ILIPOISHIA
“Kuhusiana na ndoa yake pamoja na familia yake ambayo ilisha toweka duniani. Ila kitu kinacho nishangaza ni huyo msiachana. Anafanana sana na mke wa Eddy”
“Eddy!!! EDDY ndio nani?”
Sabogo akajikuta akipata kigugumizi kwani moja ya mambo ambayo black shadow alimueleza ni juu ya jina lake halisi na hakulihitaji jina lake hilo mtu kulifahamu. Sabogo akakiinua kicha chake chenye mawazo mengi, akastuka kuona macho yake yamegongana na nesi Phidaya ambaye amesimama sekunde kadhaa akiwasikiliza mazungumzo yao.
“Unamfahamu Eddy wewe?”
Nesi Phidaya alimuuliza Sabogo aliye baki akimtumbulia macho asijue ni nini azungumze.
ENDELEA
Sabogo akatingisha kichwa akionekana kukataa kwamba amfahamu Eddy.
“Eddy ninaye mzungumza ni rafiki yangu ambaye nilisoma naye”
Sabogo alidanganya, Phidaya akamtazama kwa muda Sabogo kisha akandoka pasipo kuzungumza kitu chochote.
“Bosi”
Mpambe wa Sabogo alimuita bosi wake aliye onekana kuwa na wasiwasi kidogo.
“Nini?”
“Huyo Eddy ni nani?”
“Ehee tuachane na hizo story”
Sabogo alizungumza huku akiondoka kuelekea kwenye chumba cha mapumziko, akiwa anafikiria ni kitu gani ambacho kitatokea pale black shadow atakapo onekana sura yake.
Daktari mmoja kwa kutumia mkasi akaanza kuzichana nguo za Black Shadow ambazo zimembana sana mwilini mwak. Alipo maliza kuzichana suruali akafwatia nguo ya juu. Nesi Phidaya akaingia akiwa na kiboksi kidogo alichyo agizwa na daktari mkuu wa opareshini ambaye ni mume wake bwana Ranjiti.
“Mbona umechelewa wakati hali ya mgonjwa si nzuri?”
Alizungumza bwana Ranjiti huku akianza kuupitisha mkasi wake kwenye mikanda ya kinyago alicho vaa Black Mask.
“Samahani dokta”
Nesi Phidaya alizungumza huku akikiweka kiboksi hicho cha dawa kwenye sinia kubwa lililo jaa mikasi na visu visogo vidogo. Kabla hajamalizia kukata mikanda miwili ili kuifunua sura ya black Mask, nesi Phidaya akamshika mumewe mkono hadi madaktari wengine wawili wakashangaa.
“Vipi?”
“Meneja wa huyu mpiganaji ameniomba tusimvue kinyago chake?”
“Kwa nini?”
“Hakunieleza ni kwa nini, ila amenisisitiza kwamba tusimvue”
Bwana Ranjiti, akashusha pumzi kidogo huku akimtazama mke wake machoni, kutokana anamuamini na kumpenda sana mke wake kuliko kitu chochote, akalisikiliza ombi la mkewe. Wakaanza kazi ya kuchana sehemu ya mbavu za Black Shadow, ambazo zimevunjika. Kazi ya Phidaya ikawa ni kuwakabidhi madaktari kila wanacho kihitaji katika kazi hiyo ya upasuaji.
Oparesheni ikachukua takribani masaa manee hadi kumalizika. Dokta Ranjiti na mwenzake mmoja wakamtoa Eddy katika chumba cha upasuaji wakimuacha Phidaya na daktari mwengine wakisafisha safisha vifaa na chumba kwa ujumla.
Waandishi wa habari ambao wameweka kambi wakisubiria kupata ripoti ya hali ya Black Shadow. Wakaanza kumpiga picha akiwa anapelekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi. Kitanda cha matairi alicho lazwa Black Shadow kikaendelea kusukumwa taratibu na msadizidi wa dokta Ranjiti huku, dokta Ranjiti na yeye akiwa mbele akikivuta kitanda hicho na kuwaomba waandishi wa habari kupisha njia. Sa Yoo na Shamsa walipo sikia kwamba Black Shadow ametolewa katika chumba cha upasuaji, wakakimbilia hadi kwenye chumba walicho ambiwa kwamba Black Shadow amelazwa.
Kwa bahati mbaya wakakuta tayari Black Shadow ameingizwa ndani ya chumba hicho ambacho haruhusiwi mtu wa aina yoyote kuingia pasipi idhini maalumu ya daktari.
“Inabidi twende nyumbani”
Sa Yoo alizungumza huku akipiga usingizi kwani ni majira ya saa kumi na moja alifajiri.
“Wewe nenda siwezi kuondoka hapa hospitalini”
“Kwa nini sasa, wakati unasikia hali ya mgonjwa inaendelea vizuri?”
“Wewe nenda mimi nitabaki tu hapa”
“Shamsa twenda nyumbani japo mara moja, tukaoge, kisha nakuahidi rafiki yangu tutarudi tena hapa”
Sa Yoo akaendelea kumbembeleza Shamsa anaye onekana kuchanganyikiwa na mapenzi mazito juu ya Black Shadow, Shamsa akakubaliana na Sa Yoo kuondoka na baada ya lisaa limoja watarejea katika hospitali hiyo, ili tu aweze kumuona Black Shadow.
Nesi Phidaya baada ya kumaliza kufanya usafi katika chumba cha upasuaji, akaelekea ofisini kwake ambapo akabadilisha mavazi yake ya kazi, akapitia ofisini kwa mume wake akamuaga kisha yeye akaelekea nyumbani, kujipumzisha akisubiria kuingia tena hospitali usiku. Phidaya moja kwa moja akelekea chumbani kwake, akaingia bafuni na kuoga kisha akarudi na kuketi kwenye sofa lililomo ndani ya chumba chake.
“Mimi ni nani?”
Hilo ndilo swali ambalo siku zote linamuumiza kichwa Phidaya, kila alipo jaribu kuvuta kumbukumbu zake za nyuma hakuna kitu ambacho anakikumbuka. Ila kitu alicho ambiwa na mume wake kwamba yeye ni Phidaya, ndio jina lake halisi. Huku jina la baba yake likiwa ni Eddy.
“Phidaya Eddy”
Aliendelea kujiuliza swali hilo, akasimama na kuanza kutembea hadi kwenye kabati kubwa, akatoa albamu yenye picha zaidi ya mia tano. Akaanza kuzitazama moja baada ya nyingine. Picha zake za harusi na bwana Ranjiti, zilimfariji sana kila alipo zitazama. Akazidi kujiona ni mwanamke wa kipekee na mwenye bahati kubwa sana kwenye maisha yake kutokana na kuolewa na daktari maarufu nchini Japan na mwenye hospitali yake inayo tibu watu maarufu ndani na nje ya Japani.
Uhodari wa mume wake katika swala zima la upasuaji lilimfanya azidi kumpenda mume wake huyo japo kiumri mume wake amempita miaka kumi na tano. Akaibusu picha moja ya mume wake na kuikumbatia albamu nzima kifuani mwake, taratibu akajitupa kitandani na kujilaza.
***
Alfajiri na mapema majira ya saa moja asubuhi, Mzee Godwin akiwa na John pamoja na walinzi wake, wakakutana na Sabogo meneja wa Black Shadow, kwenye moja ya ofisi ndogo walio ichukua katika hoteli waliyo fikizia.
“Hali ya mgonjwa wako inaendeleaje?”
Mzee Godwin aliuliza huku akiwa amemkodolea macho Sabogo.
“Madaktari wamemaliza upasuaji na anaendelea vizuri”
“Sawa. Tunaweza kumuona?”
“Hapana, kutokana bado hajarudisha fahamu zake hakuna mtu ambaye ataruhusiwa kumuona”
“Ok, lengo kubwa la sisi kuja hapa Japan ilikuwa ni kuonana na yeye. Kutokana hali yake sio nzuri basi tutaondoka na kurudi America kisha baada ya siku kadhaa basi tutarejea kuonana naye kwa maana tunahitaji kuzungumza naye ana kwa ana”
“Hilo halina tatizo, ila kabla ya yote ninahitaji kufahamu kwamba nyinyi ni kina nani?”
“Sisi ni wafanya biashara kutoka Marekani, na pia ni watengenezaji wa filamu kwa hiyo tulihitaji kuzungumza naye kwa maswala ya uigizaji”
John alimuongopea Sabog, ambaye bado aliendelea kuwa na wasiwasi mwingi moyoni mwake huku akiwatazama wafanya biashara hao walio muita asubuhi yote.
“Ahaaa, kama ni hivyo nitahitaji kuzungumza naye mimi mwenyewe na atakapo kubaliana na ombi lenu basi nitawapigia simu kuja kukutana naye”
“Sawa, tutakuachia namba za simu kwa mawasiliano zaidi”
“Sawa”
Mpambe mmoja wa mzee Godwin akatoa kikadi kidogo na kumkabidhi Sabogo, aliye kipokea akakisoma vizuri kisha akikitumbukiza mfukoni mwake. Kabla hajaondoka Mzee Godwin akaomba wapige picha za ukumbusho na Sabogo aliye kubaliana na ombi hilo. Kisha naye Sabogo akatoa simu yake na kumpa mmoja wa wapambe wa mzee Godwin aliye wapiga picha kadhaa, akachuku simu yake, wakaagana na kuondoka zke.
Hapakuwa na muda mwengine wa kupoteza ndani ya Japan, mzee Godwin na John wakiwa na wapambe wao wakaelekea uwanja wa ndege wakaondoka kurudi zao bara la Amerika.
***
Kwa siku mbili mfululizo Shamsa na Sa Yoo waliendelea kusubiri kuruhusiwa kuweza kumuona Black Shadow ambaye, madaktari waliendelea kuwazuia watu wasiweze kuingia kwenye chumba hicho kwani bado hali ya mgonjwa ni mbaya. Mashabiki wengi wana mshangilia Black Shadow walijitokeza nje ya hospitali hiyo wakiwa na maua pamoja na picha kubwa ya Black Shadow, iliyo wekwa kwenye moja ya bustani katika hospitali hiyo, wakifanya maombi ya kumuombea mpiganaji huyo kuweza kupona haraka.
Shamsa na Sa Yoo nao waliungana na mashabiki hao kukesha nao katika bustani hiyo, kila watu wakiomba kwa dini yao ili mradi Mungu aweze kumponya Black Shadow ambaye hadi sasa hivi hakuna aliye muona sura yake.
Viwanda kadhaa vya nguo ndani ya Japani, vilisha anza kutegeneza nguo nyeusi zinazo fanana na Black Shadow. Nguo hizo zilizo tokea kupendwa na watu wengi ziliuzika kwa gharama kubwa, ila wananchi walizidi kuzigombani, ili mradi tu mtu azinunue na kuonekana anafanana na mpiganaji huyo aliye tokea kutingisha Japani nzima kwa umaarufu wake.
Macho ya Phidaya yakaendelea kutazama tazama kupitia kwenye dirisha kubwa la ofisi yake iliyopo gorofa ya pili kutoka chini, watu wengi walio jitokeza kwenye bustani ya hospitali hiyo wakiweka maua mengi kwenye picha kubwa ya Black Shadow.
“Huyu mpiganaji anapendwa sana ehee?”
Alijiuliza Phidaya huku akiendelea kuwatazama wananchi hao, wakubwa kwa watoto. Wababa kwa wamama. Mlango wa ofisini kwake ukafunguliwa na kumlazimu kugeuka akamuona mume wake akiingia huku sura yake ikiwa imetawaliwa na furaha sana.
“Kumbe bado hujaondoka tu mke wangu?”
“Ndio baby, vipi mbona una furaha sana”
“Yaani mgonjwa wetu amezidi kuiongezea umaarufu hospitali yetu. Nimepewa taarifa kwama kesho raisi anakuja kumtembelea mgonjwa”
“Weeeeee sema kweli mume wangu?”
“Haki ya Mungu, yaani sikuwahi kufikiria kwamba ipo siku raisi atakuja kutembelea hapa”
Bwana Ranjiti akamkumbatia mke wake na wote wakajikuta wakipongezana kwa furaha, kwani ugeni wa kesho ni mkubwa sana.
“Ila vipi mgonjwa anaendeleaje?”
“Hali yake inazidi kunipa matumaini kwa maana leo ni tofauti na jana, na juzi”
“Ila si atazinduka?”
“Ndio atazinduka tu”
“Itabidi kabla ya kwenda nyumbani nikamuone”
“Hakuna tatizo.”
Bwana Ranjiti akalisogelea dirisha kubwa na kuwaangalia wananchi walio jiotokeza kwenye hospitali hiyo, waandishi wengi wa habari nao waliendelea kuchukua matukio na kuyarusha moja kwa moja kwenye vitu vyao vya televishion na redio. Bwana Ranjiti akajikuta akizidi kufarijika na kuona kwamba mchango wa mpiganaji wake umezidi kuipa umaarufu hospitali yake.
Phidaya akamuaga mume wake na kuelekea kwenye chumba cha wagonjwa mhututi(ICU). Akavaa mavazi maalumu ya kuingilia ndani ya chumba hicho. Akaingia na kuufunga mlango kwa ndani, taratibu akaanza kupiga hatua hadi kwenye kitanda kilicho zungukwa na mashine nyingi, huku kila moja ikiwa na kazi yake mwilini mwa Black Shadow.
Macho yake Phidaya, yakaanza kukichunguza kifua cha Black Shado, kilicho funikwa nusu kwa shuka zito, huku nusu iliyo baki ikiwa imewekwa vifaa maalumu vivili vinavyo msaidia mapigo yake ya moyo kwenda vizuri.
‘Kwa nini alikataa sura yake isionekane’
Phidaya alijiuliza huku akimkumbuka Sabogo, aliye msisitiza kwamba sura ya mpiganaji huyo haitakiwi kuonekana, Taratibu Phidaya akaanza kuupeleka mkono wake wa kulia katika kinyago cha Black Shadow kwa lengo la kukitoa ili aweze kumuona.
***
Viongozi wa chama cha upinzani cha TDPP(Tanzania Democras People Party), wakazidi kuwaamini Manka pamoja na wezake. Viongozi watano wa ngazi ya juu, akiwemo mwenye kiti wao bwana Kibwila.Wakawaalika katika halfa fupi ya chakula cha usiku katika Kilimanjaro Hoteli. Viongozi hao walio changanywa na wingi wa pewa walizo kabidhiwa na wafanya biashara hao wa kike, hawakuwa na hiyana walipo ambiwa kwamba wasifike na wake zao katika halfa hiyo waliyo alikwa kwani pia itakuwa ikizungumzia kuhusiana na maswala ya kichama na na ni jinsi gani wanavyo weza kukitoa chama tawala madarakani.
Chakula kilicho andaliwa na wapishi hodari katika hoteli hiyo, kilianza kutafunwa taratibu na viongozi hao pamoja na wafanya biashara Manka na wezake. Kila mmoja alijikuta akikisifia chakula hicho kwamba nikitamu na wengine wakiri kwamba hawakuwahi kukila chakula hicho tangu wazaliwe.
Furaha na vicheko vilizidi kutawala katikati yao, huku wakijadili mambo mengi yaliyo wahi kujitokeza katika chama hicho hadi kushindwa kuingia madarakani miaka mitano iliyo pita.
“Jamani natambua kwamba tunahitaji mgombea mwenye nguvu na atakaye weza kuchukua madaraka si kweli jamani?”
Fetty alizungumza huku akiwatazama viongozi hao.
“Ni kweli kabisa”
“Pia tunahitaji kiongozi anaye weza kupambana na kila jambo linalo tokea ndnai ya hii nchi, si kiongozi kama Praygod ambaye ameshindwa kupambana na ugaidi ulio sababisha maisha ya ndugu zetu wengi kupoteza maisha yao”
“Kweli kabisa”
“Basi sisi kama mukitupa ridhaa tutatawapa nyinyi mgombe ambaye ataweza kupambana na haya yote”
“Hakuna shida kabisa, kwa maana kama mgombea atakuwa ni kati ya sisi hapa hakuna tatizo”
Bwana Kibwila alizungumza huku akitabasamu tabasamu
“Hapana bwana Kibwila, mgombea ambaye tutamsimamisha kupitia chama chenu atakuwa ni huyu hapa”
Fetty akamkonyeza Anna aliye shika romoti ya Tv kubwa iliyomo ndani ya ukumbi huo. Viongozi wote macho yaliwatoka walipo iona picha ya Mzee Godwin, kwani kila mmoja anamtambau kwamba ni gaidi wa kupindukia na inakuwaje wamsimamishe kama mgombea uraisi wao.
***
Mkono ya Phidaya ikanza kutetemeka kila alipo karibia kukishika kinyango cha Black Shadow. Akaurudisha mkono wake nyuma huku akishusha pumzi nyingi. Mapigo ya moyo yakazidi kumuenda mbio kiasi cha kumfanya aogope.
‘Naogopa nini na mimi?’
Phidaya alijisemea kimoyo moyo. Akatoa woga moyoni mwake kisha akaupeleka kwa kasi mkono wake hadi kwenye kinyago cha Black Shadow, akaufungua mkanda wa pili, kisha akaumalizia mkanda wa tatu. Taratibu akaanza kukinyanyua kinyago cha Black Shadow, asiye jitambua kwa kupoteza fahamu, hadi kinyago hicho akakitenganisha na sura yake. Moyo wake ukampasuka baada ya kuiona sura ya Black Shadow. Hofu ikamtawala, macho yakamtoka huku akiwa amenata kama amegandishwa na sumanku, kwa mbali akaanza kuhisi haja ndogo ikianza kumwagika taratibu.
SORRY MADAM (52) (Destination of my enemies)
Kwa haraka Phidaya akakirudisha kinyago cha Black Shadow kama kilivyo kuwa, akaanza kutembea kwenda nje kwa vishindo. Kabla hata hajafika mlangoni, akasikia mashine moja ikipiga mlio, ikamlazimu kugeuka kwa haraka, macho yake yakatua kwenye mashine inayo hesabu mapigo ya moyo. Kwa kasi kubwa mapigo ya moyo ya Black Shadow yakawa yanashuka.
“Mungu wangu?”
Phidaya alizungumza huku akijaribu kukiminya kifua cha Black Shadow ili mapigo ya moyo yasishuke, haikuwa kazi rahisi kwake, ikamlazimu kuminya batani ya dharusa iliyo mtaarifu daktari mkuu ofisini kwake, kwamba chumba alicho lazwa Black Shadow kuna tatizo.
Haikupita hata dakika mbili Phidaya akasikia mlango ukigongwa kwa nje, kwa haraka akakimbilia kwenye mlango, wakaingia madaktari wawili akiwemo na mume.
“Kumetokea nini?”
“Mapigo yake ya muyo yamebadilika gafla”
“Washa mashine”
Dokta Ranjiti aliwaamrisha wezake, kwahara mashine ya umeme inayo tumika katika kupandishia mapigo ya moyo ikawashwa. Kwa haraka wakaanza kuigandamiza kifuani mwa Black Shadow, na kukifanya kifua chake kustuka. Zoezi hilo wakalifanya kwa dakika kadhaa pasipo kuchoka, hadi inatimu mara ya ishirini na tano, mapigo ya moy ya Black Shadow, yakarudi katika hali yake ya kawaidia, kila mmoja akajikuta akishusha pumzi ya wasiwasi.
Walipo hakikisha kwamba Black Shadow amerudi katika hali yake ya kawaidia, wote wakatoka ndani ya chumba, Phidaya na mume wake wakaelekea ofisini.
“Baby kuna kitu nataka kukuambia”
Phidaya alizungumza mara baada ya kukaa kwenye moja ya sofa lililopo ndani ya ofisi ya mume wake.
“Jamb……..”
Kabla Dokta Ranjiti hajamalizia sentesi yake simu yake ya mezani ikaita ikabidia achukue mkonga wa simu hiyo na kuiweka sikioni.
“Habari dokta Ranjiti”
Haikuwa ni sauti ngeni sana masikioni mwake. Dokta Ranjiti akamtazama mke wake kwa macho ya kuiba kisha akaiweka miwani yake sawa na kuendelea kumsikiliza mtu aliye mpigia simu.
“Unatatizo gani?”
“Ohooo tatizo, unajua ni nini tatizo langu. Nahitaji pesa, la sivyo nitamuambia kila kitu Phidaya mwanamke unaye jifanya kumpenda”
Sauti hiyo ya kike ilimfanya dokta Ranjiti kumwagika na kijijasho chembamba, hakuweza kuzungumza jambo lolote mbele ya Phidaya. Woga wake ulimfanya kuwa mtumwa wa siri kwa mtu anaye mpigia simu.
“Unahitaji kiasi gani?”
“Ohooo hayo sasa ndio maneno. Najua hospitali yako kwa sasa inakuingizia pesa nyingi sana. Nahitaji dola milini moja, uiingize kwenye akauti yangu ndani ya masaa kumi, la sivyo. Siri inakuwa dirisha”
Simu hiyo ikakatwa na kumuacha dokta Ranjiti akiwa katika hali ya mawazo, jambo hilo Phidaya alilitambua kwamba simu iliyo pigwa imemkosesha amani mume wake.
“Baby kuna tatizo?”
“Ahaa..ahaa hapana, nahitaji kwenda bank mara moja”
“Kufanyaje usiku huu?”
“Ahaaa tutazungumza nikirudi”
Dokta Ranjita alizungumza huku akivua koti lake jeupe na kuvaa koti lake la suti, akachukua funguo ya gari lake kwenye droo ya mezani mwake, akampiga busu la mdomoni Phiday kisha akaondoka na kumuacha mke wake akiwa hajazungumza kitu alicho kuwa amekusudia kuzungumza.
***
Macho ya Shamsa yakamshuhudia dokta Ranjiti akitembea kwa kasi akitoka katika mlango wa kuingilia hospitalini. Akamuwahi na kumsimamisha.
“Sahamani dokta, hali ya black shadow inaendeleaje?”
“Vizuri, ila samahani binti nina haraka nahitaji kuondoka kunasehemu nawahi”
“Lini atapona dokta?”
“Endeleeni kukesha na kumuombea, samahani nahitaji kuwahi binti”
Dokta Ranjiti hakuona sababu ya kuendelea kuzungumza na Shamsa, akaelekea kwa haraka kwenye maegesho ya magari, akaingia ndani ya gari lake na kuondoka kwa kasi hadi baadhi ya watu walikishangaa hicho kitendo.
Shamsa akatazama huku na kule, alipo ona hakuna mtu anaye mfwatilia, akaanza kutembea kwa haraka kuelekea ndani ya hospitali, moja kwa moja akaanza kuchunguza ni chumba gani wanacho badilishia nguo manesi.
Haikumchukua muda mwingi sana kukipata chumba hicho, akaingia na kukuta hakina mtu zaidi ya madroo mengi yaliyo jengwa vizui ndani ya chumba hicho na katika kila droo kuna mlango na juu yake ukiwa umeandikwa jina la nesi anaye husika na droo hiyo. Akaanza kuvuta kitasa cha droo moja baada ya nyengine, mbili za mwanzo akazikuta zikiwa zimefungwa, ila ya tatu akakuta ikiwa haijafungwa, akaifungua na kukuta magauni mawili ya nesi huyo mwenye jina la Si Ngii.
Akachomoa gauni moja na kulipimisha kwa urefu wa mwili wake, kwa bahati nzuri limeendana naye. Akazivua nguo zake alizo zivaa, akalivaa gauni hilo haraka haraka. Nywele zake ndefu alizo kuwa amezibana kwa nyuma, akazifungua na kuzimwaga kwa chini, kwa bahati nzuri ndani ya droo hiyo akaona miwani ya macho akaichukua na kuivaa.
Akazichukua nguo zake na kuzisokomeza ndani ya droo hiyo. Akaanza kutembea kueleka mlangoni mwa chumba hicho, kabla hajafika, mlango ukafunguliwa, akaingia nesi mmoja anaye onekana kuwa na haraka, hawakusemeshana kitu zaidi ya kupishana huku Shamsa kichwa chake akiwa amekielekeza chini.
Akaanza kutembea kwenye kordo ndefu, kuelekea katika chumba alicho lazwa Black Shadow. Hakutaka kuinyanyua sura yake juu, kwani alihofiwa kustukiwa, akazidi kupiga hatua za haraka hadi kwenye mlango wa kuingila katika chumba cha wangojwa mahututi. Akashika kitasa cha mlango huo taratibu akaanza kukishusha chini huku akitazama kuli na kushoto kwake. Akausukuma mlango na kuingia ndani, akaurudishia mlango huo, akageuka na kumtazama Black Shadow, akiwa amelala juu ya kitanda huku akiwa amezungukwa na mashine kadhaa. Akaanza kupiga hatua kuelekea kitandani, hata kabla hajakifikia kitanda milio mingi ya risasi ikaanza kusikika nje ya chumba hicho, huku ving’ora vya hatari vya hospitalini hapo vikianza kulia kwa nguvu jambo lililo mstua Shamsa na kumuogopesha sana.
***
Kitendo cha Young Po,kushindwa kutetea taji lake, kilizidi kumuumiza sana. Kwenye maisha yake hakuwahi kutarajia kwamba itakuja kutokea siku atakuja pigwa na mtu katika mapambano ya ulingoni. Hasira na chuki zikazidi kumpanda kila alipo utazama mkono wake ulio vunjwa na Black Shadow.
‘Lazima nifanye kitu’
Young Po alizungumza huku macho yake yakiwa kwenye Tv kubwa iliyomo ndani ya chumba alicho lazwa kwenye moja ya hospitali. Alikuwa akitazama taarifa, kwenye kitua cha Jtv, kilicho kuwa kikitangaza kwamba siku inayo fwata raisi wa nchi hiyo atakwenda kumtembelea Black Shadow, mpiganaji aliye tokea kupendwa na watu wengi. Wivu ukazidi kumtawala Young Po, kwa haraka akachukua simu yake iliyopo mezani, akaminya namba kadhaa kwenye simu, baada ya sekunde thelathini simu hiyo ikapokelewa.
“Njooni hospitaki sasa hivi”
Young Po akakata simu, baada ya robo saa, mwanaume mmoja na mwanamke mmoja wakaingia ndani ya chumba chake.
Akawapa maelekezo ambayo anahitaji yaweze kutekelezwa usiku huo. Vijana hao hawakua na swali kwani walimeelewa kazi ambayo wamepewa na bosi wao huyo. Wakatoka hospitalini moja kwa moja wakaelekea kwenye makao yao, ambapo, wakawaelekeza vijana wengine watatu ambao waliwaacha katika nyumba yao. Mpango wa kutafuta gari ya wagonjwa, ikaanza. Halikuchukua muda mrefu sana ndani ya lisaa gari ya wagonjwa ikaletwa kwenye nyumba yao.
Bunduki zao zilizo jaa risasi za kutosha wakaziweka ndani ya gari hilo, wkila mmoja akachomeka silaha ambayo alihisi kwamba itamsaidia katika kazi hiyo. Wakavalia mavazi ya udaktari, kisha safari ikaanza kuelekea katika hospitali aliyo lazwa Black Shadow.
***
Phidaya baada ya mume wake kuondoka, hakuona haja ya kuendelea kukaa kazini, akavua mavazi yake ya kazi na kuvaa mavazi aliyo kuja nayo asubuhi. Akilini mwake akawa anafikiria kuhusiana na donge nono ambalo polisi walilitangaza kwa mtu ambaye atatoa ushirikiano wa kukamatwa muhalifu ajulikanaye kwa jina la Eddy.
‘Lazima nipate pesa hizi’
Alijisemea Phidaya huku akidhamiria kuzipata pesa kwa kuwatarifu polisi kwamba mtu wanaye mtafuta ndio huyo Black Shadow aliye lazwa kwenye hospitali yao. Akaanza kutembea kwa haraka kuelekea kwenye maegesho ya magari, Akaingia kwenye gari lake aina ya Aud A4.
‘Hakuna haja ya Ranjiti kujua’
Phidaya alijisemea kimoyo moyo huku akiwasha gari lake na kuanza kuondoka, getini akapishana na gari ya wagonjwa ikiingia huku likiwa linapiga ving’ora. Hakutaka kulifwatilia sana kwa sababu wapo madaktari wengine ambao watashuhulika na mgonjwa huyo aliye letwa. Akaingia barabarani na kuanza kuongeza mwendo kasi wa gari lake kuelekea katika kituo kimoja cha polisi kilichopo karibu na hospitali yao.
Ikamchukua dakika kumi kufika katika kituo hicho, ika kabla hajasimamisha gari lake nje ya kituo hicho, gari zipatazo kumi za polisi zilianza kutoka kwenye kituo hicho kwa mwendo wa kasi.
“Mmmm kuna nini?”
Phidaya alizungumza huku akisimamisha gari lake pembeni akizipisha gari hizi za polisi zipite, zilipo malizika akaliegesha gari lake kwenye maegesho ya hapo kituo cha polisi. Akashuka, askari mmoja wa kike alipo muona Phidaya akamkimbilia hadi sehemu alipo.
“Madam upo salama?”
Askari huyo alizungumza huku akimshika mkono Phidaya.
“Ndio nipo salama kwani kuna tatizo gani?”
“Ina maana huna taarifa kwamba hospitalini kwako kuna uvamizi wa majambazi?”
“Nini…..!!!”
Phidaya akajikuta akimtumbulia macho askari huyo.
“Hizo gari zilizo toka hapo zinaelekea hospitalini kwako”
“Twende twende”
Phidaya alizungumza huku akikimbia kwenye gari lake, huku askari huyo akimfwata kwa nyuma, wakaingia kwenye gari na safari ya kurudi hospitalini ikaanza tena kwa mwendo wa kasi sana.
***
Majambazi hao walio agizwa na Young Po, wakasimamisha gari lao karibu kabisa na mlango wa kuingilia ndani ya hospitali, manesi wawili wakatoka na kuwapokea madaktari hao walio mleta mgonjwa mmoja aliye lazwa kwenye kitanda cha matairi wakaanza kumkimbiza ndani pasipo kufahamu kwamba hao si madaktari. Wakiwa katikati ya kordo, manesi wakastukia, mgonjwa wanaye msukuma kwenye hicho kitanda akinyanyuka huku akiwa na bastola mbili mkononi mwake.
Manesi hao katika kushangaa, mmoja wao akaona usalama wake ni bora akimbie, risasi kadhaa zikamuingia kwenye mwili wake. Milio hiyo ya risasi ikawastua watu wote walio kuwa ndani na nje ya hospitali. Watu walio kuja kumuombea Black Shadow, wote wakajikuta wakianza kutawanyika kila mmoja akijaribu kuiokoa roho yake. Baadhi ya walinzi wa hospitali wakakimbila kwenye eneo la tukio huku wakiwa na bunduki zao. Majibizano ya risasi baina ya walinzi na majambazi hao walio fika hospitalini kwa lengo la kumuua Black Shadow, yakazidi kupamba moto.
Shamsa akafungua mlango wa chumba alichopo, akachungulia nje, akashuhudia nesi mmoja akiwa amelala chini, damu zikiwa zinamwagika, watu walio valia kama madaktari wakazidi kuwashambulia walinzi wanao pambana nao. Mapigo ya moyo yakazidi kumuenda mbio Shamsa, hakujua afanye nini kwa wakati huo. Hata kabla hajafikiria kitu kingine, gafla mlango ukapigwa teke, akaingia msichana aliye valia nguo za kinesi, mkononi mwake akiwa ameshika bastola.
Shamsa hakuhitaji kufikiria mara mbili kwamba huyo ni nani, Akarusha teke moja lililo tua mkononi mwa msichana huyo wa kijapani. Bastola ikaanguka pembeni, macho makalia ya msichana huyo, yakampandisha Shamsa kuanzia chini hadi juu, msichana huyo akaanza kurusha mateke mazito yaliyo mfanya Shamsa kuanguka chini sakafuni. Msichana huyo akaanza kupiga hatua za kuifwata bastola yake ilipo anguka, hata kabla hajaichukua Shamsa akajirusha na kuwahi kumdaka mguu msichana huyo na kumuangusha chini.
Msichana huyo akarusha teke moja la ambalo Shamsa alilikwepa na kuvuta chini, wakaanza kubingirishana chini, huku kila mmoja akijitahidi kukaa juu ya mwenzake, ili amshushie makonde ya kutosha.
Mbiringishano huo, ukawapeleka hadi kwenye moja ya mashine, wakajigonga hapo na kuifanya mashine hiyo kuanza kuyumba yumba na mwisho ikaanguka chini. Binti huyo alipo muona Black Shadow akiwa kitandani akajaribu kusimama ili kufanya agizo alilo tumwa, ila hata kabla hajamgusa Black Shadow, Shamsa akamvuta na kumuweka chini, na kuendelea kumshindilia ngumi nyingi za uso.
***
Majira ya saa nane usiku, Raisi Praygod akiwa amejilaza kwenye sofa lililopo pembezoni mwa kitanda alicho lala Rahab, hafla akahisi mtikisiko kwenye kitanda cha Rahab, ikambidi kuyafumbua macho yake. Akamkuta Rahab akiwa anajibiringisha kitandani. Wasiwasi mwingi ukazidi kumtawala Raisi Praygod Makuya, akasimama kwa woga. Gafla Rahab akakaa kitako kitandani, akayafumbua macho yake huku akihema, jasho jingi likimwagika.
“Rahab”
Raisi Praygod alimuuita Rahab, huku akirudi rudi nyuma, Rahab aliendelea kumuangalia raisi Praygod pasipo kumsemesha kitu cha aina yoyote. Taratibu Rahab akaanza kushuka kitandani, akasimama wima na kuanza kumsogelea Raisi Praygod aliye anza kurudi nyuma, hadi akagota ukutana, Rahab akazidi kumsogelea taratibu huku akiendelea kumkazia macho.
***
Shamsa akazidi kumshindilia ngumi, msichana huyo ambaye naye alizidi kujitahidi kumzungusha Shamsa, hadi akafanikiwa kumuangusha chini, akamkalia Shamsa tumboni, na yeye akaanza kulipiza makonde ambayo Shamsa alipatia muda mchache ulio pita. Wakaanza kubiringishana tena wakiendelea sehemu ilipo angukia bastola. Binti huyo, anaye onekana amefuzu mazoezi mengi ya kupigana, akaendelea kumshushia ngumi zilizo changanyikana na vibao Shamsa, aliye iona bastola imelala pembezoni mwake.
Askari walio fika eneo la hospitali, wakaanza kuwatoa watu katika eneo la hospitali, huku wengine wakiizunguka hospitali kuhakikisha kwamba hakuna jambazi ambaye anatoka nje ya hospitali hiyo. Askari sita wakaingia ndani wakiwa na bunduki zao, walitembea kwa tahadhari hadi kwenye kordo ambapo waliwakuta walinzi wawili wa askari wakimpa huduma ya kwanza mwenzao aliye pigwa risasi. Majambazi wawili walipoteza maisha na kubaki wawili kwenye kodro, wakiwa wamejibanza.
Mashambulinzi yakaanza upya huku askari polisi wakishirikiana na walinzi wa hospitalini wakaendelea kuwashambulia majambazi hao walio jikuta wakizidiwa nguvu. Askari polisi wakazidi kusonga mbele, kwa bahati mbaya majambazi hao wakajikuta wakiishiwa na risasi. Hapakuwa na jambo jengine la kujitetea zaidi ya wao kujisalimisha kwa askari hao.
Askari hao wakawafunga pingu majambazi wote wawili, wakiwa wanawamalizia kuwafunga pingu, wakastushwa na mlio wa risasi ulio tokea kwenye chumba kilicho andikwa ICU.
Askari wawili wakavamia ndani ya chumba hicho, wakamkuta msichana mmoja akijizoa zoa kunyanyuka, huku akiwa amemuua nesi mwenzie. Aliye endelea kuvuja damu chini.
Askari hao wakamuamrisha nesi huyo muuaji kunyoosha mikono yake juu. Nesi huyo hakuwa na ubishi taratibu akanyanyua mikono yake juu, askari mmoja akamsogelea na kumfunga pingu kwa nyuma. Askari hao wakamtoa nesi huyo nje ya chumba wakamjumuisha na majambazi wengine wawili. Wakawatoa nje kabisa kwa ajili ya kuwapeleka kituoni. Shamsa akajikuta akistuka baada ya kumuona Phidaya akimfwata katika sehemu alipo shikiliwa na polisi.
“Hawa ndio majambazi eheee?”
Phidaya alizungumza kwa sauti ya ukali, askari mmoja akamuitikia, Phidaya bila hata kujiuliza mara mbili, akamzaba kofi Shamsa, aliye kuwa akimshangaa, pasipo kuamini kwamba huyo ni Phidaya au laa, kwa maana wamefanana kila kitu. Ilibidi baadhi ya askari wamzuie Phidaya asiendelea kuwashambulia majambazi hao walio ivamia hospitali yake.
==>ITAENDELEA...
Usikose kufuatilia sehemu inayofuata kupitia ubuyublog.com
Usikose kufuatilia sehemu inayofuata kupitia ubuyublog.com
Post your Comment