Get the latest updates from us for free

mas template
Home » , » AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 27 na 28)

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 27 na 28)

Written By Bigie on Wednesday, March 7, 2018 | 3:56:00 PM

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA   

“Halooo”   
“Halooo Dany, nimekuja wewe ni nani sasa. Na hapa ninapo zungumza nina mtu wako anaitwa Lukasi msikilizee anacho kipata”
“Ahaaa, nakufaaaaa, uuuuuuuuuu”
Nilisikia sauti ya Luka akilia kwa uchungu mkali akionekana kukupoea kipigo kikali sana kutoka kwa watu walio mkamata na sauti hii sio ngeni kabisa kwangu kwa maana ni meya niliye toka kumkoromea masaa machache nyuma.
“Rafiki yako anaelekea kufa sasa, usipo leta Nyaraka ndani ya nusu saa, baba kijacho anakwenda kuiaga dunia Paaaaaaaaaaaaaaaaaaa”
Nikasikia mlio wa risasi, kisha simu ikakatwa, na kujikuta nikitazamana na Latifa anaye mwagikwa jasho uso mzima.
                                                                                           
ENDELEA
Taratibu nikaishusha simu ya Latifa kutoka sikioni mwangu huku nikiwa na wasiwasi mwingi sana, sikujua hata imekuwaje hadi Luka akaingia mikononi mwa meya.
“Viatu hivi na soksi ukivaa utatokelezeajeee”
Sauti ya mama mkubwa ilinistua na kujikuta nikimgeukia na kumtazama huku nikiweka sura ya tabasamu feki usoni mwangu ili asifahamu ni kitu gani ambacho kinaendelea.
“Vipi mbona juu juu, mwenzako anaonekana kama hana raha?”
“Ahaa ni simu ya kibiashara kuna mzigo wake umezuiwa bandarini”
Ilinibidi kumuongopea mama mkubwa.
“Kodi nini?”
“Ndio mama”
Latifa alijibu kuliongezea uzito swala hili nililo lidanganya.
“Ahaa hembu jitaidini wangu, na huyu raisi wa sasa hataki mchezo, munaweza kujikuta munaishia pabaya na biashara zinakufa”
“Ni kweli mama”
Latifa alizungumza huku akionyesha sura ya furaha kidogo ila kusema kweli wote hapa akili zetu zimechanganyikiwa. Nikavaa soksi kisha viatu. Kwa harka anikarudi chumba cha wageni, nikachukua begi lenye nyaraka na kurudi nazo sebleni.
 
“Mama una photocopy mashine?”
“Ndio ipo stoo, ila ni siku nyingi haijatumia sijuia kama inafanya kazi bado”
“Naomba unionyeshe mama yangu”
Tukaongozana na mama mkubwa hadi stoo, akanionyesha mashine hiyo, nikajaribu kuiwasha haikuwaka.
“Hujachomeka waya kwenye soketi”
Ikanibidi kuchomeka waye kwenye soketi kisha nikaiwasha, kwa bahati nzuri ikawaka. Stoo hapo kuna karatasi nyeupa za kutolea photo copy. Nikaanza kazi ya kutoa nyaraka hizo photo copy kisha nikamkabidhi hizo nilizo zitoa mama mkubwa.
“Akija mama naomba umkabidhi huu mzigo”
“Sawa”
Tukatoka hapo sebleni na kuelekea sebleni, tukaaga kisha tukatoka na Latifa, moja kwa moja tukaeleka kwenye gari. Nikaliwasha gari, na kukuta mafuta yakiwa yamejaa kwenye tanki lake. Nikaliweka sawa gari hilo na taratibu tukaanza kuondoka kuelekea getini. Mlinzi akafungua geti kisha tukaondoka, sasa hapo nikaanza kuliendesha gari hili kwa mwendo wa kasi sana kiasi cha kusababisha Latifa mara kadhaa kuguna na kunimbia kwamba niwe makini.
 
“Una namba ya Joseph?”
“Joseph yupi?”
“Yule wa ikulu, kitengo cha mawasiliano?”
“Ndio”
“Mpigie kisha nipe simu nizungumze naye”
Latifa akafanya kama nilivyo mueleza, baada ya simu kupokelewa akanikabidhi na kuiweka sikioni.
“Jose, nitumie namba ya raisi tena”
“Umeipoteza?”
“Hapana simu yangu imedumbukia kwenye maji”
“Sawa nakutumia”
“Asante kaka”
Nikakata simu na kuimrudishia Latifa simu yake.
“Sasa tunakwenda umefahamu wanahitaji ni wapi tuweze kuwakabidhi hizi nyaraka?”
“Ni wapi walikuambia?”
“Wameniambia tuonane Usagara kwa baba ubaya, tukifika hapo tuwapigie simu”
“Pao”
Nikazidi kuongeza mwendo wa gari ili kuhakikisha nusu saa linatukuta hapo sehemu ambayo tumelekezwa na majambazi hao. Ndani ya dakika ishirini na tano tayari tukawa tumesha fika kwenye eneo hilo. Latifa akaipiga namba ya simu ambayo alipigiwa nayo.
 
“Tumesha fikaa”
“Ohoo nimewaona, munaweza kushuka kwenye gari na kunifwata”
“Wewe upo kwa wapi?”
“Wewe shuka”
Niliweza kuyasikia mazungumzo yao, kutokana simu ya Latifa ina sauti kubwa kidogo, nikampokonya na kuiweka sikioni mwangu.
“Hatuwezi kushuka kwenye gari hadi tuweze kusikia sauti ya Luka”
“Ohoo kumbe, ok msikieni”
“Kakaaaa nakufaaa nisaidieniiii”
“Umemsikia”
“Ndio”
Meseji ikaingia kwenye simu ya Latifa kutoka kwa Joseph, ikanibidi kukata simu hiyo na kuipiga namba ya raisi.
“Dany unafanya nini?”
“Nazungumza na raisi kwanza”
Simu ya raisi ikaita kwa sekunde kadhaa kisha ikapokelewa.
“Habari mueshiwa, unazungumza na Agent Dany 008 kutoka NSS, tulizungumza asubihi kupitia namba yangu”
“Ndio ndio sauti yako kijana si rahisi kuweza kunipota masikioni mwangu”
 
“Sawa mkuu, vipi mpango si upo pale pale au kuma mabadiliko yoyote. Kwa maana nimeuliza hivyo kutokana simu yangu ya mkononi imeweza kuipata itilafu kidogo na namba hii ninayo itumia ni ya Agnet Latifa ambaye nimetoka naye kwenye kikosi kimoja”
“Mpango upo pale pale, sijabadilisha kitu, ila tayari amesha andaliwa mtu atakaye vaa sura yangu, na kuonekana kama mimi kwa hilo usijali”
“Sawa mkuu, huku viongozi wengi wapo kinyume na wewe mkuu. Ila nitahakikisha kwamba kila jambo linakwenda vizuri”
“Sawa kijana, saa nne usiku tutanza safari, nitakuja na walinzi wangu wawili ninao waamini”
“Sawa mkuu nitakupokea, na utakuwa unatumia namba hii kuwasiliana nami”
“Hakuna tatizo kijana”
Nikakata simu na kuirudisha kwa Latifa.
“Sasa unakwenda kuwakabidhi hizo nyaraka original?”
“Hakuna jinsi, nafanya yote haya kwa sababu Luka, mkewe ni mjamzito na anatakiwa kuweza kumuona mwanaye”
“Sawa”
 
“Wewe subiri kwenye gari, nipe simu yako, ila kuwa makini sana kwa kila kitu”
“Sawa Dany”
Nikaichukua simu yake, bastola mbili nikachomeka kwenye soksi kisha nikashuka kwenye gari nikiwa ninajiamini kupita maleezo. Nikaipiga tena namba ambayo tunatumia kuwasiliana na mtu huuyo.
“Njoo unaona hili geti jeusi”
Sauti hiyo ya Meya ikaniambia na kunifanya niangaze macho yangu kushoto na kulia, na kuliona geti jeusi kwenye upande wa kulia. Taratibu nikanza kulifwata huku sauti hiyo ya meya ikiniambia nizidi kusonga mbele taratibu. Nikafika hapo getini, nikashangaa kageti kadogo kakifunguka tu.
“Ingia”
Sauti ya meya ikaniambia kupitia simu. Nikaingia ndani  ya geti hilo, sikuamini macho yangu baada ya kukuta wasichana wapatao ishirini wakiwa wamevalia chupi pamoja na sidiria, wakiwa wamelizunguka swimming pool kubwa, huku pembeni kukiwa na vitanda vya kupumzikia vinne. Luka naye akiwa kwenye moja ya kitanda amejipumzisha huku wasichana wasili wakiwa wanamchezea kila sehemu.
 
“Karibu bwana Dany, unashangaa”
Simu bado nimeiweka sikioni, nikatazama kwenye vitanda hivyo nikamuona na meya akiwa amejipumzisha, kitu kilicho nifanya nishindwe kufanya chochote ni kundi kubwa la walinzi wa kisomali wenye bunduki wakiwa katika eneo hilo.
Nikaanza kutembea kwa mwendo wa taratibu huku nikiendelea kuyasoma mazingira ya ndani ya kajumba haka kadogo ka kifahari ila kana eneo kubwa lililo tosha kujengwa swimming pool kubwa. Wasichana wawili warefu walio jazia mapaja yao, wakanifwata hadi sehemu nilipo, wakataka kunipokea begi langu, ila nikawakatalia.
Nikashangaa nikipokea teke moja la sehemu za siri kutoka kwa wasichana hao, kitendo kilicho nifanya nijibane makend** yangu na kuanguka chini huku nikisikilizia maumivu makali sana,
Wasichana hao wakaanza kucheka kwa kejeli, huku wakianza kunipapasa na kuchomoa bastola moja baada ya nyingine.
 
“Una umbo zuri”
Msichana aliye nipiga teke hilo alizungumza huku akiondoka akiwa amebeba kabegi kangu ka mgongoni, akitembea kwa madoido, huku makalio yake makubwa yaliyo tenganishwa na kijichupi cha bikini, yakizidi kutingishika kutoka sehemu moja kwenda nyongine. Msichana wa pili akanipiga busu la shavuni huku akiondoka na bastola zangu zote.
‘Nimeingia pabaya’
Nilijisemea kimoyo moyo, nikiendelea kutazama mazingira ya ndani humu huku nikijizoa zoa taratibu kunyanyuka nilipo angukia. Nikaiokota simu ya Latifa na kuiweka mfukoni. Nikatembea kwa mwendo wa umakini huku nikimtazama Luka anaye onekana kujawa na furaha sana, cha kushangaza hakuonyesha kama ana jeraha lolote katika mwili wake, kitu kilicho nifanya nizidi kukasirika na kujilaumu kichwani mwangu kwamba mimi ni mjinga.
Sala na maombi yangu yote nikawa ninayapeleka kwa Latifa aliye kaa huko nje aweze kuingia ndani humu na kuniokoa kwa maana mwenzake sina ujanja na wala sina pa kukimbilia nimeshikika tena kisawa sawa.
 
“Danyyyy”
Meya alizungumza huku akiwa ameshika glasi ya wyne mkunoni mwake, Luka akanikonyeza huku akiachia tabasamu.
“Karibu bwana, nakuona unajaribu kujifanya supre hero, tena hapa Tanzania”
“Mumechukua document, naomba niondoke”
“Hahahaaaaaaaaaa”
Luka na meya wakacheka kicheko kilicho nifanya nizidi kuwashangaa huku hasira zikizidi kunipanda.
“Huna njia ya kwenda, ni lazima tuweze kufanya kile tulicho kipanga, ila wewe unataka kuwa kikwazo katika hili na huwa siku zote katika maisha yangu sipendi mtu ambaye ni kikwazo”
“Dany kama anavyo sema mkuu hapo, mimi nimeamua kuchana na hii kazi bwana. Nayapenda maisha yangu, nipo hapa nitakula bata hadi mimi mwenye nichoke. Si unatazama watoto wazuri hawa walivyo nona.”
Luka alizungumza huku akishika tako la mtoto mmoja wa kike na kuliminya minya kisha akalipiga piga taratibu na kumfanya msichana huyo kutoa kijimlio cha ushambenga.
“Sikuzote ndege mjanja huwa anakamatwa kwenye katundu kabovu sana, ndio wewe”
 
“Ni nini ambacho unahitaji mimi kukifanya kwenu?”
“Tunacho taka kukifanya ni kuleta roho ya mkurugenzi wa jiji basiii. Ukifani……..”
Meya hakumalizia sentensi yake akabaki akiwa ametazama kwenye laptop yake iliyopo pembeni inayo onyesha video za kamera zilizo fungwa katika eneo hili. Nikuamuona Latifa akishuka kwneye gari na kaunza kutembea kwa mweondo wa tahadhari akifwata geti la kuingilia hapa ndani.
“Muangalieni huyo msichana anaye ingia”
Meya alizungumza kupitia simu yake nikaona wasichana karibia wote wakiwa makini kutazama mlangoni. Latifa akafika getini, akatoa bastola zake zote, nikatamani kuzungumza kumueleza Latifa asiingie ndani ila nikashindwa kufanya hivyo kwa maana, kwanza hato weza kusikia chochote kwa maana kinacho onekana hapo ni video inayo chukuliwa na kamera hizo za ulinzi.
 
Latifa akausukuma mlango wa geti taratibu na ukafunguka, mbele ya geti hilo akasimama kijana mmoja wa kisomali, sote tukashuhudia kijana huyo akianguka chini ikimaanisha ametandikwa na risasi, hapo ndipo walinzi wa ndani walipo anza kuchanganyikiwa. Wakaanza kufyatua risasi pasipo mpangilio wa aina yoyote jambo lililo mfanya Latifa kuwa makini sana nje. Hapo ndipo nami nikaamua kumrukia meya, nikamuangusha chini na kumpiga kabali ya nzito. Kurupushani zangu na meya, tukajikutra tukidumbukia sote kwenye swimming pool.
Tukazama ndani ya maji huku tukiendelea kupambana vikali sana, sikutaka kuiachia shingo ya meya huyo, safari hii nikaamua kufanya maamuzi magumu kabisa, ya kumuua. Meya akajitahidi kadri ya uwezo wake kujinasua kwenye mikono yangu ila akashindwa kabisa, na mbaya zaidi ni kwamba tumezama ndani ya maji hayo yenye kina kirefu sana. Taratibu meya akaanza kutulia, huku pumzi ikimuishia. Watu wake kadhaa wakajitosa kwenye maji wakijaribu kuja kumuokoa, ila tayari wakawa wamesha chelewa. Kwani mtoa roho tayari alisha mtembelea meya huyu anaye onekena ndio mzizi wa kila kitu kinacho tokea katika mipango ya kumuangamiza raisi pamoja na mama yangu.
 
    Nikamuchia meya na kuanza kuogelea kwa kasi kwenda juu huku nikipishana na watu wake wanao uwahi mwili wa meya nilio uacha chini ya swimming pool. Nikajitokeza kwenye maji na kukuta amaiti nyingi haswa za wasichana zikiwa zimetapakaa kila eneo. Nikamuona Luka akikimbilia kwenye moja ya ukuta akijaribu kuuruka. Nikatoka kwenye swimming pool kwa haraka na kuanza kumkimbiza, huku Latifa akiaendelea kupambana na watu wachache walio salia. Sikujali milio ya risasi ua hatari ya risasi zinzo pita pembeni yangu huku wausika wakiwa wamekusudia kunilenga mimi na kuniangamiza.
 
Nikamuwahi Luka, na kumshusha kwenye ukuta huu kwa kumvuta mguu wake wa kulia. Akaanguka vibaya chini kwa kupiga uso chini. Sikulijali hilo zaidi ya kuanza kumpa makonde mazito huku nikimshushia matusi ya kila aina kwa mana usaliti alio ufanya anastahili adhabu ya kifo tu.
Ukimya ukatawala ndani ya dakika moja, nikatazama upande ambapo mashambulizi yalikuwa yanaendelea, nikamuona Latifa akipitia maiti moja baada ya nyingine. Sikuamini kama Latifa ana ujuzi mkubwa katika matumizi ya silaha. Kwa haraka Latifa akafika katika sehemu ambayo nipo nimemlaza Luka chini huku nikimshushia makonde mazito.
 
“Dany mbona unampiga mwenzako?”
“Ni msaliti huyo na yeye ndio chanzo cha sisi kuingia matatizoni”
“Mbona sielewi Dany ni kitu gani kinacho endelea?”
“Tazama kipindi ninaingia humu ndani nikamkuta huyu mpuuzi akiwa amekaa kwenye vile viti pale anakula bata na wasichana wememzunguka. Nilijiua amepata majeraha ila kumbe ni mpango wake na huyo mshenzi hapo kwenye hilo swimming pool”
Latifa akamtazama Luka jinsi anavyo vuja damu puani mwake kwa maana kipigo nilicho mshushia ni kizito sana, ukitegemea ni masaa amchache tulikuwa tunapiga stori kama marafiki, kumbe mwenzetu ana mpango wake tofauti.
 
“Jamani nisameheni, nimefanya yote kwa ajili ya familia yangu. Yote nimefanya kwa ajili ya mke wangu na mwangu aliyopo tumboni”
Lukas alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake. Akataka kunyanyuka nikamrudisha chini kwa kumpiga teke la kifuani, kitu kilicho mstua sana Latifa.
“Dany stopppppp. Huyu ni agent mwenzako”
“Lakini hawezi kufanya usaliti hata kama ni swala la familia”
“Mbona mimi umenishirikisha kwenye swala la nyaraka za mama yako, umeona uzito uliopo hapo kati ya kazi na familia?”
Latifa alizungumza kwa ukali jambo lililo nifanya nikae kimya huku ninamtazama kwa macho ya mshangao. Katika kuzubaa kwetu kwa haraka Lukas akasimama na kumpiga kabali Latifa na kumpokonya bastola yake na kumuwekea ya kichwa huku akinitazama na kutabasamu kwa dharau.
                                                                                         
                      AISIIIII……….U KILL ME 28

“Luka…..”
Latifa alijaribu kupiga kelele ila Luka akamuongezea kumkaba shingo yake kwa mkono, huku bastola akiendelea kuiweka vizuri karibu kabisa na kichwa cha Latifa. 
 
“Nyamaza wewe malaya”
“Luka hembu tulia kwanza tuyazungumze”
“Nyamaza na wewe kenge nini. Unahisi ulivyo kuwa unanitandika mangumi hapa nilikuwa siumii”
“Nalijua hilo?”
“Sasa nahitaji muniache niondoke, ukifanya chochote ninamuua Latifa hata kama ni rafiki yangu”
“Sawa sisi tunakuacha uendee, naomba umuachie Latifa kwanza”
“Noo siwezi kufanya ujinga wa aina hiyo”
Luka alizungumza huku taratibu akirudi nyuma nyuma huku akimburuta Latifa, anaye endelea kuushikilai mkono wa Luka usizidi kumkaba zaidi na zaidi.
Luka akakaribia karibu na ukuta ambao alikuwa amekusudia kuupanda hapo awali, akamsukumia Latifa kwangu, nikawahi kumdaka asianguke chini. Nikamshuhudia Luka akipanda ukuta huo na kuangukia upande wa pili na nikiasikia vishindo vyake vya kukimbia kuelekea anapo pajua yeye. 
 
“Dany”
Latifa aliita kwa sauti ya chini huku akijiweka vizuri koo lake lililo kumbana na maswaibu ya kukabwa sana.
“Ina maana Luka ni msaliti kweli?”
“Kama ulivyo weza kuona”
“POLISIIII”
Tulisikia sauti kutokea getini, ikatubidi kugeuka kwa haraka, tukakutana na kundi kubwa la polisi, wapatao sita, huku mmoja wa polisi hao niliweza kumkumbuka kwa haraka ni yule polisi niliye weza kuonana naye nyumbani majira ya asubuhi.
“Mikono juu”
Mmoja alitoa sauti hiyo tukatii mimi na Latifa, kila askari aliweza kutunyooshea bunduki yake, kila mmoja akaonekana kushangaa mauaji yaliyo tendeka eneo hili kwa maana kumetapakaa maiti nyingi kila sehemu.
Askari hao wakatufwata na kutufunga pingu za mikono huku mikono yetu wakiwa wameirudisha kwa nyuma.
 
“Ninaomba nitoe kitambulisho changu”
Latifa alizungumza huku akiminyana na askari wa kiume aliye mshika mkono.
“Hakuna haja ya kitambulisho hapa, maelezo yote mutakwenda kuyatoa kituoni”
“Niachieni nyinyi, munajua mimi ni nani?”
“Hilo hatutaki kulijua tena kaa kimya, ukileta za kuongea ongea, tutakutandika makofi mtapisho sasa hivi”
Askari huyo aliendelea kuzungumza kwa kujiamini, askari wa kike ambaye nilikutana naye asubuhi akabaki akiendelea kunitazama pasipo kuzungumza kitu cha aina yoyote. Wakatutoa nje ya geti ya nyumba hii. Tukakuta wananchi wengi pamoja na waandishi wa habari wakiwa wamekushanyika wakishangaa tukio hili huku waandishi wa habari kazi yao ikiwa ni kupiga picha.
 
“Hamujui munadili na watu wa aina gani”
Nilimuambia askari aliye pembeni yangu huku akiwa na bunduki.
“Huo ni ujinga ambao sitaki kuusikia”
“Ahaaaa ehee”
Askari wa kike naye alitembea pembeni yangu huku kwa umakini akiwa anajaribu kutaka kuzungumza jambo ila anashindwa kuzungumza. Wakaniingiza kwenye gari aina ya defender, huku Latida naye akiingizwa katika gari nyingie. Katika defender hii wakaingia askari wanne akiwemo na askari wa kike yule ninaye fahamiana naye kwa kuonana. Akaka mbele yangu huku wazake wengine wakiwa wamesimama katika sehemu ya kuingilia, huku mitutu yao ya bunduki wakiwa wamishikilia vizuri.
 
   Gari ya aliyo ingizwa Latifa taratibu ikaanza kuondoka cha kushangaza ikaeleka upande tofauti na upande ambao ninaelekea mimi. Askari huyu wa kike akanikonyeza kwa umakini mkubwa, hapa ndipo nikaanza kugundua ishara za askari huyo kwa mana ishara anazo anza kunionyesha ni ishara za kipelekezi ambazo si rahisi kwa askari polisi kuweza kuzifahamu. Ishara moja tuliyo zungumza kwa macho pasipo askari kugundua, ni kuutumia mguu wangu wa kulia. Nikaelewa ni nini anacho kimaanisha. Nikaupeleka mguu wangu wa kulia katikati ya mapaja yake na kugusa sehemu za siri. Kitendo hicho kikamkasirisha askari huyu wa kike, aliye ninasa kofi tizo hadi wezake wakashangaa.
 
“Mpumbau wewe unaidhalilisha kwa kunikanyaga sehemu zangu za siri ehee”
Alizungumza huku hasira ikizidi kumpanda, akaninasa ngumi nyingine nzito za kifua
“Afande Judith muache bwana”
“Awezi kunidhalilisha mimi nikamuacha hivi hivi”
Akanirukia na kunilaza chini, akaanza kunitandika makofi mfululizo huku askari wezake wakabaki wakiwa wamesimama, huku gari ikizidi kwenda kwa mwendo kasi, kutokana mikono yangu imefungwa pingu kwa nyuma sikuwa mnjanja wa kufanya chochote.
 
Afande Judithi, akanipiga kichwa cha pua na kunifanya nipanue mdomo, sikuamini nilipo muona akinitemea funguo ndogo ya pingu niliyo iwahi kuibana chini ya ulimi kabla sijaimeza. Akasimama na kunikalisha kitako huku nikivujwa damu.
“Pumbavu, huwa napenda waseng* kama nyinyi niwashuhulikie”
Afande Judithi alizungumza huku akihema, akanipa ishara moja ambayo nikaitekeleza ndani ya sekunde mbili kama si tatu. Nilijibenua kwa haraka na mikono yangu nikaileta mbele, ni jambo rahisi sana kwa mfanya mazoezi kufanya hivyo. Askari wakaanza kuchachawa huku akigeuza vitako vya bunduki zao wakitaka kunipiga navyo ila wakawa wamechelewa tena sana, kwani niliweza kujifungua pigu hizo kwa funguo aliyo nipatia afande Judithi. 
 
Askari aliye shusha kitako chake cha bunduki ili anipige, nikakinyaka kwa haraka kisha nikampiga teke moja ala sehemu za siri lililo mfanya aiachia buduki yake hiyo aliyo kusudia kunipiga nayo. Nikaanza kuwashuhulikia askari hawa watatu wa kiume, nikashangaa kumuona afande Judithi akinisaidia kufanya hili. 

Askari aliyopo mbele anaye endesha gari alipo ona misukosuko na vishindo vilivyopo nyuma akafunga breki za gari. Kitendo cha askari huyo kuufungua mlango, akakutana na teke zito kutoka kwa afande Judithi aliye shuka pasipo hata kujua ameshukaje. Nikasikia askari huyo ambaye ni dereva akigugumia kwa maumivu makali. Askari wote watatu nikawa nimewaweka chini ya ulinzi mkali, hakuna askari aliye weza kufuruka hata mmoja, kila mmoja akawa na akaiz ya kuugulia maumivu yake. Kwa bahati nzuri eneo tulilo tulilopo hakuna watu wengi kwa mama ni moja ya njia ambayo pembeni kuna majumba ya kifahari na nimitaa iliyo tulia kabisa.
 
Nikashuka kwenye gari hili na kuanza kuwashusha askari hawa, kila mmoja nikamfunga pingu yake, na kuwaweka pembeni ya barabara. Afande Judith akamshusha askari huyu ambaye ni dereva akiwa amelegea sikujua hata amempiga kipigo cha aina gani kwa mana amelegea hata kusimama hawezi.
“Wapapase kaam wana simu za mawasiliano”
Afande Judith aliniagiza na kujikuta nikitii, nikaanza kumkagua mmoja baada ya mwengine, mmoja nikamkuta na simu ya thamani aina ya iphone six, huku mwengine akiwa na kijisimu aina ya nokia vyenye jina maarufu la Nokia Obama.
Nilipo hakikisha kwamba hakuna ambaye ana simu, bunduki zao nikazichukua na kuingia nazo upande wa dereva ambapo Afande Judith yupo ananisubiria. Afande Judithi akaliondoa gari kwa mwendo wa kasi huku akiwa kimya, akatatoa kitambaa cheupe kwenye mfuko wa suruali yeka ya kiaskari alio ivaa na kunikabidhi.
 
“Kifute damu”
Nikafanya hivyo kwa mana kuna michuruzo ya damu inanitoka puani mwangu.
“Pole sana kwa kuweza kukufanyia kile nilicho kufanyia kwenye gari”
“Asante ila ni kwa nini ulifanya vile?”
“Ahaa, jina langu alisi ninaitwa Babyanka Martin, ni mlinzi wa siri wa raisi. Mwenzi mmoja kabla alinituma kuja kuandaa dhiara yake na kuniingiza katika kikosi cha jeshi la polisi kwa jina la Judithi Ndauka”
“I…iii ina maana unafahamu kitu gani kinacho endelea?”
“Ndio natambua mpango wako mzima kwa maana raisi aliniagiza leo kuweza kukufwatilia na nilisha mpa ripoti kwamba wewe ni mtu safi na unaifanya kazi kama vile inavyo paswa”
“Ahaa sasa unafahamu raisi anakuja kwa njia gani?”
“Kama aliweza kunipa taarifa zako, basi tambua kwamba natambua kwamba anakuja kwa njia gani. Hato kuja kupitia njia ambayo wewe unaizungumzi, kwa mana yule aliye kamatwa naye ni miongoni mwa wavujisha siri”
 
“Nani, Latifa?”
“Ndio wale askari nao pia ni miongoni mwao, pale anapelekwa kwa mkuu wa mkoa kwenda kuzungumza kile kitu kinacho endelea. Nilisha wasiliana na raisi, atakuja kupitia njia ya helcoptar na tutakwenda kumpokea majira ya saa nane usiku katika eneo la Maranzara, lipo Pogwe kwenye moja ya kiwanja cha siri sana. Hapo ninapafahamu basi itatupasa saa saba kamili tuwepo pale”
“Sawa, sasa huoni kama itakuwa ni hatari kama tukitumia gari la polisi.”
“Hatuto tumia gari la posili, ninakupeleka nyumbani kwako, kuna mtu tayari amesha lichukua gari lako na kulipeleka kwa mbunge muheshimiwa Eddy”
“Umejuaje kama nimelichukua gari hilo kwa muheshimiwa Eddy?”
“Ndio maana nilikueleza hapo awali kwamba nilianza kukufwatilia siku nzima na ratiba na mizunguko yako yote niliweza kuifahamu”
 
“Mungu wangu…..?”
“Nini?”
“Kuna zile nyaraka zipo katika eneo lile tukio”
“Ahaa hizo nyaraka kwa sasa hazina umuhimu kwa sana kwa mana maamuzi yatatoka moja kwa moja kwa raisi”
“Mmmmm”
“Yaa”
“Sasa nikuite Babyanka au nikuite afande Judithi?”
“Ni vyema sana kama ukiniita afande Judithi, jina langu halisi huwa mara nyingi sipendi liweze kujulikana kwa watu”
“Sawa, naitwa Dany”
“Nashukuru kukufahamu, japo tayari nilisha weza kulifahamu jina lako”
Tukafika katika eneo la raskazoni kwenye moja ya nyumba ambayo imejitenga mbali sana na sehemu zilipo nyumba nyingine. Afande Judithi akashuka kwenye gari, akatembea kwa hatua za haraka hadi kwenye geti, akafungua na kuniomba niingize gari hilo ikanibidi kuhamia upande wa siti ya dereva. Taratibu nikaliingiza gari hilo katika eneo la nyumba hii nak umuacha Afande Judithi anafunga geti. Alipo maliza akatembea kwa mwendo wake wa haraka hadi sehemu nilipo simama.
 
“Karibu”
Alizungumza huku akitangulia mbele, akafungua mlango wa kuingilia ndani humo kwa kutumia namba za siri, ambazo ameminya minya kwenye batani nyingi zilizopo katika mlango huu. Mlango ukafunguka na sote tukaingia ndani, akawasha taa, hapo ndipo nilipo weza kupata fursa ya kuweza kuona kila kitu kilichopo hapa sebleni.
Haikuwa seble kama nilivyo jua mimi, ila ni sehemu yenye mitambo ya mawasiliano makubwa. Afande Judithi akawasha moja ya computer yenye kiooo kikubwa kiasi, akaanza kuminya minya batani za copture hiyo kwa kasi ya ajabu sana kisha akasimama mbele yake, hazikupita sekunde tano nikaona video ya raisi akiwa amesimama eneo hilo akiwa ndani yake. 
 
“Muheshimiwa kijana Dany nimesha kutana naye”
“Upo naye hapo?”
“Ndio”
Afande Judithi akaniita kwa ishara nikasimama pemebeni yake.
“Asante sana kijana kwa kuweza kufanya kazi yako kwa uaminifu mkubwa sana”
“Asante muheshimiwa”
“Kama alivyo kueleza Babyanka, leo nitatumia njia hiyo, ila kesho kwenye msafara atakuwepo raisi huyu”
Akasimama mtu mwengine ambaye ametengenezewa sura kama raisi, akasimama pembeni ya raisi. Kusema kweli hakuna utofauti wowote na raisi, raisi huyo feki akasogea pembeni na kumuacha raisi aendelea kuzungumza na sisi.
“Ratiba ya viongozi wote ambao si waadilifu wa serikali yangu, nimeweza kuipata nawaahidi nikija huko nitahakikisha kwamba wote wanaweza kutumikia kile ambacho wamekipanda kwa muda mrefu”
 
“Sawa muheshimiwa”
“Tutaonana baadaya, na kuanzia sasa Babyanka, atakupatia mawasiliano ya kuwasiliana nami moja kwa moja”
“Sawa muheshimiwa raisi”
Afande Judithi akazima computer hiyo kisha akanigeukia.
“Unatakiwa sasa ukaoge na kukupa vitendea kazi vyako. Njoo nikuonyeshe bafuni”
Nikaongozana na afande Judithi hadi katika bafu, akanionyesha kisha akatoka, taratibu nikaanza kuvua koti la suti kisha shati. Nikavua viatu pamoja na shati kisha nikasimama mbele ya kioo huku nikijitazama majeraha niliyo yapata usoni mwangu. Nikiwa nimesimama mbele ya kioo nikaona mlango wa bafu ukifunguliwa ikanibidi kugeuka na kumuona Banyanka akiingia bafuni hapa akiwa amevalia chupi na siridia, kwa jinsi umbo lake lilivyo la kirembo nikabaki nimeduwaa.
“Tuoge wote”   
Babyanka alizungumza na kunifanya nibaki nikiwa nimekaa kimya nisijue nini cha kufanya, huku jogoo wangu akianza kuleta fujo za kutaka kusimama taratibu.
                                                                                          ITAENDELEA

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya