ILIPOISHIA
‘Ina maana huyu mshenzi bado yupo hai?’
Raisi Praygod alizungumza kimoyo moyo huku akiutazama mwili wa Lukuman kwa hasira kali
“Irudisheni sura yake halisi na mutangaze waziri Eddy Godwin amefariki dunia. Hii si ombi bali ni amri”
Raisi Praygod alizungumza kwa msisitizo kisha akatoka ndani ya chumba hicho kwa hasira na kumuacha mkemia mkuu wa serikali akiwa ameduwaa uamuzi huo ulio chukuliwa na muheshimiwa raisi.
ENDELEA
***
Vishindo vikazidi kusikika nje ya mlango wa chumba cha siri walimo Eddy aliye poteza fahamu pamoja na Samson ambaye macho yake yote ameyaelekezea kwenye mlango huo, gafla mlango huo ukafunguka, na wanajeshi wane wakajikuta wakiingia ndani pamoja na mlango huo. Samson kwa haraka akaanza kuwashambulia wanajeshi hao kwa kuwavunja shingo zao, huku baadhi yao wakitoa vilio vya maumivu makali.
Wanajeshi wengine walio kuwa nje wakajikuta wakifyatua risasi hovyo hovyo pasipo kujua ni nani anaye washambuli. Samson akatoka kwa mwendo wa kasi na kupita katikati yao na kuanza kuwashambulia kwa kuwaua kinyama pasipo huruma. Idadi ya wanajeshi wote walio weza kufika nyumbanbi kwa Eddy, wakauawa.
Bila ya kupoteza muda Samson akarudi ndani ya chumba na kumchukua Eddy aliyekuwa amemuhifadhi kwenye sehemu ambayo haikuwa ni raisi kwa risasi kuweza kumfikia. Akamuingia kwenye gari yao na kuondoka maeneo ya jumba hilo la kifahari.
Kila simu ya upepo iliyokuwa ikipigwa kwa kiongozi wa kikosi hicho kujua ni nini kinacho endelea katika eneo hilo haikuweza kupokelewa, ikabidi watumwe wanajeshi wengine watano kwenda kutazama ni kitu gani ambacho kinaendelea kwenye eneo la tukio.
Wanajeshi walio fika kwenye eneo la tukio hawakuamini macho yao kuwakuta wezao wote wakiwa wamelala chini huku wakiwa wameuwa kifo kinacho onyesha muuaji hakuweza kutumi silaha bali ni kitu chenye ncha kali kama kucha, zilizo weza kuwaparuza wengi wao kwenye sehemu mbalimbali za miili yao.
***
Mkemia mkuu wa serikali bwana Ignatus Mkama, hakuwa na jinsi yoyote yakufanya kwani amri aliyo pewa na raisi Praygod alilazimika kuweza kuitekeleza mara moja. Akaitisha mkutano na waandishi wa habari walio weza kuweka kambi katika hospitali ya muhimbili kujua ni kitu gani kinacho endelea kuhusiana na kifo cha waziri wa ulinzi Eddy Godwin.
“Nimedhibitisha ya kwamba aliye kuwa ni waziri wa ulinzi na mtoto wa waziri mkuu mstafu. Eddy Gdowin, amefariki dunia”
Waandishi wa habari wa magazeti, redio na televishion hawakusita kuuliza maswali kwa bwana Ingatus Mkama.
“Je kifo chake kimesababishwa na nini?”
“Kifo chake kimetokana na kupigizwa chini sehemu ya nyuma ya kichwa chake, ambapo kulipelekea mpasuko mkubwa kwenye ubungo wake na damu iliweza kuvuja na kupelekea ubongo wake kuweza kuganda na ndipo mauti yalipo chukua mauti yake”
***
“Kijana usipo weza kuzungumza kitu cha aina yoyote hakika unaweza ukafia katika mikono yetu”
Mmoja wa askari wapelelezi aliye ingia kwenye chumba cha mahojiano kumuhoji Briton huku akiendelea kumzunguka Briton aliye kalishwa kwenye kiti huku miguu na mikono yake ikiwa imefungwa pingu.
Briton hakuzungumza kitu cha aina yoyote tangu akamatwe kwenye chumba hicho, macho yake makali na yaliyo jaa dharau akaendelea kumtazama mpelelezi huyo ambaye mara kadhaa alimuhoji maswali ambayo hakuwa tayari kuweza kujibu.
“Ninaimani wapo watu ambao wapo nyuma yako si ndio, hembu niambie ni kina nani hao ili niweze kuwatambua”
“Nina weza kukuamini?”
Briton alimuuliza mpelelezi huyo ambaye kwa haraka akaweza kukaa kwenye kiti kilichopo mbele ya meza kumsikiliza Briton aliye patiwa matesi makali ila hakuweza kuzungumza kitu cha aina yoyote.
“Ndio kwa maana mimi siwezi kuwa kinyume na wewe, na ukiniambia ukweli basi nina uhakika nitakuwa upande wako”
“Kwa maana sisi tunahitaji watu ambao wapo nyuma yako, au unahitaji kusema kwamba waziri Eddy ndio alikuwa kiongozi wenu mkubwa au?”
Briton akatabasamu na kucheka kichoko kidogo cha dharau, akakitazama chumba chote na kukuta kameza mbili za ulinzi zikiwa katika kona tofauti katika chumba hicho, kwa uzoefu wake akatambua kabisa mazungumzo hayo yanarekodiwa na kutazamwa na watu wengi, waliopo nyuma ya kioo kikubwa ambacho hakionyeshi nje ila watu wa nje wanaweza kuona ndani.
“Kuna mtu nahitaji kuonana naye hapa hapa ndani ya Tanzania”
Maneno hayo ya Briton alipo kuwa akiyazungumza Bwana Mgwira naye ndio alikuwa amefika kwenye ofisi ya kusikilizia mahojianop hayo yanayo fanywa upande wa pili wa chumba hicho.
“Ni nani huyo?”
Mapigo ya bwana Mgwira yakaanza kumuenda mbio, kwani hakujua ni nani ambaye Biton anakwenda kumtaja, na endapo atakuwa ni yeye basi siri ya D.F.E inaweza kufichuka kwani yeye naye anaweza kufanyiwa mahojiano ili kuzungumza ana mahusiano gani na Briton.
Briton akakaa kwa muda huku akianza kukumbuka baadhi ya matukio yaliyo tokea kipindi cha nyuma akiwa ndio anaingia kwenye kundi la Al-Shabab akiwa kijana mdogo, akamkumbuka jinsi alivyo weza kuishi na Shamsa, hadi wakapotezana kwenye moja ya kazi ambayo walipewa kwenda kuvamia moja ya nyumba iliyo sadikika kwamba ina watu wanao tafutwa na bosi wao katika kipindi hicho. Akakumbuka pia jinsi jana usiku alivyo weza kukutana na Shamsa anaye amini ni wake.
Akakumbuka jinsi Shamsa alivyo muita Eddy baba, taratibu picha ikaanza kumjia kichwani mwake na kuamini kwamba mtu aliye weza kuishi na Shamsa kwa kipindi chote hicho ni Eddy.
Briton akashusha pumzi nyingi huku akimtazama mpelelezi huyo, taratibu akajinyoosha, huku maumivu makali ya kipigo alicho kipata yakiendelea kuutesa mwili wake.
“Nahitaji kuonana na binti mmoja hivi, yupo ndani ya Tanzania”
Bwana Mgwira akashusha pumzi nyingi kusikilizia ni nani huyo binti.
“Anaitwa nani?”
“Shamsa”
“Shamsa……Ila ndani ya Tanzania wasichana waoa itwa Shamsa ni wengi?”
“Nalijua hilo, ila nahitaji kuonana na huyo la sivyo hakuna chochote ambacho munaweza kukijua kuhusiana na mimi, mutanipiga hadi nife, ila sinto kuwa tayari kuzungumza chochote”
Briton akakaa kimya na kuwaahia kazi nzito wapelelezi walio pewa kazi ya kuweza kumpeleleza na kuweza kupata ukweli kuhusiana na kazi yake ya kigaidi anayo ifanya.
***
“What……..!!!!?(Nini…………..!!!!?)
Raisi Praygod alizungumza huku akiwa katika hali ya mshangao
“Ndio muheshimiwa wanajeshi wote wameuawa”
“Wameuawa kivipi?”
Raisi Praygod alibabaika huku akiwa ndani ya gari akielekea ikulu akitokea hospitali ya Taifa.
“Hata sisi wenyewe hatufahamu muheshimiwa”
“Dereva geuza gari tunaelekea nyumbani kwa waziri Eddy”
Raisi Praygod alizungumza huku akiikata simu hiyo, kichwani mwake alihisi kuchanganyikiwa. Mawasiliano yakafanywa kwa madereva wote walipo kwenye msafara wa raisi, gari zote nane zilizo ongezeka baada ya walinzi wengine kugundua raisi aliondoka ikulu kisiri pasipo wao kujua, zikageuzwa kwa mtindo ulio wafanya wananchi wengi walio kuwa karibu na barabara hiyo kushangaa, kwani ziligeuzwa kwa mwendo wa kasi sana.
Ving’ora vya gari zote zilizo tangulia mbele vikawashwa, madereva wote wagari zilizopo barabara ambayo raisi Praygod anapita, walizisogeza pembeni gari zoa, ikiwa ni amri endapo msafara wa raisi unapo pita.
Haikumchukua muda sana Raisi Praygod akafika kwenye jumba la Eddy akiwa na msafara wake na walinzi wakutosha, waandishi wa hhabari pamoja na wananchi walio kuwa karibu na eneo la jumba hilo waliweza kukushanyika nje ya geti kubwa wakishuhudia tukio jengine ambalo hapakuwa na aliye elewa ni kitu gani kilicho tokea, huku baadhi yao walio hojiwa na waandishi wa habari walidai kwamba walisikia milio ya risasi majira ya alfajiri, ila hawakuweza kutoka kohofia maisha yao, kwani tukio la jana tu liliweza kuwaogopesha kila mmoja aliye sikia au kuadisiwa.
Raisi Praygod moja kwa moja akapelekwa kwenye maiti zilizo funikwa za wanajeshi walio weza kupoteza maisha, ikafuniliwa maiti moja iliyo weza kutolewa koromeo, Raisi Praygod akajikuta akifumba macho pasipo kupenda kwa maana maiti hiyo inatisha sana.
“Muheshimiwa hadi sasa hivi hatujaweza kujua ni nani aliye weza kufanya tukio hili kwa maana hapakuwa na alama yoyote ya risasi kwenye miili ya maiti zote”
“Hakikisheni munatafuta na kutambua ni nani aliye weza kuhusika na haya mauaji”
“Sawa muheshimiwa”
***
Habari za kifo cha waziri Eddy, zikapokelewa kwa mitazamo tofauti toafauti na wananchi wa Tanzania, wengine waliweza kushangilia kwa kifo hicho kilicho dhibitishwa na mchunguzi mkuu wa serikali na kutangazwa hadharani kupitia vyombo vya hatai.
Wananchi wengine waliweza kuipokea taarifa hiyo kwa unyonge haswa wale wana mtambua waziri Eddy. Baadhi yao wakabaki na maswali mengi wakijiuliza ni kwanini kiongozi huyo aliweza kufanya tukio hilo la kuwaangamiza wananchi wasio kuwa na hatia. Shamsa akawa ni miongoni mwa wananchi walio weza kushuhudia taarifa hiyo kwenye sehemu hiyo aliyo kaa, yenye Tv ndogo kwa ajili ya watu wanao jipumzisha katika eneo hilo.
Shamsa akajikuta akipata nguvu na kunyanyuka, kijana aliye kuwa akimsaidia tayari alisha ondoka, baada ya kuitwa na baba yake walio fika kutazama dada yake aliye jeruhiwa katika tukio la kigaidi Mlimani City.
Akaanza kutembea kuelekea kwenye chumba cha kutazama maiti, akajitahidi kutembea hivyo hiyo, akijkaza kikike. Alipo hisi kuchoka, alitafuta sehemu akapumzika kwa dakika kadhaa kisha akaendelea na safari yake hiyo hadi akafanikiwa kufika kwenye jengo hilo la kuhifadhia maiti, akakuta watu wengi wakiwa wamekaa kwenye eneo hilo, baadhi yao wakimwagikwa na machozi akatambua kwamba hao ni miongoni mwa watu walio ondokewa na ndugu zao.
Ulinzi mkali wa polisi ulizidi kuimarishwa eneo zima eneo hilo la jengo la kuhifadhia maiti, hususani katika chumba alicho lazwa Lukuma ambaye anasidikika kuwa ndio Eddy.
“Samahani dokta”
Shamsa alizungumza kwa sauti ya kinyonge sana.
“Bila samahani?”
“Nahitaji kuona maiti ya baba yangu?”
“Kusema kweli mimi sihusiki na sehemu hii, kwa kukusaidia nenda pale kwenye dirisha la mapokezi ukizungumza utaweza kuonyeshwa maiti yako”
Daktari huyo baada ya kuzungumza hivyo akaondoka zake na kumuacha Shamsa akitazana kundi kubwa la watu walio kusanyika kwenye dirisha hilo, kila mmoja akijaribu kujua kama ndugu yake yupo kwenye jumba hilo. Akajikongoja hadi kwenye dirisha hilo, akasimama kwa muda kutazama kama anaweza kupata msaada wa kuuliza jina la Eddy, lengo lake kubwa ni kuhakikisha kwamba anamuona Eddy aliye fariki, kwa bahati nzuri akafanikiwa kupata kijiupenyo akafanikiwa kufika kwa dirishani.
“Namuulizia Eddy Godwin”
Shamsa alizungumza kwa sauti ya chini
“Nani hembu zungumza kwa sauti ya juu usilete lete mapozi”
Jamaa huyo aliye onekena kuchoshwa na kuti kubwa la watu alizungumza kwa hasira
“EDDY GODWIN”
Shamsa alizungumza kwa sauti ya juu, na kumfanya jamaa huyo kuanza kuchambua faili lake kwa haraka, akihisi binti huyo atakuwa anamuulizia Eddy mwengine kwani Eddy anaye mfahamu yeye anahisi ahusiani na binti huyu mwenye asili ya kiarabu.
“Binti hakuna jina kama hilo”
“Baba yangu ni waziri aliye kufa Eddy Godwin, unataka kusema humjui wewe”
Shamsa alizungumza kwa sauti ya ukali huku machozi yakimlenga lenga, na mkono wake mmoja akiwa amejishika tumboni mwake akijaribu kuyazuia maumivu makali anayo yapata. Baadhi ya watu waliyo yasikia maneno ya Shamsa wakajikuta wakimtazama marambili mbili, wengine wakianza kunong’onezana na mmoja wao akaropoka
“Jamani huyu ni mototo wa gaidi”
Kitendo cha jamaa huyo kuzungumza hivyo akamfwata Shamsa kwa nyuma na kumsukumia pembeni, na kuanza kuzua vurumai, iliyo wabidi polisi kuweza kuwahi katika eneo la tukio na kumchomoa Shamsa, aliye anza kushambuliwa kwa makofi na mangumi na wananchi hao walio kuwa na hasira dhidi ya Eddy Godwin aliye waulia ndugu zao.
***
“MAUAJI MENGINE YAKUTISHA YATOKEA KWENYE JUMBA LA MAREHEMU WAZIRI EDDY GODWIN”
Taarifa hiyo ikamfanya Rahab kunyanyuka kitandani haraka haraka na kukaa kitako, akachukua romoti ya tv hiyo iliyomo chumbani kwake na kuiwasha, akazidi kuikodolea macho Tv hiyo na kutazama baadhi ya maiti nyingi zikiwa zimefunika kwenye eneo la kiwanja katika jumba hilo analo lifahamu vizuri sana.
“Eddy”
Rahab kwa haraka, akaanza kuitafuta simu yake, akaikuta chini ya mto, akaikuta ikiwa imezima akaiwasha, kitu cha kwanza kuweza kufanya ni kumpigia Samson na kumuuliza ni kitu gani kilicho tokea, Simu ya Samson ikaita kwa muda mrefu na kukata, akarudia kupiga tena, ikaita na kukata.
Akajaribu kuipiga namba ya Eddy, ila nayo haikuita, akaitazama saa iliyomo ndani ya simu yake, ikamuonyesha ni saa nne asubuhi. Kwa haraka akashuka kitandani na kusimama wima akiwa amechanganyikiwa, akajaribu kufumba macho yake kuvuta hisia zake kutambu ni wapi alipo Eddy, ila hakuweza kuona kitu cha aina yoyote.
“INASADIKIKA MUUAJI WA WANAJESHI HUO NI KIUMBE AMBACHO SI CHAKAWAIDA, NA UPELELEZI UNAENDELEA KUFANYIKA ILI KUMPATA MUUAJI”
Maneno ya muandishi wa habari huyo yakazidi kumchanganya Rahab, akajaribu tena kuvuta hisia zake kujua ni wapi alipo Eddy, kidogo picha ikaanza kumjia kwenye hisia zake, akaona jinsi Eddy alivyo weza kutoka kwenye jumba lake akiwa ameingizwa kwenye gari na Samson, jinsi Rahab anavyo jaribu kuvuta hisia zake ndivyo jinsi damu zilivyo anza kumtoka kwenye pua zake.
Hakulijali la pua kuweza kutoka damu, akazidi kuvuta hisia zake, akaona jinsi gari aliyo panda Eddy ilivyo kuwa ikieelekea nje ya mkoa wa Dar es Salaam, ila gafla picha hiyo ikakata kwenye hisia zake.
Rahab akajitahidi tena na tena kuvuta hisia zake ila hakuweza kuona kitu chochote, akajaribu kumtafuta Samson kwenye hisia zake ila hakuweza kuona kitu chochote. Rahab machozi yakaanza kumlenga lenga, kwani tayari alihisi hali ya hatari imetokea kwa Eddy na Samso.
Akajaribu tena kuvuta hisia zake, huku nguvu za mwili zikiwa zimemuishia kabisa. Picha ya mwisho kuweza kuiona ni gari kubwa aina ya Scania ilivyo weza kuivaa gari aliyo panda Eddy na Samson na kusambaratika vipande vipande na kulipuka na watu wake waliomo ndani ya gari hilo
SORRY MADAM (36) (Destination of my enemies)
Rahab akafumbu macho yake huku akihema sana, kwa haraka akaelekea bafuni, akanawa uso wake, akarudi chumbani na kufuta matone yote ya damu, kwa haraka akafungua kabati na kuhukua suruali iliyo mbana kiasi kisha akachukua na tisheti iliyo mbana na juu akavaa kikoti. Alipo hakikisha yupo tayari, nywele zake zinazo fika mgongoni, akazikunja na kuzibana na kibanio.
Akafungua droo yake, akatoa bastola yenye magazine yenye risasi za kutosha. Akaichomeka kwa nyuma maeneo ya kiunoni mwake kisha akavaa gloves nyeusi mikononi mwake, akamalizia na kuvaa kofia nyeusi pamoja na miwani kisha akatoka chumbani kwake. Wafanyakazi wa ndani wakabaki kumshangaa bosi wao jinsi alivyo vaa kwani ni mara chache sana kuweza kuvaa hivyo. Akatoa simu yake na kumpigia Priscar.
“Andaa gari tunatoka”
“Sawa madam”
Rahab moja kwa moja akaelekea nje akiwa katika mwendo wa kujiamini, kila mlinzi aliye pishana naye alibaki kumshanga mke wa raisi imekuaje leo anatoka hivyo. Akafika kwenye maegesho na kumkuta Prisca akiwa ndani ya gari aina ya Aud Q5. Rahab akaingia na kukaa siti ya mbele tofauti na mazoea ya siku zote kwani anatakiwa kukaa siti ya nyuma kama kiongozi.
“Madam mbona leo umekaa mbele?”
“Endesha gari kwani kuna tatizo?”
“Haha hapana”
Prisca akawasha gari na kuondoka taratibu pasipo kujua ni wapi anapaswa kuelekea.
***
Katika barabara itokayo Dar es Salaam, kwenda mikoa ya Arusha na Tanga, katika kijiji cha Mkata, ajali moja mbaya na kubwa ya gari ndogo aina ya Toyota land cruser, ikiwa imegongana uso kwa uso na gari kubwa aina ya Scania lililo beba mafuta ya petrol na kusababisha mlipuko mkubwa ulio pelekea gari zote mbili kuteketea kwa moto. Gari za zima moto pamoja na askari wa usalama barabarani na wanao tuliza ghasia, wakafika eneo la tukio wakiwa makini katika kudhibiti hatari yoyote ambayo itajitokeza.
Kila aliye shuhudia ajali hiyo alizungumza chake kutokana na alicho weza kukiona wakati ajali ikijitokeza, wapo walio dai kwamba ni uzembe wa dereva aliye kuwa anaendesha gari ndogo wengine wakadai ni uzembe wa madereva wote kwani gari zote mbili zilikuwa zikienda kwa mwendo kasi sana.
Kikosi cha kuzima moto kikajitahidi kuifanya kazi yake, ila hawakuweza kuwaokoa watu wali kuwemo kwenye gari ndogo kwani moto uliweza kuwateketeza muda mrefu sana.
Walicho weza ni kuzima moto, usiendelee kuwaka.
Priscar kwa kufwata maelekezo anayo pewa na Rahab wakaweza kufika maeneo ya Mkata, na kuikuta ajli hiyo, kwa haraka Rahab akashuka kwenye gari na kujipenyeza kat5ikati ya wananchi walio zunguka eneo hilo hadi akafanikiwa kufika mbele ilipo angukia gari ya Samson. Machozi na ya uchungu yakaanza kumwagika. Hakuamini macho yake kama amewapoteza watu muhimu sana.
“Samahani mama unatakiwa kurudi nyuma”
Askari mmoja alizungumza huku akimrudisha Rahab aliye simama pasipo kujali moshi mwingi wa gari hiyo unavyo muingia mwili mwake. Hakusikiliza kauli ya askari huyo zaidi akaendelea kusimama akizidi kuto kuamini kwamba Eddy na Samson wamefariki dunia.
“No haiwezi kuwa”
Rahab alizungumza huku akigeuka nyuma na kumkuta Priscar akiwa amesimama kama kazi yake inavyo mlazimu kufanya pale mke wa raisi anapo kuwa nje ya ikulu basi anapaswa kumlinda, labda itokee Rahab akamzuia. Rahab akajikuta akimkumbatia Priscar ambaye hakujua ni kwanini basi wake huyo analia, taratibu akampitisha katikati ya watu wanao mshangaa, kisha akampeleka ndani ya gari.
“Bosi kuna tatizo gani?”
“Eddy na Samson wamefariki”
“Weeeee…………………!!!!”
Ikambidi Priscar kushuka naye kwenda kutazama kwenye gari inayo malizikia kuteketea kwa moto kama ni kweli Samson wake, aliye tokea kuanza kumpenda ndio anateketea kwa moto, Priscar na yeye akajajikuta akishindwa kujizuia. Machozi yakaanza kumwagika, ikabidi kumfwata askari mmoja na kumuuliza.
“Kaka ina maana watu wote wamekufa ndani ya hii gari ndogo?”
“Ndio dada, hatukuweza kuwaokoa, kwani wewe ni nani kwao?”
Askari hutyo aliongezea swali baada ya kumuona Priscar akimwagikwa na machozi huku akijikaza tu kuzungumza.
“Ni mume wangu?”
“Hembu ngoja”
Askari huyo akamfwata mwenzake aliye kuwa amesimama pembeni akipima pima baadhi ya mambop barabarani. Mwenzake huyo akampa kimfuko cheupe chenye kitu ndani kisha akarudi alipo simama Priscar. Askari huyo aliye onekena kumuhurumia Priscar, akatoa simu iliyo pasuka kioo kidogo ila baodo inafanya kazi.
“Na hii si ni simu yake?”
Alizungumza huku akimpatia Priscar simu hiyo, Priscar akatingisha kichwa kwamba ni ya Samson, kwani siku walipokuwa msituni aliweza kumuona nayo simu hiyo. Na ushahidi mwingine waliweza kupiga picha ya pamoja kupitia simu hiyo. Katika kuichunguza akakuta missed call, za bosi wake ikionekana Rahab alimpigia Samson.
“Hiyo simu iliokotwa na mwananchi, mita chache kutoka eneo la ajali, alikuwa mwaminifu na kutukabidhi sisi”
“Asante afande”
“Ila itabidi kufanya utaratibu wa kutoa mifupa ndani ya gari, kwa ajili ya kwenda kuzika”
Maneno ya askari huyo yakamfanya Priscar kuondoka huku akiangua kilio, ukakamavu wake alio upata katika jeshi, haumkusaidia kitu kuweza kujizuia kumwaga machozi kwa mwanaume aliye tokea kumpenda, isitoshe hakuweza kumueleza kitu kama hicho kwamba anampenda hadi mauti yalipo weza kumkuta.
***
Video ya jinsi Briton, Lukuma na mtu aliye valia mavazi meusi pamoja na kofia kofia lililo mfunika kichwani mwake, ikafikishwa mbele mkuu wa kikosi cha Al-Shabab bwana Abdulah Mohamed, akiwa na kijana wake msaidizi wa kikosi hicho wakaanza kuitazama video hiyo kwa umakini wa hali ya juu.
Mara kidogo bwana Abdulah Mohamed akastuka, kumuona binti anaye mtambua vizuri na ni binti aliye weza kulelewa na marehemu kaka yake, aliye kuwa kiongozi wao, baada ya kaka yake kufariki akashikilia yeye madaraka.
“Huyu si Shamsa?”
Alimuuliza msaidizi wake huku wakiisimamsha video hiyo, katika sehemu ambayo Shamsa aliweza kuingilia ugomvi huo akionekana kupambana na Lukuman.
“Ndio yeye bosi”
“Ohhh mwanangu, fanya fanya utume vijana wajue ni wapi alipo mwanangu huyu”
Bwana Abdulah Mohamed alizungumza huku akiwa na furaha moyoni mwake, kwani kazi moja ambayo marehemu kaka yake alimuachia ni kuweza kuhakikisha kwamba ana mtafura Shamsa popote alipo, ili miaka ya baadae Shamsa anatakiwa kuridhi kiti chao cha uongozi. Japo Shamsa hakuwa ni mtoto wa kumzaa wa kaka yake. Ila alimchukulia kama mwanaye na mambo mengi na siri nyingi sana aliweza kuambiwa na kiongozi wake huyo kuhusiana na kikundi hicho chenye makazi yake makuu mjini Mogadishu Somalia.
“Muheshimiwa tumepata ripoti kwamba yupo Tanzania”
“Tuma viajan makini, na wahakikishe wanarudi pia na Briton hapa”
Bwana Mohamed alizungumza huku akiendelea kuitazama video hiyo, alipo ona jinsi Shamsa alivyo pigwa kipigo kikali na Lukuman, aliyafumba macho yake na kujihisi maumivu makali, moyoni mwake. Ila alipo ona Briton anamvaa, Lukuman na kuanza kumshambulia basi akaamini kwamba Briton amefanya jambo sahihi kumuokoa kiongozi wao huyo mtarajiwa, wanaye mtafura miaka kwa miaka.
Kundi la vijana wanne walio kamilika katika nyanja zote kuanzia kupambana na uytumiaji wa silaha wakapewa picha ya Shamsa, na kuihidiawa aendapo watamleta kila mmoja ataoewa donge nono la dola za kimarekani laki moja, na agizo jengine wakaambiwa wahakikishe wanamrudisha Briton nyumbani na aendelea kutumikia mikono ya serikali wa Tanzania, pasipo kujua kiongozi mwake mzee Godwin ameagiza kija huyo auawe akiwa ndani ya mikono ya serikali ili asitoe siri ya kikosi chao,
***
Taarifa ya binti wa Eddy, Shamsa kuokolewa katika miono ya wananchi walio mshambulia kwa hasira, wakimshutumu ni mtoto wa gaidi, zikaifikia ofisi ya upelelezi, walio kuwa wameanza msako wa kufwatilia majina yote ya wasichana wanao itwa Shamsa, wenye asili ya kisomali nchini Tanzania. Wakiamini ya kwamba watakuwa ni miongoni watu wanao husika na kikosi cha Eddy. Ila walipo sikia kuna mtoto wa Eddy yupo mikononi mwa Polisi na yeye anaitwa Shamsa, wakapiga picha kwamba Eddy ndio aliye kuwa kiongozi wa kundi hilo, basi ikawawia urahisi kuweza kutambua Shamsa huyo ndio anye hitajika na gaidi waliye mshikilia.
Shamsa akashangaa kuona ulinzi wa polisi ukingezeka katika kitanda alicho lazwa akiendelea kupatiwa matibabu ya muhimu na madaktari.
“Eti dada kuna nini?”
Shamsa alimuuliza askari mmoja wa kile aliye simama kando yake akiwa na bastola kiunoni mwake.
“Hakuna chochote mdongo wangu, ila tunapaswa kukulinda tu”
“Kwani kuna tatizo juu yangu?”
“Hapana, ila kuna haja ya sisi kuweza kukulinda wewe kwani tuna amini kuna watu wabaya wanaweza kukufwatilia”
“Ahaa sawa”
Shamsa hakutilia mashaka sana, kwani aliamini ni kweli watu wabaya wanaweza kumvamia na kuitoa roho yake. Matibabu ya haraka yakaendelea kufanyika huku akichomwa baadhi ya sindano za kukata maumivu, ili aweze kwenda kwenye ofisi za usalama wa taifa kukutanishwa na gaidi walio mkamata.
Ndani ya masaa mawili, Shamsa akajihisi unafuu mkubwa, maumivu yote aliyo kuwa akiyahisi tumboni mwake, yakakatika. Akamueleza nesi aliye kuwa akimuhudumia kwamba yeye yupo salama tu na anahitaji kuweza kuondoka hapo hospitalini.
Kutokana nesi huyo anafahamu kinacho endelea, akamuita daktari na kumruhusu Shamsa kuweza kutoka katika hospitali, polisi zaidi ya sita wakaongozana na Shamsa kuelekea maeneo ya maegesho ya magari kwa madai kwamba wanamlinda, ila asivamiwe, ila ukweli tayari amsha anza kuhisiwa kama gaidi kutokana baba yake Eddy amefanya tukio la kigaidi ambalo kila mmoja ndani ya nje ya Tanzania ameweza kulishuhudia kwa macho yake.
“Naweza kumuona baba yangu?”
“Hapana kwa muda huu wananchi wakiweza kukuona wanaweza kuanzisha vurugu, mwili wa baba yako ukisha andaliwa basi utaonyeshwa”
Shamsa akatokea kumuamini askari huyo, wa kike ambaye kwa mara nyingi aliweza kumuuliza maswali na akayajibu kiufasaha kabisa. Waandishi wa habari walipo waona Shamsa na askari wakanza kukimbilia eneo walipo ili kupata japo habari kuhusiana na binti huyo ambaye wananchi chupu chupu wamtoe roho wakidai kwamba ni mtoto wa gaidi. Askari kwa haraka wakamuingiza Shamsa ndani ya gari na kuondoka naye katika eneo la hospitali wakiwaacha waandishi wa habari wakipiga piga picha gari hilo la polisi.
“Munanipeleka wapi?”
“Sehemu ambayo ni salama kwa maisha yako”
“Nipelekeni nyumbani kwanza”
“Hauwezi kwenda kutokana kuna mauaji ya kikatili yametokea nyumbani kwenu, walipelekwa wanajeshi kulinda ila wote waliuawa kwa hiyo inavyo onekana watu hao wana kutafuta wewe”
Kabla Shamsa hajazungumza chochote, askari huyo akatoa simu yake mfukoni na kumuwekea Shamsa tukio lililo tokea nyumbani kwao majira ya asubuhi.
Shamsa akajikuta akishika mdomo kwa mshangao, kwani maiti nyingi za wanajeshi zimelala chini zikiwa zimeuawa vibaya sana. Hofu na mashaaka vikaanza kumtawala, hapo ndipo akaamini kwamba anapaswa kulindwa na askari wote hao.
Wakamfikisha Shamsa kwenye jengo kuu la ofisi za usalama wa taifa, wakamkabidhisha kwa kikosi hicho kisha wao wakaondoka. Shamsa moja kwa moja akapelekwa kwenye chumba alicho andaliwa na kikosi hicho, chenye kila huduma kama chumba cha kisasa.
“Naitwa Pudensia, nitakuwa muhudumu wako kwa kila jambo ambalo utalihitaji humu chumbani kwako”
Mmama huyo alijitambulisha kwa Shamsa huku akiwa ameachia tabasamu pana akimtazama Shamsa.
“Asante”
“Umekula?”
“Hapana”
“Utahitaji nikuletee nini?”
“Sambusa na chai”
“Za nyama au viazi?”
“Nyama”
“Ok subiria kidogo”
Mwana mama Pudensia akatoka ndani ya chumba hicho, Shamsa akabaki akiwa na mawazo mengi ni kwanini watu hao wabaya wanamfwatilia yeye. Swali jengine lililo mjia kichwani mwake ni kwanini Eddy alikwenda kuteka Mlimani City wakatyi anajitambua ya kwamba yeye ni kiongozi anaye tazamwa na watu wengi. Machozi taratibu yakaanza kumwagika kwani hakuamini kwamba Eddy ndio tayari amesha fariki na kumuacha akiwa peke yake.
“Eddy kwa nini lakini ulifanya hivyo?”
Shamsa alizidi kulia huku akimlalamikia Eddy kwa maamuzi ambayo aliyachukua na kumpelekea kufa. Mwanamama huyo akarejea akiwa amshikilia, sahani nyenye sambusa nne, chupa ya chai pamoja na kikombe. Akamuandalia Shamsa kila kitu na kumkaribsha kula. Shamsa taratibu akaanza kula huku kichwa chake kikiwa kimetawaliwa na mawazo mengi sana. Hakujua ni nini hatima ya maisha yake kwa wakati huu.
Hata ladha ya chai hiyo hakuweza kuipata mdomoni mwake, akajilazimisha kuinywa hivyo hivyo ili mradi aimalize chai hiyo, kwani njaa inamsumbua tumboni mwake. Alipo maliza Pudensia akamuomba waongozane hadi kwenye moja ya chumba ambacho kuna mtu anahitaji kumuona na kumuambia maagizo aliyo pewa na Eddy. Kwa ujanja alio utumia Pudensia ukamfanya Shamsa kunyanyuka kwa haraka na kumuomba waongozane kwenye chumba hicho huku akiwa na shauku kubwa ya kuweza kumuona mtu huyo ni nani.
Wakafika katika chumba hicho akaingia na Pudensia, Shamsa akamkuta gaidi ambaye aliweza kumuona akipambana na mtua aliye kuja kuwaokoa. Briton alipo muona Shamsa akatabasamu, akiamini kwamba mpenzi wake huyo anaweza kumkumbuka.
“Shamsa ni muda mrefu atuja onana”
Briton alizungumza baada ya Pudensia kutoka ndani ya chumba hicho.
“Wewe ni nani?”
Shamsa alizungumza huku akikaa kwenye kiti wakitenganishwa katikati yao na meza.
“Ina maana umenisahau Shamsa wangu”
Wapelelezi waliopo nje ya chumba hicho walizidi kuyafwatilia mazungumzo hayo kwa vinasa sauti walivyo weza kuvifunga ndani ya chumba hicho.
“Siwezi kumfahamu mtu gaidi kama wewe. Niambieni ni nini alicho kuambia baba yangu Eddy”
Shamsa alizungumza kwa hasira huku akimwagikwa na machozi, Briton kwa dharau akatabasamu kisha akajivuta kidogo kwenye kiti na kumtazama usoni Shamsa
“Baba……..baba gaidi kama Eddy. Ohoooo mimi ndio niliye weza kumuua, sahamani kwa hilo”
Shamsa akasimama kwa hasira na kumrukia Briton na wote wakaanguka chini na kuanaza kumshindilia ngumi za hasira Briton aliye fungwa pingu miguuni na mikononi.
==> ITAENDELEA
Usikose kufuatilia sehemu inayofuata kupitia ubuyublog.com
Usikose kufuatilia sehemu inayofuata kupitia ubuyublog.com
Post your Comment