Get the latest updates from us for free

mas template
Home » , » TANGA RAHA- Sehemu ya Kumi ( 10 )

TANGA RAHA- Sehemu ya Kumi ( 10 )

Written By Bigie on Wednesday, February 21, 2018 | 11:34:00 AM

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA
 Simu yangu ikaingia meseji na namba iliyoleta meseji hiyo imeandikwa PRIVETE.Taratibu nikaanza kuisoma meseji hiyo
{NIPO NJE NAKUFWATILIA KILA HATUA NA HUYO MALAYA ZENA ULIYE NAYE NDANI KWAKO NITAMUUA UKISHUHUDIA}
Nikatamani ardhi ipasuke nidumbukie.Nikazidi kuchanganyikiwa pale Madam Zena aliponiaga anataka kuondoka ili akawahi kipindi chake cha kufundisha baada ya mapumziko ya saa nne asubuhi
 
ENDELEA
 “Madam ninakuomba usiondoka please”
“Kwa nini Eddy wakati nimesha kuleta hadi nyumbani?”
“Na penda tu leo unipe  kampan yako ya kukaa hapa kwangu nakuomba”

Madam Zena akajifikiria kwa sekunde kadhaa kisha akatoa simu yake na kupiga kwa mtu ila sikujua ni nani
“Sir Barongo”
 
“Nakuomba unishikie vipindi vyangu kaka yangu kama huto jali kidogo nimepata dharura”
“Nashukuru kaka yangu haya Mungu akipenda kesho”
Madam Zena akakata simu kisha akairudisha kwenye begi lake na kuniangalia huku aikitabasamu
“Sasaa hapa ninaweza kukaa kwa amani….Ehee mgonjwa una CD gani nzuri nzuri za movie”
“Kwa CD tu hapa utakesha”
Madam Zena akachukua makasha ya CD yaliyopo chini ya meza ya kioo na kuanza kuangalia kasha moja hadi jengine hadi akakuta kasha lililoandikwa PIRATE ON BLACK SEE akaitoa CD yake na kuiweka ndani ya deki kisha akarudi kwenye sofa na kukaa.Madam Zena akaanza kuguna baada ya CD hiyo kuanza kwani imeshamiri mambo ya kikubwa yanayo onyeshwa live bila chenga
“Sir Eddy hivi hizi CD unazitolea wapi?”
“Kwa nini?”
“Huwa ninazitafuta ila sizipati”
“Kuna maeneo ya pale forozi karibu na benki ya NMB kuna jamaa best yangu anaziuza”
“Bei gani?”
“Elfu tatu”
“Basi kuna vijana walinipitishia wakaniuzia kwa elfu ishirini”
“Dooo wamekutapeli hao”
 
“Tena wamenitapeli sana kwani CD lenyewe lina scratch kama nini”
“Basi nitakutafutia”
Madam Zena akaendelea kutazama CD huku akionekana kunogewa kwa jinsi watekaji wa meli katika CD hiyo wakipeana mambo matamu,Nikatazama Wallet yangu na kukuta  nina pesa ya kutosha.
“Zena ngoja nikanunue chakula cha mchana”
“Haupiki?”
“Sijisikii kupika”
“Lakini mimi si nipo ninaweza kupika”
“Utapika siku nyingine ila nakuomba kama mtu yoyote akigonga usimfungulie hadi usikie sauti yangu”
“Sawa ila ni kwanini?”
“Watu wa mtaa huu ni wasumbufu sana na wamesha anza kunizoea vibaya”
“Sawa au unaogopa vimanzi vyako vitakuja?”
“Sina manzi wala nini wewe fanya kama nilivyo kuambia……………Nikuletee kinywaji gani?”
“Kwanza unakwenda kununua nini….”
“Alafu sikukuuliza nikuchukulie chakula gani?”
“Mimi niletee chipsi yai na kuku nusu nikipata na castel mbili baridi utakuwa umeifanya siku yangu ikawa powaaa”
“Powa nitafanya hivyo ila na wewe fanya kama nilivyo kuagiza usije ukafungua mlango”
 
“Sawa Eddy nimekuelewa”   
Nikatoka chumbani kwangu na Madam Zena akaufunga mlango wangu kwa ndani lengo langu ni yeye kuweza kuwa katika hali ya usalama kwani kuna watu wameanza kunipa vitisho kwa njia ya meseji.Nikamsalimia bibi kizee mwenye umri kwa makadirio yangu unao fika miaka 70 hivi.Aliyekaa nje ya nyumba ya jirani na ninapo ishi
“Marahaba mjukuu wangu.Hujambo baba”
“Sijambo haya mimi ninapita”
“Sawa…..ila kijana nakuomba mara moja”
Nikamsogelea sehemu aliyokaa na akanionyesha sehemu ya kukaa huku macho yangu yakilichunguza eneo la hapo kwani mtu aliye nitumia meseji alidai yupo maeneo haya huku akijua nipo na nani ndani kwangu
“Kijana unaitwa nani?”
“Ninaitwa Eddy”
“Ahaaa Eddy mjukuu wangu inavyoonekana wewe ni mgeni hapa Tanga?”
‘Ndio”
 
“Wewe ni mwenyejii wa mkoa gani?”
“Morogoro ila nimeishi sana Iringa”
“Ahaaa…….Eddy wewe ni sawa sawa na mwanangu au mjukuu wangu unapoenenda kinyume inanipasa nikurekebishe”
Nikaanza kujifikiria ni makosa gani niliyo yafanya hadi huyu bibi anasema anataka kunirekebisha
“Ndio bibi”
“Eddy mwanangu wewe unatabia moja ambayo unaifanya na inanishangaza sana  na kunikera”
“Tabia gani bibi yangu?”
“Eddy wewe unatabia ya kufungulia mredio wako kwa sauti ya juu na wala huangalii kama kuna nyumba za majirani.Mjukuu wangu mimi hapa ninaugojwa wa moyo sasa nikisikia ile midundo ya jiredio lako basi unaniweka katika hali mbaya kama nini”
“Sawa bibi nime kuelewa sinto fanya hivyo tena”
‘Itakuwa vizuri sana kama ukinielewa……Na kingine mjukuu wangu kuna wasichana jana usiku niliwaona wanaingia upande wa nyumba yako”
 
“Ndio alikuwa ni Mama Fatuma na rafiki yake kidogo jina limenitoka wanaishi mtaa wa hapo mbele”
“Swadataa huyo Mama Fatuma mimi ninamjua kwa jina lake alisi anaitwa Asha……Mjukuu wangu yule mwanamke hapa mtaani kwetu hana hata rafiki na isitoshe ni mwizi sasa wewe wakaribishe karibishe ndani kwako watakuibia wakurudise nyuma kimaeneleo”
“Kumbe ni waizi…..!!?
“Mjukuu wangu wala usiseme kidogo kigogo wale ni mijiwezi hapa mtaani watu wanashindwa kukuambia tu labda kutokana hawajakuzoea……..Na mtindo wao wale ni kuwawekea waname dawa inaitwa Limbwata hiyo huweka kwenye chakula ukila tuu unajikuta unampenda hadi anakukomba kila kitu ukija kustuka umebaki mtupu hata chupi za ndani utakuwa huna”
   
Hapo ndipo nikaanza kupata picha na kujiuliza ni kwanini jana Mama Fety(Fatuma) alimuagiza mwanae aniletee chakula pasipo yeye kuja na kwanini alipokuja usiku walikuja wawili wakawa wanapeana ishara za macho na mbaya zaidi alionekana mnyonge nilipokuwa nimemuambia sijanywa chai aliyoletwa asubuhi na akaanza kunilazimisha aende kunionyesha mjii
“Mjukuu wangu hayo maneno ninayo kuambia uyaweke akilini tena sana kwani wale mabinti si watu wazuri.Na wanakijana waoo mdogo hivi wa kiume mweusi mweusi sijui anaitwa nani..?”
“Jumaa”
“Eheee huyo huyo huyo huwa wanamtuma kwenda kutazama mazingira ya chumba cha mtu wakikuona unavitu vya thamani basi ndio ukaribu unaanza na mwisho wake ni kukupuna kila kitu ulicho nacho”
Nikashusha pumzi nyingi huku nikimtazama bibi na kila kitu anacho kizungumza ni kweli kimetokea kwani siku tu niliyonunua vitu vya ndani kwangu mtoto Jumaa aliniomba aje kuangalia mpira na sikujua ni nani aliye muambia kwangu nimenunua DSTV.
 
“Mjuukuu wangu hao wanawake si wazuri kabisa yaani watakutia matatizoni wakati wewe kijana bado mbichi unatafuta maisha……Ngoja kuna dawa nikuletee uwe unajipaka mikononi hata mtu mwenye nia mbaya na wewe hata weza kukudhuru kirahisi”
“Sawa bibi”
Bibi akanyanyuka kivivu vivu na kuingia ndani mimi nakabaki ninajiuliza maswali,Gafla maswali yote yakakata baadya ya kumuona mtu aliyevalia baibui ninja akimalizikia kuingia katika upandea wa nyumba yangu na nikajua moja kwa moja anaelekea chumbani kwangu kwani katika upande huo wa nyumba ninaishi peke yangu.Nikanyanyuka haraka na kuanza kupiga hatua za kueleka nyumbani kwangu huku  nikijiuliza ni nani anaye kwenda ndani kwangu.Kitendo cha kufika usawa wa chumba changu naye mtu huyo akaingia ndani kwangu na mlango ukafungwa.Kwa haraka nikapiga hatua hadi mlangoni kwangu nikausukuma mlango nikakukta umefungwa kwa ndani.
 
“Zena…..Zena”
Nikaita mara mbili ila sikuitikiwa zaidi ya kuisikia sauti ya TV yangu.Nikagonga  mara mara tatu mfululizo na mlango ukafunguliwa na Madam Zena huku akiwa anatabasamu ila macho yake yana uwekundu kiasi.
“Eddy vipi mbona high high kuna tatizo?”
Nikachungulia na kumuona Madam Rechol akivua baibui lake na kukaa juu ya sofa langu,Kidogo mapigo ya moyo yakatulia
“Ehhe mgojwa mboa unazunguka zunguka na jua si  utajiongezea homa?”
Madam Recho alizungumza huku akinyanyuka kwenye sofa na kuja kusimama kwenye mlango
“Hapana nilikuwa nimekwenda kununua chakula”
“Sasa chakula chenyewe mbona hujaja nacho?”
 
“Ndio nataka niende hivi”
“Eddy saa zote hizo”
“Nisubirini ninakuja”
Nikaondoka na kuwaacha wakirudi ndani nikafika kwa bibi na kumkuta nje akishangaa shangaa
“Mjukuu wangu nilidhani umenitoroka”
“Hapana bibi kuna rafiki yangu nilikwenda kumkaribisha”
“Sawa,sasa mwanangu haya mafuta ni ya mti wa mzaituni yametoka huko uarabuni ila haya mafuta nimeyachanganya na dawa nyingine za asili.Utakuwa unapaka kwenye viganja vyako kila asubuhi ukiwa unataka kutoka kwenda kwenye mishuhuliko yako”
“Asante bibi yangu”
Nikachukua kichupa kidogo na kukiweka mfukoni kisha nikatoa elfu kumi na kumpa kama asante japo mara ya kwanza alisita sita ila akaipokea
“Ukiwa na shida yoyote mjukuu wangu inayohusiana na tiba asilia usisite kuniambia”
 
“Sawa bibi yangu”
Nikaondoka na kwenda kwenye baa ambayo nilinunulia chakula juzi usiku.Nikatoa idadi ya saani ninazo zitaka  kwa mpishi wa jikoni.Akaanza shughuli ya kunitengenezea chakula,Haikuchukua muda sana mpaka chakula kukamilika.Akanifungia kwenye mfuko mmoja mkuwa nikamlipa pesa yake na nikanunua bia za kopo kumi na mbili na soda mbili take away na kurudi nyumbani.
Nikiwa njiani ninarudi kwangu nikaona jamaa wawili wakinifwatilia kwa nyuma na kila nilipogeuka wakasimama na kujifanya wanafanya mambo yao.Nikaendelea huku nikianza kujiandaa kwa chochote watakachotaka kukifanya.Nikaongeza mwendo nao wakaongeza mwendo,sikuwa na wasiwasi sana kutokana nimefika karibu na nyumbani kwangu na eneo nililopo lina watu wengi wakiendelea na shughuli zao.Nikamkuta bibi nje kwake kwa kuwazuga nikaenda kukaa naye na jamaa wakapita huku wakinitazama kwa jicho la kuiba iba
“Wezi wengine walee vijana wawili walio ongozana waangalie miguu yao ilivyo mibaya”
 
Bibi alizungumza huku akiachia msunyo mkali na ikanibidi nicheke kwani jinsi sura yake alivyo iweka ikanipa nafasi ya kuyaona mapengo yake mdomoni kwake
“Huu mtaa una wezi ehee?”
“Ehhee ila hapa kwangu hawaibi”
“Kwa nini bibi?”
“Ninawatoa vibusha wao wenyewe wananijua mimi ni nani”
Nikacheka na kumpa bibi soda moja kisha nikamuaga na kwenda nyumbani kwangu,nikagonga Zena akanifungulia mlango,Cha kushangaza nikamkuta Recho amejifunga taulo huku Zena akiwa amejifunga khanga moja
“Ehee wageni naona mumebadilisha mavazi?”
“Eddy huku ndani kwako kuna joto kama nini ndio maana Rechol akavaa taulo lako”
“Na wewe hiyo khanga umeipata wapi?”
“Niliikuta hapo chini ya sofa kwa upande wa chini imeanguka au ni ya wifi?”
“Hakuana wifi wal nini….Movie haijaisha bado?”
“Bado hapa naona ikitupandisha midadi”
“Mmmmmm……… Jamani chakula nimekiweka kwenye mfuko mmoja na kama mtu utahitaji kula pekeyako nikutolee sahani kwenye kabati?”
 
“Tutakula humu humu kwani hakuna ubaya wowote tukila pamoja”
“Mmmm jamani kuwanunulia niwanunulie hata kuwatengea niwatengee?.Zena hembu nyanyuka utenge chakula”
“Yes Sir”
Sote tukajikuta tukicheka na Zena akanyanyuka na kuchukua jagi na bakulia akachota maji kwenye ndoo iliyop ndani kwangu kisha na kuanza kutunawisha mmoja baadaya ya mwengine
“Rechol kwangu umepajuaje?”
“Zena alinipigia simu akanielekeza ndio nikafika”
“Ahaa kuna jipya gani shule?”
“Hakuna chochote zaidi ya kuchoshana mishaara hawaitoi na sisi tutaendelea kutegea vipindi hivi hivi tuone kama mitoto yao haita feli”
“Ila Zena tunatakiwa kuwa na uvumilivu”
“Eddy wewe unasema hivyo kutokana kazi umeianza juzi juzi sisi wenye miaka zaidi ya mitatu kazini hapa tunajionea maruwe ruwe tu”
 
Tukaanza kula taratibu na nikajikuta nikianza kujiuliza kuwa khanga aliyo ivaa Madam Zena ameingiaje ndani kwangu.Na ninani aliye ileta ndani kwangu nikakumbuka ilikuwa ni ghanga ya Saumu rafiki wa Mama Fety,Jana usiku walipokuja alikuwa ameishika mkononi huku akiwa ameikunja
“Eddy mbona upo kimya?”
“Kuna vitu nilikuwa nina vifikiria”
Simu yangu ikaita na namba inayopiga ni ngeni nikaiacha ikaita hadi ikakata,Ikapigwa tena aikanibidi niipokee ila nikakaa kimya.Nikasikia sati ya msichana akiwa analia
“Sir Eddy nakuomba unisamehee ile ilikuwa ni hasira tu yaani umeamua kuniumiza kwa kutemea na madam Zena”
Nikajua moja kwa moja ni Rahma ilizungumza huku nikimsikia akilia kwenye simu
“Wewe ni nani mwenzangu?”
“Sir Eddy yaani hata sauti yangu umeisahau Mimi ni Rahma”
“Yupi?”
“Jamani Sir Eddy mbona unamakusudi Mimi Rahma mpenzi wako”
 
“Samahani dada utakuwa umekosea namba”
“Eddy jamani si wewe tafadhali mpenzi wangu siwezi kuishi bila wewe nimejaribu kukutoa katika moyo wangu ila nikajua mimi ndio mwenye makosa ila tafadhali Eddy mpenzi wangu nakuomba unisamehe ehee”
“Tafadhali dada nakuomba tuheshimiane nakuambia utakuwa umekosea namba na huyo mtu unaye mpigia mimi wala simjui labda atakuwa anaishi nyumba ya jirani”
Nikakata simu kwa hasira na kuizima nikawafanya Madam Rechol na Zena kuanza kucheka hadi wakaacha kula chakula
“Mamaaa weee kumbe Sir Eddy unazungumzaga pumba kiasi hicho?”
Madam Zena alizugumza huku akiendelea kucheka na kunifanya na mimi niungane nao kwenye kucheka.
“Yaani Eddy mtu akikuangalia usoni hivi atasema wewe bonge la mstaarabu kumbe pumba kama wewe hakuna…..Unamwambia mtoto wa watu eti mtu huyo anakuwa anaishi nyumba ya pili wakati humjui”
 
“Sir Eddy au umetia mbimba unakimbia majukumu?”
“Mimba wapi nyinyi wanawake munazingua”
“Ehhee jamani Eddy leo umenifurahisha…..Redio yako ni ina USB system?”
“Ndio..”
Madam Rechol akasimama na na kufungua pochi yake na kutoa FLASH kisha na kuichomeka kwenye redio akachukua rimoti na kuanza kuchagua mziki na kusikiliza na kuweka mziki unaoitwa ‘ALAJI’ na kuanza kucheza huku akiongeza sauti na kuanza kucheza huku akiyatingisha makalio yake huku ametuelekezea sisi
“Eddy umemuona mtoto huyo huko kwenu haya mambo yapo?”
 
“Yapo wapi nayajulia huku”
Mlango wa ndani kwangu ukagongwa nikajikuta nikipandwa na hasira nikijua lazima atakuwa ni Rahma nikanyanyuka na kwenda kuufungua.Nikamkuta ni bibi wa nyumba ya jirani amesimama kwa sura ya hasira huku mdomoni akiwa ameweka ugoro.
“Eddy mbona nataka tuuane wana wa mwanaume mwenzio?”
“Kwa nini bibi?”
“Si nimekuambia huo mredio wako unanipandisha mapresha”
“Haaa samahani bibi……..Wee Recho punguza sauti ya redio”
Suti ikapunguzwa na ikawa ya kawaida bibi akaniaga na kuondoka,Nikiafunga mlango na kujitupa kwenye sofa
“Eddy na wewe hivi vijibibi umevitolea wapi vinawanyima watu raha zao?”
 
“Hembu mwacheni bibi wa watu mwenyewe anadai ana ugonjwa wa moyo”
“Si afe kwani anasubiri nini……”
“Zena acha dharau je wewe si ufe kwani unasubiri nini?”
Recho akaongeza sauti ya redio hadi mwisho na kuipunguza haraka haraka na kunitazama usoni.Sikujua na jinsi kwani tayari pombe za mchana zimewachanganya.Recho akaendelea kucheza taarabu nayoimba ‘JAMANI NINA MWAGA RADHI’ huku wengine wakiitikia ‘MWAGAAAA’
Zena akawa anafungua taulo na kulifunaga.Mlango ukagongwa tane nikajua bibi amerudi tena,nikasimama na kwenda kufungua mlango.Moyo ukanistuka baada ya kumkuta ni Mama Fety amesimama huku akihitaji kuingia ndani kwangu

  ITAENDELEA

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya