Get the latest updates from us for free

mas template
Home » , » SORRY MADAM -Sehemu ya 94 & 95 (Destination of my enemies)

SORRY MADAM -Sehemu ya 94 & 95 (Destination of my enemies)

Written By Bigie on Friday, February 16, 2018 | 3:58:00 PM

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA

“Nifwateni mimi”
Binti huyo wa kimasai alizungumza na kushuka kwenye kichuguu hicho. Wote wakamfwata kwa nyuma akwapeleka kwenye moja ya handaki wanalo jificha pale kunapo tokea uvamizi.  Wakakuta wamama na watoto pamoja na wazee wakiwa wamasha ingia kwenye handaki hilo wamejificha baada ya kupigwa kwa vigelegele hivyo.
“Munaweza kujificha humu na maadui wasijue ni wapi nyinyi mulipo”
Hata kabla hawajazungumza chochote, milio ya risasi ikaanza kusikika ikirindima nje ikiashiria kwamba watu hao walio kuja kwenye kijiji hicho si wema kabisa.

ENDELEA
 Karibia watu wote ndani ya handaki miili yao ilipatwa na woga. Wamama walio kuwa na watoto wadogo waliwakumbatia watoto wao huku wakiachia vilio vilivyo wafanya Sa Yoo na Shamsa kushangaa.
“Hatuwezi kukaa humu ndani na kuona watu wasio wenye hatia wakiwa wanakufa pasipo sababu ya msingi”
Phidaya alizungumza huku akiwatazama Shamsa na Sa Yoo ambao muda mwingi waliwatazama wanamama hao na watoto wanavyo angua vilio.
“Una maana gani?”
Binti huyoo wa kimasai aliuliza huku mwili ukimtetemaka. Shamsa akataka kuchomoa bastola yake, ila Sa Yoo akamuwahi mkono huo na kumzuia.
“Sio sehemu yake hii”
Sa Yoo alizungumza huku akiondoka kwenye handaki hili, akapandisha ngazi huku nyuma yake akifwatia Phidaya na Shamsa.
 
“Tafadhali usitoke baki humu ndani”
Shamsa alimueleza binti wa kimasai ambaye aliwafwata kwa nyuma walipo kuwa wakitaka kutoka. Bimti huyo akawa muelewa na kurudi ndani ya handaki.
   Milio ya risasi iliendelea kurindima, huku vijana wa kimasai wanao tumia silaha za jadi wakiendelea kuteketea kwa maana uweozo wao wa kupambana ni mdogo kuliko uwezo wa wanajeshi hao.
Hapakuwa na mazungumzo zaidi ya kuhakikisha kwamba wanatetea kijiji hicho kinacho poteza watu wake kwa sababu yao. Kila mmoja akakimbilia katika sehemu  ambayo anaweza kuhakikisha kwamba haonekani na kuanza kujibu mashambulizi ya wanajeshi hao
                                                                                                                      ***
“ARGAAAAAAAAAAAAAAAAAAA…………..”
Ukelele mkali ulisikia katika moja ya chumba kilichopo chini ya ardhi kwenye handaki ambalo, mikaka kadhaa ya nyuma iliyo pita, lilikuwa likitumika kama maficho ya majambazi wa kike walio tokea kuitingisha serikali ya Tanzania.
Sura ya Rahab iliyo jaa hasira na uchungu mwingi ikaendelea kuonekana mbele ya uso wa raisi Godwin ambaye amening’inizwa hewani kwa mikono yake kufungwa na kamba ngumu ya manila, kila mkono umefungwa upande wake, na miguu yake nayo imefungwa kila mmoja upande wake. Huku mwili wake ukiwa hauna nguo hata moja.
Kitu ambacho Rahab anakifanya ni kila mara kupiga teke kwa chini kwenye sehemu za siri za Mzee Godwin na kumfanya atoe ukelele mkali.
“Niue tu lakini sio kunifanyia unyama wa aina hii”
Mzee Godwin aliye jaa damu kwneye sura yake iliyo chakaa kwa kipigo kilali alicho patiwa na Rahab, alizungumza huku akimtazama Rahab, aliye mjibu kwa kumtandika ngumi moja kali ya uso, na kuzifanya damu kuzidi kumtoka raisi Godwin kwenye sura yake.
 
“Mume wangu Praygod, alikufa kifo kikali cha kikatili na wewe ndio msababishaji wa hili”
“Mimi sifahamu hilo”
“Ahaaa ufahamu si ndio?”
“Ndio sifahamu”
“Basi kwa kipigo hichi utafahamu tu”
Rahab akachukua mashine maalumu ya shoti, akachukua nyaya mbili za hasi na chanya moja akaifunga katika uume wa mzee Godwin na mwengine akaufunga kwenye gololi za mzee huyo, kisha akarudi mezani ilipo mashine hiyo yenye swichi ya kuongezea mtetemesho wa shoti.
 
Bila hata ya huruma, Rahab akaiwasha mashine hiyo na kumfanya mzee Godwin kutetemeshwa karibia mwili mzima. Mzee Godwin alizidi kulia kwa maumivu makali sana anayo yapata. Tangu kwenye maisha yake yote hakuwahi kuweza kukutana na maumivu makali ya namna hiyo japo alikuwa ni mwanajeshi na aliweza kukutana na waalifu wengi alio weza kuwabana na mashine hiyo ya shoti ila kwa sehemu alipo wekewa nyanya hio ndivyo jinsi alivyo zidi kuona maisha yake yanakwenda ukingoni hata kabla ya kufanikisha malengo yake ya kuifanya nchi ya Tanzania kuwa na utawala wa kifalme na si wa uraisi tena.
 
Maumivu makali aliyo yapata yakapelekea mzee Godwin kupoteza fahamu hapo hapo. Hilo wala halikumuogopesha Rahab alicho kifanya ni kuzima mashine hiyo. Akachukua ndoo kubwa, akaingia bafuni akakinga maji kwenye bomba hadi, ndoo hiyo ikajaa. Akarudi nayo kwenye chumba cha mateso, akamwagia maji hayo mzee Godwin na kumfanya kustuka kutoka katika hali ya kupoteza fahamu.
“Zoezi letu linaendelea pale pale”
                                                                                      **(MASAA KUMI NYUMA)
     Baada ya Phidaya kuingia ndani, kwa haraka Rahab akapiga hatua hadi pale alipo lala raisi Godwin, akapiga na kitako cha bunduki kichwani na kumfanya raisi Godwin kuzimia hapo hapo. Kutokana na uwezo wake wa ziada wa nguvu zake ambazo siku nyingi hazitumii, kutokana na watu walio mzunguka. Akambeba mzee Godwin begani mwake na kutoka naye hadi nje, akamuingiza kwneye moja ya gari la askari wake alio kuja nao hapo.
 
Akaingia upande wa dereva na kuondoka eneo hilo, kwa mwendo wa kasi huku miyoni mwake akiwaomba msamaha weze kwa kitendo hicho cha kuondoka na Mzee Godwin ambaye wanamuwinda wote.
Rahab akazidi kuendesha gari hiyo kuelekea katika barabara ya Tegeta, inayo pitia mkoa wa Pwani, njia nzima Rahab akawa anaomba kutoweza kukutana na kizuia ambacho jana yake waliweza kukutana nacho.
     Maombi ya Rahab hayakuweza kufanya kazi kwani kizuizi hiyo kilikuwepo tena kwa muda huo ulinzi ulizidi kuongezwa kutokana na taarifa iliyo tolewa kwamba raisi wa nchi ametekwa na wanawake ambapo picha zao ziliswambwazwa kwa haraka kupitia vyombo vya habari. Ukaguzi wa gari zote zinazo pita katika kizuizi hicho ulifwanywa kwa umakini mwingi.
 
Taratibu Rahab akalisimamisha gari lake pembeni. Akashuka na kufungua kwenye butiya gari hilo. Kwa bahati nzuri akakutan silaha moja inayo tumika katika kufyatulia mabomu yanayo itwa ‘Rocate Ranger’. Bila hata ya kujiuliza maswali mara mbili mbili. Akalifunga bomo moja, kisha akasimama katikati ya barabara. Akavuta pumzi nyingi huku mzinga huo akiwa ameuweka begani mwake. Akalifyatua bomu hilo lililo kwenda kwa kasi na kulipua magari ya polisi yaliyo kuwa karibu na kizui hicho. Mlipuko mkubwa wa gari mbili za pilisi ukawafanya askari na wanajeshi walipo katika eneo hilo kuchanganyikiwa.
Akarudu kwenye buti na kuurudisha mzinga huo, kisha akachukua bunduki aina ya MK 47, iliyo chomekwa magazine zenye risasi za kutosha. Akachukua magazine sita na kuzichomeka kwenye mfuko wa surulai yake. Alipo hakikisha kwamba yupo sawa, akafunga buti ya gari hilo na kuanza kufyatua risasi kuelekea walipo wanajeshi na polisi huku akiwafwata.
 
Shambulizi hilo lilizidi kuwaangusha wanajeshi na askari ambao  wala hawakutarajia kama kuna ambushi ya namna hiyo inaweza kuokea eneo hilo kwa wakati huo.
Askari walijaribu kurudisha mashambulizi lakini hawakuweza kwani adui yao hawakumuona kwa haraka ila walicho kumbana nacho ni risasi tu. Watu walio kuwa kwenye magari yao walichanganyikiwa, wengine walishaka na kukimbia kuyaokoa maisha yao, ila wengine walibaki kwneye magari yao wakiamini kwamba hiyo ndio sehemu watakayo okoa maisha yao.
Jinsi  watu walivyo tawanyika ndivyo jinsi ilivyo wachanganya wanajeshi wachache walio bakia, kwa maana hawaruhusiwi kushambulia raia ambao hawana hatia. Rahab ambaye kwa mara kadhaa alijibanza kwenye magari, aliendelea kuwashambulia na kuwaa wanajeshi na askari wote.
 Akaanza kuwakagua askari na wanajeshi mmoja hadi mwengine kuangalia aliye hai, alimshindilia risasi, aliye kufa alimuacha.
 
“Pumbavu”
Rahab alizungumza baada ya kuona shambulizi lake limekamilka. Akarudi kwenye gari na kumkuta mzee Godwin ndio  anastuka, huku akijitingisha kichwa chake akijaribu kufikiria ni eneo gani ambalo yupo. Akampiga kisukusuku cha shingo na kumfanya azimie tena.
Akawasha gari na kuanza kuipitisha pembeni ya barabara hadi kwenye kizuizi kilicho wekwa. Akashuka akamvua mwanajeshi mmoja nguo  zake akaziweka begani na kurudi kwenye gari, akamtoa mzee Godwin naye akamuweka begani. Akavuka kizuizi hicho cha geti na kumuingiza mzee Godwin kwenye moja ya gari la jeshi. Akaliwasha na kuondoka eneo hilo kwa mwendo wa kasi. Kila aliye badi katika neo hilo hakuamini kujiona amesalimika na wanajeshi na askari walio kuwa wakiwakagua magari wamesalimika.
 
     Rahab akaanza kuvua nguo zake moja baada ya nyingine. Huku akiliendesha gari hilo la jeshi kwa mwendo wa kawaida. Akazivaa nguo za mwanajeshi aliye mvaa na kuendelea na safari yake. Moja kwa moja akaelekea kwenye msitu ambao kuna handaki lao ambalo ni miaka mingi imepita hajafika.
 
Akafanikiwa kufika katika handaki hilo, akashuka huku bunduki yake ikiwa mkononi, akayachunguza mazingira hayo yaliyo yaa nyasi nyingi. Akafungua mfuniko wa handaki, na kuanza kushuka taratibu kwenye ngazi za kueleka chini. Japo kuna giza nene sana, ila hakuweza kuogopa. Akafika sehemu anayo fahamu kuna swichi ya kuwashia taa ndani ya handaki hilo. Akaiwasha mwanga mkali ukatwala ndani ya handaki hilo. 

Akaendelea kukagua chumba kimoja hadi kingine. Ila vitu akavikuta vikiwa vimechanguka changuka kwneye baadhi ya vyumba, alipo ridhishwa na chumba hicho, akatoka kwenye handaki. Akaelekea kwenye gari, ila kitu kilicho mstua ni mlango mmoja wa gari hilo la jeshi kuukuta wazi. Kwa haraka akakimbilia hadi kwenye gari, akamkuta mzee Godwin akiwa hayupo. Ila kwa bahati nzuri, michiziri ya damu na alamaza za miguu, iliyo jichora kwenye ardhi kutokana na ardhi hiyo kulowana na mvua iliyo nyesha usiku katika eneo hilo. Akaanza kuifwatilia miguu hiyo kwa mwendo wa kasi na kwa tahadhari kubwa. Hakufika mbali akamuona mzee Godwin akijikongoja akijaribu kukimbia.
 
Akamuwahi na kumuangusha chini. Mzee Godwin akajaribu kuonyesha ubavu kwa Rahab, ila alicho kutana nacho ni aibu tupu kwake, kwani kipigo kikali aliambulia kutoka kwa binti huyo anaye onekana kuwa na nguvu ambazo hata mzee Godwin zilimuogopesha kwa maana hata ngumi anayo mshushia ina ujazo mkubwa hata zaidi ya mwanaume.
 
Uso wa mzee Godwin ulichanwa maeneo ya jicho la kushoto kwa ngumi nzito iliyo tua eneo hilo sekunde chache zilizo pita na kusababisha damu nyingi kumwagika. Rahba alipo hakikisha raisi Godwin amelegea twepele tepwele. Akaanza kumburuza hadi lilipo gari, akafungua nyuma ya gari hilo aina ya ‘Pick Upp’ kulipo funikwa na turubai. Akakutana na mashine moja kubwa ya shoti pamoja na baboksi aliyo yafungua akakuta yana chokleti, biskuti pamoja na juisi, vyakula ambavyo wanavitumia wanajeshi pale wanapo kuwa wameweka kambi sehemu.
 
Kabla hajalifunika bosky hilo akaona kamba kubwa ya manila iliyo pembeni ya boski pamoja na kisu kidogo cha kukunja na kukunjua.
Akaichukua kamba hiyo na kumfunga Mzee Godwin kwenye miguu na kuanza kumburuza kuelekea ndani ya handaki hilo. Mzee Godwin akajikuta akishangaa handaki hilo kwa maana hata yeye kuna kipindi  alisha wahi kujificha humo. Rahab akafungua chumba kimoja akatoa kitanda kilicho kuwa katika chumba hicho na kuvihamishia sehemu nyingine. Alipo maliza ndani ya chumba hicho kuna vyuma vilivyo chomekwa kwenye ukuta.
 
Akachukua kamba hiyo ya manila, akazikata katika kamba nne na kumfunga mzee Godwin ambaye hajiwezi kufanya chochote, kwenye mikono pamoja na miguu. Alipo hakikisha amemaliza zoezi hilo dogo. Akamvua nguo zake zote na kubakiwa mtupu. Kisha akampandisha kwenye vyuma hivyo na kumchanua kama vile watu wanao wamba ngozi ya ng’ombe au mbuzi.
    Akarudi kwenye gari, akaihamishia mizigo yote iliyopo kwenye gari hilo ndani ya handaki, alipo hakikisha kila kitu kimekwisha akafunga handaki kwa ndani na kuingia kwenye chumba alipo mzee Godwin na kuanza kumuhoji maswali ambayo mzee Godwin hapo mwanzo hakushirikiana naye katika kumjibu ila kipigo kilipo anza akajikuta akijibu kwa kusua sua. Ila alipo anza kupigwa sehemu zake za siri, hapo ndipo alipo mjua Rahab ni mkatili sana
                                                                                                                     ***
      Milio ya risasi ilisikika kupitia simu ya upepo iliyopo kwenye moja ya meza katika chumba cha mawasiliano ndani ya ikulu.
“Unaisikia hiyo milio”
Manka alizungumza kwa kufoka huku akimtazama makamu wa raisi, aliye mkazia jicho. Manka akaichukua simu hiyo ya upepo na kuisogeza karibu na mdomo wake.
“Waziri wa ulinzi ninazungumza hapa, tupeni ripoti ni kitu gani kinacho endelea?”
“Muheshimiwa, tunashambuliwa huku na wanakijiji”
Sauti ilisikika kwa kila mtu katika chumba hicho na kiwafanya wote kuwa kimya.
“Wanakijiji gani?”
“Ni wamasaidi wana silaha za jadi muheshimiwa. Vijana wangu wanazidi kupungua muheshimiwa”
“Nimesema rudisheni majeshi nyuma”
Gafla makamu wa raisi akampokonya Manka hiyo redio ya upepo na kuisogeza mdomobi mwake na kumfanya Manka kukasirika.
 
“Nimesema yoyote atakaye ingilia opareshini hii, muueni sawa”
“Sawa mkuu”
Manka, akakunja ngumi huku akiyang’ata meno yake. Kitendi cha makamu  wa raisi kumgeukia huku akiishusha simu hiyo ya upepo kutoka katika usawa wake wa mdomo, akakutana na ngumi moja ya shavu iliyo muangusha chini hadi miwani yake kubwa kiasi ikaangukia pembeni. Makamu wa raisi akajaribu kurudisha kombora hilo, alilo patiwa na Manka ila akajikuta akikutana na ngumi nzito mbili zilizo tua kifuani mwake, zikamnyumbiasha na kumuangusha chini.
Viongozi na wafanyakazi walio kuwa katika chumba hicho wote wakajikuta wakishangaa, kwani wengi wao ndani ya chumba hicho wapo kinyume na makamu  wa raisi kwa maana ana tumia mamlaka yake vibaya.
 
Manka akapiga hatua hadi alipo anguki makamu wa raisi anaye jizoa zoa kunyanyuka. Akaiokota simu ya upepo huku akimtazama mzee huyo, aliye itibua hasira yake.
“NIMESEMA KAMA WAZIRI WA ULINZI, RUDISHENI MAJESHI NYUMA NA MURUDI KAMBINI”
“Sawa madam”
Manka akaiweka simu yake pembeni. Kabla hajafanya kitu chochote simu yake ikaita, akaitoa mfukoni na kuipokea pasipo kupokea.
“Manka ninakuomba unirudishie Erickson wangu”
Sauti ya Agnes ilisikika masikioni mwa Manka na kujikuta akiwatzama watu waliomo ndani ya chumba hicho cha mawasiliano. Akatoka katika chumba hicho ili azungumze vizuri na Agnes.
“Una uhakika na unacho kizungumza?”
“Ndio nina uhakika wa asilimia mia moja wewe ndio uliye mchukua Erickson”
“Hembu nisikilize wewe malaya. Urafiki wangu mimi na wewe usiwe ni chanzo cha kuzungumza upumbavu kama huo, na kama ungekuwa na uchungu na huyo Erickson ungemtafuta tangu jana sawa”
 
“Ahaaa mimi leo Malaya si ndio?”
“Ndio, si ndio kazi uliyo kuwa unaifanya udogo wako, tena iwe mwisho kunitafuta”
Manka akakata simu, alipo geuka nyuma akamkuta John akiwa na mlinzi wake, akawatazama kwa macho makali na kusubiria wanacho taka kukizungumza.
“Ninasikia kwamba mkuu ametekwa?”
“Sio swali hilo ni jibu”
“Hadi sasa hivi mumefikia wapi?”
“Unauliza hivyo kama nani?”
“Kumbuka kwamba mimi ndio msaidizi wake kwenye chama cha D.F.E”
“So nikusaidieje ikiwa wewe ndio msaidizi wake?”
Majibu ya Manka yakamkatisha hata tama John ya kitu ambacho alipanga kukizungumza kwa wakati huo. Manka akaondoka, na kurudi katika chumba cha mawasiliano ambapo  humo kwa watu ambao sio wahusika wa ngazi za juu au si mfanyakazi wa kitengo hicho cha mawasiliano haruhusiwi kuingia.
 
‘Anajiona jeuri, nitamuangusha’
John alijisema kimoyo moyo huku akiwa amekasirika. Akakumbuaka maneno aliyo yasikia akiwa wanamkaribia Manka sehemu alipo kuwa amesimama
‘…….Ungekuwa na uchungu na huyo ERICKSON ungemtafuta tangu jana sawa’
“Nirudishe kwenye gari sasa hivi”
John alizungumza huku akiendela kuyafikiria maneno hayo. Wakapifaka kwenye maegesho kabla hajaingizwa kwneye gari, akawa amepata picha kamili ya kitu alicho kuwa akifikiria.
“Erickson yupo humu ikulu”
“Umejuaje bosi?”
“Huyu Manka nahisi alikuwa anazungumza na Agnes ambaye anahangaika kumtafuta huyo Erickson”
“Sasa mkuu unahitaji mimi nifanye nini?”
“Hakikisha unajua ukweli na kama yupo humu ndani yah ii ikulu, hakikisha kwamba unamuua”
“Sawa mkuu”
                                                                                                               ***
      Agnes akakata simu aliyo kuwa ameiweka loudspeaker na wezake watatu alio kuwa nao ambao ni Anna, Fetty na Halima walisikia mazungumzo yote na wote wakajikuta wakiwa wamechukizwa na maneno ya Manka.
“Ina maana anatumia mabavu kukuchukulia mpenzi wako si ndio?”
Fetty alizungumza huku macho yakiwa yamemtoka.
“Ndio maana yake.”
 
“Ni lazima tumuonyeshe sisi ni nani kwa maana naona hatujui vizuri”
“Kitu kingine kama nilivyo waambia ni lazima kumrudisha Rahab kwenye timu na kitakacho fwata hapa ni lazima kumuangusha Manka na baba yake”
“Umoja”
Halima alizungumza huku akinyoosha mkono wake wa kushoto alio kunja ngumi, wote wanne wakaikutanisha mikono yao ya kushoto walio kunja ngumi.
“Umoja ni nguvu, utengango ni udhaifu”
Walizungumza kwa pamoja huku wakikumbatia kwa pamoja, wapanga kuuangusha utawala wa mzee Godwin na mwanaye Manka

SORRY MADAM (95) (Destination of my enemies)

“Sasa jamani na hivi nyeo vyetu inakuwaje?”
Halima aliwauliza wezake huku akiwatazama.
“Vyeo tunaitumia kuiangusha serikali taratibu hadi wao wenyewe watafurahi na mziki wetu”
Fetty alizungumza kwa kujiamini na kuwafanya wezake kufurahi kwa yale waliyo yapanga.
 ***
   Kadri muda uliyo zidi kwenda ndivyo wanajeshi walivyo zidi kuteketea japo walijitahidi kadri ya uwezo wao kujibu mashambulizi, ila mikuki ya vijana wa kimasai nao iliwadhuru sana kwa sumu kali iliyo kuwa katika mikoku hiyo.
“Tusarendee, majeshi yote yarudi nyuma”
Mkuu wa jeshi alizungumza na wanajeshi wote wakaanza kurudi nyuma. Wakaingia kwenye magari yao na kurudi walipo toka. Kitendo hicho kikawashangaza sana, Shamsa, Phidaya na Sa Yoo ambao kwa bahati nzuri hawakuudhurika kwa risasi.
Kazi ikawa ni kuanza kuwasaidia majeruhi, ambao walikuwa wengi. Kila Sa Yoo alipo zitazama maiti za vijana hao moyo wake akahisi ukimuuma sana kwa maana hakupenda kuona damu za vijana hao zina mwagika kwa makaosa yao.
“Inabidi tuondoke kwenye hiki kijiji. Kukaa kwetu hapa kunaweza kukaleta matatizo mengine kwa wanakijiji”
“Lakini Shamsa hatuwezi kuondoka pasipo kuweza kufanya msaada wowote kwa wanakijiji hawa, tukumbuke sisi ndio chanzo”
 
“Sasa Sa Yoo unahisi tunawasaidia kitu gani?”
“Tuwasaidie hata pesa”
Phidaya alizungumza na kuwafanya Sa Yoo na Shamsa kumtazama usoni kila mmoja akishangaa kauli hiyo kwa maana wanatambua kwamba hawana pesa yoyote ya kuweza kuwasaidia wananchi hawa.
“Natambua ni wapi pesa za Eddy alipo zificha na ninaimani kwamba zitatosha kuwapatia wananchi hawa”
“Zipo wapi?”
“Zipo kwenye ile nyumba yetu”
“Sasa unataka kurudi tena kule, uhisi kwamba kutakuwa na walinzi wanalinda pale”
“Mimi nitakwenda”
Shamsa alizungumza na kumfanya Phidaya kustuka kwa maana anaamini kwamba siri ya sehemu zilipo pesa hizo ni yeye na mume wake.
“Unafahamu zilipo?”
“Ndio, nyinyi bakini kuesabu familia wa wanakijiji hichi na kila familia tutaipatia  milioni kumi kumi”
“Sawa”
Phidaya akamkabidhi Shamsa Phidaya, wakaagana naye na akaelekea kwenye gari, akapanda ndani ya gari hilo, akaliwasha na kuondoka na kuwaacha Sa Yoo na Phidaya wakitoa misaada kwa vijana wa kijijini hapo walio pata majeraha.
                                                                                                                  ***
   John akiwa ndani ya gari kuondoka ikulu, simu ya mlinzi wake ikaita, akaitoa mfukoni, alipo tazama jina akampunguza mwendo wa gari na kulisimamisha, akaipokea simu hiyo na kumsogezea John karibu na sikio lake.
“Ndio”
“Muheshimiwa ndio tunafika Tanzania muda huu na tupo uwanja wa ndege”
“Sawa ninakuja”
“Tuelekee uwanja wa ndege”
“Sawa bosi”
Safari ikaanza huku John akilini mwake akiwaza ni walipi alipo mkuu wao Mzee Godwin.  Wakafanikiwa kufika uwanja wa ndege kuwapokea viongozi baadhi wa kikosi cha D.F.E Walio wahi kufika Tanzania kwa ajili ya kikao kikubwa cha kujadili namna na jinsi wanavyo weza kumpata mkuu wao.
Viongozi hao kutoka Marekani, Japan, Uingereza na Urusi, wakapanda kwenye gari maalumu ambalo John aliwakodishia. Moja kwa moja akawapelekea katika hoteli ya Serena. Huku viongozi wengine wa kikundi hicho wakiendelea kuwasili ndani ya Tanzania kadri muda ulivyo zidi kwenda.
 
    Kwa siku iyo John na mlinzi wake hawakuweza kulala kabisa, kwani wageni walizidi kumiminika, na wote wakiwa na agenda ya kutaka kujua ni kitu gani kilicho pelekea hadi kiongozi wao mkubwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha.
Siku iliyo fwata viongozi zaidi ya themanini kutoka katika nchi mbalimbali duniani, wakakusanyika katika ukumbi uliupo katika hoteli hiyo. John akiwa amekamimu nafasi ya Mzee Godwin kama mwenye kiti akawa ndio kiongozi mkubwa wa kuendesha kikao hicho.
“Inaonekana kwamba ulinzi umekuwa ni mdogo wa kiongozi hadi kuweza kutekwa kirahisi hivi tena na mabinti wadogo namna hii”
 
Mmoja wa kiongozi kutoka Afrika kusini alizungumza kwa ukali sana huku wengine wakimsikiliaza.
“Siamini kabisa kiongozi wetu kukamatwa, kama hilo swala lingetokea kwenye nchi nyingine hapo kweli ningesema kwamba ni mpango mkubwa. Ila kinacho onekana hapa ni uzembe wa kumlinda kiongozi”
“Bwana Zuma, hembu kaa chini. Kinacho takiwa kutolewa hapa ni mawazo ya jinsi gani ya kuweza kumpata muheshimiwa sio maswala ya kutupiana lawama, kwa maana walinzi aliwekewa lakini katika tukiohilo walinzi hao nao pia walipoteza maisha”
John alizungumza kwa ukali na kumfanya mzee huyo aliye onekana kuwa na hasira zaidi ya wezake kukaa chini kwa amri ya mwenyekiti John.
                                                                                                       ***
“Madam nimefanikiwa kujua ni sehemu gani alipo madma Mery”
Mpelelezi wa siri wa Manka aliweza kumletea Manka ripoti hiyo akiwa ndani ya ofisi ya baba yake akichukua jukumu la kuendesha nchi, huku makamu wa raisi akiwa amemuweka chini ya kizuizi cha walinzi wa ikulu hii ni kutokana na kutumia mamnalaka yeka vibaya.
 
“Yupo wapi?”
“Ofisi za N.S”(Nation Security)
“Andaa gari nahitaji kwenda huko kuonana naye”
“Sawa madam”
Alipo toka kijana wake huyo anaye muamini sana. Akawasha laptop ya baba yake iliyopo hapo mezani. Kitu alicho kutana nacho ni mkutano unao endelea katika hoteli ya Serena.
‘Huu mkutano umeitishwa lini?’
Manka aliwaza akilini mwake kwa maana yeye pia ni miongoni mwa wanachama wa chama hicho kilicho undwa na baba yake mzee Godwin. Mlango ukagongwa akaingia askari anaye linda nje ya mlango wake.
“Muheshimiwa kuna mgeni wako anakuhitaji”
“Ninani?”
Kabla askari huyo hajamaliza kuzungumza mlango ukafunguliwa na Erickson akaingia huku akiwa amevalia nguo maalumu wanazo vaa wagonjwa wanapo lazwa.
 
“Umeweza kutembea!?”
Manka aliuliza huku akimshangaa Erikcson aliye jikongoja hadi kwenye moja ya sofa lililopo humo ndani ya ofisi. Taratibu akaka huku mkono wake wa kulia ukijishika kwenye upande wa mbav alipo fanyiwa uparesheni.
“Mbona umetoka kule Erickson?”
“Nilikuwa nahitaji kukuona”
“Ila si una maumivu jamani?”
Manka alizungumza huku akichuchumaa mbele ya Erickson.
“Hapana dokta amenichoma sindano ya kupunguza maumivu. Nikaona nikufwate huku nionane na wewe, nikuulize kuhusiana na muheshimiwa kama amepatikana?”
“Bado hajapatikana ila anaendelea kutafutwa kona zote za Tanzania, nina imani atapatikana tu”
 
“Walio mkamata wamepatikana?”
“Amepatikana mmoja ambaye anaitwa Madam Mery ila wengine hawajapatika”
Kukamatwa kwa madam Mery kidogo kukamstua Erickson ila hakuhitaji mstuko wake kuweza kujionyesha usoni mwake. Mlango ukafunguliwa akaingia kijana wake aliye muagiza kwenda kuandaa magari.
“Muheshimiwa kila kitu kipo sawa”
“Sawa”
Kijana huyo akatoka na kumuacha Manka na Erickson wakiwa wametazamana. Taratibu Manka akajisogeza karibu na uso wa Erickson akazikutanisha lipsi zake na lispi za Erickson huku akwa ameyafumba macho yake. Erickson hakuhitaji kuzikwepesha lipsi zake kwa maana hiyo ingeweza kumletea Manka maswali mengi.
“Kuna sehemu nakwenda mara moja, sinto tumia muda mwngi baada ya lisaa ninaweza kuwa nimerudi”
“Sawa”
“Umekula?”
“Ndio”
“Basi nisubirie humu ninakuja”
“Sawa”
 
Manka akambusu tena Erickson shavuni mwake na kunyanyuka. Akatoka nje ya ofisi hiyo ya baba yake pasipo kujua kwamba mtu aliye muacha ndani ya ofisi hiyo ni adui yao namba moja. Manka akaingia kwenye gari moja inayo tumiwa na raisi. Msafara wa gari tatu za ikulu zinazo fanana zikaondoka eneo la ikulu. Erickson aliye simama kwenye dirisha alipo hakikisha kwamba gari hizo zimetoka kwenye geti la ikulu. Taratibu akarudi kwenye kiti kilichopo nyuma ya meza iliyo na mafaili kadhaa pamoja na laptop.
“Nilazima tuweze kumpata kiongozi wetu wa D..F.E”
Maneno hayo yakamstua sana Eddy na kujikuta akitazama mutano huo kwa umakini, alipo muona John akapata uhakika kwamba watu hao ndio wahusika katika kikosi hicho.
“Mungu wangu?”
Eddy alisha kwa maana wengi wa watu walio kuwemo kwenye kikao hicho wengi ni viongozi wa mataifa makubwa duniani na ni watu wanao heshimika mbele ya jamii.
                                                                                                  ***
   Manka akafika katika makao mkuuu ya ofisi za Nation Security.  Akapokelewa na mkuu wa kitengo hicho. Moja kwa moja akapelekwa kwenye chumba cha mahojiano na kukuta Madam Mery akiwa anahojiwa.
“Hadi sasa hivi amezungumza nini?”
Manka aliuliza huku akiwa katika chumba cha pili akimtazama madam Mery kupitia kioo kilicho watengeanisha na chumba hicho cha pili cha mahojiano.
“Hadi sasa hivi hajazungumza chochote zaidi ya kukaa kimya”
 
“Nahitaji nizungumze naye private na si chumba hicho”
“Ila mkuu huyo ni muhalifu anaweza kukudhuru”
“Hapana hawezi kunidhuru andaeni chumba na muniletee nizungumze naye”
“Sawa madam”
Mkuu huyo akawaamuru vijana wake wampeleke Manka kwenye chumba kingine ambacho hicho hakijategwa kamera wala vinasa sauti. Baada ya Manka kuingia, dakika tano mbeleni akaletwa madam Mery akiwa amefungwa pingu mikononi mwake.
Madam Mery kumuona Manka akastuka sana, askari walio mleta ndani humo wakatoka nje na kuwaacha wawili.
“Naona unashangaa sana kunioana hapa ehee?”
“Unahisi kuja kwako ndio kutanifanya mimi kuweza kuzungumza munacho hitaji kunihoji?”
“Hapana mimi wala sikuja na hayo. Lililo nileta hapa ni kuweza kuzungumza ukweli kati ya uhusiano uliopo kati yako mimi na wewe”
“Sijakuelewa?”
“Naamini unamtambua Joyce  Magoa”
Madam Mery kusikia jina hilo akamkazia macho Manka kwa maana jina hilo analitambua vizuri na ni jina la dada yake aliye potezana naye kwa miaka mingi sana na wala hana habari kuhusiana na yeye.
 
“Umemjuaje huyo mtu?”
“Hujanijibu, nimekuuliza kwamba  una mfahamu?”
“Ndio ninamjua”
“Ni nani kwako?”
“Ni dada yangu”
“Basi huyo alikuwa ni mama yangu, aliye nileta mimi duniani”
Madam Mery akajikuta akisimama kwenye kiti alicho kuwa amekilia, kwa mshangao mkubwa alio upata kwa manaa kwenye maisha yake hakuwahi kusikia kitu kama hicho.
“Haiwezekani msichana katili kama wewe na mwenye baba katili kama Godwin kuwa ni watu wenye mahusiano na dada yangu”
“Natambua ya kwamba unaamini kwamba sisi ni makatili. Hilo mimi wala silishangai sana kwa maana roho ya ukatiili alinipandikiza baba yangu. Kwa sasa nijitahidi kwa kadri ya uwezo wangu kuweza kuiweka familia yangu sehemu moja na sihitaji igawanyike tena”
 
“Siwezi kuwa na familia kama hiyo?”
“Mama, niamini katika hilo”
Madam Mery alipo mtazama Manka usoni, akaamini kitu anacho kizungumza kinatoka moyoni mwake kwa maana sura yake imejaa upole huku machozi yakinza kumbubujika. Madam Mery akaanza kukumbuka matukio mengi ya nyuma kabla hata Eddy hajaletwa kwenye shule aliyo kuwa anafundisha. Mzee Godwin aliweza kumjali na kumchukulia kama ni mdogo wake, hata nafasi ya kuweza kufinidisha katika shule ile aliweza kutafutiwa na mzee Godwin na hakujua ni kwa nini mzee huyo alitokea kumchunuku sana.
Pia madam Mery akakumbuka siku ya kwanza mzee Godwin anamleta Eddy katika shule hiyo, na kumkabidhi kwake na kumuambia kwamba amchukulie kama mwanaye. 
 
“Wewe ni mama yangu mdogo. Sina sababu nyingine ya mimi kuweza kuzungumza maneno hayo mbele yako. Kila ninacho kizungumza kinatoka moyoni mwangu. Na kilicho nileta hapa nahitaji kukuondoa mikononi mwa hawa watu, sihitaji wakutese. Nimeishi miaka zaidi ya ishirini na saba sina mama, tafadhali mama mdogo, naomba uchukue jukumu la kunichukulia kama mwanao”
 
Manka alizungumza huku machozi  yakimwagika usoni mwake. Madam Mery naye taratibu machozi yakaanza kumwagika usoni. Akaanza kumchunguza Manka taratibu kuanzia usoni, hapo sasa sura ya dada yake akaanza kuigundua, japo aliachana na dada yake wakiwa watoto sana pale wazazi wao walipo fariki na yeye kuchukuliwa na wafadhili ambao walimpeleka kumsomesha shule za jijini Dar es Salaam na kipindi amekua na kurudi kumtafuta dada yake kijijini alipo muacha, hakuweza kukuta nyumba wala mashamba yao kwa maana sehemu hiyo ilisha badilika na kujengwa majengo ya kifahari yaliyo badilisha kabisa taswira ya kijiji hicho.
   Taratibu madam Mery akanyanyuka na kumsogezea Manka mikono yake, akaishika mikono yote miwili ya Manka iliyopo sehemu moja na kumnyanyua. Wakakumbatia huku wote wakimwagikwa na machozi mfululizo.
                                                                                                       ***
   Shamsa akafanikiwa kufika barabani, pasipo kukutana na kikwazo chochote. Gari hiyo ya raisi akaitelekeza barabarani na kuanza kutembeakuifwata barabara hiyo inayo eleke Dar es Salaam. Kutokana ni usiku wa manane hapakuwa na gari lolote ambalo liliweza kupita. Hakuchoka akazidi kutembea kusonga mbele. Hadi inafika majira ya saa kumi na noja mabasi na magari makubwa yaendayo mikoani yakaanza kupita moja moja. Hadi inafika saa kumi na mbili na nusu, gari moja ndogo aina ya Premoe, akaisimamisha na dereva wa gari hilo akasimamisha gari lake umbali kidogo kutoka sehemu alipo Shamsa. Aliye anza kulikimbilia hadi sehemu lilipo simama.
 
“Binti unakwenda wapi?”
Mzee huyo mwenye kitambi kikubwa kinacho karibia kugusa mskani wa gari hiyo alizungumza huku akimtazama Shamsa anaye mwagikwa na jasho.
“Nahitaji kwenda Dar”
“Sawa ingia kwa manaa na mimi ndio ninapo elekea huko huko”
“Asante”
Shamsa akatazama siti za nyuma za gari hilo na kuona hakuna mtu. Akafungua mlango na kupanda.
“Binti asubuhi yote hii unatembea barabarani peke yako huogopi?”
 
“Hamna nilikuwa ninafanya mazoezi?”
Kwa jicho la kuiba mzee huyo akamtazama Shamsa vizuri kuanzi chini hadi juu, kwa nguo alizo zivaa Shamsa hazikuonyesha kabisa kama ni nguo za mazoezi kwa mana ni ngumu sana kwa mtu kuweza kufanya mazoezi akiwa amevalia jinzi na tisheti iliyo katwa mikono.
“Mbona maeneo hayo ni nyika tu hakuna hata nyumba?”
Swali la mzee liliendana na wasiwasi mwingi kwa maana alisha weza kuona picha ya Shamsa jana usiku kwenye taarifa ya habari kwamba ni binti anaye sadikika kumteka raisi Godwin.
“Ahaaa huwa ninafanya mazoezi kwa juhudi sana”
Mzee huyo hakuridhishwa kabisa na jibu alilo lisema Shamsa. Akilini mwake akapanga babisa akifika kibaha kwenye kituo cha polisi ni lazima kwenda kumripoti binti huyo na kujivunia dau la dola laki moja lililo tangazwa na serilali kwa mtu ambaye atatoa ushirikiano kukamatwa kwa mabinti hao watatu mmoja akiwa ni huyu aliye kuwa naye ndnai ya gari lake.
 
“Vizuri”
Mzee huyo alijibu huku akitingisha kichwa. Wasiwasi wake alio kuwa nao tayari Shamsa alisha anza kuustukia. Mzee huyo akazidi kukanyaga mafuta hadi akafanikiwa kufika Kibaha. Akkunjaa upande wa pili wa barabara na kuanza kuelekea kilipo kituo cha Polisi
“Huko ndio Dar?”
“Ahaa kuna jamaa ninakwenda kumuona hapo mbele kidogo”
Shamsa akachomoa bastola na kuielekezea kwenye tumbo la mzee huyo, huku akiwa amekazia macho na kama atafanya uzembe hali ya hewa itaharabika.
“Ukilete ujinga nalipasua hili tumbo lako lililo jaa maji”
Shamsa alizungumza huku jasho likimwagika na kumfanya mzee wa watu kusimamisha gari lake, huku mwili mzima ukimtemeka, na haja ndogo ikianza kuichafua suruali yake ya kitambaa aliyo ivaa.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts