ILIPOISHIA
“Eddy…yu…..”
Sa Yoo hakumalizia sentensi yake kwa maana aliweza kumona Eddy akiwa amekumbatiwa na mwanamke wengine, tena mwanamke huyo akionekana kumpiga mabusu mfululizo kila sehemu ya uso wake. Madam Mery akafanikiwa kuona tukio hilo.
“Yupo wapi?”
Phidaya aliuliza, huku akitazama sehemu aliyo kuwa ameangalia Sa Yoo, Phidaya na Shamsa wote wakastuka kwa kumuona Eddy akiwa anadendeka na mwanamke mwengine, wote wawili kwa pamoja wakaanza kutembea kwa mwendo wa haraka kuelekea katika eno alilo simama Eddy na Agnes, wanao dendeka pasipo kujali wingi wa watu walio kuwa katika eneo hilo.
ENDELEA
Sa Yoo na Madam Mery wote kwa pamoja wakawawahi Phidaya na Shamsa ambao kwa pamoja wanaonekana kujawa na hasira ya kumuona Eddy akiwa anafanya uchafu huo mbele yao.
“Munatuzuia nini?”
Shamsa alizungumza kwa hasira huku akijaribu kutaka kumpita Sa Yoo aliye simama mbele yake.
“Munataka mufanye nini sasa?”
Sa Yoo aliwauliza kwa sauti ya juu hadi baadhi ya askari wakawatazama. Wanajeshi wanne walio valia vitambaa vilivyo andikwa MP, wakawafwata Shamsa na wezake walipo simama.
“Hamruhusiwi kuingia katika eneo hili”
Mwanjeshi mmoja alizungumza huku akiwa amewakazia macho Shamsa na Phidaya ambao wanaonekana kwamba ni vigego wanao taka kwennda katika eneo ambalo limesha zungushiwa utepe wa alama ya njao wenye maandishi meusi yaliyo andikwa ‘DANGER’
“Sisi tunataka kumuona Ed…..”
Shamsa alijikuta akiropoka ila kwa haraka Sa Yoo akawahi kumzimba mdomo.
“Waheshimiwa tumewaelewa, kidogo wezetu wamechanganyikiwa na hili tukio”
Madam Mery alizungumza huku akimshika mkono Phidaya, wakaondoka eneo hilo huku wakisindikiwa na wanajeshi hao wenye mitutu ya bunduki. Mara kwa mara Shamsa aligeuka nyuma na kumuangalia Eddy anaye onekana kusahau kabisa kama ana mke wake.
“Ndio mumefanya nini sasa?”
Shamsa alizungumza kwa kufoka huku akimtazama Sa Yoo kwa macho ya hasira, Sa Yoo hakulijali hilo zaidi ya kutafuta sehemu na kukaa, kwani wote hawakujua ni nini kilicho tokea hadi wakamuona Eddy akiangua kilio akiwa katika eneo hilo.
“Tunatakiwa kujua ni kitu gani kinacho endelea, na si muda wa kakaa na kugombana”
“Madam Mery nakuheshimu sana, ila wewe umekuwa chanzo cha Eddy kuwa na yule mwanamke na bado munaendelea kumtetea tetea, inabidi yule mwanamke tumshike tumbamize hadi akome”
Shamsa alizidi kuzingumza kwa hasira, madam Mery hakumjibu kitu cha aina yoyote kwa maana anatambua hiyo ni hasira na baada ya muda fulani itakwenda kupotea. Phidaya alikaa kimya huku akiendelea kuumia kimoyo moyo. Picha ya mwanamke ambaye yupo na Eddy, mara kadhaa ikawa inamrudia kichwani mwake. Hakuweza kuyazuia machozi yake kwa maana maumivu aliyo nayo ni makali sana japo anatambua mume wake yupo hapo kwa kazi fulani.
‘Inakuwaje wapigane mabusu hadharani?’
Hilo ni swali alilo liwaza Phidaya mara kadhaa kichwani mwake, akijaribu kutazama ndani kama anaweza kumuona Eddy na huyo mwake, ila hakuweza kuwaona kutokana na wingi wa watu wanao zidi kumiminika kutoka maeneo mbalimbali kujua kushuhudia tukio hilo la kutisha.
***
“Erickson haupo sawa mume wangu madaktari wamekuja kukuchukua wakuwahishe hospitalini”
“Nipo sawa Agnes”
“No haupo sawa, madaktari mchukueni”
Agnes aliwaambia madaktari ambao wamefika sehemu hiyo kwa ajili ya kuwachukua majeruhi kama Eddy. Eddy akatazama pende zote haswa sehemu ulipo mwili wa raisi Praygod, ili utambulisho wake usijulikane, taratibu akaondoka na kuongozana na madaktari huku Agnes akifwata kwa nyuma. Eddy akalala kwenye kitanda kidogo cha wagonjwa, kikanyanyuliwa na kuingizwa kwenye gari ya wagonjwa. Madaktari hao wawili wakaingia kwenye gari hilo huku wakifwatiwa na Agnes aliye kaa karibu sana na Eddy.
Wakafika katika hospitali ya Muhimbili. Eddy akashushwa kwenye kitanda na moja kwa moja akapelekwa kwenye chumba cha kupatiwa huduma ya kwanza.
“Dokta mimi nipo salama, naomba niondoke zangu”
Eddy alizungumza huku akikaa kwenye kitanda hicho, daktari akabaki amemtumbulia macho. Eddy akasimama wima, akapiga hatua hadi mlangoni, akafungua na kuondoka zake na kumuacha daktari akiwa bado ameduwaa.
“Honey vipi mbona umetoka?”
“Nipo salama”
“Kweli mpenzi wangu?”
“Ndio, nahitaji kuelekea nyumbani muda huu”
“Ok basi twende pamoja nikapafahamu kwako”
“Hapana tutakwenda siku nyingine kwa leo ninakumba niende peke yangu na sinto hitaji unifwate”
Eddy alizungumza kwa sauti yenye msisitizo hadi Agnes mwenyewe akajikuta akimuogopa. Eddy ahakutaka kupoteza muda. Moja kwa moja akatoka eneo la hospitali huku Agnes akimfwata kwa nyuma. Eddy bila yakujali, akamuita bodaboda mmoja wa pikipiki, akapanda na kuondoka.
“Nipeleke bahari beack hoteli”
“Sawa”
Dereva bodaboda akaondoa pikipiki na kumuacha Agnes akiwa anashangaa shangaa asijua ni nini cha kufanya.
***
Katika maiti zilizo pangwa sehemu moja zilizo jeruhiwa kwa bomu hilo, huku baadhi ya maiti hizi zikiwa zimepoteza viungo huku nyingine zikiwa zimejeruhiwa kwa majeraha madogo madogo, mwili wa Rahab ukawa ni mmoja wapo. Madaktari ambao mara kwa mara walizipitia maiti hizo ili kuzifanyia vipimo kwamba ni kweli wamefariki au laa, wakajikuta wakishangazwa kumuona dada mmoja aliye valia baibui jeusi akinyanyuka taratibu huku macho yake akiwa ameyafumba.
Askari polisi baadhi waliokuwa katika eneo hilo waliweza kulishuhudia hilo jambo ambalo liliwaogopesha sana madaktari kwani ni zaidi ya mara sita waliweza kufanya vipimo kwa kila maiti na kudhibitisha kwamba wameiaga dunia na kitu kilicho kuwa kinasubiriwa ni gari ambalo litakua katika eneo hilo na kubebe maiti zote hizo.
Rahab akayafumbua macho yake na kutazama eneo zima jinsi lilivyo haribiwa vibaya. Hakumsemesha mtu zaidi ya kuangalia maiti zilizo mzunguka. Akamuona mume wake raisi Praygod akiwa amelazwa pembeni sana huku mwili wake wote ukiwa umechanguka vibaya sana, hata sura yake si rahisi kuigundua kwa haraka. Kitu cha kuweza kukifahamu kwa haraka ni nguo alizo kuwa amezivaa. Taratibu Rahab akapiga hatua hadi kwenye mwili wa raisi Praygod huku machozi yakimwagika, hakujali kwamba umechanguka changuka vipi, akaukumbatia huku akiachia kilia kikubwa.
Waandishi wa habari baadhi hawakusita kulirusha tukio hilo, moja kwa moja kwenye televishion zao. Madaktari baadhi wakapata ujasiri na kwenda kumtoa Rahab katika mwili huo na kumuweka pembei wakisaidiana na askri polisi, walio anza kumfariji Rahab kunyamaza.
‘Hii sura kama sio ngeni kwangu’
Mkuu mmoja wa polisi alijiuliza swali kimoyo moyo huku akimtazama Rahab usoni. Mtu anaye muona hapo ndiye mwenyewe mke wa rasisi Praygod aliye achia madaraka baada ya kuangushwa kwenye uchaguzi.
“Koplo Ludovic mchukueni huyo mwanamke mumpeleke sehemu sala, kisha nitakuja huko mutakapo mpeleka”
“Sawa mkuu”
Wakamchukua Rahab aliye legea tikitiki kwa kuishiwa na nguvu za mwili kwa maana alicho kiona hakukitarajia kabisa kwenye maisha yake. Wakampeleka Rahab kwenye moja ya hoteli, huku daktrari maalumu akiwa akiwa ameandaliwa katika kumtunza. Koplo Ludovick pamoja na Koplo Mwanamkasi, waliweza kumgundua Rahab na kila mmoja akwa na swali ya kitu alicho weza kukiona.
“Huyu ni mke wa raisi mstaafu”
“Ndio koplo Mwanamkasi, nashangaa kuweza kumuona anaililia ile maiti pale”
“Mmmm kuna kitu kitakuwa kinaendelea hapa”
“Ngoja R.P.C aje naamini atakuwa na jibu sahihi katika hili”
Kopla Ludovick akampigia simu R.P.C John Massawe, wakamtaarifu sehemu walipo na huduma waliyo anza kumpatia mgonjwa wao.
“Nitakuja hapo baada ya nunu saa”
“Sawa mkuu”
***
Eddy akafika hotelini aiwa amechoka huku mawazo mengi yakiwa yamemtawala kichwnai mwake. Moja kwa moja akaelekea hadi chumbani kwake. Cha kushangaza hakumkuta Phidaya. Kwa haraka akaelekea chumbani kwa Shamsa pia hakumkuta, akaenda chumbani kwa madam Mery naye pia hakumkuta.
“Watakuwa wamekwenda wapi hawa?”
Eddy alizungumza huku akirudi chumbani kwake, akajitupa kitandani, huku nguo zake zikiwa zimechafuka sana. Gafla mlango ukafunguliwa na kumfanya Eddy kunyanyuka haraka kitandani. Macho yake yakakutana na macho ya Phidya yaliyo vimba kwa kulia muda mrefu. Wakabaki wakiwa wametazamana kwa dakika kama mbili kisha kwa haraka Phidaya akamfwa Eddy akasimama mbele yake, akampiga kofi zito Eddy lililo tua shavuni mwake, kisha akamkumbatia huku akilia.
“Kwanini, kwanini, kwanini”
Phidaya alizungumza huku akilia, akizidi kumkumbatia Eddy, mkono wake wa kulio ukimpiga piga Eddy mgongoni. Eddy hakujibu kitu chochote zaidi ya kuzidi kumkumbatia Phidaya wake. Phidaya akaendelea kulia huku akiwa ameegemeza kichwa kifuani mwa Eddy.
“Shiiiiiiiiii, usilie mke wangu nipo hapa”
Eddy alizungumza kwa sauti ya upole iliyo jaa mapenzi mazito, hadi Phidaya mwenyewe akatulia, hata kasi ya kulia ikapungua. Taratibu wakaachiana na wote wakaka kitandani. Phidaya akamtazama Eddy kuanzi juu hadi chini akionekana kumshangaa sana.
“Imekuwaje mume wangu?”
Swali la Phidaya, likamfanya Eddy kukaa kimya kwa sekunde kadhaa, akashusha pumzi nyingi na kumtazama Phidaya usoni anaye onekana kuwa na shahuku kubwa ya kutaka kufahamu ni kitu gani kimempata mume wake.
“Raisi Praygod, ame……”
“Amefanyaje?”
“Amefariki”
Mungu wangu!!”
Phidaya kwa mshangao akajikuta akisimama wima huku macho akimtolea Eddy. Phidaya mwili mzima akahisi ukishikwa na ganzi, taarifa aliyo isikia hakutarajia kwani raisi Praygod ni jana tu alikuwa akizungumza naye na akimshawishi juu ya swala kumpa ruhusa Eddy katika kazi yake ya kuhitaji kulipiza kisasi.
“Eddy sijakusikia vizuri, hee……hee hembu rudia tena”
“Raisi Praygod amefariki kwa kulipuka kwa bomu, hata Rahab mwenyewe sina uhakika kama yupo hai au laa”
Phidya taratibu akajikuta akikaa chini kabisa, huku machozi yakimwagika usoni, taarifa aliyo ipata aimenyong’onyeza kwa kiwango kikubwa sana.
“Sasa Eddy tutafanyaje jamani, ahaaaaaa”
Phidaya alizungumza huku akiendelea kulia. Sa Yoo akatoka chumbani kwake na kwenda kumuona Phidaya, akafika mlangoni na kujikuta akisimama baada ya kusikia Phidaya akilia. Wasiwasi ukampata akataka kuondoka hapo mlangoni, ila akasita na kusimama ili kusikiliza vizuri.
“Hata mimi nimechanganyikiwa, akili yangu hapa haifanyi kazi kabisa”
“Aahahaaa Praygod kwanini umekufa lakini. Wewe ndio tulikuwa tunakutegemea”
Sauti ya Phidaya, Sa Yoo aliweza kuisikia vizuri, taratibu Sa Yoo akajikuta akiufungua mlango na kuingia ndani akiwa kama haamini kitu alicho weza kukisikia masikioni mwake.
“Umesema raisi amekufa?”
Sa Yoo alimuuliza Eddy swali, na kumfanya Eddy kutingisha kichwa akimdhibitishia Shamsa kwamba ni kweli alicho kisikia ndicho kilichopo mbele yao
***
Macho ya John muda wote hakuyabandua kwenye televishion chanel baadhi kuweza kusubiria juu ya mpango wake wa kumuangamiza Erickson, mwanaume aliye weza kuteka penzi la msichana ambaye ni muda mwingi amekuwa anamfikiria japo kuwa hakuweza kumueleza ukweli juu ya hisia zake. ‘Breking News’ iliyo weza kuonyeshwa kwenye kituo cha televishion cha ITV, ilimfanya kuweza kukaa kwa umakini akisikilizia ni kitu gani kijana wake alicho kifanya.
Kitu kilicho mshangaza ni kumuona Erickson akiwa analia huku akiwa karibu na mwili wa mtu aliye lipuliwa na bomu hilo la kisasa lenye muonekano kama simu ya mkononi ila sivyo na si rahisi kwa mtu kuweza kuligundua kwa haraka.
“Fu*k”
John alituka kwani hakutegemea kumuona Erickson tena kwenye maisha yake.
“Lazima ufe Erickson siwezi kushare demu na wewe”
John aliendelea kuzungumza peke yake, ndani ya chumba cha hoteli alipo panga kwa muda machache. Akaendelea kutazama taarifa hiyo, ila baada ya muda fulani, akaweza kulishuhudia tukio la Agnes akikumbatiana na Erickson huku wakipena mabusu motomoto mbele ya waandishi wa habari. Laiti kama angekuwa na miguu na mikono ninaamini angenyanyuka na kwenda kulizuia tukio analo lifanya Erickson an Agnes. Ila kutokana na kutoa kuwa na viungo hivyo John alijikuta kimwaga matusi mfululizo juu ya tukio hilo. Mlango wa chumbani kwake ukafunguliwa, akaingia kijna wake aliye kuwa amemuagiza.
“Ndio umefanya nini sasa?”
John alizungumza kwa hasira huku akiwa amemtolea macho kijana wake huyo.
“Nimefanya kama vile ulivyo niagiza”
“Unaona jamaa bado yupo hai, hajafa”
Mlinzi wa John akaigeukia luninga iliyopo kwenye chumba hicho, akamshuhudia Eddy akiwa amekumbatiana na Agnes.
“Bosi nipe siku kadhaa nitakuwa nimekamilisha hii kazi”
“Fanya uniletee kichwa cha Erickson hapa”
“Sawa mkuu”
***
Swala la mlipuko katika jengo la kibiashara la Mlimani City, likamstua hata raisi Godwin ambaye hakutegemea kama mpango wao walio upanga katika chama chao cha D.F.E umeweza kuwahi kwa kiasi hicho. Kwa haraka akachukua simu yake ya mkononi na kumpigia John na kumuagiza afike ikulu mara moja.
K itu kingine kilicho zidi kumuumiza akili ni jinsi alivyo weza kumuona Erickson kwenye televishion akiwa analia, ikionekana ni mmoja wa waadhiriwa wa mlipuko huo wa bomu.
‘’Baba baba kuna mlipuko um…….”
Manka hakuweza kuimalizia sentensi yake mara baada ya kuingia ndani ya ofisi ya baba yake na kumkuta akitazama taarifa hiyo ya habari.
“Baba kuna mtu anataka kumuua Erickson wangu”
Manka alizungumza huku machozi yakimlenga lenga na kumfanya raisi Godwin kumgeukia na kumtazama kwa macho ya mashangao.
“Erickson wako. Unamaanisha nini?”
Manka hakujibu kitu chochote zaidi ya kukaa kimya huku akiendelea kumwagikwa na machozi. Kwa mara ya kwanza raisi Godiwn ndio ameweza kuziona hisia za mapenzi za mwanae mpendwa Manka akimlilia mwanaume.
“Ina maana unampenda ERICKSON FORRD?”
“Ndio baba”
Manka alijibu na kuzidi kumpandisha hasira raisi Godwin, kwa mtu aliye taka kusababisha kifo cha kijana aliye pendwa na mwanae.
“Mshezi aliye fanya hivyo nakuahidi nitamuua aliye tegesha bomu hilo sawa mwanangu”
“Sawa baba”
Manka alizungumza huku akimkumbatia Mzee Godwin, pasipo wao kuweza kujua kwamba huyo wanaye muita Erickson Forrd ndio Eddy Godwin.
SORRY MADAM (85) (Destination of my enemies)
Haukupita muda mwingi John pamoja na mlinzi wake tayari wakawa wamesha fika ikulu, moja kwa moja John akapelekwa katika ofisi ya raisi Godwin, akamkuta akiwa yupo na Manka, sura zao wote zinaonyesha wana jambo ambalo limewaudhi sana.
“Naamini umeliona tu hilo tukio lililo tokea leo”
“Tukio gani muheshimiwa”
“Tazama kule kwenye tv, hili tukio limetokea makusudi kwa mtu, aliye fanya hili alilenge kumuangamiza Erickson Forrd, Je unavyo hisi wewe ni nani aliye fanya hili tukio?”
Swali la raisi Godwin likamstua sana John, taratibu akashusha pumzi yake na kuwatazama wote, Manka na baba yake kisha akameza fumba la mate na kuzungumza.
“Muheshimiwa, inabidi nitume vijana waweze kuchunguza hili tukio kwa maana lipo nje ya mpango wetu tulio panga kulipua kwenye ukumbi wa Dar Live”
“Hayo mamabo ya Dar Live, leo yasimamisheni. Kwa hiki kilicho fanyika leo Mlimani City nitahitaji jibu ndani ya masaa ishirini na nne sawa”
Raisi Godwin alizungumza kwa sauti ya ukali iliyo mfanya hadi John kuogopa na kuhisi amegundulika, ila hakuwa na uhakika kama ni kweli raisi Godwin ametambua ni yeye au laa.
“Sawa mkuu nitakuletea jibu”
“Ondoka nenda kalishuhulikie sasa hivi”
“Sawa mkuu”
Mlinzi wa John akaingia na kumchukua bosi wake, wakaondoka. Njia nzima ndani ya gari John hakuzungumza kitu cha aina yoyote zaidi ya kufikiria ni kitu gani ambacho anaweza kukiunda kikaendana na ukweli wa tukio lililo tokea.
***
Taratibu Sa Yoo akanyanyuka na kutoka katika chumba cha Eddy, uso wake ulio jaa huzuni nyingi pamoja na machozi uliweza kumstua madam Mery aliye kuwa akitoka chumbani kwa Shamsa.
“Sa Yoo vipi, mbona hivyo?”
Shamsa hakujibu chochote zaidi ya kutembea kama kama hajamuona madam Mery anaye msemesha. Wote wakainngia chumbani na kumkuta Shamsa akiwa amejifunga taulo akitaka kwenda kuoga.
“Vipi tena, Sa Yoo mbona hivyo”
Shamsa alizungumza huku akiwa amekodolea macho Sa Yoo, aliye kaa taratibu kwenye sofa, huku akiendelea kumwagikwa na machozi.
“Sa Yoo eleza kama kuna tatizo na sisi tufahamu basi ukikaa kimya hivyo unatuweka wezako katika hali tata”
“Raisi Praygod na madam Rahab wamefariki dunia”
“What……….?”
“Ahahaaa acha utani Sa Yoo bwana watakufaje kufanye wakati jana tulikuwa nao”
Shamsa alizungumza huku akitabasamu, akiamini kabisa kwamba kitu kilicho zungumzwa ni uongo. Kwa jinsi Madam Mery alivyo tulia kwa mbali machozi yakimlenga lenga, ndio kitu kilicho anza kumstua Shamsa.
“Unataka kusema wamekufa. Nani kakuambia hiyo taarifa?”
“Eddy amedhibitisha hilo”
“Eddy. Eddy yupo wapi?”
“Chumbani kwake”
Shamsa akatoka hivyo hivyo na taulo lake alilo jifunga hadi chumbani kwa Eddy na kumkuta wakiwa wamekaa kitandani pamoja na Phidaya huku wamekumbatiana.
“Eddy eti ni kweli raisi Praygod na madam Rahab wamefariki dunia?”
Sauti ya Shamsa inawafanya Eddy na Phidaya kuachiana. Wanamtazama Shamsa aliye simama mbele yao akionekana kuwa na mashaka.
“Ndio amefariki, kwenye mlipuko wa bomu”
Shamsa taratibu anajikuta akipoteza furaha yake huku akimtazama Eddy usoni anaye onekana kujawa na huzuni. Hakuna aliye weza kuzungumza kitu cha ina yoyote zaidi ya ukimya kutawala kwa maana katika mpango wao, umeingia dosari kubwa inayo onyesha dalili ya kushindwa katika kuukamilisha mpango wao wa mapinduzi.
***
Taratibu Rahab akanyanyuka kitandani na kukaa kitako. Macho yake yakamtazama daktari aliyopo pembeni yake akimchunguza afya yake.
“Unaendeleaje?”
“Nahitaji kuondoka”
“Sahanani muheshimiwa hauwezi kuondoka pasipo amri ya R.P.C John Masawe”
“Nimekuambia ninahitaji kuondoka na sihitaji kusubiria amri ya mtu yoyote”
Kabla daktari hajajibu koplo Mwanamkasi akaingia ndani humo huku akiwa ameongozana na koplo Ludovick.
“Hawa ndio walio wekwa ili kunilinda?”
Rahab alizungumza huku macho yake yakiwa mekundu, dhairi anaonyesha ana hasira kali sana. Rahab akanyanyuka kitandani na kuchomo sindano ya dripu iliyo chomwa kwenye mkono wake wa kulia. Kopla Mwanamkasi akajaribu kumzuia Rahab asitoke hapo, ila gafla akastukia akipigwa mtama ulio muangusha chini na kumlaza sakafuni hadi daktari pamoja na koplo Ludovick wakabaki wameduwaa.
“Sihitaji mtu anifwatlie, nitamuua. Na wewe pisha njia”
Taratibu koplo Ludovick akampisha Rahab, aliye toka chumbani hapo na kuubamiza mlango huo kwa kasi. Akiwa katika lifti ya kushukia kwenye gorofa hilo la hoteli, akavua baibui alilo kuwa amelivaa lililo jaa vumbi pamoja na damu damu. Akabakia na suruali pamoja na shati alilo kuwa amevalia kwa ndani. Lifti ilivyo funguka hakutazama na watu usoni walio kuwa wakiisubiria lifti hiyo kushuka, ili wapende kwenda juu. Akatoka kwenye hoteli hiyo na kupishana na gari la R.P.C likiingia katika eneo hilo.
“Nipeleke bahari beach”
Rahaba alimuambia dereva mmoja wa bodaboda, wakaondoka eneo la hoteli. Safari yao ikachukua nusu saa, wakawa wamesha fika hotelini. Akatoa noti mbili za shilingi elfu kumi na kumkabidhi dereva huyo ambaye hawakukubaliana hata bei. Moja kwa moja akaelekea chumbani kwake, akaingia bafuni na kuoga kisha akavaa nguo nyingine za kikikazi na kutoka chumbani kwake.
Macho ya Rahab yakakutana na macho ya Shamsa anaye toka kwenye chumba cha Eddy. Shamsa pasipo kutegemea akajikuta akipiga kelele za kuogopa na kuanguka chini. Kwa haraka Eddy na Phidaya wakatoka chumbani kwao na kumkuta Rahab akiwa anajaribu kumnyanyua Shamsa aliye anguka chini. Kila mmoja akabaki akiwa ameduwaa. Madam Mery pamoja na Sa Yoo nao wakatoa katika chumba chao baada ya kuzisikia kelele za Shamsa.
“Rahab!”
Madam Mery akashangaa huku akianza kupiga hatua za kumfwata Rahab sehemu alipo chuchumaa, akimsaidia Shamsa kunyanyua.
“Imkuwaje?”
“Hata mimi sifahamu. Mnyanyue kwa huko”
Madam Mery na Rahab wakasaidiana katika kumyanyua Shamsa, wakampeleka katika chumba cha Shamsa huku Eddy, Phidaya na Sa Yoo wakifwata kwa nyuma. Wakamwagia maji ya baridi Shamsa kichwani, akazinduka kutoka katika hali ya kupoteza fahamu.
“Tulia ni salama”
Eddy alizungumza huku akimshika Shamsa mkono aliye kurupuka tena baada ya kumuona Rahab. Shamsa akatulia taratibu huku akiwatazama watu wote waliomo ndani ya chumba hicho.
“Shamsa, najua utakuwa unahisi kwamba nimekufa, ila kusema kweli sijakufa nipo hai”
“Mbona Eddy alisema umekufa?”
“Hapana hata mimi mwenyewe nilijua kwamba Eddy amekufa, ila kusema kweli aliye kufa ni Praygod.”
Wau wote wakaka kimya ndani ya chumba wakimtazama Rahab usoni anaye zungumza kwa huzuni kubwa sana.
***
Mpango wa mazishi ukaanza kufanyika, Eddy pamoja na Madam Mery wakaufwatilia mwili wa raisi Praygod na kufanikiwa kuupata katika hospitali ya muhimbili. Japo ni mwili ulio haribika sana ila hapakuwa na jinsi ya kufanya zaidi ya kuhakikisha wanaupeleka katika nyumba yake ya milele. Mwili wa raisi Praygod ukaandaliwa vizuri, kisha ukapakizwa kwenye magari ya kukodisha yanayo beba masanduku ya maiti. Moja kwa moja wakaeleka bagamoyo kwenye nyumba ya raisi Praygod, aliyo ijenga kipindi yupo katika uongozi wa nchi.
Mazishi hayo yaliyo udhuriwa na watu wachache sana, waliopo kwenye mpango wa kuupindua uongozi wa raisi Godwin, yakafanyika huku Eddy akishika nafasi ya kuwa kama mchungaji wa kumfanyia maiti ibada takatifu.
“Kifo cha muheshimiwa raisi ni changamoto kwenye maisha yetu. Tuamini kwamba kufa kupo. Tupo kwenye mapambano, mapambano ya kuyaokoa maisha ya wamiliomi ya Watanzania. Tusilie hadi kumkufuru Mungu kwa maana hatujui kesho zamu itakuwa ni ya nani”
Eddy alizungumza kwa uchungu mkubwa huku biblia yake ikiwa mkononi mwake. Macho yake aliwatazama Shamsa, Rahab, Madam Mery, Sa Yoo pamoja na Phidaya. Wote wapo katika hali ya majonzi mengi sana.
“Alikuwa ni kiongozi mmoja mahiri, hodari aliye weza kuipigani na kuitete Tannzani kwa hali na mali. Hadi juzi tukio la kufariki kwake, alikutana na mimi pale Mlimani City, ili kunipa moyo katika kuendeleza mapambano juu ya sisi kuweza kufanya”
“Kwangu ninamchukulia kama mjomba. Nisiongee sana, kwa maana nina imani tukianza kufwatilia juu ya nani aliye weza kutega bomu, nina imani tutaweza kumpata na kujua adui zetu ni nani na nani”
“Katika jina la baba la na la mwana na la roho mtakatifu, Amen”
“Amen”
Wote wakaitika kwa paoja. Eddy akachukua chepe na kuanza kufukia kaburi la raisi Praygod. Shamsa, akaona .naye akachukua chepe jengine na kuendelea kufukia kaburi la Raisi Praygod. Wote walio salia, wakaelekea stoo, kila mmoja akarudi na chepe lake na kuendelea kusaidiana katika kuufukia jeneza. Haikuwachukua muda mwingi wakawa tayari wamesha maliza kuufukia mwili wa marehemu. Siku hiyo hiyo wakalitengenezea kaburi hilo kwa simenti, hadi inafika saa tatu usiku kazi ikawa imesha malizika ya kulijengea kaburi.
“Nawashukuru kwa kujitoa kwenu katika kuhakikisha kwamba munaulaza mwili wa mume wangu katika sehemu husika. Nyinyi kwangu ni familia kwa sasa, sina ndugu zaidi ya nyinyi na wala sina mtu ninaye weza kusama kwamba nitamkimbilia pale nitakapo kuwa na tatizo. Nawapenda sana na nitaomba kuanzia leo tuwe kitu kimoja”
Rahab alizungumza na wezake wakiwa katika meza ya chakula.
“Hilo lisikupe wasiwasi kwa upande wangu, nitahaikisha kwamba tunasaidiana wote katika kufanya mapinduzi kaika nchi hii”
Sa Yoo alizungumza huku akinyanyuka kwenye kiti alicho kuwa amekaa. Akanyoosha mkono wake wa kulia kwenye meza, Shamsa naye akanyanyuka na kuuweka mkono wake juu ya mkono wa Sa Yoo. Watu wote walio bakia wakanyanyuka na kuiweka mikono yao sehemu ilipo mikono ya Sa Yoo na Shamsa.
“Kwa pamoja tunaweza, kwa pamoja mabadiliko ni lazima kuweza kuyafanya”
“Kuanzia leo hii ni timu, ambayo nakwenda kuipa jina la SHADOW TEAM”
Eddy alizungumza huku akiwatazama wote machoni.
“Shadow, kwa nini umeiita Shadow team?”
Madam Mery aliuliza huku akitabasamu.
“Timu yetu itafanya kazi kama kivuli. Akili, Umakini, na Maarifa ndio vitu vya pekee vitakavyo weza kutupatia ushindi katika mpango wetu”
“Eddy mimi sijui kutumia bastola naomba unifundishe”
“Usijali Sa Yoo, kuanzia kesho mazoezi yatakuwa ni kwa wote”
“Hakuna haja ya kuondoka haoa nyumbani kwangu. Kama ni silaha na kiwanja cha mazoezi kipo kama munavyo weza kuona wenyewe”
Rahaba alizungumza na kuzidi kuwapa watu moyo juu ya kazi wanayo kwenda kuifanya. Wakakubaliana Eddy atarudi katika hoteli waliyo kuwepo atakusanya mizogo yao yote ksha atarudi nayo Bagamoyo walipo wezake.
Alfajiri na mapema Eddy akaondoka Bagamoyo na moja kwa moja akaelekea hadi ilipo nyumba yake, kwa haraka akaelekea katika chumba chake cha siri, akachukua silaha za kutosha pamoja na pesa za kutosha, akazipakiza katika gari alilo pewa na Rahab kwa ajili ya atumizi. Akaelekea katika maduka ya Laptop, akanunua Laptop sita aina za Apple Mackbook zenye uwezo mkubwa katika matumizi yake, kisha akanunua simu sita zenye uwezo ambao anaamini zitarahisisha kazi yao. Alipo hakikisha kwamba kila kitu kipo sawa alicho kihitai, akaelekea hotelini na kuchukua kila kilicho chao, japo pesa waliyo kuwa wamelipia hapo hotelini haikuwa imekwisha.
***
Katika maisha yake yote, Agnes ndio ameanza kuyapata maumivu ya mapenzi. Tanngu siku ya mwisho anaachana na Erickson wake katika hospitali ya Muhimbili, hadi leo hajaonana naye wala namba ya simu anayo ipiga haipatikani. Kitu kilicho zidi kumchanganya akaanza kuingiwa na hisia mbaya za wivu na kuhisi kwamba huenda Erickson anaweza kuwa na mwanamke mwengine.
“No niamuamuamini Erickson wangu hawezi kunifanyia kitu kama hichi”
Agnes alizungumza mwenyewe kama mwenda wazimu ndani ya ofisi yake. Akiwa katika mawazo hayo huku simu yake ikiwa mkononi akijaribu kupiga simu mara kadhaa namba ya Erickson ambayo hadi wakati huu haipatikani hewani, mlango wake ukagongwa.
“Ingia”
Akaingia secretary wake, aliye valia suti nzuri iliyo ukaa mwili wake vizuri.
“Eheee, kuna nini?”
“Kuna wageni wamekuja wanahitaji kukuona wewe”
“Ila Happynes si nilisha kuambia kwamba sihitaji mgeni yoyote leo ofisini kwangu sipo vizuri”
“Ndio nilijaribu kuwaambia hivyo, ila wakaniambia kwamba wametoka ikulu”
Agnes baada ya kusikia ikulu ikambidi kuwa mpole, akaiweka simu yake pembeni na kumuambia awaruhusu watu hao kuweza kuingia ofisini kwake. Secretary wake akatoka, na kuwaambia wageni hao waweze kuingia ofisini kwake.
Agnes hakuamini kumuona John akiwa ameongozana na mlinzi wake anaye msukuma kwenye kiti chake cha matairi sehemu yoyote ahayo hitaji kwenda.
“Karibuni”
Agnes alizungumza huku akiachia tabasamu la kawaida akionyesha kuto kuufurahia ugeni huo uliopo mbele yake. John akamuomba mlinzi wake kuweza kutoka nje ya ofisi kwa maana mazungumzo anayo kwenda kuyazunumza hapo ni muhimu sana.
“Nikusaidie nini?”
“Naamini huna la kunisaidia ila mimi ndio ninapaswa kuweza kukusaidia”
John alizungumza kwa kujiamini huku akimtazama Agnes usoni anaye onekana kustushwa kidogo na kauli hiyo.
“Usistuke sana kwa maana mimi ni mtu mwema sana kwako, na siku zote sihitaji kukuona una wasiwasi mwingi katika moyo wako wala maisha yako”
“Samahani John, sijajua una maanisha nini?”
“Ninacho kimaanisha ni kuhusiana na Erickson si ndio?”
Agnes baada ya kusikia jina la Erickson akajikuta akikaa vizuri kwenye kiti huku akimtazama John usoni kwa umakini sana.
“Labda nikuulize swali, tangu siku ulipo achana na Erickson uliweza kuwasiliana naye?”
“Hapana, nampigia hapatikani”
“Na unatambua ni nani aliye sababisha mlipuko wa juzi?”
“Ngoja kwanza mbona unauliza swali ambalo unatambua mimi simjui huyo muhusika”
“Ok nitakueleza. Mtu aliye weza kufanya shambulizi la ugaidi ni Eddy”
“Eddy, Eddy yupi?”
“Nyanyuka utoe simu kwenye mfuko wangu wa shati”
Agnes kwa haraka akanyanyuka kwenye kiti chake moja kwa moja akamfwata John sehemu alipo kaa, akaitoa simu ya John.
“Ingia sehemu ya picha, humo ndani ipo picha moja na huyo utakaye muona ndio mtu ambaye kwa sasa pia ndio anaye mshikilia mpenzi wako Erickson”
Kwa haraka Agnes akiwa kama amchanganyikiwa, akaingia upande wa picha, akaufungua kwa haraka. Sura ya picha aliyo kutana nayo si ngeni kabisa katika kumbukumbu zake, kwa maana ni miongoni mwa mtu waliye pewa kazi ya kumtafuta.
Agnes mwili mzima akaijikuta ukimtetemeka kwa hasira kali huku akiendela kuitazama picha ya Eddy.
“Huyo ni mtu aliye weza kutambua mpango wenu wa nyinyi kumtafuta. Na kitu alichokuwa anapanga kukifanya ni kuhakikisha anaanza kuwatanguliza nyinyi kuzimu, kisha anawafwatia wale walio wapa kazi ya kumfwalia. Ameona akimuua Erickson basi wewe utateteraka na itakuwa ni rahisi kwa wewe kuweza kufa”
Uongo wa John ukazidi kumuingia Agnes akilini kisawasawa, kila jinsi alivyo zidi kuitazama picha ya Eddy ndivyo jinsi hasira ilivyo zidi kumpanda hadi akajikuta akitamani kuivunja simu hiyo aliyo ishika.
“Kumbuka mtu anye fata katika kuuawa ni wewe Agnes, Eddy amemteka Erickson kuwa makini”
Kwa hasira Agnes akaitupa chini simu ya John, huku akihema kwa hasira kama Simba jike aliye uliwa watoto wake alio wazaa muda mchache ulio pita.
Post your Comment