wapo kwenye kikaa.
“Kidogo ziara ya muheshimiwa inafanya watu tuwe bize bize”
“Sawa mkuu karibu kikao ndio kilikuwa kinakusubiria wewe”
 
“Musijali”
Taratibu nikaitoa simu yangu mfukoni na kuiwasha taratibu huku nikiitoa mlio wa simu. Nikaweka sehemu ya kurekodia na kunaza kuyarekodi mazungumzo hayo yote.
“Raisi atakuja kwa njai ya barabara na si ndege kama tulivyo dhania. Ataingia hapa jijini Tanga majira ya saa nne asubihi na moja kwa moja ataelekea katika hospitali ya Bombo kuona wagonjwa, japo hiyo haikuwepo katika ratib yake. Akitoka hapo atatembelea masoko sasa haijawekwa bayana ni soko gani ambalo anaweza kulitembelea.”
“Tageti yetu kubwa ni mkutano wa adhara atakao ufanya hapo uwanja wa Mkwakwani, tuhakikishe kwamba wadunguaji wanakaa maeneo ya mbali na uwanja na waweze kumupiga risasi”
 
“Sawa mkuu tumekuelewa katika hilo, ila kuna jengine limejitokeza?”
“Lipi tena?”
“Hadi sasa hivi hatujafanikiwa kumuua mkurugenzi wa jiji na inavyo onekana kuna mtu ana msaidia, japo hadi sasa hivi hatujajua ni nani?”
“Sasa huo ni ujinga munao ufanya, mwana mama yule mzembe mzembe inakuwaje ana wasinda kirahisi hivyo?”
“Tusamehe mkuu kwa maana hatukujau haya yote”
“Na yule binti ambaye mumempandikiza nyumbani kwake yupo wapi?”
Nikasikia ukimya ukiwa umetwala, nikazidi kuwa makini kusikilizia kama kutakuwa na hatua zozote zitasikika zikiusogelea mlango ila haikuwa hivyo.
“Mbona hamunijibu?”
“Mkuu hadi sasa hivi hatufahamu ni wapi alipo”
“Shiti…..hii sasa ni hatari hakikisheni kwamba munampata tena sasa hivi sawa”
 
Nilipo sikia hivyo, sikutaka kuendelea kukaa kwenye ngazi hizo, nikashuka kwa haraka na kurudi shemeu nilipo ingilia kwenye ukuta, nikapata na kutokea upande wa nje nilihofia kupita getini ninaweza kuonekana kwa maana kuna taa zenye mwanga mkali. Nikakimbilia kwenye gari langu sehemu nilipo liacha, nikaingia ndani na kujifungia huku macho yangu yote yakiwa ninatizama kwneye geti la jumba hilo. Nikaona gari nyeusi aina ya Toyota Harriera ikitoka ikaelekea upande wa pili wa barabara huku ikiwa katika mwendo wa kasi sana. Nikayasikiliza mazungumzo yote niliyo yanyaka kupitia simu yangu nikaona yameingia vizuri sana. 
 
    Nikawasha gari na kuondoka eneo hili kwa kasi huku moyoni nikiwa nina furaha ya kuweza kujua mipgango ya hatari nani watu gani ambao wanamchukia raisi kwa maana amekuwa ni raisi asiye ogopa viongozi wezake, ana waadabisha wale wazembe wote wanao tumia nchi na maliasili zake kuwakandamiza wali wengi na wenye maisha ya chini. Nikafika hospitalini nilipo muacha Yudia, kwa ajili ya kuimarisha ulinzi wa Yudia. Mapokezi sikumkuta nesi niliye mkuta, haikunitisha sana kwa sababu nina amini kwamba nesi huyo anafanya kazi na daktari wake.

 Saa ya simu yangu inaonyesha saa kumi na moja na nusu asubuhi. Nikafungua mlango wa chumba cha daktari kimya kimya, kwenye kiti cha daktari huyo kipo kitupu, ila nilipo tazama kwenye pazia lilizo ziba kitanda hicho nikasikia miguno miguno. Kwa utaratibu nikanyata hadi kwenye pazia hilo, taratibu nikalifungua huku bastola yangu ikiwa mkononi mwangu. Sikuamini macho yangu, baada ya kumkuta nesi, daktari na Yudia aliye lala kitandani akiwa hajitambui wakiwa uchi kabisa. Daktari akimtomb** nesi wake, huku nesi wake akinyonya kitumbua cha Yudia, huku wawili hao wakionekana kuwa na furaha sana kwa kitendo hicho
 
  AISIIIII……….U KILL ME 22

“Hii ndio kazi niliyo kupa”
Nilizungumza kwa sauti nzito na kumfanya dokta na mzee wake kustuka na kuachiana pale walipo niona ni mimi. Wote wakanikodolea macho huku wakionekana kushangazwa sana uwepo wangu. Miili yao dhairi nikaiona jinsi inavyo tetemeka kwa woga.    
Daktari akayashusha macho yake hadi kwenye kiganja changu cha mkono wa kulia nilipo ishika bastola yangu, hapo ndipo woga ulipo mzidi hadi akajikuta akipiga magoti chini akiwa hivyo hivyo ajavaa kitu chochote mwilini mwake.
“Ohooo tusameee sieeeee”
Daktari alizungumza huku machozi yakimwagika na uzee wake sikutegemea kabisa kwamba anaweza kufanya vitu vya kijinga vya namna hii. Nikamtazama Yudia aliye lala kitandani nikatambua dhairi kwamba hajui kitu kinacho endelea. Nesi huyo akaanza kumwagikwa na haja ndogo pale nilipo ishika vizuri bastola yangu. 
 
“Tusameee sieee ni shetani tu alitupitia”
Mzee hyo aliendela kuzungumza. Sikuwa na kitu cha kuzungumza zidi ya kuwakazia macho, kwa ishara nikamuamrisha daktari kusimama. Akasimama kwa kasi huku akwia amejikakamaza kama afande aliye muona mkuu wake.
“Mumemuhudumia mgonjwa wangu?”
“Ndio mkuu, ndio mkuu”
“Vaeni nguo zenu, nakusubiria huku”
Nikatoka ofisini kwake na kukaa kwenye kiti na kumsubiri, hazikupita hata dakika mbili daktari akatoka huku akiwa anamalizia kuufunga mkanda wa suruali yake. Akasimama mbele yangu kwa adabu kubwa sana. Sikuificha bastola yangu kwa kuamini kwamba ndio kitu anacho kiogopo daktari huyo na kwa sasa ninaweza kumuamrisha kitu chochote na anakifwata.
“Huyo mwenzako yupo wapi?”
“Yupo ndani mkuu”
“Muite sasa”
“Wewe toka bwana unafanya nini huko”
Daktari alimkoromea nesi wake huyo ambaye alitoka huku akiwa tayari amesha vaa gauni lake. Nikamtazama kuanzi juu hadi chini.
“Leo nimekuta mimi, ninawasemehe ila kesho anaweza kuwakuta kiongozi wa kiserikali, unahisi hii hospitali yako itakuwa katika mazingira gani?”
 
“Itafungiwa mkuu”
“Nani alitoa wazo la kumshirikisha mgonjwa wangu kwenye upuuzi wenu huo?”
Wote waka kaa kimya, nikaikoki bastola yangu kwa kuwatisha, mlio huo mdogo ukawafanya kuchachawa huku kila mmoja akimnyooshea mwenzake kidole kwa woga.
“Sasa natoa amri, mgonjwa wangu aishi kwa maficho ndani ya hospitali hii hii, sinto hitaji mtu hata mmoja kuweza kufahamu kwamba yupo hapa. Laiti ikitokea mtu akifahamu basi vichwa vnyenu vitaingia risasi za bastola hii”
Nilizungumza huku nikiwa nimesimama, daktari na nesi huyo wakaitikia kwa kutingisha kichwa wakimaanisha kwamba wameelewana na kile nilicho kizungumza.
“Chakula vinjwaji vyote vitakuwa juu yenu, sasa ole wenu mgonjwa wangu apate tatizo, kifo kitabaki pale pale sawa”
“Sawa sawa”
Daktari akazungumza huku akinitumbulia macho. Nikawatazama kwa macho ya kuwatisha kila mmoja akajifumbata kama kifaranga kilicho nyeshewa na mvua.
“Asubuhi njema”
 
Nikatoka ofisini na kuelekea nje lilipo gari langu, nikaingia na kueleka hadi kwenye hoteli ya Panori nikalipia chumba kimoja, muhudumu akanipatia ufunguo na nikaeleka katika chumba hicho. Baada ya mlango wa kuingilia ndani ya chumba hichi, nikakichunguza kwa haraka ili kuweza kutambua kwamba kinausalama, nikakikuta kina usalama wa kutosha.
Nikafunga mlango wangu kwa ndani kwa kutumia funguo niliyo pewa na muhudum na kutoa bastola yangu nikaiweka mezani, kisha ni nikatoa simu yanu na kumpigia Joseph. Simu ya Joseph ikaita kwa muda na kukata. Kutokana nina kaharufu ka damu za Yudia zilizo nimwagikia na kukaukia kwneye tisheti yangu, nikavua nguo zangu na kuibeba tisheti yangu na kuingia nayo bafuni. Nikaanza kuoga huku mawazo mengi yakitawala kichwa changu nikijaribu kujiuliza ni kitu gani ambacho ninaweza kukifanya kwa wakati huu. Sikuwa na jibu lolote lililo tokea kichwani mwangu. Nilipo maliza kuooga, nikaifua tisheti yangu, nilipo ridhika na kufua kwangu nikaianika bafuni humu humu juu ya bomba la mvua.
 
    Nikatoka bafuni huku nikiwa kama nilivyo zaliwa, nikachukua taulo na kuanza kufuta maji sehemu mbali mbali za mwili wangu huku kwenye kidonda changu nikiwa makini sana kuhakikisha sikitoneshi, kwa mana bado kina maumivu kwa mbali. Nikajifunga taulo hilo na kukaa kitandani, nikaichukua simu yangu juu ya meza na kurudia tena kuipiga namba ya Joseph, ikaita pasipo kupokelwa.
 
“Halooo Dany”
Nikasikia sauti nyuma yangu, kwa haraka nikakurupuka na kuiwahi bastola yangu mezani, na kutazama ni nani anaye niita. Nikakutaana na dada mwenye asili ya kiarabu, aliye valia gauni refu jeupa, huku nywele zake akiwa ameziweka katika mtindo ambao unamfanya apendeze sana.
“Wewe ni nani na umeingiaje humu chumbani kwangu ikiwa nimeufunga mlango wangu?”
Niliuliza huku nikiwa nimemnyoosha bastola, dada huyo aliye simama kwenye kona ya chumba hichi, hakuonyesha kuogopa wala kushangaa bastola yangu niliyo msikia. Ndio kwanza akaachia tabasamu pana na kicheko cha kejeli kidogo. Akanipandisha na kunishusha na kuanza kupiga hatua kukifwata kitanda.
 
“Simama hapo hapo, nitakuchangua ubongo, jibu swali langu kabla hali ya hewa haijachafuka humu ndani”
“Sawali, kwani kuna swali umeniuliza”
Alizungumza huku akikaa kitandani, mapasuo wa gauni lake hilo, likaonyesha paja lake lililo pana na lililo nona kwa unene wake.
“Usiniletee dharau za kijinga umelisikia swali langu, wewe ni nani?”
“Ohooo unataka kunifahamu mimi ni nani?”
“Ndio”
“Mmmm…..Ngoja nianze kujitambulisha jina langu, ninaitwa OLVIA. OLIVIA HITLER”
“Olvia Hitler?”
Niliuliza kwa mshangao mkubwa sana kwa maana jina hilo sio mara yangu ya kwanza kuweza kulisikia, na kipindi nilipo kuwa mdogo marehemu baba aliweza kutuadisia mimi na mama kwamba rafiki yake ambaye nina mumita baba mkubwa Eddy, anasumbuliwa na jini linalo itwa Olvia Hitler.
 
“Naamini jina langu sio geni sana kichwani mwako?”
“Ndio sio geni, unataka nini?”
“Nimekuwa nikikulinda tangu ulipo toka nyumbani kwa Eddy, hadi unafika hapa hotelini, nikaona sio mbaya nikakupa salamu japo ujue kila unalo kifanya basi kuna kiumnbe kina kulinda”
Japo nimeshika bastola yangu ila mikono, miguu vyote vina nitetemeka. Ujanja wangu wote umeniishia ujasiri wote umekwisha. Simu yangu ikaita na sote tukabaki tukiwa tunaitazama simu hiyo.
“Poke ni Joseph anapiga, anataka kukuuliza ni kitu gani unacho hitaji.”
Sehemu ambayo simu ipo ni vigumu sisi sote kuweza kufahamu ni nani anaye piga ila yeye amefahamu mtu anaye piga.
“Kabla ya kupokea, muombe namba ya raisi”
“Namba ya raisi?”
“Ndio kisha nitakuambia nini cha kufanya”
Taratibu nikaisogelea simu yangu ilipo, huku bastola yangu nikiwa bado nimemuelekezea Olvia Hitler. Nikaichukua taratibu na kuitazama, nikakuta ni Joseph ndio anaye piga, nikaipokea na kuiweka sikioni.
“Dany vipi?”
“Safi za asubuhi?”
“Safi kaka, samahani sikuweza kuisikia simu yako, nilikuwa nimelala”
 
“Usijali kwa hilo. Nina shida moja naomba unisaidie”
“Shida gani kaka?”
“Ninaiomba namba ya simu ya raisi”
“Namba ya raisi kuna nini huko?”
“Wewe naomba nitakufahamisha ndugu yangu”
“Sawa, ila nakuomba usinitaje kwamba mimi ndio nimekupatia”
“Sawa ndugu”
Joseph akakata simu na mimi nikabaki nikiishusha taratibu huku nikimtazama Olvia Hitler.
“Utaendelea kunishikia bastola yako hadi saa ngapi?”
“Hilo halikuuhusu”
“Ohoo, ok tuangalie kama halinihusu”
Kufumba na kufumbua nikajikuta bastola yangu ikinipokonya na Olvia akawa ameishika akiwa kitandani, sikujua ametumia njia gani kuweza kunipokonya bastola yangu.
“Hapo je inanihusu au hainiusu?”
Sikuwa na jibu la kuzungumza, nikiwa bado katika kushangaa shangaa simu yangu ikaingia meseji, nikaifungua na kukuta namba ya raisi niiyo tumia.
“Amesha kutumia, sasa mpigie raisi na umuambie mipango yote inayo endesha na meya pamoja na mkuu wa mkoa. Muambia raisi kwamba aweze kufunga safari leo na aje kupitia boti kwenye bahari na wewe ndio ukawe mtu wa kumpokea”
“Hivi unahisi atanielewa kweli na kuniamini?”
“Ndio nitamfanya akuelewe”
Nikamtazama Olvia Hitler huku nikipiga namba ya raisi na kuiweka sikioni. Simu ikaanza kuita taratibu, hazikupita sekunde nyingi simu ikapokelewa.
 
“Halooo”
Niliisikia sauti ya raisi hapo ndipo nikaamini na kitambua kwamba ni raisi mwenyewe anaye zungumza kwa muda huu.
“Shikamoo muheshimiwa raisi. Unazungumza na Daniel agnent wa NSS 008”
“Marahaba nikusaidie nini kijana?”
“Kuna taarifa ambazo ninapenda kuzifikisha kwako moja kwa moja pasipo kupitia kwa wakuu wangu. Hizi taarifa ni kuhusiana na usalama wa safari nzima ya hapo kesho kuja jijini Tanga”
“Ndio nakusikiliza”
“Kuna mpango wa siri wa viongozi wakuu, walio panga kukuua katika dhiara yako uliyo panga kuja Tanga, nimeweza kuwata taariafa viongozi wangu wa ngazi za juu ila sijaona kitu chochote kilicho weza kuchukuliwa hatua zaidi ya kuwaona viongozi hao wakijaribu kuungana na hao walio panga kukuangamiza”
“Kijana unayo yazungumza yana ushahidi?”
“Ndio muheshimiwa, ninaweza kukutumia kupitia nji ya whatsapp sasa hivi”
 
“Sawa nipigie niupitie kisha nitakupigia”
“Sawa muheshimiwa”
Nikakata simuu na kuanza kutuma picha na sauti niliyo irekodi kwenye simu ya raisi. Ndani ya dakika vitu vyote vikapigiwa tiki la rangi ya bluu ikiashiria kwamba vimepokelewa.
“Umepa nyaraka za mama yako?”
Olvia Hitler aliniuliza huku akinitumbulia macho.
“Sijazipata”
“Unategemea nini wakati raisi wako anakuja kesho?”
“Sijajua ni wapi ya kuzipata”
Olvia HIteler akanyamaza kimya akionekana kufikiria kitu. Akanyanyua kichwa chake na kunitazama kisha akaanza kuzungumza.
“Nyaraka hizo zimefichwa ofisini kwa meya, kwenye meza yake anyo kalia kwenye faili la chini kabisa hapo ndipo zilipo”
“Sasa nitaweza kuzipata vipi?”
“Wewe ni mpelelezi hapo tena unaniuliza utazipata vipi, nisha kupa njia ya kuweza kuzipata kabla ya kufanya mengine nenda kazichukue sawa”
“Sawa”
Simu yangu ikaita nilipo itazama kwenye kioo chake nikakuta ni raisi ndio anaye nipigia. Nikaipokea na kuiweka sikioni mwangu.
 
“Asante sana kijana, sa…..sasa hapa umepanga nini au nisije kabisa Tanga?”
Raisi alizungumza kwa kubabaika sana, kitendo kilicho nishangaza hata mimi mwneywe.
“Hapana dhiara yoko iwe pale pele muheshimiwa, ila ninacho kuomba uweze kuondoka Dar es Salaamu kupitia botii usiku wa leo. Ondoka na walinzi wako unao waamini ukisha fika Tanga mimi ndio ninakaye kupokea katika ufukwe wa Mwambani”
“Sawa sawa kijana nitafanya hivyo na msafara wangu wa kesho je?”
“Awepo raisi feki ambaye anaweza hata kuvalishwa sura ya bandia”
“Basi nitafanya hivyo kijana asante sana na Mungu akubariki”
“Asante muheshimiwa”
Simu ikakatwa, Olvia Hitler akaachia tabasamu pana kisha akanyanyuka kitandani na kunisokela sehemu nilipo simama, akalifungua taulo langu na kunishika jogoo wangu na kumninya taratibu, kitu kilicho ufanya mwili wangu mzima kusisimka kupita hata nilivyo wahi kushikwa na mwanamke yoyote kwenye maisha yangu.
 
ITAENDELEA

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya