ILIPOISHIA
Kwa bahati nzuri, Shamsa akamkuta Eddy akiwa tayari amemaliza kuoga na kuvaa nguo zake pamoja na kinyago chake. Eddy katika kumduwaa, Shamsa aliye mjia kwa kasi, ndani ya bafu hilo akiongozana na waandhishi wa habari. Akastukia Shamsa akimkumbatia kwa nguvu bila hata kusita Shamsa akaanza kumnyonye denda black shadow, huku waandishi wakifyatua kamera zao kupiga picha za kuweka kwenye magazeti yao.
ENDELEA
Kitendo hicho kikampa Eddy kigugumizi, akataka kumuita Shamsa ila sauti haikutoka akajikuta akiugulia tu huku akijaribu kumtoa Shamsa mwilini mwake.
Mabaunsa na wapambe wa Sabogo wakawa tayari wamesha ingia ndani ya bafu. Mabaunsa wakambeba juu juu Shamsa aliye anza kupiga kelele za furaha.
“I love you black shadow”(Nakupenda black shadow)
Waandishi wa habari nao wakatolewa ndani ya bafu hilo. Akabaki Eddy na Sabogo.
“Hao ndio mashabiki kiongozi inabidi uwavumilie tu”
Eddy hakujibu kitu zaidi ya kubaki kimya, akimfikiria Shamsa.
‘Huyu mtoto amepatwa na nini?’
Alijiuliza swahi hilo kichwani mwake.
“Kiongozi?”
“Mmmmmmm”
Eddy alistuka kutoka katika dibwi la mawazo mengi
“Huyu binti amekuumiza nini, tumchukulie hatua za kisheria?”
“Hapana muacheni, na kama inawezekana kesho nahitaji akae meza ya VIP”
“VIP tena! Au umesha mzimikia tukamlete upate naye burudani usiku mzima. Kwa maana anaonekana kama changudoa”
“Fanya kama nilivyo kuagiza kufanya”
Eddy alizungumza kwa sauti nzito hadi Sabogo mwenyewe akabaki kimya na kutingisha kichwa akimaanisha kwamba amemuelewa.
Shamsa akamkuta Sa Yoo nje ya ukumbi, akamkimbilia na kumkumbatia kwa nguvu rafiki yake huyo huku akishangilia kama ameokota kipande cha dhahabu barabarani.
“Vipi nieleze umefanikiwa?”
“Ndio yaani ninafuraha achaa. NAKUPENDA BLACKKKK SHADOOOOOOWWWWWWWWW”
Shamsa alizungumza kwa sauti kubwa kama mwenda wazimu. Hata baadhi ya watui wakabaki wakimshangaa. Kutokana yupo nje ya ukumbi amboa mpiganaji huyo ametoka kuzichapa ulingoni muda mfupi ulio pita. Kila mtu akaamini kwamba binti huyo amechanganyikiwa kwa upendo kama wanachanganyikiwavyo wasichana wengine wanapo waonaga watu maarufu duniani.
Njia nzima ndani ya gari Shamsa, aliendelea kumzungumzia black Shadow. Kumbukumbu ya jinsi alivyo mrukia black shadow na kumnyonya denda, zikawa zinamrudia rudia. Hadi ikafikia kipindi akaanza kuutathini mwili wa mpiganaji huyo, akiwa hana nguo.
“Huli chakula?”
“Nimeshiba”
Shamsa alijibu huku akielekea chumbani kwake mara baada ya kufika katika nyuma wanayo ishi na Sa Yoo. Akaingia ndani kwake na kuufunga mlango kwa funguo. Haraka haraka akazivua nguo zake zote na kubaki kama alivyo zaliwa. Akasimama mbele ya kioo kikubwa cha kabati na kuanza kujichunguza huku akigeuka geuka akiliangalia umbo lake lililo jengeka vizuri.
“Mimi mzuri, kesho nawahi mapemaa ukumbini nimuone black shadow”
***
Ndani ya ndege ya kifahari aina ya Jet, Mzee Gdowin na John, pamoja na walinzi wao wawili. Waliendelea kuzungumza mambo mengi kuendelea kikundi chao ambacho kina watu wengi sana dunia. Ndege iliendelea kupasua mawingu kuelekea bara la Asia, ikitokea Amerika ya kaskazini. Ni safari ambayo imewachukua masaa mengi kadhaa, ila lengo na zumuni lao ni kwenda kuishuhudia fainali ya mapambano inayo endelea ndani ya Japani.
Wametokea kujikuta wakimpenda black shadow, mpiganaji mwenye ujuzi mkubwa sana katika maswala ya kupigana, wameona ni vyema wamchukue huyo ili awe miongoni mwa washirika wao ili kuzidi kujitanua kwenye kikuni chao.
Mara kadhaa wakajikuta wakitazama baadhi ya video za mapambano manne ya black Shadow. Ujuzi wao wa kupigana ulizidi kuwachanganya, na kutamani ndege hiyo iweze kufika katika muda mchache. Kwani wanahofia matajiri wengine duniani wanaweza kujitokeza na kumchukua black shadow katika mambo mbalimbali, ikiwemo uigizaji wa filamu.
“Mzee usiwe na hofu tutampata tuu. Nguvu ya kila kitu tunayo”
John alizungumza huku akimtazama Mzee Godwin anaye onekana kuwa na wasiwasi mwingi sana.
“Hawa marubani sijui wanaiendeshaje hii ndege, naona tunachelewa”
“Tutafika tu”
Masaa manne mbele teyeri wakawa wamefika nchini Japani, majira ya saa nne asubuhi. Wakapokelewa na mwenyeji wao ambaye moja kwa moja akawapeleka hadi kwenye hoteli moja ya kifahari.
“Pambano linaanza saa ngapi?”
Aliuliza mzee Godwin baada ya kupumzika kwa dakika kadhaa baada ya kufika hotelini.
“Saa nne usiku”
“Ahaa, hatuwezi kuonana na huyo black shadow muda huu kabla ya pambano?”
Mzee Godwin alimuuliza mwenyeji wao bwana Jackson Lee.
“Kusema kweli itakuwa ni ngumu kutokana black shadow yupo kwenye maandalizi ya pambano la usiku”
“Sawa kila kitu kiwekeni sawa, hata kesho muutaarifu uongozi wake kwamba ninahitaji kufanya naye kikao”
“Sawa mueheshimiwa”
***
Kengele ya mlangoni ndio iliyo mkurupusha Sa Yoo. Akajizoa zoa kitandani kwake na kuiangalia saa yake ya ukutani na kukuta ni saa tano na dakika tano asubuhi. Akasimama na kujinyoosha mara kadhaa huku akipiga miyayo. Taratibu kwa wenge la usingizi akaanza kutembea kuelekea mlangoni. Akafika mlangoni na kuminya moja ya batani ambayo pembeni yake kuna kitivii kidogo cha ukutani kinacho muonyesha mtu aliyopo nje ya mlango. Akamuona kijana mmoja aliye valia tisheni yekundu na kofia nyekundu akiwa amesimama, huku mkononi mwake akiwa ameshika boksi.
Uvaaji wa kijana huyo ukamuashiria Sa Yoo kwamba huyo ni mlete mizigo kutoka katika kampuni moja kubwa ya kutuma mizigo ndani ya Japani. Akafungua mlango na kumtazama kijana huyo.
“Wewe ndio Ms Shamsa?”
“Hapana ila unaweza kusema shida yako”
“Kuna mzigo wake hapa nimeagizwa kuuleta kama yupo basi nahitaji kuweza kumuona”
“Umetokea wapi?”
“Madam kama wewe si muhusika basi, siwezi kukuambia kwamba unatokea wapi?”
“Mmmmmm”
Sa Yoo aliguna kisha akaanza kumuita Shamsa kwa sauti kubwa. Shamsa aliitikia baada ya muda akatoka akiwa amejifunga taulo akiashiria kwamba naye ndio kwanza anaamka.
“Kuna mzigo wako hapa”
Sa Yoo alizungumza huku akiondoka mlangoni na kwenda kujibwaga kwenye sofa na kujilaza kumalizia malizia usingizi wake.
“Naamini wewe ndio ms Shamsa?”
“Ndio”
“Kuna mzigo wako hapa kutoka kwa Mr Sabogo”
“Mr Sabogo ndio nani?”
Sa Yoo baada ya kusikia hilo jina akakurupuka na kukimbilia mlangoni akiwa katika sura ya furahja
“Humjui wewe Mr Sabogo, si yule mzamini wa black shadow”
Shamsa kusikia hivyo akawa kama mtu aliye changanyikiwa kwa haraka, akasaini kwenye karatasi maalumu ya kijana huyo kisha wakaagana naye kijana huyo na kuufunga mlango. Akaanza kulifungu boksi hilo. Macho yao wote yakatua kwenye ua zuri jekundu, linalo nukia vizuri, Sa Yoo akalitoa ndipo wakaziona tiketi mbili zilizo kuwa chini ndani ya boksi.
“VIP TIKETIIIIIII UUUUUUUUU”
Shamsa alizungumza huku akiruka juu kwa furaha, Sa Yoon aye akampokonya moja wote wakajikuta wakiruka ruka kwa kushangilia kupata mualiko huo kutoka kwa black shadow.
Kila mmoja akawa anaombea muda na masaa yaweze kukimbia kwa haraka ili wafike ukumbini kushuhudia pambano ambalo si kwasababu watu wanalipenda, ila Shamsa anampenda mpiganaji wa pambano huyo ambaye ni black Shadow
Majira ya saa mbili usiku Sa Yoo na Shamsa wakawa wamefika katika ukumbi wa mapambano. Kwa siku hiyo hawakupita katika lango wanalo pita watu wa kawaidia ila walipita katika lango la kuingilia katika viti maalumu vya watu wenye hadhi ya juu. Kila sehemu Shamsa alipo pita alitazamwa na watu kwani habari za yeye kumbusu black shadow, zilienea kwenye magazeti mengi. Kwa msaada wa muhudumu katika sehemu hiyo maalumu wakaonyeshwa viti vyao vya kukaa, ambavyo mbele yake kuna kioo kikubwa na kigumu kinacho onyesha pambano hilo kwa ukaribu zaidi kutokana na lensi ya mvutano iliyo tengenezwa kwenye kioo hicho.
“Munatumia kinywaji gani?”
Dada muhudumu aliwauliza, kila mtu akaseme kinywaji anachho kihitaji. Watu walizidi kumiminika katika ukumbi, kila mtu aliitafuta siti yake na kuweza kukaa kusubiria muda muafaka wa pambano hilo liweze kufika.
Ulinzi mkali ukaimarishwa katika sehemu ya VIP, mzee Godwin na John ambaye muda wote maisha yake ni yakusukumwa kwenye kiti maalumu cha matairi. Wakaingi katika sehemu hiyo. Wakakaribishwa katika sehemu waliyo andaliwa, ambapo kuna wadada sita walio valia chupi aina ya bikini na sidiria wakiwa wamesimama, kwa ajili ya kuwapa huduma ya kuwachua chua miili yao pale watakapo kuwa wakiendelea kuliangalia pambano hilo.
Vipaza sauti vilivyomo ndani ya uwanja vilianza kutoa sauti ya kike ya mtangazaji wa pambano wa siku ya leo. Kelele zilizidi kurindima kila mahali, watu walikuwa kama wameingiwa na pepo la kushangilia kila walipo sikia jina la black shadow.
Wadada wengi walishika mabango yaliyo andikwa ujumbe tofauti tofauti wakionyesha hisia zao za kumpenda mpiganaji huyo, aliye jizolea umaarufu katika kipindi kifupi tu.
Macho ya Shamsa yakaendelea kutazama huku na kule, mara kadhaa alijaribu kuyapitia mabango ya wasichana waliyo yashika, akajikuta akiingiwa na woga pamoja na wivu wa kumkosa mpiganaji huyo katika swala zima la mapenzi.
“Anaye kuja kwenu kwa sasa ni BLACK SHADOWWW”
Uwanja mzima ukasimama huku watu wakimshangilia. Eddy hakuamini kupata idadi kubwa ya watu wanao mshangilia, kila alipo pitisha macho yake huku na kule aliona baadhi ya watu wakiwa wamevaa mavazi kama yake. Akaanza kutembea kwa kujiamini kuelekea uwanjani. Hakusita kupita karibu na washabiki walio kaa karibu na njia ya kuelekea ulingoni. Akawapa mikono kuashiria kwamba anawapenda kama wanavyo mpenda.
Akaingia ulingoni na kuendelea kuzunguka huku mkono wake mmoja wa kulia akiwa ameunyoosha juu, kwa ishara ya kuwasalimia watu. Muendesha shuhuli akamkaribisha Yong Po. Mashabiki wake nao wakasimama na kumshangilia mpiganaji huyo anaye sifika kwa kuweka rekodi ya kuwavunja vunja wapiganaji anao kutana nao. Hakuwa mwenye mwili mkubwa wa kutisha, ila sura yake iliyo komaa na yenye upara ulio kolezwa mafuta hadi unameta meta, ndivyo vilivyo mfanya Eddy ahofie kidogo. Ili kupoteza hofu hiyo ikambidi Eddy ashushe pumzi nyingi na kujiweka sawa huku akinyoosha nyoosha viungo vyake.
Muendesha shuhuli akatoka uwanjani na kuwaacha Eddy na mjapani huyo aliye komaa sana akionekana ni mpambanaji wa kipindi kirefu cha nyuma. Refarii akasimama katikati yao, akawapa sheria zinazo takiwa kufwatwa, alipo hakikisha kila mmoja ameelewa sheria hizo. Akaanzisha mpambano.
Young Po akaanza kuruka ruka huku akiichezesha miguu yake kwa kasi, jambo lililo mfanya Eddy kutazama miguu hiyo inavyo kwenda, kwani hakujua ni muda gani, mpinzani wake huyo atarusha teke. Kufumba na kufumbua Eddy akajikuta akiwa ameanguka chini, hakuelewa hata teke hilo la kifuani amepigwa muda gani.
Eddy akanyanyuka kwa haraka na kupanga mashambulizi, akarusha ngumi kadhaa baadhi zikampata Young Po ila baadhi alizikwepa. Yoong Po hakuwa nyuma, na yeye akaendelea kutupa mashambulizi ya kustukia kwani tayari alisha weza kumsoma Eddy kupitia mikanda ya video aliyo cheza jana. Alimgundua kwamba black Shadow ni mwepesi sana katika kukwepa, kurusha ngumi na mateke.
Pambano likazidi kufaana, watu walizidi kushangilia kila pale mmoja kati ya wapiganaji alivyorusha makonde kwa mwenzake.
Kila mmoja wa mashabiki hadi inatimu robo saa, hakuweza kujua mshindi ni nani kwani wapiganaji hao walijitahidi kila mmoja kufanya awezalo kuhakikisha kwamba anajibu makonde ya mwenzake.
Jasho likazidi kuwatirika wapiganaji, hata Shamsa mwenyewe, japo amekaakatika sehemu ambayo ina kiyoyozi cha kutosha ila naye jasho lilimwagika kila alipo shuhudia black shadow anapigwa.
Shamsa akajikuta akiaanza kuingiwa na furaha moyoni mwake baada ya kuanza kuona black shadow anamzidi Young Po. Si Shamsa pekee bali hata mashabiki wa black shadow nao walianza kumshangilia. Mzee Godwin na John nao hawakuwa nyuma kumshangilia mpiganaji huyo waliye muhitaji kwa udi na uvumba. Yong Po alipigwa ngumi moja takatifu ya shingoni iliyo muangusha chini na kulala kifudi fudi.
Uwanja mzima ukanyanyuka kwa kushangilia, refarii akamsogelea Yong Po. Akainama na kumuuliza kama ana weza kuendelea na pambano.
“Nipatie”
Young Po alizungumza kwa sauti ya tabu, kwa siri kubwa refa rii, akatoa kidoge kimoja cha kuongeza nguvu, akampatia Young Po, bila mtu kuona, Young Poul akakimeza, huku akiendelea kulala chini kama mtu aliye poteza fahamu. Refa akasimama na kuanza kuhesabu moja, mbili hadi alipo fika nane Young Pu akasimama wima. Kila mtu akashangaa, kumuona Yong Po amesimama. Eddy aliye anza kujawa na furaha akiamini kwamba amemshinda mpiganaji mwenzake, furaha hiyo ikakata, akabaki akiwa ameshangaa.
Refarii akaruhusu pambano kuendelea, Eddy akamsogelea Yong Po na kumtandika makonde kadhaa ya nguvu, ila Young Po aliyumba kidogo na kukaa sawa. Yong Po akaanza kurusha makonde ambayo kila Eddy alipo jaribu kuyazudia yalimshinda nguvu. Ngumi nyingi zilitua kifuani mwa Eddy, akaanguka chini mzima mzima huku akimwaga damu mdomoni mwake.
Shamsa alisimama huku akiwa amelitoa jicho, la kuto kuamini anacho kiona. Kila Eddy alipo jaribu kusimama, alijikuta akianguka chini. Young Po hakuishia hapo, akamsogelea Eddy karibu, akamtandika teke moja la mbavu lililo mfanya Eddy kutoa ukelele mkali wa maumivu. Young Po akamkalia Eddy mgongoni na kuanza kumshindilia ngumi za mbavu kwa sehemu aliyo mpiga teke. Eddy akaendelea kuugulia kwa maumivu huku damu zikimwagika mdomoni mwake.
Young Po akazidisha ngumi, nyingi, akaona haitoshi akampiga Eddy kabari ya shingo, huku mkono wake mmoja ukianza kulivuta maski la Eddy ili amvue ili sura ya black shadow ionekane kwa kila mtu, kwani ni watu wengi hawamfahamu black shadow sura yake jinsi inavyo onekana.
SORRY MADAM (50) (Destination of my enemies)
Eddy hakukubali hata kidogo kwa kinyago chake kiweze kuvuliwa usoni mwake, ni bora afe ila si kinyago chake kuweza kuvuka. Akaanza kuminyana na Young Po kuhakikisha kwamba hamvui kinyago, japo kabala inaendelea kumpotezea nguvu na pumzi ila akazidi kujitahidi kuhakikisha kwamba kinyago hakivuki.
Young Po akabadilisha zaoezi la kumvua kinyago Eddy, ila alicho kifanya ni kuzidi kumminya kabari, macho yakazidi kumtoka Eddy. Damu zikazidi kumchuruzika pembezoni mwa mdomo wake. Hali ikazidi kuwa mbaya kwa upande wake. Kila shabiki wa black shadow akajikuta akiwa katika mshangao wa aina yake. Wapo walio shika vichwa vyao, wapo walio shika midomo. Wapo walio yatoa macho yao wakiwa hawaamini kwamba black shadow anakwenda kuuawa na Yong Po. Kila anaye ifahamu historia ya Young Po, aliweza kuutambua ukatili wake. Wamama wengi na mabinti walijikuta wakimwagikwa na machozi.
Refarii alipo muona black shadow ametulia kabisa tuli huku akiwa ameyafumba macho yake akapiga magoti kwa haraka na kuanza kuunyanyua mkono wa black shadow juu. Mkono ukarudi chini, akaunyanyua kwa mara ya pili ya tatu, mkono ukarudi chini.
Akaanza kuhesabu moja kuelekea kumi.
‘Eddy, Eddy, Eddy’
Sauti ya Phidaya ilianza kusikika masikioni mwake, kila alipo jaribu kuyafumbua macho yake kutazama ni wapi alipo Phidaya ila hakuweza kumuona. Mwanga mkali mweupe, ukampiga machoni mwake. Akamshuhudia Junio akiwa amesimama mbele yake amevalia mavazi meupe yanayo ng’aa, mgongoni mwake akiwa na mbawa mbili nyeupe na kubwa.
‘Baba bado muda wako. Pambana. Simamaaaaa upiganeee’
SSauti kali ya Junio, iliyo jaa hali ya kama mingurumo ya radi iliyo na mwangwi ndani yake, vikamfanya Eddy kustuka.
“Tis………”
Refa rii hakuimalizia sentensi yake, mara baada ya kumuona Eddy amestuka na kufumbua macho yake. Wachukua video camera, walijitahidi kuivuta sura ya Eddy karibu, watu wanao tizama pambano hilo kwenye tv kubwa iliyopo ndani ya ukumbi na televishion wakajikuta wakianza kushusha pumzi. Eddy kwa haraka akaipeleka mikono yake yote miwili, shingoni mwake, akaushika mkono wa Young Po, akanza kuutoa tararibu huku akijitahidi kujigeuza kutoka chini, ili asimame.
Ukumbi umzima ukasimama kwa kushangilia, macho yakamtoka Young Po. Hakuamini kwamba kabala yake ndio inaanza kutolewa taratibu taratibu. Shamsa akajikuta akimkumbatia Sa Yoo, na kuanza kumwagikwa na machozi ya furaha.
Mzee Godwin akajikuta akinyanyuka kwenye kiti alicho kaa na kunza kupiga makofi. John naye akajikuta akimuomba mpambe wake amfute machozi ya furaha yanayo mwagika.
Eddy akafanikiwa kuichomoa kabari hiyo, mkono huo huo wa Young Po uliokuwa umemkaba, akauvuta vizuri alipo hakikisha kwamba amekumata kisawa sawa, kwa kutumia goti lake la mguu wa kuliia, akaubamiza mkono huo, mithili ya mtu anaye vunya vipande vya mua virefu, vilivyo ungana. Mkono huo ilio komaa mifupa yake, ukafanikiwa kuvunjika. Young Po, akaruka na kuanguka chini huku akiwa ameushikilia mkono wake ulio vunjika, na kiwiliwili cha mbele cha mkono huo kikiwa kinaning’inia.
Refa akamsogelea Young Po akamuuliza kama anaweza kuendelea na shindano. Akatingisha kichwa kwamba hawezi kuendelea. Refa akaruhusu kengele ya ushindi igongwe na mpambano ukawa umemalizika. Ukumbi mzima ukafura kwa kelele za kushangilia. Hata wale ambao ni mashabiki wa Young Po nao wakahamia kwa black Shadow. Fataki nyingi zinazo mwaga karatasi nyinginyingi zikaanza kupigwa hewani, ulingo mzima ukatawaliwa na mvua ya vikaratasi.
Eddy akatabasamu huku akiwapungia mashabiki mkono kushoto huku mkono wa kulia ukiwa umeshika eneo ambalo mbavu zake zinauma. Maumivu makali ya mbavu, yakamfanya Eddy kuanguka gafla uwanjani. Madaktari ambao wanamuhudumia Young Po, baadhi wakamuwahi Black Shadow. Kila daktari aliye mgusa black Shadow kwenye kifua chake akajikuta akishtuka kwani, mapigo ya moyo hayafanyi kazi kabisa.
Heka heka za kumuwahisha hospitalini black shadow zikaanza, kila shabaki akawa na hamu ya kujua ni kitu gani kimepata black shadow. Machela ikaletwa ulingoni, akawekwa vizuri, akawekewa kifaa cha kumsaidia kupumua. Madaktari wakaanza kumtoa black shadow ukumbini. Mashabiki wakapiga makofi wakionekana kumuheshimu black shadow, aliye poteza fahamu.
Akaingizwa kwenye gari ya wagonjwa na kuwahishwa hospitalini kwa matibabu zaidi. Shamsa na Sa Yoo wakaingia kwenye gari lao mara baada ya kutoka uwanjani kwa haraka na kuanza kulifukuzia gari la wagonjwa linapo elekea.
“Sa Yoo ongeza mwendo”
Shamsa alizungumza huku akijipangusa machozi usoni mwake. Sa Yoo akazidi kuongeza mwendo kwani anazitambua hisia za rafiki yake juu ya mpiganaji huyo.
Wakafanikiwa kufika katika hospitali ambayo walilishuhudia kwa mbali gari la wagonjwa likiingia.
Wakashuka kwa haraka na kuelekea mapokezi, wakakuta waandishi wa habari wachache wakiwa wanamalizia malizia kumpiga picha black shadow aliye ingizwa kwenye chumba maalumu cha X rays.
Waandishi wa habari walipo muona Shamsa na kugundua ni binti ambaye wanahisi ni mpenzi wa black shadow, wakamgeukia na kuanza kumpiga picha jinsi anavyo lia.
Kwa haraka Sa Yoo, akavua kikoti chake na kumfunika Shamsa kichwani ili waandishi wasiendelea kumpiga picha anavyo mwagikwa na machozi kisha akamtoa rafiki yake na kumpeleka katika chumba maalumu cha kusubiria majibu.
“Jikaze tu Shamsa atakuwa salama”
Sa Yoo alizungumza huku akikiweka kichwa cha Shamsa begeni mwake na kuendelea kumbembeleza aache kulia
***
Harakati za uchaguzi zikaanza kuendelea kuendelea katika nchi ya Tanzania. Vyama mbali mbali vikaendelea kujipanga jinsi gani wanaweza kuongoza maeneo mbali mbali kupitia viongozi wao ambao watawapitisha katika vikao vyao mbalimbali ambavyo wanapaswa kuvifanya. Chama cha TSD(Tanzania Society Development), kinacho ongozwa na mwenyekiti wake Raisi Praygod Makuya. Kikajikuta kikiwa katika wakati mgumu sana baada ya mwenyekiti wake kukataa kuendelea kuongoza muhula unao fwata kwa madai ya kumuuguza mke wake ambaye haijulikani ni lini anaweza kuamka na akafariki.
Wazee wa chama na wenyeviti wa chama wa mikoa wakakutana katika ukumbi wa hoteli kubwa ya Serena kufanya mkutano wa kumuomba mwenyekiti wao aweze kukubali kugombania tena kwa maana wananchi bado wanamkubali sana, kwani kwa miaka yake mitano aliyo kuwa madarakani nchi ya Tanzania imeweza kupiga hatua katika sekta nyingi sana, japo kuwa kuna mapungufu machache yaliyo jitokeza katika kipindi chake ikiwemo ujambazi, ugaidi na mambo mengi mabaya.
“Kusema kweli, niliyo yafanya nimeyafanya kwa msaada wenu ninyi. Ila kwa sasa akili yangu haipo sawa kabisa katika kuendelea na uongozi. Tumsimamisheni mtu mwengine basi aweze kugombania uraisi”
Raisi Praygod alizungumza huku akiwatazama wanachama wezake walio jawa na sura za huzuni.
“Ila muheshimiwa wewe ndio mtu ambaye unafaa, kusimama katika chama. Hatukuwa na mawazo ya kumfikiria mtu mwengine kusimama kwenye chama kugombania nafasi hii”
“Makamu wangu si yupo?”
“Muheshimiwa tunamuheshimu makamu wako wa raisi, ila kumbuka yule alikuwa ni chaguo lako na si chaguo la wananchi ukisema kwamba tumsimamishe mtu mwengine, chama hiki kitakufa katika dira ya siasa”
Wakaendelea kumbembeleza raisi Praygod Makuya hadi akakubaliana nao kusimama tena katika muhula mwengine wa kugombania uraisi. Wanachama wezake wakajikuta wakijawa na furaha mioyoni mwao. Ila raisi Praygod hakuwa na furaha sana moyoni mwake kwani mke wake hali yake bado inaendelea vilevile. Madaktari bingwa kutoka nchi mbalimbali kubwa duniani. Waliweza kuingia ndani ya Tanzania kwa lengo la kumtibu Rahab, ila mbinu zao za kumtibu hazikuzaa matunda kwani hali ya Rahab haikuweza kubadilika jambo lililo zidi kuwachanganya sana madaktari.
***
Chama pinzani cha TDPP(Tanzania Democras People Party), hadi wakati huu hakikuwa na mgombea wa uraisi. Chama hicho kilicho jipatia umaarufu mkubwa kwa wananchi wa wafuasi wengi, bado kilijikuta kikiendelea kumsikilizia mgombea atakaye simamishwa na chama tawala cha TSD. Chama hicho kikajikuta kikijipatia fedha nyingi kutoka kwa wadhamini wanadada walio jitambulisha kwamba wao ni wafanya biashara kutoka Marekani. Japo wao ni watanzania ila waliwaomba viongozi wa TDPP, kukubali msaada wao lengo lao kubwa ni kuhakikisha kwamba wakakitoa chama tawala madarakani.
Manka akiwa ndio kiongozi wa wezake, wakiwa ndani ya mkutano wa chama cha TDPP, wakatoa mchango wa bilioni tano za kimarekani, ili kukiwezesha chama hicho kuweza kupambana katika kukitoa chama tawala madarakani.
Ukumbi mzima ukalipuka kwa furaha, wanachama na viongozi wao wakajikuta wakishangilia kwa furaha, kwani ni msaada wa pesa nyingi sana. Hapakuwa na aliye weza kutambua ni nini mpango wa mabinti hao ambao wameungana nao na kuwa ni kitu kimoja
***
Madaktari wakagundua kwamba black Shadow amevunjika mbavu mbili, wakamtoa ndani ya chumba cha kupigia X rays na kumuwahisha katika chumba cha Oparesheni. Sabogo na wapambe wake tayari wakawa wamesha fika katika hospitali hiyo na kuendelea kusikilizia kitu kinacho endelea, japo upande mmoja wana furaha ya ushindi mkubwa walio upata, ila kwa upande mwengine wamepata huzuni kwani mpiganaji wao yupo katika hali mbaya.
Kitu kilicho muumiza kichwa Sabogo ni jinsi ya moja ya makubaliano yake na black shadow, ambayo hakupenda sura yake ionekane na mtu yoyote, mbaya zaidi anatafutwa ndani ya Japani nzima.
“Bosi sasa itakuwaje?”
Mmoja wa wapambe wa Sabogo alimuuliza bosi wake juu ya hilo.
“Inabidi nizungumze na daktari wa oparesheni”
“Sawa”
Kwa bahati nzuri kuna nesi alitoka kwenye chumba cha upasuaji, kwa haraka Sabogo akamsimamisha, ila akajikuta akiwa amemkodolea macho pasipo kuzungumza kitu cha aina yoyote. Uzuri wa nesi huyo, ulimfanya mpambe wa Sabogo, atambue kwamba bosi wake amepata udhaifu fulani kwa nesi huyo. Sabogo akastuka kidogo baada ya kugongwa bega kidogo na mpambe wake.
“Nakusikiliza kaka, nina haraka nahitaji kwenda nilipo agizwa”
“Ahaaa……aaha…a..Nilikua nasema, nasema eti, nakuomba usimtoe kinyago mgonjwa wetu”
“Kwa nini, inabidi tumtoe kinyago chake ili kuhakikisha kwamba mfumo mzima wa damu katika mwili wake unakwenda vizuri”
Macho ya Sabogo yakatua upande wa kushoto mwa kifua cha nesi huyo na kusoma jina lake, mapigo ya moyo yakazidi kumuenda mbio.
“Nesi Phidaya”
“Ndio nakusikiliza”
“Nakuomba sana musimtoe kinyago chake mpiganaji”
“Tutaangalia, naona muda hauniruhusu”
Nesi Phidaya akaondoka na kumuacha Sabogo akiwa amebaki amemkodolea nesi huyo macho hadi akapotelea kwenye kona na kushusha pumzi nyingi.
“Bosi mbona kama unamshangaa huyu nesi umependa nini?”
“Hapana kama ninamfahamu?”
“Una mfahamu!!!”
“Ndio nimesha wahi kumuona”
“Kumuona wapi?”
Sabogo akasogea pembeni kwenye viti vya plastiki vilivyo jengewa kama benchi wakakaa na mpambe wake ambaye ndio msiri mkubwa na mshauri wake kwa miaka mingi.
“Kuna siku black shadow, alinisimulia historia yake ya nyuma”
“Historia gani?”
“Kuhusiana na ndoa yake pamoja na familia yake ambayo ilisha toweka duniani. Ila kitu kinacho nishangaza ni huyo msiachana. Anafanana sana na mke wa Eddy”
“Eddy!!! EDDY ndio nani?”
Sabogo akajikuta akipata kigugumizi kwani moja ya mambo ambayo black shadow alimueleza ni juu ya jina lake halisi na hakulihitaji jina lake hilo mtu kulifahamu. Sabogo akakiinua kicha chake chenye mawazo mengi, akastuka kuona macho yake yamegongana na nesi Phidaya ambaye amesimama sekunde kadhaa akiwasikiliza mazungumzo yao.
“Unamfahamu Eddy wewe?”
Nesi Phidaya alimuuliza Sabogo aliye baki akimtumbulia macho asijue ni nini azungumze.
==>ITAENDELEA...
Usikose kufuatilia sehemu inayofuata kupitia ubuyublog.com
Usikose kufuatilia sehemu inayofuata kupitia ubuyublog.com
Post your Comment