Get the latest updates from us for free

mas template
Home » , » SORRY MADAM -Sehemu ya 33 & 34 (Destination of my enemies)

SORRY MADAM -Sehemu ya 33 & 34 (Destination of my enemies)

Written By Bigie on Tuesday, February 21, 2017 | 12:22:00 PM

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWAILIPOISHIA
Kitendo hicho kikiwa kinaendelea Shamsa aliweza kushuhudia damu ikimtoka mtu ambaye anaamini amekuja kuwasaidia na kuwaokoa.Bila ya uwoga na wala pasipo kuhofia maisha yake, Shamsa akasimama wima na kuanza kupiga hatua za kwenda walipo simama watu hao walio muweka kati mtu aliye valia mavazi meusi tupu.
 
Eddy akabaki akiwa katika mshangao mkubwa, baada ya kumuona Shamsa akikaribia katika eneo hilo ambalo ni hatari kwa maisha yake. Eddy akajaribu kutingisha kichwa chake kumzuia Shamsa asiweze kusogelea eneo hilo, ila ndio kwanza Shamsa akaongeza mwendo wa kuwasogelea akiwa amejiandaa tayari kwa kupigania watu wote waliomo ndani ya jengo hilo.

ENDELEA
“Am sorry dady”(Samahani baba)
Shamsa alizungumza huku akiruka hewani na kushusha teke zito kwa Lukuman akitambua kwamba ni baba yake. Eddy akataka kuzungumza kitu ila akastukia akipigwa mtama na Briton, ulio mpeleka chini, hakutaka kupoteza hata sekunde moja kwa kofia lake kuweza kuanguka alicho kifanya ni kuliweka sawa na kunyanyuka huku akichechemea.
“Baba kwa nini umeamua kufanya hivi?”
 
Shamsa alizungumza huku machozi yakimwagika usoni, Lukuman akabaki akiwa ameshangaa kwa kuitwa baba, ili kupotezea akarusha ngumi nzito kifuani mwa Shamsa, na kumfanya binti huyo kuto ukelele wa maumivu huku akianguka chini na kujikunja. Briton na Eddy wakajikuta wote wakimtazama Shamsa anaye garagara chini kwa maumivu makali. Kumbukumbu na sura ya Shamsa vikaanza kumjia Briton, akaanza kufikiria ni wapi alipo isikia sauti hiyo ya maumivu ya msichana huyo mwenye asili ya kiasia.

Kumbukumbu zake zikatua kipindi ambacho, walikuwa ni miongoni mwa mateka walio weza kuingizwa katika kambi ya kundi la Al-Shababu, akiwa ni kijana mdogo mwenye umri wa miaka kumi na tano. Miongoni mwa mateka ambao waliokuwa kipindi hicho, Shamsa ni mmoja wapo kipindi hicho Shamsa alikuwa bado binti mdogo.
 
Anakumbuka siku moja wakiwa katika mazoezi ya lazima, Shamsa alipewa kijana mwengine ambaye walimkuta ndani ya kambi hiyo, apambane naye, kutokana Shamsa hakuwa mzoefu na alikuwa ni binti mdogo na mpole sana, kijana huyo pasipo huruma aliweza kumbutua vya kutosha Shamsa, na kitu ambacho anakikumbuka zaidi, ni pale kijana huyo alipo mpiga Shamsa ngumi ya kifuani na binti huyo akaanguka hivyo hivyo kama alivyo anguka sasa hivi. 

Britona akakumbuka alipo jitoa katikati ya vijana wezake walio zunguka duara hilo wakiwatazama Shamsa na kijana mwengine jinsi walivyo kuwa wakipigna. Akamvaa kijana huyo na kumshindilia ngumi za hasira hadi kijana huyo akapoteza maisha yake.
 
‘Naitwa Shamsa’
Sauti hiyo ilipita masikioni mwa Briton na kukumbuka siku alipo muuliza jina bintyi huyo na kutokea kumpenda, kupita maelezo. Briton akastushwa na buti zito la Lukuman lililo tua tumboni mwa Shamsa, dadi akanyanyuka kidogo juu na kutua chini puu.
 
“Ahagraaaaaaaaaa”
Briton akamuacha Eddy na kwenda kumvaa Lukuman, na kumuangusha chini kama mzoga, hadi Eddy akabaki akishangaa. Briton akaanza kumshindilia mangumi ya uso Lukuman, kila alivyo zidi kumshindilia mangumi mazito hayo ndivyo alivyo kuwa akikumbuka tukio la Lukuman kumpiga msichana ambaye alizama ndani ya moyo wake na kuahidi atamtunza ndani ya moyo wake hadi siku ambayo atakuja kumuona. Eddy kwa haraka akapiga goti moja chini na kumnyanyua Shamsa aliye poteza fahamu.
 
“WOTE TOKENI NJEEEEEE”
Ikawa kama fungulia mbwa, kila mmoja aliye jiweza alijitahdi kutoka nje akikimbia, hapakuwa na mtu aliye hitaji kujihusisha na ugovi wa watekaji hao wawili, kila mtu alijitahidi kuizingatia roho yake kwanza mambo mengine yatafwata baadaye. Eddy akamuweka Shamsa kwenye moja ya meza, baada ya kugundua yupo hai, kisha yeye akandoka akihofia askari walio anza kuingia ndani ya jengo hilo kuweza kumkuta na kumtambua.
 
Ndani ya dakika moja Brina na watui wake wote wawili, walijikuta wakiwa wamelala chini, kila mmoja akishika eneo la mwili wake lililo tole pande la nyama, kwa kucha kali ambazo Samson alizitumia katika kuwadhuru waasi hao.

 Mmoja wao koromeo lake liliweza kutolewa nje, na yupo katika hatua za mwisho mwisho za kuiaga dunia huku mikono yake miwili ikiwa imeshika sehemu koromeo lake lilipo chomolewa, ili damu isitoke.
 
Mwengine alitobolewa tumboni na utombo wake wote ukavutwa nje pasipo huruma. Brian miguu yake yote miwili, ilivunjwa vunjwa vipingili pingili zaidi ya kumi kwa kila mguu, na kuacha akiendelea kulia kwa maumivu makali. 

Samson alipo hakikisha kazi yake imekamilika akatoka ndani ya chumba hicho na kuwaachia woga mwingi mafundi mitambo, kila mmoja akiwa haamini kama amepota, na hapakuwa na aliye weza kutoka katika sehemu aliyo jificha hadi walipo sikia sauti za polisi,walio jitambulisha mara baada ya kuingia ndani ya chumba hicho.
 
“Upo salama?”
Samson alimuuliza Eddy mara baada ya kumkuta akiwa amesimama juu ya paa akiwatazama jinsi wananchi wanavyo pokelewa na ndugu zao walio weka kambi katika eneo hilo kuhakikisha kwamba wanawaona ndugu zao. 

Japo si desturi ya watu wengi kukumbatiana ila kila aliye muona ndugu yake alijikuta akimkumbatia kwa furaha, wengine wakiendelea kuita majina ya ndugu zao wakizidi kuwatafuta katikati ya mamia ya watu walio weza kutoka ndani ya jengo hilo. Wachache kati ya waliopo nje ya jengo, walijikuta wakiingiwa na wasiwasi mwingi na wengine wakiangua vilio baada ya kupata taarifa au kuona miili ya ndugu zao walio fariki.
 
“Ndio japo si sana”
Eddy alizungumza kwa ufupi huku akiendelea kutazama huku na huku, akabahatika kuweza kumuona Shamsa akiwa amebebwa kwenye machela na kuingizwa ndani ya gari ya wagonjwa, hapo roho yake ikaweza kutulia
“Tuondoke zetu muheshimiwa”
“Usiniite muheshiwa niite……..”
“BLACK SHADOW”
 
 ***
“I.T.V:WANANCHI WALIO TEKWA WAMEACHIWA USIKU HUU”
“T.B,C:MAMIA YA WANANCHI WALIO TEKWA NDANI YA JENGO LA BIASHARA MLIMANI CITY WAACHIWA HURU”
“Star Tv:GAIDI MMOJA AKAMATWA, NA ALIYE KUWA WAZIRI WA ULINZINA NDIO MTEKAJI MKUU AMEKUTWA AMEKUFA”
 
Kila muandishi wa kitua cha habari aliye kuwepo katika eneo la tukio la Mlimani City aliweza kuzungumza taarifa hiyo kwa jinsi ya habari aliyo weza kuipata kwa wakati huyo. Watu wote walio kuwemo ndani ya ofisi ya maalumu ya matukio ya raisi Praygod Makuya wakajikuta wakipiga makofi wakifurahia tukio hilo, kila mmoja alikumkumbatia raisi kwa furaha, wakimpongeza kwa kazi nzuri, Rahab naye wakampongeza kwa kuwa pamoja nao katika kazi nzito ya kushinda kwenye mativ makubwa yaliyomo ndani ya ofisi hiyo wakilifwatilia tukio zima.
 
“Ila hili ni fundisho inaonyesha ni jinsi gani serikali yetu haijajipanga katika kuimarisha ulinzi. Hivyo basi kuanzia leo maeneo yote ya mipaka nitahakikisha ninaongeza vikosi vya ulinzi na usalama, ili kuhakikisha hawa maharamia hawawezi kuingia tena ndani ya nchi yetu”
Raisi Praygod alizungumza kwa sauti ya juu, watu wote wakampiga makofi kwa wazo hilo alilo weza kulitoa.
 
‘KUSEMA KWELI MIMI NIMSHUKURU YULE MTU ALIYE VALIA NGUO NYEUSI, KWELI ALIAMUA KUJITOA YAANI HUWEZI AMINI MWANANGU ALIMUONA AKI…………”
Dada huyo anaye hojiwa na mundishi alijikuta akimwaga machozi huku akiwa ameshikilia mkono mwanye wa kike, akajipungusa machozi kidogo kisha akendelea kuzungumza,
‘YAANI KUSEMA KWELI YULE KAKA NI JASIRI SANA, NITAMSHUKURU TENA SANA’
Muandishi wa habari akamuhoji mtu mwengine aliye vua shati lake na kulishika mkononi, akionekana kuwa katika hali ya furaha.
 
‘AISEE  CHALAA WANGU MIMI HUKU DAR SIRUDI TENE, YAANI NIMEKUJA FANYA SHOPING HATA UKINIULIZA SASA HVI SIKUMBUKI NI KIPI KILICHO NILETA HAPA, TENA YULE MAN WANGU ALIYEKUWA ANARUSHA RUSHA MATEKE YANII YULE MAN NIME MMAINDI KICHIZI, YAANI CHALAA ANARUSHA VISU HUYO, JAPO NILIKUWA NIMELALA CHINI, ILA NIKAWA NACHABO MARA KWA MARA KUONA JINSI JAMAA ANAVYO WAANGUSHA WALE NGEDERE YANII CHALAA WANGU NAKUKUBALI SANA’
Kijana huyo mwenye lafudhi ya kichaga alizungumza bila hata ya kupumzika kwa furaha aliyo kuwa nayo hadi ikamlazimu muandishi wa habari kumkatisha na kumuhoji mtu mwengine.
 
    ***
Eddy na Samson wakafika nyumbani, moja kwa moja wakelekea kwenye chumba cha siri cha Eddy, ikawa ni kazi ya Samson kuhamisha vitu baadhi vilivyomo ndani ya chumba hicho na kuviingiza ndani ya gari. Mamumivu makali yakazidi kuutesa mguu wa Eddy, jasho jingi likanza kumwagika mwilini mwake, kwani hakuweza kumumbia Samson kama ana jeraha kwenye mguu wake, kwa kiasi cha damu kilicho weza kumtoka akajikuta akilegea na kupoteza fahamu.
 
“Eddy Eddy”
Samson aliita huku akimtingisha Eddy aliye jilaza kwenye kochi mara baada ya kuingia ndani ya chumba hicho, akitoka kupoleka baadhi ya vitu. Katika kumtazama vizuri suruali yeka mguu mmoja umelowana na damu nyingi, katika kumkagua kagua akakuta shimo lililo ingia risasi.
 
“Shitttttt”
Samson akanyanyuka kwa haraka na kukimbilia kwenye kabati lenye sawa pamoja na vifaha vya kutibia majeraha kwa haraka akaanza kumuhudumia kujaribu kuitoa risasi iliyomo ndani ya paja kabla hata sumu yake kusambaa kila eneo la mwili. Ndani ya muda mchache akafanikiwa kuitoa risasi hivyo na kulifunga jeraha hilo. 
 
“Damu”
Samson akataka kutoa damu yake ili amuongezee Eddy, ila akasita akachukua simu yake na kumpigia Rahab ila simu yake haikuwa hewani, ikabidi atume ujumbe wa maandishi mafupi(massage). 

Akataka kumbeba Eddy na kumpeleka ndani ya gari, ila akasikia vishindi vya kama watu wakikimbia nje ya nyumba, kwa haraka akaufunga mlango, akachukua moja ya kiti cha chuma kilichopo ndani ya chumba hicho, akakisogeza karibu na ukutani kisha akapanda juu yake kuchungulia kwenye kijidirisha kidogo kilichopo upande wa juu kabisa wa dirisha hilo. Kundi kubwa la wanajeshi wenye silaha wapo nje ya nyumba ya Eddy wakijiandaa kuvamia ndani ya nyumba hiyo.
 
***
Raisi Praygod baada ya kutoka ofisini kwake majira ya saa kumi na moja alifajiri moja kwa moja akaelekea ndani kwake, akiwa ameongozana na mke wake. Kitendo cha kuingia ndani, wakanza kunyonyana midomo yao taratibu, hisia za kimapenzi zikapenda katikati yao, kila mmoja akaoeneka kuwa na hamu kali na mwenzake, Rahab akanza kumvua nguo mume wake, alipo bakiwa mtu, naye akachojoa za kwake na wote wakaangukia kitandani. 

Furaha ya raisi Praygod ni kusikia mwizi wa penzi lake amefariki na yupo katika chumba cha kuhifadhia maiti Muhimbili, huku akipanga kukipambazuka vizuri aende kumuona mwizi wake huyo aliye fariki  na aibu kubwa kama gaidi.
 
Furaha ya Rahab,, ni jinsi ambavyo Eddy aliweza kuahakikisha ameifanya kazi hiyo pasipo kuweza kujulikana. Kwa furaha zao kwa ujumla wakajikuta wakipiga mechi kana kwamba hawajachoka kabisa, Hadi mechi inafikia mwisho, Rahab akashuka kitandani huku akiwa anapepesuka kwa kuchoka, moja kwa moja akelekea bafuni kujimwagia maji.
Raisi Praygod akiwa amejilaza chali huku akihema kama mtu aliye fukuzwa, akajikuta akishangilia kimya kimya kwa Eddy kuweza kufariki. 

Akashuka kitandani na kujinyoosha, kabla hata hajapiga hatua mbele simu ya mke wake iliyo anguka chini ikaingia ujumbe wa maandishi, akaiokota taratibu na kuirushia kitandani, akapiga hatua mbili kuelekea bafuni, ila roho yake ikasita, akarudi hadi kitandani na kuichukua simu ya Rahab. 

Pasipo kujishauri mara mbili akaufungua ujumbe ambao jina limejitokeza kwa ufupi ‘SAM’. Akatingisha kichwa mara mbili kuyaweka macho yake sawa, kurudia kuusoma ujumbe huo wa meseji.
 
{MADAM EDDY, AMEPIGWA RISASI YA MGUU NA ANAHITAJI DAMU NIMUWEKEE YAKWANGU?}
“EDDYYYYYY………………………???”
Raisi Praygod akabaki akiwa amejiuliza, kugeuza shingo yake nyuma akamkuta Rahab akiwa amesima nje ya mlango wa bafuni akijifuta maji kwa taulo.
                                                                                
SORRY MADAM (34)  (Destination of my enemies)

Raisi Praygod baada ya kugundua kwamba Rahab hajastuka kwa lolote kwa haraka akaifuta meseji hiyo kisha akaizima simu na kuirudisha kimya kimya na kuirudisha kitandani.
“Baby kaoge upumzike”
 
Rahaba alizungumza kwa sauti ya upole, huku akipiga hatua za kuelekea kwenye kabati kubwa kubwa, akatoa kigauni kidogo cha kulalia, na kumuacha mume wake akielekea bafuni kuoga. Msongo wa mawazo ukaanza kukiumiza kichwa cha raisi Praygod, kwani haelewi kama Eddy amekuwa vipi hai. 

Akafungulia bomba taratibu maji yakaanza kumwagikia mwilini mwake huku akiendelea kujiuliza maswali ambayo mengi alijikuta akiwa amekosa majibu. Akamaliza na kurudi chumbani kwake na kumkuta Rahab akiwa tayari amesha jilaza kitandani huku akiwa amejifunika shuka kubwa na zito.
 
“Vipi ulali leo?”
“Nahitaji kutoka tena”
“Unakwenda wapi saa hizi mume wangu”
“Kuna kazi nahitaji kuweza kuifanya ofisini mara moja”
“Mmmmm……Haya mwaya”
Rahab akajigeuza upende wa pili wakitanda, raisi Praygod akavaa nguo za mazoezi(track suit), kisha akatoka ndani ya na kuelekea ofisini kwake.
“Nahitaji twende Muhimbili kuutazama mwili wa waziri Eddy”
Raisi Praygod alimuambia Lube, wote kwa pamoja wakatoka usiku huo huo, akachukua walinzi wengine wanne wakaondoka ndani ya ikulu
 
    ***
   Uvamizi wa jeshi katika jumba la waziri wa ulinzi mstafu anaye sadikika amefariki katika jaribio la kuteka jengo la biashara la Mlimani city, ukazidi kusonga mbele ikiwa ni amri kutoka kwa amiri jeshi mkuu raisi Praygod Makuya, akiamini katika jumba hilo kuta kuwa na mambo ya siri ambayo serikali kama serikali hawayafahamu.
 
Upelelezi ukazidi kufanyika kila kona ya jumba hilo, kitu kilicho zidi kuwapa mashaka wanajeshi hao ni damu iliyo kutwa ndani ya gari lililo kuwa na baadhi ya silaha katika maeneo ya maegesho katika jumba hilo.
“Muheshimiwa kuna dalili ya uhai wa watu humu ndani”
Mwanajeshi mmoja alizungumza mara baada ya kutafuta kila sehemu ila hawakuona mtu wa aina yoyote.
“Endeleeni kutafuta kila konaaa”
“Sawa Captain”
 
Wanajeshi wapatao ishirini na tano kama walivyo agizwa na mkuu wao wa kikosi wakazidi kufanya uchunguzi huku wakichangua changua kila chumba kuangalia kama kuna mtu kwani damu hiyo inaonekana ni mbichi kabisa. 

Wasiwasi mwingi ukazidi kumjaa Samson, kwani endapo chimba hicho cha siri kilichopo chini ya ardhi kikifahamika basi inaweza ikawa ni shida kwao. Akatoa simua yake mfukoni na kupigia Rahab ila hakupatikana hewani, akajaribu kupiga zidi na zaidi ila namba haikupatikana.
 
“Muheshimiwa kuna chumba hapa chini”
Sauti moja ilisikika nje ya mlango wa chumba hicho, macho ya Samson akayeelekezea mlangoni, mapigo ya moyo yakazidi kumuenda mbio, akamtazama Eddy, ila bado hajazinduka kutoka kwenye kupoteza fahamu. 

Samson akaiwahi swichi ya ukutani na kuzima taa zote, macho yake yakabadilika, na kuwa katika hali ya kutisha. Kaptain wa kikosi akafika hadi nje ya chumba hicho alipo itiwa na wanajeshi wake. Chini ya mlango huo kuna matone kadhaa ya damu yakiashiria kwamba mtu huyo ameingia ndani ya chumba hicho.
 
“Vunjaa mlangoo”
Kiongozi huyo alitoa amri, iliyo anza kutekelezwa mara moja kwa vijana wake kuurukia mlango huo kwa kutumia mabega yao. Samson akasimama katikati ya mlango huo akimsubiria atakaye anza kuingia ndani basi atakuwa ni alali yake.
 
  ***
“Nini…………..”
Mzee Godwin aliuliza kwa hasira huku akiwa ameiweka simu yake sikioni.
“Ndio muheshimiwa yule kijana amekamatwa na polisi na sasa yupo katika uchunguzi”
“Pumbavu wewe, hakikisha huyo kijana hazungumzi kitu cha aina yoyote na ikishindikana basi muuee”
“Ila muheshimiwa kijana huyo si wakwetu ni wa Al-Shabab na endapo tukimuua si itakuwa ni mtafaruka?”
“Nimekuambia muue”
 
Simu ikakatwa, bwana Mgwira, akabaki akiwa ameishika simu yake kwa wasiwasi asijue ni nini cha kufanya kwani tayari amesha pokea oda kutoka makao makuu kwa bosi wake. Bwana Mgira akatazama saa yake ya mkononi na kukuta ni saa, kumi na moja alfajiri na ninusu saa tangu aingie nyumbani kwake akitokea ofisini ya raisi akiwa kama miongoni mwa washauri wa ngazi ya juu wa raisi Praygod. Bwana Mgira kwa haraka akakumbuka mkuu wa polisi wa kanda maalumu ni rafiki yake wa muda mrefu kwa haraka akaitafuta namba ya muheshimiwa huyo anaye amini wakati huu bado atakuwa macho kutokana na jukumu zito walilo toka kulifanya masaa machache ya nyuma.
“Ndio muheshimiwa”
Sauti nzito ilisikika kutoka upande wa pili wa simu.
“Huyu mtuhumiwa muliye mshikilia ameweza kungumza kitu chochote?”
 
“Bado muheshimiwa, ila vijana wanazidi kumbana, ili aweze kusema kwamba kundi la waziri Eddy, lipowapi”
“Kwai inavyo wezekana kukawa na walio salia katika kundi hilo kwa maana kiongozi wao ndio huyo amesha kufa?”
“Hilo sina uhakika nalo kutokana bado mtuhumiwa hajazungumza kitu chochote hadi sasa hivi japo bado anapewa mateso makali ila hajazungumza”
“Basi kuna kuna……..”
Bwana Mgwira akajing’ata ng’ata akitamani kuzungumza jambo.
 
“Vipi kuna tatizo?”
“Hapana, basi hakikisheni anazungumza kwa maana hali ya usalama bado si shwari ndani ya hii nchi”
“Usijali muheshimiwa hilo nalo tutalifanyia kazi hapata kuwa na shida yoyote.”
Bwana Mgwira Akaka simu na kushusha pumzi nyingi akiwa anajiuliza ni jambo gani aweze kulifanya kwa Briton aliye shikiliwa na jeshi la polisi. Waz likamijia kichwani na kujikuta akitabasamu huku akiitazama simu yake.
                                                                                                ***
   Taratibu macho ya Shamsa yakaanza kufunguka, akaanza kutazama kila sehemu kuona ni wapi alipo. Kando yake upande wakulia akaona kitanda ambacho amelazwa mama wa makamo kidogo, kageuka upande wa kushoto na kukuta kitanda kingine kikiwa kimekaliwa na mama mmoja huku binti mdogo akiwa amelala kwenye kitanda hicho akiwa ametundikiwa dribu la maji. Shamsa akajaribu kunyanyuka ila maumivu makali yakapita kwenye tumbo lake na kujikuta akirudi tena na kulala kama alivyo jikuta awali.
 
Kumbukumbu ya mwisho ikamjia kipindi alipo jikuta akiwa amepigwa teke zito la mwisho na Eddy, lililo mfanya kuwa katika hali hiyo aliyo kuwa nayo kwa kipindi hichi. Machozi ya yakaanza kumwagika pembezoni mwa macho yake, hakuamini kama Eddy aliye kuwa akimpenda na kumchukulia kama baba yake amebadilika na kuwa jambazi wa kuweza kutoa roho za raisi wasio na hatia. Akiwa katika hali hiyo akapita nesi karibu na kitanda chake, akalazimika kumuita ili kumuhoji baadhi ya maswali.
 
“Eti nesi hapa nipo wapi?”
“Hapa ni Muhimbili hospitali ya Taifa, Muhimbili na hii ni wodi ya watu walio pata matatizo kwenye tukio la ligaidi Mlimani City”
“Ahaa sawa asante”
Nesi huyo akaondoka ila kabla hajafika mbali Shamsa akamuita tena na kurudi hadi kilipo kitanda cha Shamsa.
“Hivi yule kiongozi wa watekaji yupo wapi?”
“Nani………. Waziri Eddy Godwin?”
“Eheee”
“Yule ameshakufa aliuwa kwa na mwenzake aliye kuwa akishirikiana naye”
“Nini?
“Ndio amekufa mbona unashangaa sana?”
“Ahaa ahaha hapana”
 
Shamsa alizungumza huku machozi yakianza kumlanga lenga tena, nesi huyo akandoka na kumuachia Shamsa simanzi kubwa, na likiwa ni moja ya pigo jengine kubwa sana, kwani mtu anaye mtemea ndio hoyo tayari amesha iga dunia. 

Shamsa taratibu akaanza kushuka kitandani huku maumivu makali yakiendelea kumsumbua kwenye tumbo lake, akaanza kutembea huku akiyumba yumba mara kadhaa akalazimika kuweza kujishikiza kwenye baadhi ya vitanda hadi akafanikiwa kutoka nje ya wodi hiyo ya wanawake. Akatazama eneo zima nje ya wodi hiyo, idadi kubwa ya watu mchanganyiko ipo nje ya wodi hiyo, wengine wakiwemo ni ndugu na jamaa walio kuja kuwatembelea ndugu zao.
 
“Raisi amekuja yupo mochwari kule”
Madaktari wawili walio pita kwa mwendo wa kasi huku wakiwa wamevalia makoti meupe walipita karibu na Shamsa wakizungumza mada iliyo mfanya Shamsa, kuichambua kwa haraka kichwani mwake na kugundua ujio wa raisi Praygod Makuya kwenye hospitali hiyo ni kuweza kutazama mwili wa aliye kuwa miongoni mwa watumishi wake waadilifu ndani ya serikali yake waziri wa ulinzi bwana Eddy Godwin.
 
“Wewe, wewee”
Shamsa alimuiita kijana mmoja aliye simama karibu yake, kwa sauti ya unyonge inayo ashiria kwamba bado ni mgonjwa, kwani hata sura yake inaashiria kuonekana ni mtu anaye sumbuliwa na maumivu makali kwenye moja ya maeneo ya mwili wake. Kijana huyo akasogea hadi sehemu alipo Shamsa ili kumsikiliza ni haja gani aliyo kuwa nayo
“Eti mochwari ni wapi?”
“Ni kule”
Kina huyo alimuonyesha kaskazini mwa sehemu hiyo waliyo simama kwa kutumia kidole, Shamsa akajaribu kupiga hatua moja mbele, ila akayumba sana hadi kijana huyo akamdaka.
 
“Dada upo sawa kweli?”
“Ndio nipo sawa”
“Hapana dada haupo sawa”
Kijana huyo alizungumza kwa msisitizo, kwa maumivu makali ya tumbo taratibu Shamsa akajikuta miguu yake ikianza kumuishia nguvu, taratibu akajikuta akikalishwa chini kwa msaada wa kijana huyo aliye msihikilia mwili wake ili asianguke.
 
“Muheshimiwa huu si mwili wa waziri Eddy Godwin. Mtu huyu alivalia sura ya bandia ili kuweza kuitumia katika uhalifu wake ili kumshafulia muheshimiwa waziri mstaafu”
Mkemia mkuu wa serikali alizungumza huku mwili wa Lukuma ukiwa umelazwa juu ya meza iliyopo ndani ya chumba cha uchunguzi, huku sura yake halisi ikiwa imeonekana na sura bandia inayo fanania na sura ya waziri Eddy ikiwa imesha tolewa.
 
‘Ina maana huyu mshenzi bado yupo hai?’
Raisi Praygod alizungumza kimoyo moyo huku akiutazama mwili wa Lukuman kwa hasira kali
“Irudisheni sura yake halisi na mutangaze waziri Eddy Godwin amefariki dunia. Hii si ombi bali ni amri”
Raisi Praygod alizungumza kwa msisitizo kisha akatoka ndani ya chumba hicho kwa hasira na kumuacha mkemia mkuu wa serikali akiwa ameduwaa uamuzi huo ulio chukuliwa na muheshimiwa raisi.

 ==> ITAENDELEA

Usikose kufuatilia sehemu inayofuata kupitia ubuyublog.com   

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts