Get the latest updates from us for free

mas template
Home » , » SORRY MADAM -Sehemu ya 55 & 56 (Destination of my enemies)

SORRY MADAM -Sehemu ya 55 & 56 (Destination of my enemies)

Written By Bigie on Monday, April 24, 2017 | 11:43:00 AM

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWAILIPOISHIA
ILIPOISHIA
“Mungu wangu…..!! Umezinduka?”
Phidaya alizungumza huku akipiga magoti chini, akakinyanyua kichwa cha Black Shadow, akakiweka kwenye mapaja yake, akijaribu kumpa huduma ya kwanza mgonjwa, macho ya Eddy yaliyo jaa machozi ya maumivu makali ya mbavu zake zilizo piga chini, alipo kuwa akijaribu kunyanyuka kitandani ili kumuona mwanamke mwenye sauti ya inayo fanana na Phidaya, yakatua usoni mwa nesi huyo, akajikuta akistuka kwani ni Phidaya mwenyewe, ndiye aliyepo mbele yake akimuhudumia.

ENDELEA
Kwa haraka Phidaya,  akakiweka kichwa cha Black Shadow chini, akamnyoosha ili asiendelee kujikunja na kusabaisha nyuzi alizo shonwa kwenye mbavu kuachia. Akatoa simua yake na kumpigia daktari msaidizi wa dokta Ranjiti, akamuelezea hali ya mgonjwa aliyo kuwa nayo.
“Phidaya……”
Black Shadow akajitahidi kumuita Phidaya na kumfanya astuke na kumtazama mgonjwa wake.
 
“Unalijua jina langu…..?”
“Phid….aa…ya mk……”
Black Shadow hakumalizia sentensi yake akatulia kimya akazimia tena. Phidaya akazidi kuchanganyikiwa ndani ya dakika moja mbeleni daktari akafika akiwa na dawa maalumu za kupunguza maumivu, wakasaidia na Phidaya kumnyanyua Black Shadow na kumrudisha kitandani mwake. Dokta akamfantia uchunguzi wa haraka, cha kumshukuru Mungu hapakuwa na itilafu iliyo weza kujitokeza kwenye mshono wake.
 
“Amepoteza fahamu kutokana na muumivu makali sana”
Dokta Yan alimuambia Phidaya aliye onekana kuwa na wasiwasi mwingi.
“Ila dokta Yan, huyu mgonjwa anaonekana kama kunijua mimi”
“Kukujua wewe kivipi?”
“Ameniita jina langu la Phidaya”
Dokta Yan akabaki akiwa na mshangao asijue ni kitu gani kinacho endelea. Kila mara Phidaya akajikuta akijifuta jasho usoni mwake na kitambaa chake, mapigo ya moyo wake hayakutulia kabisa kiasi cha kumfanya ahisi kuna jambo ambalo Black Shadow analitambua, isitoshe maneno yake ya mwisho yaliyo katika katika alipokuwa akizungumza ndio yalizidi kumchanganya.
 
“Hivi atazinduka kweli?”
“Ndio nesi atazinduka, ila itamchukua kama masaa mengine tisa hadi kumi, kwa maana sindano nilkiyo mchoma inapunguza mumivu taratibu taratibu”
“Isije akawa akaka kwa muda mrefu kama alivyo kaa?”
“Hapana atakuwa salama tu nesi, ila nikuulize swali?”
“Uliza tu”
“Mbona una wasiwasi mwingi sana juu ya huyu mgonjwa tofauti sana na mara ya kwanza?”
“Kusema kweli dokta Yan mimi sielewi kabisa kichwa change, nahisi kuna kitu ambacho najaribu kukikumbuka ila nashindwa kujua ni kitu gani hicho”
 
Macho yakamtoka dokta Yan, wasiwasi mwingi na yeye ukamtawala ila akajikaza asiweze kuuonyesha mbele ya Phidaya. Akamuomba Phidaya aondoke akaendelee na kazi zake. Phidaya hakuwa na hiyana yoyote kwa daktari huyo msaidizi wa mume wake. Akaondoka na kuelekea ofisini kwake akamuacha Phidaya akiwa amesimama jirani kabisa na kitanda cha Black Shadow.
 
Phidaya kwa mara nyingine, akajikuta akianza kumvua Black Shaodow kinyago alicho kivaa, akafanikiwa kumaliza kukivua kinyago hicho na kukishika katika mkono wake wa kushoto. Sura nzuri ya Black Shadow, ikamfanya aitazame kwa muda mwingi sana zaidi ya dakika kumi.
Wazo moja likamjia kichwani mwake, akatoa simu yake na kuingia upande wa kamera kisha akampiga Black Shadow picha nne, alipo maliza akamvalisha kinyago chake kama kilivyo kuwa na kutoka zake ndani ya chumba hicho.
                                                                                                 ***
“Ndio dokta kuna jambo nahitaji kukuambia”
Dokta Yan, alizungumza kwenye simu yake mara ya kuingia ofisini kwake na kujifungia kwa ndani. Simu hiyo iliyopo hewani, anazungumza na dokta Ranjiti akiwa ndani ya gari akirudi kutoka kwenye mgahawa alipo kwenda kuonana na Kim.
“Jambo gani hilo?”
“Ni kuhusiana na mke wako”
“Amefanyaje?”
“Nahisi anaanza kuutafuta ukweli juu yake”
“Umelijuaje hilo?”
“Anadai kwamba yule mgonjwa mpiganaji amezinduka, na amemuita jina lake”
“U…uuu..nasema mpiganaji amezinduka…..?”
 
“Ndio amezinduka na amemuita mkeo jina lake na hapa kunaonekana kuna kufamiana”
“Sasa umefanyaje wewe”
Dokta Ranjiti alizungumza huku akionekana kama amechanganyikiwa kwa taarifa aliyo pewa.
“Ilinibidi nimchome sindano ya usingizi, ili hadi utakapo rudi tuweze kujua tunafanyaje”
“Kazi nzuri Yan, nipo njiani nakuja sasa hivi”
Dokta Yan akakata simu na kukaa vizuri kwenye kiti chake akimfikiria mgonjwa waliye muweka katika chumba cha siri, kwani yeye ni mtu wa karibu wa dokta Ranjiti  na anafhamu kila kitu ambacho kimetokea kati ya Phidaya na Ranjiti.
                                                                                                    ***
   Mawazo ya Shamsa yote yakahamia kwa Phidaya, mwanamke aliye mchukulia kama mama yake, ambaye alimpatia upendo mkubwa  kama alivyo kuwa amepatiwa kwa marehemu mama yake. Tangu aweze kuishi na Phidaya kwa miaka zaidi ya mitatu, alitokea kumpenda mama huyo, kwani wote asili zao zimeenda na ilikuwa ni vigumu sana kwa watu kuwatofautisha hao kama si mtu na mama yake. Asili yao ya kihidi ndio ilizidi kuwafanya wafanane japo si sana.
 
“Shamsa una waza nini?”
Sa Yoo alimuuliza Shamsa aliye jilaza kwenye sofa ndani ya sebule yao, huku miguu yake akiwa ameiweka juu ya meza kubwa ya kioo iliyopo jirani naye. Shamsa akashusha pumzi kidogo kisha akaishusha miguu yake kwenye meza na kukaa sawa.
 
“Namfikiria yule nesi kule hospitalini”
“Sasa ndio anakufanya uwe katika mawazo kiasi hicho, kama ni ugomvi si ulisha isha”
“Hapana si hivyo Sa Yoo”
“Ila ni nini?”
Ýule ni mama yangu”
Sa Yoo macho yakamtoka kama ameona kitu cha kushangaza sana na chakutisha, taratibu Sa Yoo akajiweka vizuri kwenye sofa alilo kaa na kuendelea kumtumbulia macho Shamsa.
 
“Mbona unanitumbulia macho yako hivyo, unaniogopesha bwana”
“Hamna Shamsa, nashangaa, inakuwaje yule nesi awe mama yako?”
“Kweli ni mama yangu, ila cha kushangaza tulisha mzika, yeye, bibi na mdogo wangu wa kiume anaitwa Junio”
“Sasa, Shamsa unataka kuniambia siku hizi watu wanaweza kurudi kutoka wafu au….?”
“Sa Yoo sio hivyo hata mimi nashangaa kwanini imekuwa hivyo”
 
“Ahahaa hapana Shamsa bado hujanishawishi”
“Hembu lete Laptop”
Sa Yoo akanyanyuka na kuichukua Laptop ilipoto kwenye meza ya chakula akarudi nayo na kukaa kwenye sofa alilipo Shamsa. Akaiweka mezani na Shamsa akaifungua na kuiwasha, wakasubiria kwa sekunde kumi na tano ilipo waka, Shamsa akaingia kwenye mtandao wa ‘google’ akaandika jina lake, haikuchukua sekunde jina lake likawa limejitokea kwenye kioo cha laptop hiyo akaingia kwenye sehemu ya picha, zikafunguka picha nyingi, picha ya kwanza kabisa kuonekana ni yake  akiwa na Phidaya pamoja na Junio. Macho yakamtoka Sa Yoo. 

Akaivuta laptop karibu kudhibitisha picha anayo inaoa kweli nesi aliye muoana anafanana kabisa na mtu anaye muona amesimama na Shamsa. Mwanga wa Laptop hiyo ukaanza kufifia huku taa nyekundu ndogo ikiwaka chini kidogo ya kioo hicho.
“Ohoo inaisha chaji, hujaichomeka kwenye kebo ya umeme hembu inama uivute hiyo kebo”
 
Sa Yoo alizungumza na Shamsa akafanya kama alivyo ambiwa, gafla Laptop hiyo ikarushwa mbali na kuangukia chini, huku kioo cha dirisha la karibu walipo kaa, likipasuliwa na risasi ambayo imeingia na kumkosa Shamsa aliye inama chini kuvuta kebo hiyo na kutua kwenye laptop.
“Sa Yoo inama chini”
Shamsa alizungumza kwa sauti kali, Sa Yoo bila hata kuuliza akalala chini kabisa ya sakafu.
“Shamsa ni nini hicho”
“Ni risasi hiyo”
Risasi mfululizo zikaanza kumiminika ndani ya sable yao, meza ya kioo ikapasuliwa, kila mmoja akawa amelala chini na kujibanza kwa chini kwenye sofa walilo kuwa wamelalia.
                                                                                                         ***
  Kim baada ya kukabidhiwa kazi na dokta Ranjiti ya kumuua Shamsa hakuona haja ya kupoteza muda wala kujipanga kwani mtu ambaye anakwenda kumuu kwake ni sawasawa na siafu mdogo ambaye anaweza kuminya minya chini kwa kidole chake kimoja. 

Akarudi nyumbani kwake na kuingia kwenye compyuta yake, akalisaka jina la Shamsa Eddy, akafanikiwa kulipata, kwa utaalamu wake alio kuwa nao kwenye maswala ya mtandao akafanikiwa kufahamu hadi nyumba anayo ishi binti huyo alipo, hakikisha kwamba amefanikiwa kumpata, akafungua droo lake kubwa, ambapo akachukua budnuki yake aina ya L115A3 AWM yenye uzito usio pungua kilo 16 ikiwa na risasi zake tano ndani ya magazine. 

Akaiingiza kwenye begi lake kubwa, akachukua na bastola zake mbili, akazichomeka kwa kiunoni kwa nyuma, akajiweka sawa na kutoka nje ya nyumba yake. Akaliweka begi lake ndani ya gari lake aina ya Range Rover, na taratibu akaanza kuondoka kuelekeaeneo la tukio.
 
Lee Si, aliweza kumuona Kim akiwa anatoka nyumbani kwake, kama alivyo agizwa na bosi wake Madam Phidaya, akaendelea kumfwatilia mtu huyo ambaye amepewa kazi na dokta Ranjiti.
Kim hakustuka kwamba anafwatiliwa hadi alipo fika katika eneo la karibu kabisa na nyumba ambayo anaishi Shamsa. Kwa uzuri karibu na nyumba hiyo kuna moja ya dorofa linalo endelea kujengwa ila ni takribani wiki mbili ujenzi wa jengo hilo umesimamishwa kutokana na uchunguzi unao fanyiwa mkandarasi wa gorofa hilo.
 
Kim akapanda hadi gorofa ya tano akiwa na begi lenye bunduki yake hiyo kubwa, ambayo mara nyingi anaitumia kwa mauaji ya mtu mmoja mmoja. Akaitoa bunduki yake hiyo na kuifunga, akaiweka sawa kwenye moja ya dirisha linalo elekea kwenye nyumba ya Shamsa.
   Kwa kutumia Lensi ya bunduki hiyo akafanikiwa kuwaona mabinti wawili wakiwa wamekaa kwenye sofa huku wakionekana vichwa kwa nyuma. Kitu kilicho mchanganya hakujua kati ya hao mabinti wawili yupi ni muhusika anaye paswa kuuawa. 

Akamlenga shabaha binti wa kwanza upande wa kushoto kwake, ila binti huyo alipo inama kidogo aliweza kuina sura yake, na kutambua kwamba sio ambaye anatakiwa kumuu. Akaihamishia shabaha yake kwa binti wa kulia kwake, alipo hakikisha kwamba amemuweka vizuri kwenye tageti, akafyatua risasi, ila binti huyo aliinama chini kabla ya risasi hiyo kufika na kutua kwenye laptop ambayo hapo mwanzo binti huyo alikuwa ameiziba.
 
”Shitii…….”
Kim alizungumza huku akiwa ameyakaza meno yake, kwani tangu aanze kuifanya kazi ya mauaji hakuwahi kumkosa shabaha yule aliye kusudia kumuua, hata iweje, ila kwa huyu binti sijui imekuwaje. Binti wa pili naye akapotea kwenye tageti yake na risasi aliyo kuwa amemlenga ikatua kwenye meza ya kioo na kupasuka pasuka. Sofa ndilo lililo haribu mpango mzima wa Kim kumuua Shamsa, kila alipo jaribu kuwatafuta hakuweza kuwaona.
 
Lee Si, alishushudia mpango mzima ukiwa unaendelea kwa muuji na wanao paswa kuuliwa, akiwa amekaa ndani ya gari lake mbali kidogo na nyumba ambayo ishi Shamsa.
“Hapa ndipo atakapokuwa anaishi yule binti”
Lee Si alizungumza huku akitazama jinsi Kim akipiga risasa zinazo toka kimya kimya kutokana na bunduki anayo itumia kufungwa kiwambo cha kuzuia risasi.
 
“Hapana naweza kufanya kitu”
Lee Si akawasha gari lake, akakanyaga mafuta kwa kasi na kwenda kulipaki mbele ya mlango wa nyumba ya Shamsa, kwa utaalamu mkubwa akajirusha nje ya gari baada ya kulisimamisha, akaupiga teke mlango huo na ukafunguka, jambo lililo washangaza Sa Yoo na Shamsa, hata Kim mwenyewe akashangaa kuona gari nyekundu ikiwa imesimama nje ya mlango wa Shamsa.
                                                                                                     ***
“Vipi mwenzetu tulisikia kwamba unaumwa?”
Halima alimuuliza Rahab huku akijipangusa machozi ya furaha yaliyo mtiririka usoni mwake.
“Yaa kweli nilikuwa ninaumwa?”
“Nini zaidi”
Fetty alimuuliza Rahab huku akiwa ameupitisha mkono wake mmoja mabegani mwa Rahab.
“Ahaa ni malaria tu ilinishika nusu iniue”
Rahab aliongopea
 
“Doo pole sana”
“Sasa mke wa raisi inakuwaje anaumwa Malaria hadi ikulu kuna mbu kweli?”
Anna alitania huku akicheka, wote wakajikuta wakiangua kicheko, wakamkaribisha Rahab na kuketi naye kwenye masofa yaliyomo ndani ya chumba chao.
“Vipi unatumia kilevi, au ndio umestaarabika Mrs President”
“Hapana jamani, bado nina dozi musije mukaniua mwana wa mwenzenu. Haya niambieni yaliyo wakuta kwa maana nasikia mulikufa nyinyi?”
“Ni kweli kama tetesi ulivyo sizikia kwamba tumekufa ila ndivyo dunia inavyo jua, ila ukweli hatujakufa”
 
Fetty akaanza kuadisia mkasa wa wao tangu walipo achana, wakiamini kwamba rafiki yao huyo alikamatwa kwenye tukio la mwisho la wao kuvamia benki hadi wao walivyo pitia matatizo mengi pamoja na mateso. Hawakumficha ujuzi walio upata kwa bwana Rusev, na jinsi alivyo watelekeza na kuangukia mikononi mwa Wamarekani. Mateso makali waliyo pitia wakiwa gerezani hadi kuokolewa na Mzee Godwin na kurudi tena Tanzania.
Machozi yakamwagika, Rahab, kwani historia hiyo iliyo wapata wezake imemsikitisha kupita maelezo, na yeye akawaadisia mambo yote yaliyo mpata kwenye maisha yake hadi kuolewa na raisi Praygod, ila kitu alicho waficha wezake na nguvu zake za ajabu alizo kuwa nazo.
 
“Ila unampenda huyo mumeo”
Agnes aliuliza huku akiwa amekazia macho Rahab.
“Ahaaa hivyo hivyo tu maisha yanasonga”
“Mmmmm ila kunaonekana ikulu ni kuzuri, mwenzetu huna hata doa”
Wote wakacheka, Rahab akatambulishwa kwa Jaquline na Manka. Wakaendelea kupiga piga stori kuhusiana na mpango wao wa kuingia ikulu kupitia kura za wananchi.
 
“Musijali nitahakikisha munaingia ikulu na si munatambua raisi Praygod ni mmoja wa target yetu ambaye bado hatujafanikiwa kuiangusha?”
Rahab alizungumza huku akiwatazama wezake wote ndani ya chumba, Fetty akatingisha kichwa akimaanisha kwamba anakumbuka.
“Basi nitakuwa nikiwaeleza kila kitu ambacho kitakuwa kinaendelea ndani ya ikulu”
Wote wakampigia makofi Rahab, kila mmoja akaamini ushindi wa Mzee Godwin kuingia ikulu upo karibu kuiva.
                                                                                                       ***
   Dokta Ranjiti akasimamisha gari lake eneo la maegesho na kushuka kwa haraka, akaanza kutembea kwa kasi kueleka ofisini kwake, akili yake alihisi inakwenda kuchanganyikiwa, swali kubwa alilo jiuliza, imekuwaje Black Shadow, alitambue jina la mke wake. Kila alipo jaribu kuhisi labda Black Shadow, aliweza kusoma koti la mke wake, ambalo kila mfanya kazi wa hospitalini kwenye nguo yake ya kazi huwa kuna jina.
 
 Hilo nalo halikumuingia kabisa akilini, akafungua ofisi yake na kukaa kwenye kiti chake cha kuzunguka, kwa haraka akampigia simu dokta Yan, ndani ya dakika tatu akawa amefika kwenye ofisi ya dokta Ranjiti.
“Hembu nieleze ilikuwaje kuwaje?”
Dokta Ranjiti alizungumza kwa sauti ya chini ya kunong’oneza, kwani swala hilo ni nyeti sana na halikupaswa mtu yoyote kuweza kulisikia.
“Kwa madai yake amesema kwamba mgonjwa alimuita baada ya kuzinduka”
 
Naye dokta Yan alizungumza kwa sauti ya chini.
“Sasa huyo Black Shadow amemjuaje mke wangu?”
“Hata mimi sitambui dokta, au anaweza kuwa ni rafiki wa karibu wa huyo mume wake uliye niambia?”
“Yaweza kuwa, au unaonaje tukamfunue sura yake, kwa maana najishangaa tumemfanyia mgonjwa upasuaji hata kuiona sura yake”
 
“Hapo kweli umenena dokta”
Dokta Ranjiti akashusha pumzi nyingi, huku akimtazama dokta Yan, rafiki yake wa muda mrefu sana. Kwa pamoja wakanyanyuka, na kutoka ndani ya ofisi kuelekea katika chumba cha siri walipo mlaza Black Shadow.
   Phidaya akaitazama picha ya Black Shadow kwenye simu yake, akayafumba macho yake kwa muda mrefu, huku akihakikisha kwamba anajaribu kumkumbuka mtu huyo, kwani kila alipo jaribu kuitazama picha hiyo mapigo yake ya moyo yalimuenda kasi sana.
 
 Kwa mbali sana sauti ya Black Shadow, ikaanza kumjia kwenye kumbukumbu zake, sauti hiyo alianza kujitahidi kuifananisha na mtu ambaye kichwani mwake hayupo. Machozi ya uchungu akajikuta yakimtoka taratibu. Hakujua ni kwanini machozi hayo yanamtoka, ila yakazidi kumtoka. Ikamlazimu kuyafumbua macho yake na kujifuta tena machozi yake kwa kitambaa.
 
“Nimekuaje mimi”
Phidaya alizungumza huku akiikodolea macho picha hiyo, akaanza kuikuza vizuri kuna alama akaiona shingoni mwa Black Shadow, picha kubwa akilini ikamjia akamuona mwanaume aliye valia suti nyeusi akiwa amesimama mbele ya watu wengi, walio huzuria sherehe ambayo kwenye kumbukumbu zake, Phidaya hakuijua ni sherehe gani. Taratibu na kwahisia Phidaya akayafumba macho yake huku akiendelea kuikumbuka alama hiyo ya shingoni. Busu lililo mjia kwenye kumbukumbu zake, alilo lipiga mpiganaji huyo likamstua kutoka kwenye kumbukumbu zake, akafumbua macho yake.
 
Mapigo ya moyo yakaanza kumuenda mbia, safari hii yakiwa na kasi kubwa sana. Akanyanyuka huku machozi yakimlenga lenga, akili yake ikamtuma kueleka katika chumba cha siri. Bila ya kupoteza muda akaanza kukimbia kuelekea kwenye mlango wenye lifti inayo kushusha chini kwenye chumba hicho cha siri. Akaingia kwenye lifti iliyo anza kumpeleka chini taratibu.
 
Dokta Ranjiti na Dokta Yan, wakaingia kwenye chumba walicho mlaza Black Shadow, wakasimama jirani kabisa na kitanda cha Black Shadow, kwa ishara dokta Ranjiti akamuagiza dokta Yan amvue, kinyago Black Shdow. Dokta Yan kwa mikono yake miwili, akamvua Black Shadow, kinyago chake.
Moyo wa dokta Ranjiti ukadunda kwa kasi kama mtu anaye jaza mpira wa baiskeli kwa pampu, macho yakamtoka, jasho likamwagika. Hadi dokta Yan akaligundua hilo kwa mwenzake.
 
“Dokta Ranjiti vipi?”
“Hu..yu ndio mume wa Phidaya, anaitwa Eddy”
Kauli ya dokta Ranjiti ikamsimamisha gafla Phidaya jirani kabisa na mlango wa chumba alicho lazwa Black Shadow, akaanza kunyata taratibu, hadi kwenye upenyo mdogo wa mlango huo ulio rudishiwa, akamuona dokta Yan, akiwa ameshika kinyago cha Black Shadow mkononi, huku mume wake dokta Ranjiti mikono yake miwili akiwa ameikusanya kichwani mwake akiwa katika taharuki kubwa akimshangaa Black Shadow aliye lala kitandani hajitambui.
                                                                                                 
SORRY MADAM (56)  (Destination of my enemies)

“Sasa tutafanyaje dokta Ranjiti”
Dokta Yan aliuliza huku naye wasiwasi mwingi ukiwa umeanza kumuingia. Dokta Ranjiti hakuwa na jibu la kujibu, mwili wake wote unachemka kwa joto kali, lililo sababishwa na wasiwasi mwingi sana. Akaanza kutembea kwa hatua kuelekea mlangoni. 

Kwa haraka Phidaya akakimbia hadi kwenye moja chumba kinacho tumika kama stoo ya kuhifadhia madawa ya hospitali hiyo na kujibanza humo. Dokta Yan akakirudishia kinyago cha Black Shadow na kutoka, akamkuta dokta Ranji akiwa amesimama kwenye lifti akimsubiria wapandishe juu. Wakaingia wote wawili kwenye lifti huku kila mmoja akiwaza lake kichwani mwake, pasipo kujua mambo yote waliyo yazungumza Phidaya mkewe amayasikia.
Phidaya akachungulia nje akiwa ndani ya chumba cha stoo alicho ingia, alipo ona kuna usalama kwa haraka akaanza kutembea kuelekea kwenye chumba alicho lazwa Black Shadow.
 
Akafungua mlango na kuingi, kisha akaufunga kwa ndani kuhakikisha kwamba hakuna mtu ambaye anaweza kuingia ndani ya chumba hicho yeye akiwa ndani. Akatembea kwa hatua za taratibu hadi kwenye kitanda cha Black Shadow, taratibu akapiga magoti chini, huku akimtazama Black Shadow, shingoni mwake. Maneno ya mumewe dokta Ranjiti yakaanza kumjia kichwani, machozi yakaanza kumwagika, kiasi cha kumfanya ajikute akiangua kilio cha uchungu sana.
 
‘Hu..yu ndio mume wa Phidaya, anaitwa Eddy’
Kila maneno hayo yalivyo zidi kujirudia kichwani mwake ndivyo jinsi hasira yake ilivyo zidi kumpanda na kumchukia sana mume wake.
“Ina maana huyu ni mume wangu?”
Phidaya alijiuliza huku kiganja chake cha kushoto kikipapasa kifua cha Black Shadow.
 
“Imekuwaje Ranjiti akanioa?”
Phidaya hakupata jibu kabisa ya maswali yake, kwa hasira akasimama na kuelekea mlangoni, hakuona haja ya kuendelea kukaa na kujiliza kama mtoto wakati ana uwezo wa kumkabili Ranjiti na kumuuliza kila kitu ambacho kilitokea kwake. Akaingia kwenye lifti na kupandisha juu. Kwa mwendo wa hasira na sura iliyo jikunja Phidaya akazidi kutembea kuelekea kwenye ofisi ya mume wake, hata baadhi ya menesi na wafanyakazi wanao mtambua, walijikuta wakimshangaa.
 
Akiwa anamalizia kupandisha ngazi ya mwisho, ili kuanza kutembea katika kordo ndefu ilipo ofisi ya mumewe, simu yake ikaata, hakuwa mwingine balia ni Lee Si. Akaiweka sikioni alicho kisikia kikamstua na kuzidi kuichanganya akili yake.
                                                                                                             ***
“Nimekuja kuwasaidia”
Lee Si, alizungumza huku akiwa amejibanza sehemu ambayo si rashisi kwa Kim kumuona akiwa katika gorofa anapo fanya mashambulizi yake. 
 
“Tambaeni kwa kuja kwangu huku, haraka”
Shamsa, bila hata kujiuliza, akapiga sarakazi kazaa kwa kasi na kuangukia sehemu alipo simama Lee Si. Sa Yoo kila aliposikia mshindo wa kitu kikipiga kwenye sofa hiyo, alijikuta akipiga kelele za woga, huku akiendelea kulala chini mikono yake akiwa ameiweka kichwani mwake.
“Dada nyanyuka twende”
Lee Si, alizungumza huku akimtazama Sa Yoo aliye endelea kulala chini na kujikunyata. Shamsa akaangaza macho yake huku na huku, akaiona bastola ya Lee Si, akiwa ameishika mkono wake kushoto huku mkono wa kulia akimuimiza Sa Yoo, kunyanyuka haraka.
Shamsa pasipo kuomba akaibeta bastola ya Lee Si, kwa haraka akaikoki akaanza kubingiria kuelekea alipo Sa Yoo, akajibanza kwenye sofa.
 
“Sa Yoo kimbia nakulinda sawa”
“Mmmmmm”
Sa Yoo alitingisha kichwa na kukataa kwenda popote hapo chini ya sofa ndio kwenye usalama wake, kibao kikali kutoka kwa Shamsa kikatua shavuni mwake, na kumfanya amtumbulie macho yake makubwa Shamsa.
“Kimbiaaaa”
Shamsa akaitoa mikono yake juu kidogo na kuanza kufyatua risasi kuelekea kwa Kim aliyopo gorofani. Tukio hilo likiwa linaendelea Sa Yoo alichomoka kama mshale na kukimbia kwa Lee Si.
 
Shamsa kwa haraka naye akimbilia walipo wezake, huku risasi kadhaa zikimkosa kosa na kugonga kwenye vitu vingine, wote kwa pamoja wakatoka nje na kuingia katika gari ya Lee Si. Gari hiyo ikageuzwa kwa utaalamu wa hali ya juu, na kuondoka kwa kasi katika eneo hilo.
Kim alipo ona hivyo, akaicha bunduki yake kubwa na kuanza kushuka kwa kasi kwenye gorofa hilo. Akafika katika eneo alipo lisimamisha gari lake. Akaingia na kuanza kulifukuzia gari la Lee Si.
 
Mwendo kasi wa gari la Kim, likazidi kuwakaribia Shamsa na wezake, woga mwingi ukazidi kumtawala Sa Yoo muda wote akiwa ndani ya gari mapigo ya moyo wake yalizidi kumuenda mbio.
Barabara yenye kona nyingi na iliyopo mlimani, mithili ya bararaba ya mlima Kitonga iliyopo mkoani Iringa nchini Tanzania, Lee Si alizidi kujitahidi kuzikata kona hizo kwa mtindo ambao  alisaidia sana kumuacha Kim kwa umbali kidogo japo gari la Kim lina uwezo mkubwa wa kukimbia, kuliko gari anayo iendesha Lee Si.
 
    Kim kila alipo likaribia gari la Lee Si hakusita kupiga risasi kadhaa zilizo pasua kioo cha nyuma, Shamsa akatoa magazine ya bastola aliyo nayo, akakuta ikiwa imebakiwa na risasi mbili tu, na alipo muuliza Lee Si kama ana magazine ya ziada, hakuwa nayo. Kim akatoa simu yake mfukoni na kumpigia bosi wake, kitendo cha bosi wake kupokea simu, risasi moja kutoka kwa Kim, ikapiga kioo cha pembeni cha dereva na kumfanya Kim kuiachia simu yake na kuwahi kuushika mskani, kuhakikisha gari linarudi barabarani kwani wote walijikuta wakipiga kelele baada ya gari hiyo kuyumba na kutaka kujitosa kwenye korongo.
 
“Sa Yoo hamia siti ya mbele”
Shamsa alitoa mri na wala si ombi, Sa Yoo, akafanya kama alivyo ambiwa nyuma akabaki Shamsa mwenye. Akashusha pumzi zote akanyanya kichwa na kulitazama gari la Kim linavyo wafwata kwa kasi. Akalifumba jicho lake moja, akamuweka Kim kwenye mabano ya macho yake, akafnyatua risasi moja, ikapiga kwenye kioo cha mbele upande alio kaa Kim, cha kushangaza kioo hicho hakikuweza kupasuka, zaidi ya kutoa nyufa chache.
“Mungu wangu”
Sa Yoo alizungumza huku akijibanza chini, Kim, alipo ona hatari ya binti huyo, akaona asilete masihara kwani muda wowote anaweza kupoteza maisha.
 
“Vipi?”
Lee Si alimuuliza Shamsa
“Gari yake haiingii risasi”
Mambo yote yanavyo endelea Phidaya anayasikia kupitia kwenye simu kwani simu ya Lee bado ipo hewani, Risasi kadhaa zikapiga matairi ya nyuma ya gari ya Lee Si, gari yao ikayumba, na kuanza kuserereka barabarani, Kim akaongeza mwendo kasi wa gari lake na kuligonga gari la Lee Si, kwa kasi kilaanza kushuka kwenye maporomoko yaliyomo pembezoni mwa barabara na kuwafanya Shamsa na wezake kupiga kelele za kufa.
                                                                                                       ***
  Mwili mzima ukaanza kumtetemeka Phidaya, ndani ya sekunde kadhaa hakuweza kusikia kitu chochoe kutoka kwenye simu hiyo kwani ilikatika na kubaki akiwa katika alama ya kuuliza. Lee Si kijana wake na Shamsa ambaye anamtegemea kqatika kurudisha kumbukumbu zake, ndio hao wamesha poteza maisha kwenye ajali.
 
“Hapana hawajafa”
PPhidaya alizungumza huku akibadilisha safari na kueleka ofisini kwake, akachukua funguo ya gari lake na kutoka pasipo kusemeshana na mtu wa aina yoyote. Akaingia kwenye gari lake, kwa haraka akaondoka katika eneo la hospitali na kwenda pasipo julikana, lengo lake na kuweza kuhakikisha kwamba  anazungumza na Shamsa
                                                                                                       ***
 Kim akafunga beki za gari lake na kusimama pembezoni mwa barabara na kulitazama gari la Lee Si linavyo endelea kuteketea kwa moto. Moyoni mwake akajawa na furaha kubwa kwani kazi yake imekuwa rahisi japo iliingia ugumu kidogo. 

Akatazama pande zote za barabara hakuona mtu gari yoyote inayo kuja katika eneo hilo. Akarudi kwenye gari lake na kuingia, akaondoka kwa mwendo wa kasi huku akivua gloves zake nyeusi alizo kuwa amezivaa kwenye viganja vyake. Akachomoa simu yake kwenye mfuko wa suruali yake na kuchagua namba ya dokta Ranjiti, akaipiga na kuiweka simu yake sikioni.
 
“Ndio dokta”
‘Vipi umefanikiwa kumaliza kazi?’
“Ndio kila kitu kimekwenda kama nilivyo tarajia”
‘Basi nakuomba tuonane kwenye karakana yangu mida hii kuna kazi ninahitaji kuweza kukupatia”
“Sawa mkuu”
Kim akakata simu, na kuirudisha mfukoni, mwendo wa dakika kumi na tano mbele akapishana na gari za polisi nne pamoja na gari mbili za zima moto zikiwa zinaelekea katika eneo walipo pigiwa simu na wasamaria wema kwamba kuna gari ndogo imepata ajali na kuteketea kwa moto.
“Mumepoteza”
Kim alizungumza huku akiongeza mwendo kasi wa gari lake na kuzidi kutokomea, safari hii akielekea kwenye karakana la dokta Ranjiti.
 
 ***
Muda wote tangu watoke hospitalini, macho yao yote ni kwenye lango kubwa la karakana, analo hifadhia ndege zake nne za kusafriria masafa marefu na mafupi. Dokta Ranjiti yeye wasiwasi haukuweza kupungua hata kidogo ila kwa upande wa dokta Yan, wasiwasi ulisha muisha kwa kile kitu walicho kizungumza njia nzima kwenye gari walipo kuwa wakitoka kuelekea kwenye karakana hilo. 
 
Hospitali hawakukaa kabisa baada ya kutoka katika chumba cha siri, roho ya mauaji juu ya watu wanao taka kumfanya amkose Phidaya ikaendelea kumtesa kiasi cha kuchukua maamuzi magumu kwa watu hao. Simu aliyo pigiwa na Kim kwamba ameifanya kazi ya kumuua Shamsa. Imekamilika, kidogo ikazidi kumpa matumaini ya ushindi na kumtoa wasiwasi alio kuwa nao.

 Utajiri wake akaona si kitu mbele ya penzi lake kwa Phidaya mwanamke aliye chukua asilimia kubwa sana ya maisha yake. Tangu siku ya kwanza kuweza kumuona katika hospitali ya Aghakani nchini Tanzaia, alipo letwa hajitambui, alichanganyikiwa sana. Kikwazo cha yeye kumpata Phidaya kilikuwa ni mume wake pamoja na mama yake mke, ila kwa kazi aliyo weza kuifanya alifanikiwa kumchukua Phidaya pasipo mtu yoyote kugundua, japo watu wengi waliweza kuhudhuria mazisha yake.
 
  Dokta Ranjiti akastuka kutoka katika dibwai la mawazo la jinsi alivyo mpata Phidaya, baada ya kusikia honi ikipigwa nje ya karakana yake yenye ukubwa wa viwanja vitatu vya mpira wa miguu. Wafanyakazi wa eneo lake wakalifungua geti la eneo hilo, ambapo gari ya Kim ikaingia na kuwafwata hadi walipo simama, naye Kim alilisimamisha gari lake pembeni na kushuka.
Wakaalimiana na moja kwa moja wakaelekea kwenye moja ya ndege kwa ajili ya mazungumzo muhimu. Wote watatu wakajifungia ndani ya ndege hiyo na kuanza mazungumzo yao.
 
“Ninacho hitaji mimi ni kumzika huyo Black Shadow, apotelee mbali kabisa”
“Ila huoni kama inaweza kuleta skendo chafu kwa hospitali yako, na kupelekea uchunguzi ukafanyika dhidi yako dokta?”
Swali la Kim, likamfanya dokta Ranjiti kukaa kimya na kukosa cha kuzungumza, dokta Yan akajikoholesha kidogo kisha akatoa na yeye wazo lake.
“Unaonaje ukafanya kama uvamizi na kumchuku mgonjwa na ukaondoka naye na kwenda kumzikia mbali kabisa”
“Uvamizi kwenye hospitali yenu?”
 
“Ndio, tutahakikisha kwamba walinzi hawastukii hilo swala, na wewe utatoka naye, tunacho kihitaji ni wewe kumzika, au kumchoa moto ateketee kabisa ushahidi wake usionekane”
“Sawa nimewaelewa wakuu wangu, ila nahitaji fungu langu muliandae mapema”
“Sikia Kim nipo tayari kukupa kiasi chochote cha pesa, ili mradi huyo mwanaharamu afee. Siwezi kumpoteza mke wangu kwa mpumbavu mmoja”
“Sawa dokta nimekuelewa, kazi inaanza saa ngapi?”
Wote wakatazamana na dokta Yan akatoa jibu, wakakubaliana, wakaagana na Kim, mioyoni mwao wakiwa wamejawa na amani wakisubiria utekelezaji wa kazi yao kuweza kufantika mara moja.
                                                                                                                 ***
Phidaya, akasimamisha gari lake kwenye moja ya kituo cha kuongeza mafuta, akamuomba muhudumu wa kituo hicho kilichopo pembezoni kidogo mwa mji kumuongezea mafuta kwenye gari lake.
“Chooni hapa ni wapi?”
Mfanyakazi huyo alimuonyesha Phidaya akashuka na kuelekea katika sehemu ya vyoo alivyo onyesha, kutokana haja ndogo ilimsihika akaona ajisaidie kwenye moja ya choo cha kike. Akamaliza haja yake, akatoka na kusimama kwenye moja ya sink la kunawia mikono.
 
“Yaani naona hata huruma, sijui kama atakuwa amepona mtu mule ndani”
Mwana mama mmoja alizungumza na simu yake huku akiwa ameibana kwenye sikio lake, huku akisadiwa na bega lake la kulia, huku mikono yake akinawa kwenye moja ya sinki.
“Yaani nimefika pale, nikakuta moshi mwingi, sasa nikawa najiuliza ni kitu gani kinatokea kwenye lile korongo, kushuka na kwenda kutazama hivi nikakuta gari likiteketea kwa moto. Mwanao akanishauri tuwapigie polisi, basi ndio tumewaacha wapo eneo la tukio wakiwa na zima moto”
 
“Haya mwaya mume wangu, nakupenda, sisi ndio tupo njiani tunarudi”
Mwana mama huyo alipo maliza kunawa akaitoa simu yake aliyo kuwa ameibana na kuirudisha kwenye kipochi chake. Phidaya hakusita kumuuliza ni kitu gani alicho kuwa anakizungumzia kwenye simu.
“Ni ajali ya gari moja ndogo nimeikuta inateketea kwenye maporomoko kwenye milima ya Kishing”
“Hiyo gari ina rangi gani?”
Phidaya aliuliza huku mapigo ya moyo yakimuenda mbio, hakutamani kuweza kujibiwa kama jibu analo lifikiria kwamba gari hilo ni la rangi nyekundu.
 
“Lile gari ni larangi nyekundu hivi.  Yaa ni larangi nyekundu”
Phidaya akahisi kama haja ndogo inaanza kumtoka tena, akashusha pumzi na kutoka pasipo hata kumuaga mama huyo, kutokana barabara aliyopo sio mbali sana na barabara inayo kwenda kwenye milima hiyo, akaingia kwenye gari lake na kulipa pesa aliyo aliyo paswa kulipa. Akaondoka kwa kasi hata muhudumu aliye kuwa akimuhudumia akabaki akiwa anashangaa
 
Kwa mwendo kasi wa gari yake, na umahiri wa kuliendesha gari hilo, akafanikiwa kufika katika eneo la tukio ambapo alikuta watu wengi wakiwemo waandishi wa habari, askari wa ulinzi na kikosi cha zima moto wakiwa wamelizunguka gari lililo pondeka pondeka.
 
Phidaya aliweza kuligundua gari hilo kwani ni miongoni mwa magari yake anayo ya penda na nigari ambalo alimpatia kijana wake kwa ajili ya matumizi yake binafsi. Nguvu za miguu akahisi kwamba zinakwenda kumuishia, kwa ishara akamuita mmoja wa askari aliye weza kugongana naye macho alipo kuwa akitazama tazama watu waliopo katika eneo hilo.
 
“Madam umefwata nini huku?”
Uzuri polisi huyo aliweza kumtambua Phidaya kwa haraka kwani ni miongoni mwa askari ambao waliweza kuhusika katika oparesheni ya kuwakamata majambazi walio vamia hospitali yake siku chache zilizo pita.
“Nilipigiwa simu kwamba gari ya kijana wangu imepata ajali, mwili wake upo wapi?”
“Kusema kweli, ndani ya gari hatukukuta mwili wa mtu yoyote. Hata tulipo jaribu jaribu kutazama pembeni kuona kwamba labda mtu au watu walio kuwemo ndani ya gari hilo watakuwa wameangukia pembeni hatukuweza kuwapata”
“Unasema kweli?”
 
“Ndio Mrs Ranjiti, siwezi kukutania”
Kidogo hata nguvu za miguu zikamjia Phidaya, akajikongoja kongoja kwenda kuchungulia kwenye korongo hilo huku akiongozana na askari huyo sehemu alipo onyeshwa gari ilipo kutwa, alijikuta akitoa macho kwani ina umbali mrefu sana.
‘Sasa kama wametoka watakuwa wapi’
Phidaya aliiuliza huku akiendelea kuchhungulia chungulia bondeni kwenye korongo hilo.

 ==>ITAENDELEA...

Usikose kufuatilia sehemu inayofuata kupitia ubuyublog.com     

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts