ILIPOISHIA
‘Hawanijui hawa’
Eddy alizungumza huku akishuka kwenye gari bastola yake akiwa ameichomeka kwa nyuma.
“Nyinyi ni wakina nani?”
Eddy aliwauliza huku akijiweka sawa kwa lolote litakao kwenda kujitokeza, ukimya wa barabara hiyo inayo elekea ikulu na majira haya ya usiku iliwafanya Lube na wezake kuweza kuilisikia swali hilo walilo ulizwa. Hapakuwa na aliye jibu zaidi ya wao kuanza kujitawanya na kumzingira Eddy na kumuweka kati tayari kwa kumshambulia.
ENDELEA
Eddy akawatazama kwa huku akiwahesabu jinsi walivyo kaa, taratibu akalivua shati lake na kubaki tumbo wazi, Lube akamuamrisha mwenzake mmoja kufanya shambulizi kwa Eddy anaye onekana kujiamini sana. Kitendo cha jamaa kumfikia Eddy, akakutana na teke zito lilotua kifuani kwake na kumuangusha chini kama mzigo. Ikawabidi wengine kushanga kwani kila mmoja hakuamini kama kiongozi huyo anaweza kufanya tukio la aina hiyo.
Wote watatu walio bakia wakamvamia Eddy kwa kasi, kila mmoja akijaribu kupiga sehemu yake anayo iweza kupiga katika mwili wa Eddy, ila kila walivyo jaribu kupambana, ndivyo jinsi walivyo weza kukutana na mapigo makali yaliyo wachanganya kiasi cha kuwafanya kila mmoja kujikuta akiwa na maumivu upande wake. Lube alipo gundua Eddy amewazidi kila jambo. Kwa bahati nzuri akaona gongo moja pembezoni mwa barabara. Akarudi nalo hadi sehemu wanapo endelea kupambana wezake, huku gongo hilo akiwa amelificha nyuma ya mgongo wake.
“EDDYYYYYYYYY……..”
Lube akamuita Eddy kwa sauti ya juu na kumfanya Eddy ageuke kutazama mtu anaye muita, ila gafla gongo zito likatua, kichwani mwake na kumfanya Eddy kuyumba, kijana mmoja akamsindikiza na teke zito lililo muangusha Eddy chini na kupoteza fahamu.
“Mbebeni haraka haraka”
Lube alizungumza, kabla hata hawajamnyanyua mwanga mkali wa gari ukawamulika, na kuwafanya wasimama kulitizama gari hilo ni la nani majira hayo ya usiku. Gari hiyo ikafunga breki na kusimama, akashuka mtu ambaye wote wanamfahamu.
“Huyu Samson amefwata nini hapa”
Mmoja wao alizungumza kwa sauti ya chini huku wakimtazama Samson akitembea na kuwafwata sehemu walipo.
“Bosi tufanyaje?”
Mmoja wao aliuliza huku kila mmoja akijiweka sawa. Samson akawatazama kisha akawakazia macho, wote wakajikuta wakishikwa na woga mkali kwani macho ya Samson yalibadilika na kutisha sana
***
Agnes na Jaquline wakashuhudia jinsi Halima na wezake wanavyo pata mateso gerezani. Video hizo zikawamfanya Agnes kumwagikwa na machozi ya uchungu, uzuri wa wezao hao wote umepotea, alama nyingi za makovu zimetawala kwenye miili yao.
“Munaweza kuamua sasa, kufanya kazi na sisi au wezenu waendelee kupata mateso na mwisho wa siku hukumu ya kuuawa itakuwa dhidi yao”
Kabla hawajajibu mlio wa simu ukalia kutoka kwenye mfuko wa mmoja wa walinzi, akaitoa simu hiyo na kuipokea kisha akaiweka sikioni mwa John
“Ndio mkuu”
“Leo ninakuja mako makuu kila kitu ukiweke sawa”
“Sawa mkuu”
Simu ikakatwa John akashusha punzi kidogo, kwa taarifa aliyo weza kuipata kwa mkuu wake Mzee Godwin. Akaagiza ulinzi uzidi kuimarishwa na vijana waweze kujiandaa kumpokea mkubwa wao huyo anaye tokea barani Afrika.
“Tumekubali, ila kwa sharti moja”
Jaquline alizungumza huku akimtazama John machoni huku akiwa amemkazia macho, John akatingisha kichwa chake kumruhusu Jaquline kuendelea kuzungumza.
“Hatuta weza kufanya kazi yoyote na nyinyi hadi pale tutakaopo waokoa wezetu”
“Mmmmmmm, nitarifikiria”
“Waandalieni sehemu inayo stahili wao kuwepo”
John akatoa agizo lake kwa vijana wake, wakawachukua Jaqulne na Agnes na kuwapeleka kwenye moja ya chumba kilicho na huduma za kila kitu wakisubiria juu ya jibu watakalo pewa na John.
Mzee Godwin akaagana na bwana Abdulah Mohamed mkuu wa kikosi cha kigaidi cha Al-Shabab, wakaingia kwenye ndege ya kifahari aina ya Jet inayo ingia abiria watano pamoja na marubani wawili. Tom na Manka tayari walisha ingia kwenye ndege hiyo wakimsubiria baba yao aliye kuwa akipiga stori za hapa na pale na kiongozi huyo waliye aihidiana kupanga baadhi ya mipango takayo kuwa kabambe katika kutawala baadhi ya maeneo kwa kutumia nguvu.
“Mumemechoka ehee”
Mzee Godwin aliwauliza wanae hao huku akijiweka vizuri katika siti aliyo kaa
“Ahaa kidogo tu”
Tom alijibu
“Mmmm mimi nimechoka sana tu baba, hapa natamani tufike huko tunapo kwenda”
“Musijali haita chukua masaa mengi tutakuwa tumefika”
***
Mihemo mizito pamoja na mingurumo anayo itoa Samson ikawafanya Lube na wezake kuzidi kutetemeka, mmoja wao akachomoa bastola yake na kumfyatuia baadhi ya risasi kwa Samson, ila jambo la kushangaza risasi hizo ziliingia mwilini mwa Samson ila katika sehemu zilipo ingia jeraha lake likapona ndani ya sekunde chache.
Kwa kasi ya ajabu Samson akamkimbilia jamaa aliye mpiga risasi, akamkamata shingo, kwa mkono mmoja akamnyanyua juu, huku akizidi kukoroma na macho yake yakiwa yamebadilika na kuwa kama simba aliye na hasira kali.
“Ondokeni hapaaa”
Samson alizungumza kwa sauti nzito, huku akimuachia aliye mpiga risasi hakuhitaji kumdhuru na kuwafanya Lubne na wezake wote kuondoka katika eneo hilo, wakaingia ndani ya gari lao na kuondoka kwa mwendo wa kasi kila mmoja akiwa haamini alicho weza kukiona kwa binadamu huyo wanaye mtambua kama Samson.
Samson akambeba Eddy begani na kumuingiza kwenye gari lake na kuondoka naye.
“Madam nimempata”
John alizungumza kupitia simu yake huku akiwa amesimamisha gari lake pembezoni mwa barabara huku Eddy akiwa amemlaza siti ya nyuma.
“Safi sasa hakikisha unampeleka kwenye eneo ambalo si rahisi kwa mtu kuweza kutambua”
“Sawa madam”
Samson akakata simu na kuendelea na safari, Samson kitu alicho weza kukumbuka ni moja ya handaki ambalo Rahab alimueleza kwamba yalikuwa ni maficho yao kipindi walipo weza kukutana kwa mara ya kwanza, na handaki hilo lipo nje ya mji. Usiku huo huo akafunga safari hadi nje ya jiji la Dar es Salaam, akifwatisha maelekezo anayo tumiwa kwa njia ya meseji na Rahab aliyopo ndani ya ikulu
“Mke wangu leo unachati sana”
Raisi Praygod alimuuliza Rahab, mara baada ya kuingia ndani ya chumba chao dakika kadhaa zilizo pita, ila mapokezi ya leo yapo tofauti sana na siku nyingine za nyuma, kwani alisha zoea kufanyi mapokezi ya mabusu motomoto.
“Kuna taarifa ninaisoma hapa”
“Taarifa gani ambayo raisi siifahamu?”
“Aihusiani na Tanzania”
“Mmmm saw………..”
Raisi Praygod hakuimalizia sentesi yake simu yake ikaita, akaitoa kwenye mfuko wa koti lake la suti na kukuta Lube ndio anaye mpigia, akamtazama Rahab kwa macho ya kuiba kisha akaipokea.
“Mmmmmm”
“Mkuu tumeshindwa Samson sio binadamu”
Raisi Praygod akashindwa kuzungumza chochote zaidi ya kutoka ndani ya chumba chake cha kulala na kwenda kuzungumzia sebleni, na kumpa nafasi Rahab ya kumpigia simu Samson.
“Sio binadamu kivipi?”
“Yaaani yaani macho yake yamekuwa kama, samba”
“Ahahaa Lube hembu pangilia sentesi zako nikuelewe”
“Yaani Samson ni jinni”
“Jini, mupo wapi?”
“Ndio tunaingia hapa getini”
“Basi njooni ofisini kwangu”
Raisi Praygod akakata simu na kujikuta uchovu wote alio kuwa nao ukimuishia na kuanza kutembea hatua za haraka kuelekea ofisini kwake.
“Samson imekuwaje ukaonyesha uhakisia wako”
“Samahani madam”
“Siku nyingine hakikisha kwamba uhalisia wako unapo uonyesha kwa mtu yoyote, usiye muamini hakikisha kwamba unaitoa roho yake”
“Sawa madam”
“Mumesha fika”
“Ndio tunafika”
“Kesho nitakuja hakikisha kwamba humuachi peke yake”
Samson akasimamisha gari lake pembezoni mwa handaki alilo elekezwa akashuka na kufungua mfuniko wa chuma ambao pembezoni mwake akakuta jiwe kubwa. Mazingira ya eneo hilo yanaonyesha kuna watu wametoka katika eneo hilo siku chache zilizo pita.
Akaingia ndani ya handaki hilo akiwa peke yake, akalichunguza handaki hilo kwa umakini, alipo hakikisha usalama upo akarudi kwenye gari akambeba Eddy na kumpeleka kwenyemoja ya chumba chenye kitanda, akamlaza vizuri kisha yeye akatoka na kukaa kwenye moja ya kiti kilichopo kwenye seble kubwa ndani ya handaki hilo
Raisi Praygod akajikuta akishusha pumnzi nyingi baada ya kuambiwa mambo yaliyo tokea, kichwani kwake akajikuta akimuwa Eddy na Samson.
‘Rahab’
Raisi Praygod akakumbuka kwamba mtu aliye weza kuurudisha uhadi wa Samson ni Rahab, kwa haraka akanyanyuka na kuwaacha vijana wake ndani ya ofisi hiyo na moja kwa moja akaelekea chumbani kwake na kumkuta Rahab akiwa amelala. Jinsi anavyo zidi kumtazama ndivyo jinsi uchungu na wivu unavyo zidi kumtawala kila akimkimbuka Eddy na kuvuta baadhi ya kumbukumbu jinsi Eddy alivyo mfanya mke kitandani hasira kali ikazidi kumpanda hadi akahisi kifua chake kumpasuka.
Akavua nguo zake zote na kubaki kama alivyo zaliwa, akalifunua shuka alilo jifunika Rahab na kumkuta akiwa kama alivyo zaliwa, kwa papara akajikuta akianza kumpapasa kila eneo la mwili wa Rahab ila kitu kilicho mshangaza siku ya leo, jogoo wake halikuweza kusimama kitu kilicho mfanya Rahab kuyafumbua macho yake na kumtazama mumewe kisha akatabasamu kwa dharau
“Endelea kufanya unacho kifanya”
Maneno ya Rahab yakamfanya raisi Praygod mapigo yake ya moyo kumuenda mbio kiasi cha kujikuta jasho likimwagika mwili mzima na kujikuta akijilaza pembezoni mwa Rahab ikiashiria kwamba ameshindwa jogoo wake ameshindwa kuwika
SORRY MADAM (28) (Destination of my enemies)
“Mke wangu kweli unanipenda?”
Raisi Praygod alimuuliza Rahab kwa sauti ya upole sana hadi Rahab akajisikia huruma ndani ya moyo wake, taratibu akajinyanyua kitandani akamtazama mume wake usoni jinsi anavyo onekana kufedheheshwa na kitendo kilicho weza kutokea muda mchacha ulio pita.
“Nakupenda sana Pray”
“Kwa nini………”
Raisi Praygod akajikuta akiikatisha sentesi yake, kwani hakuhitaji kumfanya mke wake kuweza kugundua kwamba amesha wastukia mahusiano yake na Eddy.
Rahabu taratibu akaushusha mkono wake hadi kwenye jogoo wa raisi Praygod na kuanza kuishika taratibu, msisismko mkubwa ukauvaa mwili wa raisi Praygod na kumfanya jogoo wake kusimama haraka sana hadi mwenye akajishangaa ni kitu gani ambacho ameweza kukifanya mke wake, kwa haraka akajikuta akijigeuza na kumlaza Rahab chali, kisha akampanua miguu yake na mkono wake wa kulia akaupeleka kwenye kitumbua cha Rahab na kuanza kukichezea kwa haraka, akiwa na wasiwasi jogoo wake anaweza kulala tena ikawa fedheha.
***
Alfajiri na mapema Eddy akanyanyuka kitandani huku akiwa amechoka na kichwani kwake maumivu makali akiyahisi kama kuna vyuma vinagongana ndani ya kichwa chake. Akajitahidi kutazama kila kona ya chumba hicho, hakujua ni wapi ambapo yupo. Akakumbuka tukio la mwisho jana, ni watu wanne walio mzingira na kupigana naye, hakuweza kuwafahamu kwani watu hao walizifunika sura zao na walionekana macho yao tu.
Akajinyoosha kidogo kisha akasimama, mlango wa chumba hicho umerudishiwa kidogo na haujafungwa moja kwa moja. Akapiga hatua na kutoka nje ya chumba hicho, akamkuta Samson akiwa amekaa kwenye kiti ambacho mbele yake kuna computure kadhaa akionekana kuwa bize akisoma soma mambo yaliyomo ndani ya computer hiyo.
\
“Umeamka”
Samson alianza kuzungumza mara baada ya kumuona Eddy amesimama nje ya mlango huo akimtazama pasipo kuzungumza kitu chochote.
“Ndio, hapa ni wapi?”
“Hapa ni makazi mengine mapya, yenye usalama kwako”
“Kwa nini nipo hapa?”
Samson akanyanyuka kwenye kiti hicho, akamsogelea Eddy, kwa sauti ya upole akamuelezea tukio la mwisho la jinsi yeye alivyo weza kumuokoa kutoka mikononi mwa watu wa raisi Praygod Makuya.
“Ina maana raisi yeye ndio aliye watuma”
“Ndio yeye ndio yupo nyuma ya hili, ila Madam amaeniambia kwamba nikuweke hapa hadi atakapo kuja”
“Na yeye anafahamu juu ya hao watu?”
“Hapana ila mimi ndio niliye weza kumuambia kwamba kuna watu walityuma kuja kukudhuru”
Eddy akashusha pumzi nyingi huku akishika maeneo ya nyuma ya kichwa chake akionekana maumivu yakiendelea kumuumiza sana.
“Shamsa Shamsa yupo wapi?”
Eddy alimuuliza Samson huku akiwa amemtumbulia macho. Kwa muonekanano wa Samson anaonekana kuto kujua Shamsa aneye mzungumzia Eddy, hatambua ni wapi alipo.
“Ohhh Mungu wangu, Samson nitafutie mwanangu tafahali nakuomba, mwanangu amechukuliwa na huyo mwanaharamu Makuya”
“Sawa nitalifwatilio hilo”
Eddy katika kutazama tazama kwenye chumba hicho akaona kamera moja ikiwa juu ya meza zenye computure hizo, akapiga hatua na kuifwata, akaichukua na kuiwasha.
“Hii ni yakwako?”
“Ndio, nilikuwa nayo kwenye gari”
“Ile miguu yake ya kusimamia ipo wapi?”
“Nimeicha ndani ya gari”
“Naomba ukaniletee tefadhali”
Samson hakupingana na Eddy akatoka ndani ya handaki hilo, akafungua mlango wa nyuma wa gari lake na kuchukua miguu maalumu ya kusimamishia kamera, ambayo mara nyingi kuwa ni mitatu ila ipo katika sehemu moja. Samson akamkabidhi Eddy miguu hiyo, Eddy akaichanua kwa haraka, akaifunga kamera hiyo aina ya Canoon 7D, alipo hakikisha kwamba ipo katika sehemu ambayo inafaa. Akachukua moja ya kiti na kukaa.
“Hapo unanipata vizuri?”
Eddy alimuuliza Samson, ambaye alitingisha kichwa akiashiria kwamba amejaa vizuri kwenye frame ya kamera hiyo. Eddy akaanza kuzungumza maneno ambayo hata Samson akajikuta akiwa anashangaa kwani hakujua ni kwanini Eddy ameamua kuzungumza maneno hayo.
“Zima kamera”
Eddy alimuamuru Samson, naye akafanya hivyo. Eddy akaichukua kamera hiyo, akasogea hadi kwenye moja ya computer, akachukua waya aina ya USB, unaotokea kwenye moja ya CPU ya computer moja, akauchomeka kwenye kamera hiyo na kuanza kunakilini video aliyo zungumza na kuiingiza kwenye computer alipo hakikisha amemaliza, akaanza kuifanyia uhakiki. Yote yakiwa yanaendelea Samson hakuhitaji kuzungumza kitu cha aina yoyote kwani hakujua ni nini haswa mpango wa Eddy.
Eddy alipo hakikisha ameimaliza kazi hiyo, akaingia kwenye moja ya mtandao kwa kupitia enternet akaiba freguency za chanel zote za telvishion nchini Tanzania. Pasipo kuomba ushauri wa mtu yoyote akaituma video hiyo kwenye chanel zote za televishion, na kila jambo lililo kuwa likitizamwa kwa wakati huo kwa kila chanel, likasimama na kuingia video aliyo ituma Eddy kwa Watanzania wote.
***
“Ndugu Watanzania wezangu, nimatumini yangu muwazima wa Afya. Nina imani kwamba mumeshangaza sana na kuona hii video kujitokeza kwa muda kama huu, huku baadhi yenu nikiwa nimewakatishia kile mulicho kuwa mukikitazama.”
Sauti inayo toka kwenye luninga ya moja iliyomo ndani ya chumba kimoja, ikaanza kupenya taratibu kwenye masikio ya binti ambaye ni siku ya pili sasa amelala pasipo kujitambua.
“Nichukue nafasi hii kuwashukuru wale wote ambao mumeweza kunitumia rambirambi na kuguswa na msiba wa familia yangu, kusema kweli nimefarijika na kuamini kwamba watanzania ni watu wakarimu wenye upendo katika mioyo yao japo si wote.”
“Katika kuzungumza hayo yote niende kwenye pointi yangu ya msingi iliyo nifanya kuituma video hii kwa uma.Kuanzi tarehe hii ya leo, nimeamua kujivua rasmi uwaziri wa Ulinzi wa nchini Tanzania. Najua kwa upande mmoja itakuwa ni huzuni kwa wale ambao nimesha wahi kuwafanyia wema na kuzitetea haki zao, ila pia itakuwa ni sherehe na furaha kwa wale ambao wanakwenda kinyume na sheria za nchi hii.”
“Hivyo basi, mali ulinzi ambavyo vyote nilipatiwa na serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania, ninavirudisha kwao. Nitabaki kuwa Eddy, EDDY GODWIN. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Tanzania asanteni kwa kunisikiliza.”
Video hiyo ikaisha na vitu vilivyo kuwa vikiendelea kwenye chanel mbalimbali vikaendelea kama kawaidia.
“Haaa huyu jamaa ana maana gani sasa”
Kijana aliyo ndani ya chumba hicho alizungumza akiwa ameitumbulia macho Tv yake, akiwa katika mshangao huo, binti aliye mlaza kitandani kwake taratibu akanyanyuka akionekaa kuchoka sana.
“Hapa nipo wapi?”
“Ahaa hapa upo ndani kwangu”
Kijana huyo alizungumza huku akitabasamu sana, kwa haraka akanyanyuka kwenye sofa moja alilo kaa nakwenda kitandani kumfwata binti huyo.
“Wewe ni nani?”
“Mimi naitwa Dulla, wewe je unaitwa nani?”
Binti huyo badala ya kujibu kitu chochote, akajitazama mwili mzima, hapakuwa na alama yoyote ya yeye kuumia. Mavazi yake aliyo yavaa siku ya mwisho kabla hajatekwa na mtu asiye mjua ndio hayo hayo aliyo yavaa.
“Nahitaji kwenda nyumbani”
Binti huyo alizungumza huku akijaribu kushuka kitandani ila Dulla akamzuia kwa kumshika kwenye paja la mguu wa kushoto, kwa kitendo cha haraka Dulla akajikuta sura yake ikiwa imekandamizwa kwenye godoro huku mkono wake alio kuwa umeshika paja la binti huyo mrembo sana, ukiwa menyongorotwa kwa nyuma na kumfanya kutoa mlio wa maumivu makali, ila haukusikika sana kwani sauti yote iliishia kwenye godoro hilo.
“Wewe ni nani?”
Binti huyo alizungumza kwa sauti ya ukali, huku akiwa amekaa juu ya kiuno cha Dulla na kuzidi kuunyongorota mkono huo kwa kuurudisha nyuma kwa nguvu.
“Mimi ni Dullaaaaaaa”
Kijana huyo alizungumza huku akilia kwa maumivu makali
“Wewe ndio uliniteka eheee?”
“Hapana nilikusaidia tu mimi”
Kwa maumivu makali anayo yapata Dulla yakamfanya sautio yake kuwa yakilio jambo lililo mfanya binti huyo kidogo kumuamini Dulla sio mtu mbaya kwake. Akamuachia na kushuka kitandani, akakitazama chumba vizuri na kugundua ni chumba cha mtu ambaye anaanza maisha hivi karibuni.
Dulla akanyanyuka taratibu huku wasiwasi mwingi ukiwa umemjaa moyoni mwake, woga wa kumuogopa binti huyo ukazidi kumvaa na kujikuta akikaa kimya, akiwa anamtazama binti huyo kwa macho ya woga.
“Samahani”
Dull hakuamini kama msichana huyo anaweza kumuomba msamaha kwa tukio alilo weza kulifanya, Dull akatingisha kichwa chake kukubali msamjaha huo hii ni baada ya kinya chake kushindwa kuzungumza kwa kigugumizi.
“Umenifikishaje hapa?”
“Hapa nilikueleta ukiwa hujitambu, majuzi nilikuwa nipo pembezoni mwa fukwe za bahari, nikifanya fanya mazoezi. Ila kwa bahati nzuri niliweza kukuona ukiwa umesimama kwenye moja ya bustani katika jumba la kifahari. Ila ulipo kuwa pale, nyuma yako nikamuona mtu aliye valia suti nyeusi pamoja na shati jeupe.”
“Sikusikia mtu huyo alicho kizungumza, ila ulipo geuka nikashangaa akikupiga ngumi, kisha akakubana na kitambaa cheupe puani mwako, nilijificha baada ya kumuona mtu huyo akija upande wa ufukweni karibu sana na nilipo mimi.”
“Yule jamaa alikuingiza kwenye moja ya jiwe kubwa kama mwamba lenye tobo kubwa ambapo mtu ukiingia humu si rahisi kwa watu kuweza kukuona.”
Dulla alizungumza kwa sauti ya upole huku akimeza mafumba ya mate ya hapa na pele, kisha akaendelea kuzungumza.
“Yule jama baada ya kuondoka, mimi nikakuchukua na kukuingiza kwenye kigari change nilicho kuwa nimekiweka pembezoni mwa barabara na kukuleta hapa nyumbani kwangu.”
“Haya ni maeneo gani?”
“Mbezi mwisho”
Binti huyo akapiga hatua hadi dirishani akafungua dirisha na kuchungulia nje ambapo akaona ukuta tu ukiwa umepita katika eneo hilo. Akalirudishia pazia kama alivyo likuta na kumtazama kijana huyo anaye onekana mpole, akamchunguza vizuiri akajiridhisha moyoni mwake anaweza kummudu kama atamletea fujo yoyote.
“Nikuandalie chai?”
Dulla alizungumza binti huyo hakujibu kitu cha aina yoyote, likawa ni jibu tosha kwa Dulla kwamba anaweza kuandaa chochote kitu kwani tangu amuokoe binti huyo hakuna kitu alicho weza kukiingiza tumboni mwake. Dulla akaandaa kifungua kinywa kwa binti huyo na kukiweka mezani, binti huyo taratibu akaanza kufakamia soseji na mayai yaliyo andaliwa vizuri na kijana huyo huhu akishushia na mafumba ya chai.
“Umejitahidi katika kupika”
“Ahaa asante sana”
Dulla akajibu kwa kufurahi sana kwani aliweza kulishuhudia tabasamu la binti huyo anaye onekana ni mkali sana na nimtu asiye penda uzembe wa aina yoyote.
“Hapa unaishi na nani?”
“Peke yangu, leo nipo mapumziko, mimi ni daktari. Nina mwaka mmoja kazini”
“Ahaaa sawa, naomba maji ya kunywa”
Dulla akanyanyuka na kulisogelea friji lake dogo, akafungua na kutoa jagi lililo jaa maji, akayamimina kwenye glasi moja kubwa kiasi kisha akamkabidhi binti huyo ambaye hadi wakati huu hakulitambua jina lake anaitwa nani. Binti huyo akayagugumia maji hayo kwa mfululizo, kisha akaiweka glasi hiyo juu ya meza na kumtazama Dulla
“Asante kwa chakula chako, nahitaji kurudi nyumbani”
“Ahaa mbona mapema sana?”
“Nimekuambia nahitaji kurudi nyumbani sawa”
Sauti ya ukali ya binti huyo ikamfanya Dulla kustuka na kujikuta akinyanyuka na kuanza kuitafuta funguo ya gari lake ni wapi ilipo, alipo hakikisha ameiipata akamgeukia binti huyo aliye simama karibu na mlangoni tayari kwa kuondoka.
“Tunaweza kwenda”
Dulla alizungumza kwa sauti ya upole huku akishika kitasa cha mlamgo wa kutokea tayari kwa kuondoka.
***
“Maana yake ni nini kufanya hivi?”
Raisi Praygod aliwauliza baadhi ya washauri wake alio waita ofisini kwake mara baada ya kuiona video ya waziri wa ulinzi bwana Eddy Godwin.
“Labda atakuwa ameungana na baba yake”
Mshauri wake mmoja alizungumza nakumfanya mwengine kuongezea neon
“Kweli damu ni nzito kulilo maji na mototo wa chui ni chui tu hawezi kuwa paka”
“Sasa tumfanye nini?”
“Kikubwa huyo ni kumkamata na kuhakikisha kwamba anataja ni wapi alipo baba yake”
Mshauri huyo, kazi yake ni kuwasoma wezake kwani ni miongoni mwa wanachama wa D.F.E, na yeye ndio mvujishaji wa siri zote za ikulu kwa Mzee Godwin.
“Au muheshimiwa unaonaje ukamtangaza kama most wanted”
“Most wanted ni lazima kuwe na kidhibitisho cha kumfanya yeye kuwa ni mmoja wa watu wanao tafutwa”
“Muheshimiwa kama ni ushahidi basi hiyo kazi niachie mimi, nitahakikisha nay eye tunamfanya kama tulivyo mfanya baba yake”
Wote watano akiwemo raisi Praygod wakajikuta wakitabasamu wakiamini mpango wao umekwenda sawa sawa, lakini yote yaliyo kuwa yakiendelea ndani ya ofisi hiyo Rahab aliweza kuyasikia, hii ni baada ya kuingiza kinasa sauti kwenye suti ya mumewe pasipo yeye kujijua wakati akiwa anamuandaa wakati wa asubihi akielekea kwenye kikao hicho na washauri wake.
Rahab akatabasamu huku akiitazama simu yake aliyo iunganisha moja kwa moja na kinasa sauti hicho. Akaachia tabasamu na kujiapiza washauri wote wa ofisi ya mume wake ni lazima wafe kwani wanataka kuipoteza furaha yake ambayo ni Eddy Godwin.
==> ITAENDELEA
Usikose kufuatilia sehemu inayofuata kupitia ubuyublog.com
Post your Comment