Get the latest updates from us for free

mas template
Home » , » SORRY MADAM -Sehemu ya 86 & 87 (Destination of my enemies)

SORRY MADAM -Sehemu ya 86 & 87 (Destination of my enemies)

Written By Bigie on Saturday, February 10, 2018 | 12:59:00 PM

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA

Agnes mwili mzima akaijikuta ukimtetemeka kwa hasira kali huku akiendela kuitazama picha ya Eddy.
“Huyo ni mtu aliye weza kutambua mpango wenu wa nyinyi kumtafuta. Na kitu alichokuwa anapanga kukifanya ni kuhakikisha anaanza kuwatanguliza nyinyi kuzimu, kisha anawafwatia wale walio wapa kazi ya kumfwalia. Ameona akimuua Erickson basi wewe utateteraka na itakuwa ni rahisi kwa wewe kuweza kufa”
Uongo wa John ukazidi kumuingia Agnes akilini kisawasawa, kila jinsi alivyo zidi kuitazama picha ya Eddy ndivyo jinsi hasira ilivyo zidi kumpanda hadi akajikuta akitamani kuivunja simu hiyo aliyo ishika.
“Kumbuka mtu anye fata katika kuuawa ni wewe Agnes, Eddy amemteka Erickson kuwa makini”
Kwa hasira Agnes akaitupa chini simu ya John, huku akihema kwa hasira kama Simba jike aliye uliwa watoto wake alio wazaa muda mchache ulio pita.

ENDELEA
   John akabaki akishangaa jinsi simu yake ilivyo gawanyika vipande vipande chini. Hakuzungumza chochote zaidi ya kumeza mate tu. Agnes kwa haraka akrudi kwenye kiti chake na kukaa.
“Nitampata vipi huyo Eddy?”
Agnes alizungumza huku sura yake ikiwa imejikunja ndita zilizo upoteza uzuri wak wote ambao, John muda mchache alivyo ingia ofisini hapo alikuwa akiufurahia sana.
“Ungana na mimi, na utaweza kumpata Eddy”
Kabla Agnes hajazungumza kitu cha aina yoyote, simu ya Agnes ikaita na kumfanya kuitazama kwa haraka, kitu kilicho mshangaza ni kuona jina la Erickson likijitokeza kwenye simu yake, kabla hajaipokea akamtazama John kwa macho makali kisha akaipokea.
                                                                                                                       ***
   Eddy taratibu akajikuta akipunguza mwendo kasi wa gari lake, baada kwa mbali kidogo kuona msusuru wa magari ukiwa umesimama. Hakujua ni kitu gani kilicho polekea gari hizo kusimama. Taratibu akalisimamisha garni lake nyuma ya gari lililpo mbele yake. 
 
“Kuna nini?”
Eddy alizungumza mwenyewe huku akiitooa simu yake mfukoni. Akakuta ikiwa imezima kutokana na kuisha kwa chaji, na siku mbili hizi hakuitumia kabisa kutokana na matatizo yaliyo weza kujitokea. Akachukua waya wa chaji na kuuchomeka katika sehemu ya USB, iliyo kwenye gari lake, taratibu chaji ikaanza kuingia. Pasipo kujua ni kitu gani kipo mbele yake, akazidi kusogeza gari lake taratibu kuifwata foleni hiyo. Hadi zimebaki gari mbili mbele yake ndipo Eddy anagundua foleni hiyo imesababishwa na ukaguzi mkali wa jeshi la polisi wakisaidiana na jeshi la kujenga taifa wakikagua magari yote yanayo ingia na kutoka katika mkoa wa Dar es Salaam.
 
“Shitii”
Eddy akajikuta akitoa macho na kuanza cha kufikiria ni nini cha kufanya kwa maana askari hao wanakagua gari zima hadi kwenye buti. Bahati mbaya ni kwamba kwenye buti ya gari lake amebeba silaha anazo zimiliki kinyume na sheria. Kitu kingine kinacho zidi kumpagawisha nyuma yake kuna magari mengi ambayo nayo yapo kwenye msururu huo wa kukaguliwa. 
 
“Agnes Agnes”
Eddy alizungumza huku kwa haraka akijitahidi kuiwasha simu yake, kwa bahati nzuri akaiwasha japo ina asilimia tano za chaji, ila akajitahidi hivyo hivyo kumpigia Agnes akiamini anaweza kuapata msaada kwake. Tayari gari la mbele yake lilisha anza kukaguliwa, huku askari wengine wawili walio shikilia mbwa wawili wakubwa, wakilisogelea gari lake huku bunduki zao zikiwa begani. Kitendo cha Agnes kupokea simu, simu ya Eddy ikazima chaji tena.
 
“Fu*k”
Eddy akajikuta akiachia tusi zito huku akiitazama simu hiyo, kwa haraka akakumbuka anasimu ambazo ni mpya ameziweka siti ya nyuma, akageuka kwa haraka na kuichukua moja, akatoa chip kwenye simu yake na kuiweka kwenye simu moya. Kwa haraka akaiwasha, simu ikiendelea kuwaka tayari askari wa mbele alisha anza kumpa isha ya kulisogeza gari lake kwenye sehemu yanapo kaguliwa. Ikambidi taratibu kulizogeza gari lake, mbaya zaidi mbele kuna geti la chuma pamoja na miba mirefu iliyo kaa mfumo wa chuma iliyo tandazwa barabarani endapo utajaribu kukimbia na kuikanyaga miba hiyo basi tairi za gari lako zote zitapata pancha. 

Kitu kingine ambacho ni ngumu kuweza kuwakimbia askari hao, ni magari makubwa ya jeshi yaliyo katika pande zote mbili za barabara yakiwa  yamefungwa mitutu mikubwa ya bunduki, zenye uwezo wa kulichakaza gari lako vibaya ndani ya dakika moja pale tu utakiuka sheria na kuwakimbia. Mbwa hao wakubwa, walio fundishwa mbinu za kunusa kitu chochote ambacho si cha usalama, wakanza kulizunguka gari la Eddy hususani sehemu ya buti, ambapo ndipo zilipo bunduki, mabomu pamoja na vibunda vya pesa za kigeni. Askari mmoja akagonga kioo cha upande wa Eddy alipo kaa kwa ishara akimuomba kushuka haraka. 
 
Eddy akamtazama askari huyo, aliye anza kuishika bunduki yake vizuri huku akiwa amemkazia macho, taratibu akashuka kwenye gari huku akiwa ameshika simu yake mkononi.
“Muheshimiwa fungua buti, tunahitaji kukagua”
Askari mmoja alizungumza huku akimtazama Eddy kwa umakini.
“Munataka kukagua nini?”
“Hilo wewe halikuuhusu fungua buti tukague usitupotezee muda bwana”
“Siwezi kukagua gari kwa maana mzigo ulio kuwemo humo ni wa muheshimiwa waziri Agnes”
“Bwana wewe, sisi hatujali kama ni mzigo wa waziri au laa. Tutancho hitaji fungua buti tuangalie ni kitu gani ulicho bebe. Utakuta nyinyi ndio munao lipua lipua raia wema”
 
Askari huyo mwenye nyota mbili begani mwake, akazidi kumuamrisha Eddy kwa sauti kali yenye msisitizo na kuwafanya askari pamoja na wanajeshi walio kuwa eneo hilo kuwa makini kila mmoja na silaha yake.
“Muheshimiwa mimi siwezi kufungua, kwa maana sio makubaliana niliyo agizwa”
Eddy alizungumza huku akifunga mlango wa gari lake na funguo, kitendo kilicho zidi kumkasirisha askari huyo aliye jikuta akitandika ngumi ya tumbo Eddy na kuwaamrisha askari wake, kumpigisha magoti Eddy huku waking’ang’aniana kumpokonya funguo ya gari.
                                                                                                                ***
    Agnes akaitolea macho simu yake baada ya kuona imekata, kwa haraka akaipiga namba ya Erickson na kuambiwa kwaba haipatikani kwa wakati huu, jambo lililo mfanya kunyanyuka tane kwenye kiti chake na kuipiga tena namba ya Erickson na majibu akayakuta ni yale yale, kwamba haipatikani.
“Mbona hapatikani”
Agnes alizungumza mwenyewe huku akiitazama simu yake kwa umakini. John kwa kiherehere akajikuta akiuliza ni nani huyo, Agnes akamtazama kwa jicho kali kisha akaachia msunyo mkali, huku akimpandisha na kumshusha John.
 
“Unataka kujua ni nani ikiwa wewe kama nani?”
“Ahaaa labda naweza kukusaidia”
“Kwanza nakuomba utoke ofisini kwangu, nahitaji kuwa peke yangu”
“Ila hatijazungumza mazungumzo”
“John kama ni mazungumzo ya mtu aliye mteka Erickson wangu naomba yaishie hapa kwa leo sawa, kichwa change hakipo sawa”
Agnes alizungumza huku akiupiga hatua hadi mlangoni, akaufungua na kuuacha wazi, kwa ishara akamuomba John kutoka ofisini hapo.
“Ahaaa kumbe mwenyewe huwezi kutoka, Weee njoo umchukue mtu wako”
 
Agnes alizungumza kwa dharau na kumfanya John kujisikia vibaya moyoni mwake, ila ndio hivyo hawezi kufanya kitu chochote ukiachilia kutokuwa na viungo ila mtu anaye zungumza hivyo ni mtu anaye utesa moyo wake kwa kiasi kikubwa sana. Mlinzi wa John akaingia na kumtoa bosi wake. Agnes akaufunga mlango kwa nguvu, na kurudi kwneye kiti chake. Akaipiga tena namba ya Erickson kwa bahati nzuri ikaanza kuita kitu kilicho mfanya kushusha punzi huku akiwa na shauku kubwa ya kutaka kujua ni kitu gani anacho taka Erickson. Simu ikapokelewa.
“Halooo”
 
Agnes alizungumza kwa sauti ya mapenzi, ila sauti alizo zisikia zikamfanya ake vizuri kwenye kiti chake.
‘Achia funguo wewe mwana haramu mkubwa’
‘Akileta ujinga mpigeni risasi’
‘Lakini hamna haki ya kunipi……aahaaaaa’
‘Nyamaza Nguruwe wewe’
‘Simu yake ipo hawani hiyo hembu ikate kuna mtu naona ameipokea’
Simu ikakatwa na kumfanya Agnes mwili mzima kuishiwa nguvu, akatamani kunyanyuka na kwenda kumfwata John, aliye mueleza kwamba Erickson wake ametekwa na mtu anaye itwa Eddy ila akajikuta akishindwa kabisa, woga na wasiwasi mwingi vikaujaa mwili waka, hata simu aliyo ishika mkononi mwake akaiweka mezani taratibu akahisi ni nzito sana kwake.
 
‘Akilite ujinga mpigeni risasi’
Sauti hiyo ikajirudia kwa haraka kwenye kichwa cha Agnes, na kujikuta akishusha pumzi na kujikaza kupoteza wasiwasi unao ufanya mwili kuishiwa na nguvu kwa haraka akaichukua simu yake na kuipiga tena namba ya Erickson, ikaita kidogo ikakatwa, akarudia kwa mara ya pili ikaita na kukatwa. Akapiga kwa mara ya tatu akakuta haipo hewani ikiashiria kwamba imezimwa na watu hao.
‘Lakini hamna haki ya kunipi…….aahaaaaa’
Sauti hiyo ya Erickson ikamfanya Agnes kumwagikwa na machozi, akifikiria mateso anayo yapata Erickson mwanaume aliye mpenda kupita kitu cha aina yoyote.
                                                                                                          ***
   Eddy akawa yupo radhi kufa ila si kuachia funguo aliyo ishika, anayo minyana na askari wawili wanao hitaji kuichukua ili kufungua gari lake. Tukio lake likawafanya askari na wanajeshi wote kuelekezea mitutu yao ya bunduki eneo la tukio. Simu ya Eddy ikaita, akaipokea ila askari mmoja akampiga teke na simu yake kuangukia pembeni ikiwa hewani
“Achia funguo wewe mwana haramu mkubwa”
Askari mmoja alizungumza huku akizidi kuung’amg’ania mkono wa kulia wa Eddy ulio shikilia funguo ya gari.
 
“Akilete ujinga mpigeni risasi’
Mkubwa wao alizungumza huku akiangalia vijana wake wanavyo minyana na Eddy aliye lala kwenye lami, huku mkono wenye funguo akiwa ameulalia.
“Lakini hamna haki ya kunipi……aahaaaaa”
Mkuu wao huyo akamshindilia Eddy teke la mbavu lililo mfanya akatishe sentensi yake na kuugulia na maumivu makali sana.
“Nyamaza Nguruwe wewe”
Mkuu huyo aliye mrefu na mweusi, alizungumza na kumtandika Eddy teke jengine la mbavu na kuzidi kumfanya Eddy kutoa ukelele wa maumivu.
“Simu yake ipo hawani hiyo hembu ikate kuna mtu naona ameipokea”
 
Askari mmoja alizungumza na kumfanya askari mwengine kuiokota simu ya Eddy na kuikata, kisha akaiweka mfukoni mwake. Foleni ya magari ikazidi kuongezeka na kuwafanya watu kuchukizwa na zoezi hilo, kwa maana askari wameacha ukaguzi na kushindana na mtu mmoja anaye leta ubishi katika kuitoa funguo ya gari lake, wanalo hisi limebeba vitu ambavvyo ni haramu.
“Mbona wanachukua muda mrefu?”
Manka alimuuliza dereva wake, wakiwa ni miongoni mwa magari yaliyo simama foleni yakitokea Bagamoyo, kuelekea Dar es Salaam.
 
“Sijui kwa nini?”
“Hembu shuka nenda kaangalie ni kitu gani wanacho kifanya kwa maana hakuna gari linalo ruhusiwa”
“Sawa madam”
Dereva huyo akashuka na kuyapita magari saba yaliyopo mbele yao, ndipo alipo weza kushuhudia tukio la askari wakiminyana na mmoja wa watu aliye lala chini, wakimtandika virungu, akionekana kuwa ni mbishi kutii amri aliyo pewa. Dereva akarudi kwenye gari.
“Kuna nini?”
“Ahaaa kuna mtu naona anapigwa virungu na askari sijua amewagomea kitu”
“Daaaa ni mwanaume au mwanamke”
“Ni mwanaume”
 
“Sasa hawa nao wanaleta mambo yakiseng* inakuwaje mtu mmoja afanye watu tukae zaidi ya robo saa kwenye foleni. Wamshike na kumuweka kando waruhusu magari mengine.”
Manka alizungumza huku akishuka kwenye gari, akionekana kuchukizwa, kwa mwendo wa haraka akazipita gari zilizopo mbele yao hadi sehemu ya geti, askri walipo mtazama wakaweza kumtambua.
“Kuna nini hapa?”
“Ahaa ni yule kijana pale anakataa kutoa funguo ya gari lake, likaguliwe”
Mwanajeshi mmoja alizungumza huku akimuonyesha Manka sehemu tukio linapo endelea. Manka kwa hasira akazidi kupiga hatua kuelekea eneo hilo la tukio, kila askari na mawanajeshi aliye muona akampigia saluti.
 
“Kama ni mbishi si mumtupi………”
Manka hakumalizia sentensi yake ya mwisho, baada ya kuona mtu anye leta ubishi huo ni Erickson, mwanaume anaye jaribu kuhakikisha anamuingiza kwenye imaya yake ya mapenzi.
“Acheni, acheni, acheni”
Manka alizungumza huku akiwasogeza askari wanao mpiga Eddy kwa virungu. Kwa haraka akapiga magoti chini kila askari akabaki akishangaa, kumuona bosi wao akimnyenyekea mtu waliye mshushia kipigo kizoto.
“Erickson nini tena baba yangu?”
 
Manka alizungumza huku akimnyanyua Erickson anaye mwagikwa na damu za mdomo na puani, kwa kipigo alicho kipata, Eddy hata hakumuona Manka vizuri, kwani ukungu mwingi ulitawala kwenye macho yake.
“Kwa nini munapiga pipiga tu watu nyingi mbwa”
Manka alizungumza kwa hasira, hapakuwa na askari aliye jibu chochote wote wakaka kimya. Manka akajitahidi kumyanyua Erickson aliye ishiwa nguvu kabisa hadi akasimama.
 
“Nani ametoa amri apigwe”
Askari wengine wanye vyeo vya chini, wakamtazama bosi wao. Manka akamtazama mkuu huyo wa polisi kwa macho makali yaliyo jaa hasira.
“Si….iimu yangu”
Erickson(Eddy) alizungumza huku akimnyooshea mkono taratibu kwa askari aliye idumbukiza simu mfukoni. Kwa haraka askari huyo akaitoa simu hiyo mfukoni mwake na kumkabidhi haraka Manka aliye mkata jicho kali baada ya kunyooshewa mkono na Erickson.
 
“Wewe kabla ya siku haijaisha nikuone ofisini kwangu”
Manka alizungumza huku akimkazia macho mkuu wa polisi, ambaye amenywea kama mwanaume aliye achia hewa chafu mbele ya mama mke wake.
“Gari yangu”
Eddy alizungumza huku akikabidhi funguo Manka, aliye ichukua kwa haraka haraka.
“Njooni mumshike mumuingize kwenye gari, munamtoke nini mimacho”
 
Askari wawili wakamshika Eddy, Manka akafungua mlango wa upande wa dereva, kisha akaingia askari hao wakamzungusha Eddy hadi upande wa pili, wakamuingiza kwenye siti ya mbele, wakamfunga na mkanda. Manka taratibu akageuza gari na safari ya kuelekea Dar es Salaam ikaanza huku kwa upande mmoja moyoni mwake akiwa amejawa na furaha kwa kuweza kumpata Erickson.
 
“Hii kweli ni bonge la movie”
Jamaa mmoja alizungumza, huku akisogeza gari lake katika sehemu lilipokuwa gari la Eddy. Akaitazama video aliyo irekodi ya tukio zima la Eddy kushushushiwa kipogo na polisi. Bila ya kujiuliza mara mbilimbili akairushia kwenye mtandao wa kijamii wa Facebok kwenye akaunti yake huku akiandika maandhishi yaliyo someka ‘Hawa ndio askari wetu wa Tanzania’. Ndani ya dadika moja watu zaidi ya elfu moja wakawa wameitazama video hiyo, huku kila mmoja akitoa maoni yake juu ya tukio hilo.
                                                                                                          ***
“Jamani njooni muone”
Sa Yoo alizungumza huku akiwa ameshika ‘tablet’ ya madam Mery aliye muomba ili kuperuzi peruzi kwneye mtandao.
“Tuone nini?”
 
Shamsa aliuliza huku akiwa ameshika kisu pmoja na kiazi mkononi mwake anacho kimenya wakiandaa chakula cha mchana. Sa Yoo hakujibu kitu zaidi ya kukaa kimya akiitolea macho video iliyo rushwa mtandanoni inayo onyesha Eddy akipigwa na askari. Madam Mery aliye kaa pembeni ya Sa Yoo, akajisogeza na kuangalia ni kitu gani ambacho Sa Yoo anakitazama.
 
“Huyo si Eddy?”
Madam Mery aliuliza na kuwafanya Phidaya, Shamsa na Rahab kunyanyuka walipo kaa na kusogea sehemu walipo Sa Yoo na madam Mery. Phidaya akajikuta akimpokonya Sa Yoo tablet hiyo na kuishika vizuri kumuangalia  jinsi mumewe anavyo shushiwa virungu na polisi hao. Phidaya akahisi kuchanganyikiwa kwa mana hakujua ni kitu gani ambacho kimekuta mume wake. 
 
“Watakuwa wamemstukia kwamba ndio Eddy nini?”
Sa Yoo aliuliza huku akimtazama Madam Mery usoni aliye tingisha kichwa kukataa alicho kisema Sa Yoo.
“Manka”
Shamsa alizungumza huku akiwa amesimama pemeni ya Phidaya anaye tazama video hiyo mwili mzima ukimtetemeka.
“Manka”
Madam Mery akasogea na kutazama video hiyo, akamuona jinsi Manka akimsaidia Eddy na kuondoka naye. Phidaya akaiachia tablet hiyo, ila Shamsa akaiwahi kuidata kabla haijafika chini. 
 
“Phidaya kaa chini utulie”
Rahab alizungumza huku akimshika Phidaya na kumkalisha chini, dumbuwazi lililo mpata Phidya likamfannya kukaa kimya asizungumze chochote, ila macho yake yanaonyesha ni jinsi gani alivyo jawa na hasira pamoja na uchungu wa kushuhudia mumewe akipokea kipigo hicho kama mwizi.
“Kuna hatari ya Eddy kugunduliwa”
“Kwa nini unazungumza hivyo madam Mery?”
“Manka ni dada yake Eddy, baba mmoja ila mama tofauti”
“Sasa hapo atajulikana vipi wakati sura yake haionyeshi kabisa kama ni yabandia?”
“Hata kama ni ya bandia ila tunatakiwa kuingia kazini kuhakikisha tunamrudisha Eddy hapa la sivyo kila kitu kinakwenda kuharibika”
 
Madam Mery alizungumza kwa msisitizo, wakaacha kila walicho kuwa wakikifanya. Wakaingia katika vyumba vyoa kila mtu akabadilisha nguo alizo kuwa amevaa, kwa maana walishinda na nguo za kufanyia kazi za jikoni ikiwemo kanga.  Wote watano wakaingia kwenye gari jengine la Rahab aina ya Prado, safari ya kuelekea Dar es Salaam ikaanza
“Ila namba ya Eddy madam Mery si unayo?”
Sa Yoo alizungumza huku akimgeukia madam Mery aliye kaa siti ya nyuma.
“Hapana”
“Mimi nimeishika kwa kichwa”
Rahab alizungumza huku akiongoza mwendo kasi wa gari. Rahab akamtajia Sa Yoo namba ya Eddy. Sa Yoo akaipiga namba hiyo ambayo haipo hewani.
“Vipi?”
Shamsa alizungumza huku wasiwasi ukiwa umemjaa sana,
“Hapatikani”
                                                                                                              ***
“Naku..fa, naku…fa”
Eddy alizungumza kwa tabu, na kumfanya Manka kustuka na kumtazama jinsi alivyo jilaza kwenye siti hiyo.
“Erickson usife nipo pamoja na wewe”
Manka alizungumza huku akizidi kuongeza mwendo kasi wa gari lake. Eddy hakujibu kitu cha aina yoyote, taratibu akaanza kukoroma kama mtu anaye kata roho, jambo lililo zidi kumuogopesha sana Manka. 
 
“Erick, Erickson”
Manka aliita huku mkono mmoja akimtingisha Eddy anaye zidi kukoroma, huku damu zikimtoka puani. Machozi yakaanza kumlenga lenga, Manka furaha ya kuwa na Erickson maishani mwake, akaanza kuona inaingia doa. Manka njia nzima akawa anapiga honi kuomba kupishwa, hakutamani kuweza kuona kifo cha Erickson kinatokea mbele ya macho yake. Majiara ya saa kumi jioni tayari akawa amefika kwenye foleni ya Mwenge.
Kila alipo mtazama Erickson aliye lala kimya, kwenye siti akatamani alipaishe gari lake hili kupita na kumuwahisha hospitalini, ila haikuwa hivyo ni lazima kufwata foleni hiyo. Jasho jingi likazidi kumwagika Manka japo ndnai ya gari kuna A/C ya kutosha ila haikufanya kazi. 
 
Gari zilipo ruhusiwa, Manka, akajitahidi kuongeza mwendo, akili yake yote inamtuma kumpeleka Erickson katika hospitalli ya Aghakan.
Hadi anafika hospitalini tayari ilisha timu saa kumi na moja jioni, kwa haraka kitanda cha matairi kikatolewa, Erickson akapandishwa kwenye kitanda na moja kwa moja akapelekwa kwenye chumba cha matibabu.
“Muheshimiwa tunakuomba usubiri nje”
Daktari mmoja alimzuia Manka baada ya kumuona akiitaka kuingia ndani ya chumba hicho. Kwa haraka mwili wa Erickson ukapigwa X-ray kuangalia ni sehemu gani ina tatizo. Damu nyingi, ikaonekana imevilia kwenye mbavu za upande wake wa kulia, unao onekana kujeruhiwa kwa kupigwa mara kadhaa.
 
“Group la damu yake ni nini?”
Daktari alimuuliza nesi, aliye mpa zoezi la kuipima damu ya Erickson.
“Ni group O plus”
“Mungu wangu, hiyo damu dokta imetuishia katika benki yatu ya damu”
Nesi mwengine alizungumza huku akimatazama daktari huyo. Daktari akaka kimya huku akimtazama Erickson waliye muwekea mshine za hewa ya oksijeni, inayo msadia kuhema. Daktari akatoka katika chumba hicho na kumkuta Manka akiwa amesimama nje ya chumba hicho.
“Daktari vipi, mgonjwa anaendeleaje?”
 
“Mgonjwa wako, anaupungufu wa damu nyingi. Kundi la damu ambalo analo sisi imetuishia hapa hospitalini”
“Ni group gani la damu?”
“Ni O plus”
“Naomba muniangalie mimi kana ninaweza kumchangia damu”
Hapakuwa na muda wa kupoteza Manka akaingizwa kwenye chumba cha kupimia damu, kwa bahati nzuri group la damu yake linaendena kabisa na group la damu ya Erickson hadi daktari akshangaa.
“Huyu mgonjwa ni nani yako?”
“Ni mpenzi wangu”
Wakamruhusu Manka kutoka nje ya chumba cha kutolea damu. Daktari akawaomba manesi wake kuitanguliza dumu katika chumba cha upasuaji kisha, yeye akaipima DNA kati ya Manka na Erickson. Kisha akaelekea katika chumba cha upasuaji na kuwakuta madaktari wezake wakiendelea na kazi ya kumshuhulikia Erickson aliye anza kupasuliwa upande wa mbavu za kulia sehemu damu ilipo vilia. 
 
Hadi inafika saa mbili usiku tayari wakawa wamefanikiwa kuta madonge ya damu yaliyo vilia kwenye mbavu za Erickson. Dokata Nelson akarudi katika chumba cha kupimia damu, akatazama vipimo vya DNA, akabaki akitoa macho kwani Manka na Erickson vipimo vinaonyesha ni damu moja, ikimaanisha ni ndugu.
“BINGO”
Dokta Nelson alizungumza huku akiachia tabasamu pana, akiamini utajiri upo mbele ya maisha yake endapo ataifichua siri hii mbele ya wahusika.
                                                                                     
 SORRY MADAM (88)   (Destination of my enemies)

   Dokta Nelson akaanza kuaandika majibu hayo kwenye karatasi sahihi ya kuandikia majibu hayo, alipo hakikisha ameyamaliza, akayaweka kwenye bahasha kubwa na kutoka katika ofisi yake kwa ajili ya kuelekea nyumbani kwake
                                                                                                               ***
“Hii video inaonyesha Eddy amaondoka na Manka kutumia gari lako madam”
Sa Yoo alizungumza huku akirudia kuitazama video hiyo ambayo imerushwa katika mtandao wa Facebook. 
 
“Ndio”
“Nitajie namba za gari?”
“Za nini?”
“Nahitaji kulitafuta kwa satelait”
Rahab akamtajia Sa Yoo namba za gari lake, kwa utaalamu mkubwa ambao Sa Yoo anao kwenye maswala ya ‘IT’, akaanza kuisika gari hiyo, hazikupita dakika nyingi tayari alama ya gari hilo ikawa inaonyesha kwamba lipo katika hospitali ya Agakhan.
“Hapa ndipo lilipo”
Sa Yoo alimuonyesha Rahab ambaye anaendelea kukanyagia mafuta ya gari lake, safari ikazidi kusonga, kitu kilicho mchukiza Rahab ni foleni aliyo ikuta maeneo ya Mbezi Beach kueleka Mwenge. Hapakuwa na jinsi zaidi ya kukaa kwenye foleni hiyo inayo kwenda kwa mwendo wa taratibu. 
 
Masaa yakazidi kusonga mbele huku foleni ikisogea taratibu hadi ikafika zamu ya wao kuruhusiwa, wakaendelea na safari yao. Hadi wanafika hospitali ya Agakhan ni majira ya saa nne kasoro usiku. Kweli wakalikuta gari la Eddy likiwa sehemu ya maegesho, wakalikagua na kulikuta lipo salama.
“Sasa watakuwa wapo wapi?”
Phidaya laliuliza huku akionekana kujawa na wasiwasi mwingi usoni mwake.
“Tujigaweni inabidi kwenda kuuliza kila sehemu”
“Sawa”
Wakajigawa kila watu wakaelekea kwenye upande wake lengo ni kuhakikisha kwamba wanampata Eddy katika wakati huo.
                                                                                                              ***
  Kitendo cha Eddy kutolewa katika chumba cha upasuaji kikafufua matumaini mapya ya Manka aliye kaa nje ya chumba cha upasuajia kwa masaa kadhaa akisubiri Eddy kufanyiwa huduma hiyo. Moja kwa moja Eddy akapelekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi ambacho kipo gorofa ya chini kabisa. Huku muda wote Manka akiwa nyuma ya kitanda hicho kinacho sukumwa na manesi wawili mmoja akiwa mbele huku mwengine akiwa nyuma.
 
Kabla Manka hajaingia kwenye chumba hicho, simu yake ya mkononi ikaita na kumfanuya asimame, akakuta ni jina la baba yake kipenzi Mzee Godwin, taratibu akaipokea na kuiweka sikioni
“Upo wapi mwanangu?”
“Baba nipo hospitali?”
“Hospitali?”
“Ndio baba Erickson amepigwa na maaskari”
“U…u…upo hospitali gani?”
“Nipo Agakhan”
“Nakuja sasa hivi”
Mzee Godwin alizungumza akionekana kupaniki kwa hasira kali, akionyesha dhahiri kukasirishwa na tukio hilo, Manka akairudisha simu yake mfukoni na kuingia katika chumba hicho cha wagonjwa mahututi.
 
“Ila muheshimiwa utakiwa kukaa humu kwa muda mrefu hichi ni chumba cha wagonjwa mahututi”
“Siwezi kuondoka na kumuacha mpenzi wangu katika eneo hili sawa nesi”
“Nimekuelewa muheshimiwa”
Nesi huyo hakuwa hakuwa na kitu cha kuzungumza zaidi ya kukubaliana na matakwa ya Manka yote ni kutokana na Manka kuwa ni kiongozi serikalini. Hazikupita dakika nyingi ving’ora vya polisi vikasikika nje ya eneo la hospitali na kuwafanya watu wengie walipo eneo la nje ya hospitali kushangaa ujio huo wa raisi ambao ni wa gafla sana.
“Yes nakwenda kufichua bomu”
Phidaya aalisikia sauti hiyo ya kiume ikitokea kwenye moja ya ofisi.
 
“Bomu?”
Phidaya akaiuliza mara mbili mbili na kujikuta akifungua mlango wa ofisi hiyo pasipo kubisha hodi kwa maana ni siku chache zimepita tangu mlipuko wa bomu ulio pelekea kuyaangamiza maisha ya raisi Godwin ulipotokea. Daktari huyo akaonekana kustuka baada ya kumuona Phidaya akiwa amesiamama mbele ya meza yake huku mlango akiwa ameufunga.
“Phidaya?”
Daktari huyo akajikuta akiita jina la Phidyaa huku mwili mzima ukimtetemeka sana. Phidaya akabaki akishangaa kila alipo jaribu kuzivuta kumbukumbu zake juu ya ni wapi aliwahi kumuona daktari huyu hakuweza kukumbuka kabisa, Phiday akapiga hatua mbili mbele huku akiwa amemkazia macho daktari huyo aliye tamani hata kujirusha dirishani kutoka gorofani ili afe ila si Phidaya kumsogelea.
 
“Nisamehe Phidaya”
Daktari alizungumza huku mwili mzima ukimtetemeka hadi haja ndogo akahisi ikimwagika. Bahasha yenye majibu ya DNA ikamdondoka mkononi mwake na kuzidi kurudi nyuma hadi akafika ukutani na pemeni yake kuna dirisha la vioo lililo wazi.
“Sio mimi niliye kuua ni Ranjiti aliye panga mpango wa ku…ku…fany…a wewe ufe”
Phidaya akatingisha kichwa, na kuanza kujua ni kitu gani ambacho kinamfanya daktari huyo kuwa muoga kwa kiasi hicho.
“Kwa hiyo ukaona ni utu kunitenganisha na mume wangu si ndio?”
Phidaya alizungumza sasa kwa kujiamini huku taratibu akizidi kupiga hatua za kumfwata daktari huyo anaye onekana kuzidi kuweweseka kwa woga.
 
“Haa….aahaa panaa”
“Nyionyeshe ni bomu gani ulitaka kwenda kulifichua”
Dokta Nelson mimacho ikamtoka, sasa muda huu mkojo ukaanza kushuka kwenye mapaja yake hadi ukatokeza kwenye suruali yake na kumfanya Phidaya kuona kabisa dokta huyo amejikojolea
“Niambiee nionyeshe hilo bomu”
Kwa ishara dokata Nelson akamuonyesha Phidaya baasha iliyo anguka chni, Phidaya akaitazama bahasha hiyo kisha akatabasamu kwa dharau kwa maana kitu ambacho dokta Nelson anamuonyesha akihendani kabisa na kitu ambacho amemuuliza kwa muda huu.
 
“Unautani na mimi eheee?”
“Si….siiku tanii”
“Nionyeshe sasa hilo bumu”
“Li….liipo ndani y….a hiyo bahasha”
Dokta Nelson alizungumza huku taratibu akijisogeza hadi sehemu ya dirisha, Phidaya akamtazama kwa macho makali ya kujiamini kisha akapiga hatua kubwa mbili za vishindo kumtisha dokta Nelson ambaye anautumia udhaifu wa makosa aliyo yafanya kwa miaka kadhaa kumtingisha, gafla dokta Nelson akapanda dirishani na kujirusha nje na kumfanya Phidaya kukimbilia hadi dirishani, kitu alicho kishuhudia chini kikamfanya Phidaya kufumba macho kwa sekunda kadhaa kisha akatazama tena. Kichwa cha dokta Nelson, kimetua kwenye kiwe kubwa na kupasuka hapo hapo, hadi ubongo ukatoka.
 
“Pumzika salama”
Phidaya alizungumza huku akiondoka hapo dirishani, akafika mlangoni akasimama kwa sekunde kadhaa, akatazama nyuma, chini ilipo anguka bahasha aliyo kuwa anaonyeshwa na dokta Nelson. Akarudi taratibu hadi sheenu ilipo, akachuchumaa na kuitazama vizururi, akapeleka kidole taratibu akiamini ni bomu japo hana ukweli nalo.
 
Taratibu akainyanyua bahasha hiyo, ila wepesi wa bahasha hiyo ukamfanya aitazama vizuri kwa kuifungua ndani, akaona karatasi mbili nyeupe. Vilio vinavyo tokea chini lilipo dirisha la ofisi ya dokta Nelson kukamstua Phidaya na kujikuta akiikunja bahasha hiyo na kuishika mkononi na kuanza kutoka ofisini humu.
 
Kundi la watu walio valia suti nyeusi huku mmoja wao akiwa amevalia suki ya kaki, ukamfanya Phidaya kusimama akiwa hapo hapo mlangoni na kuwatizama watu hao. Mmoja wao akamtambua kwa haraka sana kwamba ni baba yake mkwe Mzee Godwin ambaye naye pia akapunguza mwendo kasi na kumkazia macho Phidya aliye simama katika mlango wa kutokea katika ofisi ya dokta Nelson.
‘Phiday kimbia’
Ndio sauti ya pekee aliyo isikia akilini mwake, bila hata ya kujiuliza mara mbili mbili, akaanza kutimua mbio na kuwafanya walinzi wawili wa raisi Godwin kuanza kumfukuza Phidaya wakimuhisi  kuna jambo amelifanya pasipo kujua uhasama ulipo kati ya Phidya na kiongozi wao wanaye mlinda.
Mzee Godwin akaanza kuembea kwa mwendo wa kujiuliza maswali mengi kichwani mwake huku akijiuliza ni kwanini Phidaya yupo katika eneo la hapo hospitalini.
                                                                                                      ***
     Raisi Godwin akiwa ndani ya gari akielekea katika hospitali ya Agakhan, meseji  ikaingi kwenye simua yake ya mkononi, akaufunua ujumbe huo wa maneno ulio tumwa na dokta Nelson.
 
{MUHESHIMIWA NINA BAHASHA YAKO INA UKWELI WA KILA KITU JUU YA EDDY UNAYE MTAFUTA}
Kwa haraka Mzee Godwin akampigia dokta Nelson aliye mtumia ujumbe huo.
“Ukweli gani bwana mdogo?”
“Ni juu ya huyo Eddy unaye mtafuta, yaani ni panya mdogo sana muheshimiwa”
Raisi Godwin akawatazama walinzi wake alio nao ndani ya gari kisha akazungumza.
“Nipo njiani ninakuja hapo hospitalini kwako usitoke”
“Sawa mkuu”
Raisi Godwin akakata simu, hawakuchukua muda mrefu wakawa tayari wamesha fika kwenye hospitali ya Agakhan, walinzi wake wakashuka kwenye gari, mmoja akamfungulia mlango naye akashuka, akaitoa simu yake mfukoni na kumpigia Manka kumuuliza yupo wapi.
 
“Nipo ICU baba nimekaa na mgonjwa”
“Ok nakuja”
Mlinzi mmoja akamuuliza nesi juu ya wapi vilipo vyumba vya ICU, nesi huyo kwa bahati nzuri ni miongoni mwa manesi wali shuhulika katika upasuaji wa Erickson. Moja kwa moja nesi huyo akawaongoza hadi kilipo chumba alicho lazwa Erickson.
“Nisubirini hapa”
Raisi Godwin akaingia peke yake katika chumba hicho na kumkuta Manka akiwa amekaa pembeni ya kitanda alicho lazwa Erickson aliye wekewa mashine za kupumulia na mashine za kuhesabu mapigo ya moyo.
 
“Ilikuwaje?”
Raisi Godwin alizungumza huku akimtazama Manka usoni aliye anza kulengwa lengwa na machozi usoni mwake.
“Askari walimpiga”
“Askari gani?”
“Nitawashuhulikia baba mmoja baada ya mwengine.”
Manka alizungumza kwa kujiamini huku akimtazama baba yake usoni. Mzee Godwin taratibu akapiga hatua hadi kitanda alicho lala Erickson aliye fumnikwa na shuka jeupe. Mzee Godwin akautazama uzuri wa kijana huyo akajikuta akitingisha kichwa, kisha akamtazama Manka jinsi alivyo jawa na uchungutaratibu akamfwata Manka alipo simama.
“Atapona, hakikisha askari hao wote walio husika na hili swala unawashuhulikia”
“Sawa dady”
“Kuna daktari ninakwenda kumuangalia mara moja hapo juu nitarudi”
“Sawa”
 
Mzee Godwin akatoka katika chumba hicho akawacha walinzi wake wawili mlangoni hapo kisha yeye akaondokana na walinzi wengine sita. Wakaingia kwenye lifti moja kwa moja wakaelekea gorofa ya tatu ya hospitali hiyo. Wakakiwa wanatoka kwenye lifti hiyo wakitembea kwenye kordo ndefu ya gorofa hilo, Mzee Godwin akamuona Phidaya akitoka katika chumba cha ofisi ya dokta Nelson. Mkononi mwa Phidaya ameshika bahasha, ambayo Mzee Godwin hakuitilia maanani sana.
 
Kitendo cha Phidya kuanza kukimbia, kikamfanya raisi Godwin na walinzi wake kuanza kuhisi kuna tatizo, kwa haraka mzee Godwin akaongeza mwendo na kuingia katika ofisi ya dokta Nelson, hawakukuta mtu yoyote zaidi ya kusikia kelele zikitoke chini ya gorofa kupitia dirisha hilo. Mlinzi mmoja kwa haraka akakimbilia dirishani na kuona kundi la manesi pamoja nawatu wengine wakitazama mwili wa dokta Nelson ulio vunjika kichwa.
 
“Muheshimiwa njoo uone”
Raisi Godwin akapiga hatua hadi dirishani, hakuamini kumuona dokta Nelson akiwa amekufa kifo cha kikatili hasira ikampanda na kuwageukia walinzi wake.
“Hakikisheni munamshika yule msichana muliye muona haraka iwezekavavyo.”
“Sawa mkuu”
Walinzi watatu wakatoka kasi na kumuacha mzee Godwin akiwa na mlinzi mmoja, anaye muamini kupita walinzi wote.
“Turudi chini”
Raisi Godwin alizungumza kwa msisitizo huku akitangulia mbele na mlinzi wake akimfwata kwa nyuma.
                                                                                                                    ***
  Agnes akiwa njia ndani ya gari lake akirudu nyumbani kwake, meseji ikangia kwenye simu yake kupitia mtandao wa Whatsapp. Taratibu akaichuku simu yake aliyo kuwa ameitupia upande wa pili wa siti. Akaufungua ujumbe huo ambao umetumwa na namba ngeni. Video aliyo tumiwa ikamfanya asimamishe gari lake pembeni na kuitazama kwa umakini.
 
Macho yakamtoka baada ya kumuona Ericskon wake akipokea kichapo kitakatifu kutoka kwa askari, virungu ambavyo askari hao wanamtandika Erickson vikamfanya Agnes kujikuta akilengwa lengwa na machozi ya uchungu. Ila alipo muona Manka akimsaidia Erickson kidogo wasiwasi ukampungua, kwa haraka akaitafuta namba ya Manka kwenye orodha ya namba zake kwenye simu na kumpigia. Simu ya Manka ikaita kwa mara kadhaa ila haikupokelewa.
 
Akarudia zaidi ya mara kumi ila Manka hakupokea simu na muda mwengine alikatiwa simu. Akatuma meseji kwa Manka na kumuuliza yupo hospitali gani, ila meseji zilisomwa na hakurudishiwa majibu.
 
“Ohhhh Mungu wangu, au Erickson wangu amekufa nini?”
Agnes alizungumza mwenyewe huku machozi yakimwagika usoni mwake, akajitahidi hivyo hivyo kuendesha gari lake hadi nyumbani kwake, huku mawazo mengi yakitawala kichwani mwake. Kwa haraka akaingia bafuni na kuoga, kabadilisha nguo na kuvalia nguo ambazo si rahisi kwa mtu kuweza kumgundua kwamba yeye ni waziri, kwani amevalia suruali ya jinzi, tisheti kubwa kidogo pamoja kikoti juu yake. Akapigilia na kofia iliyo ificha sura yake, akatoka haraka hadi kwenye gari lake ambalo mara nyingi halitumii, aina ya BMW X5. Alipo hakikisha amefunga mkanda wa gari lake, akampigia simu Fetty.
“Ehee shoga upo wapi?”
“Nipo nyumbani. Vipi mbona unazungumza kiunyonge?”
“Nahitaji msaada wako”
“Zungumza”
 
Agnes akamuelezea Fetty kila kitu kuhusiana na kitu alicho fanyiwa Erickson kisha akamuelezea jinsi Manka anavyo mkatia katia simu.
“Hembu ngoja nimpigie na mimi nimuulize yupo wapi?”
“Sawa, mimi nipo ndani ya gari ukiniambia tu mimi naelekea huko huko asiniletee ujinga wake”
“Tulia nimpigie”
Agnes akaka ndani y a gari lake hadi simu yake ilivyo ita tena na kupigiwa na Fety.
“Ndio dada”
“Best yako yupo Agakgan, anadai Erickson yupo ICU”
“Mungu wangu asante”
“Ok kuwa makini si unajua tena mtoto wa mkubwa”
“Sawa”
 
Agnes akawasha gari lake na kuondoka nyumbani kwake, kwa ujuzi wa kulijua jiji la Dar es Salaam, akakatiza kwenye vichochoro kuzikwepa foleni majira haya ya usiku. Hadi anafika hospitalini tayari imesha timu saa nne usiku. Akasimamisha gari lake kwenye maegesho ya eneo hilo, kabla hajafungua mlango akashangaa mlango wa nyuma akifungua mtu kwa haraka na kuingia na kulala kwenye siti na kumfanya Agnes kugeuka kwa haraka na kumtazama mtu huyo ni nani.
                                                                                                                   ***
   Phidaya akageuka nyuma na kuwaona askari wawili walio valia suti wakimfwata kwa kasi kitendo kilicho mfanya kuzidi kukimbia kwa uwezo wake wote. Rahab akiwa kwa mbali akamuona Phidaya akikatiza kwa kasi, mara hajakaa sawa akawaona askari wawili wakimfwata kwa kasi wakitoka katika majengo wakielekea kwenye maegesho ya magari. Rahab akafwata kwa nyuma ili kuwazuia askari hao, huku naye akiwa katika mwendo kasi.
 
Phidaya katika kutizama tizama kwake kwenye maegesho ya magari, akaona gari moja likisimama kwenye maegesho ya hapo hospitalini. Kwa haraka pasipo hata kuuliza Phidaya akafungua mlango wa nyuma wa gari hilo na kuingia na kumfanya muendeshaji aliyopo humo ndani kugeuka kwa kasi na kumuangalia.
“WEWE NI NANI?”   
Muendeshaji ambaye ni mwanamke mwenzake, alimuuliza kwa sauti ya ukali huku akiwasha taa ya ndani ya gari lake kuiona sura ya Phidaya vizuri.
                                                                                      ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 88 YA SIMULI HII.


Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts