Get the latest updates from us for free

mas template
Home » , » AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 33 na 34 )

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 33 na 34 )

Written By Bigie on Saturday, March 10, 2018 | 3:19:00 PM

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA 
ILIPOISHIA  

Kutokana sikuwa nimekaa sehemu yoyote nikageuza na kutoa chumba huku nikiufunga mlango wa chumba vizuri. Nikaanza kutembea kwenye kordo hii huku nikiwa makini kutazama nyuma na mbele. Mlango wa chumbani cha mbele ukafunguliwa, ikanibidi kupunguza mwendo  wa kutembea, macho yakanitoka baada ya kumuona K2 na Lukas wamesimama mlangoni hapo huku wakipigana mabusu ya mdomoni, huku Lukas akiwa amejifunga taulo kiunoni na K2 akiwa amevalia suti yeusi, ila vifungo vya shati lake vikiwa havikajaa vizuri, kwa bahati mbaya, K2 akanitazama, kitu kilicho mstua sana hata Lukas naye alivyo niona akakimbilia ndani.
   
ENDELEA   
Nikamtazama K2 kwa macho makali yaliyo jaa hasira. Sikutaka kumsemesha chochote zaidi ya kumpita na kuanza kushuka kwenye ngazi kwa kasi.
“Dany, Dany”
Niliisikia sauti ya K2 ikiniita kwa nyuma yangu, sikuona haja ya mimi kuweza kusimama, zaidi ya kuendelea kushuka kwneye ngazi.
“Dany nakuamrisha kama bosi wako, simama”
Kauli ya K2 ikanifanya nigeuke taratibu na kumtazama kwa macho yaliyo jaa dharau, nikamtazama jinsi anavyo hema kwa kuchoka kwa kukunikimbiza, kwenye ngazi hizi.
“Ndio bosi”
“Dany umefikaje fikaje huku?”
“Hicho ndicho kilicho kufanya unisimamishe?”
“Ahaa… kwa maana wewe unaumwa?”
“Kwa hiyo?”
“Sio vizuri kutembea tembea”
“Ehee”
“Ndio”
“Ok”
Nikaanza kushuka tena kwenye ngazi na kumfanya K2 kuniwahi na kunishika mkono wangu wa kulia, nikageuka kwa haraka huku mkono wake nikiwa nimeachanisha kwa nguvu na mkono wangu.
“Hembu nisikilize wewe malaya usiye jitambua. Cheo chako unakitumia katika kutembea na vijana si ndio?”
Nilimfokea K2 hadi akarudi nyuma huku  akiwa amenitumbulia macho ya woga sana.
“Upumbavu wako wote ulio kuwa unaufanya, na hichi nilicho kiona leo nimeutambua. Sasa mwisho uwe leo sihitaji mauhusiano na wewe tena. Umenielewa?”
 
Nilizungumza kwa sauti nzito huku tinda za sura yangu zikiwa zimejikunja kisawa sawa. K2 hakuzungumza kitu cha aina yoyote zaidi ya kukaa kimya, woga ukiwa umemjaa. Nikaanza kushuka kwneye ngazi huku nikiwa nimejawa na hasira kali, K2 hakuthubutu hata kunyanyua mguu wake na kunigfwata, nikafika mapokezi na kumkuta msichana ambaye ni muhudumu wa hii hoteli.
“Nahitaji maji makubwa na mzinga wa Vodka”
“Sawa”
Dada huyo akafungua friji kubwa lililopo nyuma yake na kunikabidhi chupa kubwa ya maji, kisha akanipatia na mzinga huo wa Vodka.
“Naweza Kulipa kwa creadit card?”
“Ndio”
Nikatoa waleti yangu, na kuchomoa kadi ya malipo, akaipisha kwneye mashine moja ya kulipa kisha akanirudishia kadi yangu, taratibu nikaanza kazi ya kuzipandisha ngazi hizo nikielekea gorofani. Sikumkuta K2 katika sehemu ambayo nilimuacha. Moja kwa moja nikaelekea katika chumba nilicho muacha Babyanka, nikafungua mlango wa chumba hichi na kuufunga kwa ndani.
“Hei nimerudi”
 
Nilizungumza kwa sauti nzito huku nikiweka chupa ya maji mezani, kisha nikakaa kwenye sofa huku mzinga huu wa pombe ukiwa mkononi mwangu.
“Na huo mzinga wa nini sasa?”
“Nahitaji kukata uchovu?”
“Dany hapana bado hatujaimaliza kazi tafadhali usinywe”
Babyanka alizungumza huku akishuka kwenye kitanda, akaniwahi kunipokonya mzinga huu wa pombe kali.
“Naomba unirudishie huo mzinga”
Nilizungumza huku nikiwa nimekasirika kiasi cha kumshangaza Babyanka kwani ni muda mchache nimetoka nikiwa katika hali ya kawaida.
“Hapana Dany siwezi kukupa huu mzinga”
“Moja, mbili, tatu”
 
Nilihesabu namba hizo huku nikimtazama Babyanka usoni, akaupigiza mzinga wa pombe chini kwenye sakafu na ukavunjika kitu kilicho niudhi maradufu na kujikuta nikutandika kofi zito la shavu na kumfanya ayumbe na kuangukia kwenye kitanda. Kusema kweli akili yangu imechangayikiwa kwa tukio la K2 alilo lifanya, mbaya ni mwanamke ambaye tayari alisha anza kuziteka hisia zangu japo ni mke wa mtu ila mapenzi ya kuiba nayo yana wivu wake. Isitoshe Latifa alisha zungumzia swala la K2 kutoka na mmoja wa jamaa amabaye yupo katika kitengo kingine cha serikali na nilichukualia ni mazungumzo ya kawaida kumbe hata Lukas ambaye naye alikuwa akiyasikiliza mazungumzo hayo kumbe naye ni mume mwenzangu.
“Dany ni akili yako au?”
Babyanka alizungumza kwa hasira huku akiwa amenitumbulia macho makali sana.
“Am sorry”
Nilizungumza huku nikikaa kwenye sofa, Babyanka akanifwata hadi katika sehemu niliyo kaa, akakaa pembeni yangu huku akionekana kuhitaji kufahamu ni kitu gani ambacho kimenipata kwa muda mfupi tu ambao nillikuwa nimetoka.
“Dany kama kuna kitu nimekuudhi naomba unisamehe”
“No hujaniudhi?”
 
“Sasa imekuwaje upo katika hali kama hiyo?”   
“Ahaa, hapana”
Nikajitahidi sana kurudi katika hali ya kawaida, huku nikifumba macho yangu na kutoa pumzi nzito ili kukipa kifua changu nafasi ya kutoa hasira iliyo nishika.
“Kuna mtu amekuudhi, niambie ni nani?”
“Hapana hakuna, ila sahani sana kwa kukupiga?”
Nilizungumza huku nikimgeukia Banyanka, nikaona alama za vidole kwenye shavu lake jambo ambalo lilinifanya nijisikie vibaya sana kwa maana kitu nilicho mfanyia hakustahili kabisa kukutana nacho. Nikakipeleka kiganja changu hadi kwenye shavu la Babyanka, nikalishika taratibu huku nikimsogeza kichwa chake karibu yangu, taratibu tukajikuta tukinyonyana denda kitendo kilicho nifanya hasira yangu yote kupotea kifuani mwangu. 

Tukaendelea kunyonyana denda tena safari hii, ni denda la hisia kali kati yetu, taratibu tukaanza kuvua nguo zetu, huku kila mmoja akiwa na raha ya kufanya kitendo hichi. Tukabakiwa kama tulivyo zaliwa, nikamnyanyua Babyanka na kumkalisha kwenye mapaja yangu, taratibu akamkalia jogoo wangu. Nikakishika kiono chake kwa nguvu, na kuanza kunyanyua na kumshusha kwenye jogoo wangu. Babyanka akanipa ushirikiano wa kutosha.
“Ohoo Dany, fuc** me my beutful puss”
“Real”
“Yeaah”
“I got it”
Tuliendelea kuzungumza mazungumzo yaliyo leta hamasa kubwa kwenye pambano hili ya kuiburudisha miili yetu. Ikafika hatua sote tukajikuta tukikamilisha mechi hii kwa pamoja huku kila mmoja akiwa amepiga shuti moja moja kwenye goli la mwenzake.
 
“Asante Babyanka”
“Asante na wewe Dany”
Taratibu Babyanka akatoka mapajani mwangu na kukaa pembeni ya sofa huku akiwa anahema kwa nguvu, jasho likimwagika usoni mwake.
“Dany nikuulieze kitu?”
“Uliza?”
“Una mwanamke?”
“Hapana sina?”
“Ucha kunitani?”
“Huo ndio ukweli wangu kwa nini nikudanganye wakati sina”
“Makazi yako ni hapa Tanga au wapi?”
“Kwangu ni Dar es Salaam ila mama ndio yupo hapa Tanga”
“Mimi kwetu ni Dar es Salaam sema kazi ndio hivyo imenifanya niwe Tanga, ila tukirudi hivi ikulu nitaomba uhamisho nibaki Dar es Salaam”
“Itakuwa ni vizuri”
“Dany tukaoge muda umekwisha”
Babyanka alizungumza huku akisimama na kueleka bafuni, nikamfwata kwa nyuma hadi bafuni, tukaoga.
“Hili kovu lako ni la nini?”
 
“Moto uliniunguza kuna mtu nilimuokoa kwenye moto”
“Pole, na kidonda bado hakijapona vizuri ehee?”
“Yaa bado hakijakauka vizuri”
Tukamaliza kuoga, tukarudi chumbani kila mmoja akavaa nguo zake, tulipo hakikisha kwamba tumejiweka sawa na silaha zetu tukiwa tumezichomeka kwenye viuno kama tulivyo  kuwa tumezichomeka mara ya kwanza, tukatoka chumbani huku tukiwa tunatembea kwa kujiamini sana. Tukatoka nje ya hoteli, nikaingia kwenye gari na kuliwasha, Babyanka akazunguka upande wa pili wa gari hili na safari ya kuelekea uwanja wa Mkwakwani ikaanza. Tukafika eneo hilo na na kukuta msafara wa raisi ndio unatoka, tukaunga kwenye msafara huo huku gari letu likiwa la mwisho kabisa. Tukaeleka hadi kwenye hoteli ya Mkonge, tukashuka kwneye gari letu na moja kwa moja tukamfikia raisi feki, walinzi wake wakataka kutuzuia, ila raisi mwenyewe akawaruhusu watuache tuwe karibu yetu. 
 
Nikiwa katika kutazama tazama kila kona ya hoteli hii, nikamuona K2 naye akiwa na vijana wengine kutoka ofisini kwetu wakiwa nao ni miongoni wa waimarishaji ulinzi wa raisi huyu ambaye pasipo wao kufahamu kwamba raisi huyu sio sahihi.
Raisi akaingia kwenye chumba chake ambacho kilisha andaliwa katika hoteli hii kwa ajili ya mapumziko ya muda mfupi kisha usiku atapata chakula na wazee wa mji huu. Raisi akatuomba kuweza kuonana na sisi, kila mlinzi wake mmoja alishangaa kwa maana hawakuwahi kutuona katika msafara mzima. Tukaingua chumbani kwake, akatukaribisha kwenye viti na kukaa.
 
“Poleni kwa majukumu mazito muliyo pitia”
“Asante”
“Muheshimiwa dhiara yake imekwendaje?”
“Imekwenda vizuri  japo kulitokea mambo ya hapa na pale ila tuliweza kuyatatua na raisi amerudi akiwa salama salimini.
“Ohoo asante Mungu kwa maana moyo wangu muda wote ulikuwa na wasiwasi, isitoshe mimi sio raisi halisi”
“Ila mtu akikutazama hawezi kufahamu kama wewe sio raisi”
“Kweli wataalamu walio nifanyia hii oparesheni ni wachini, kusema kweli hata mimi mwenyewe nilijishangaa pale nilipo jitaza kwenye kioo”
“Hhaaa”
“Basi asubuhi na alfajiri, nitarudi Dar es Salaam kama raisi alivyo zungumza anahitaji tuweze kurudi wote”
“Sawa, sisi gari letu lipo safi”
Babyanka alijibu huku tukimtazama raisi huyu, ambaye hata ukae naye karibu basi huwezi kumjua kwamba sio raisi mwenyewe.
 
“Ila ninawaomba musikae mbali na mimi?”
“Usijali katika hilo, kazi yetu ni kuhakikisha kwamba wewe unakuwa salama”
“Nitashukuru sana, ila kuna watu wanahitaji kuniua, na huu ndio mpango ambao upo kwa sasa”
Raisi huyu alizungumza huku machozi yakimlenga lenga, kwa maana watu wanao muwinda raisi wanamuwinda yeye wakuhisi kwamba ni raisi mwenywe.
“Ni kina nani hao?”
“Kwa sasa sijaweza kupata ripoti yao ila moyo wangu unahisi kuna kitu kibaya kitatokea usiku wa leo, ninawaomba sana tuweze kurudi Dar es Salaam pamoja nikatolewe hii sura ya bandia niwe katika amani kwa maana nimeona kazi ya kuwa raisi”
“Sawa muheshimiwa”
“Ninawaomba usiku wa leo muweze kulala chumbani kwangu”
“Sawa”
Tukaendele kuzungumza mambo mengi na raisi huyu feki hadi walinzi wake wanao mlinda wakaingia chumbani kutazama ulinzi wake, wakatukuta tukiwa tunacheka na kufurahi.
 
“Muheshimiwa muda wa kuonana na wazee umetimi”
“Basi nipeni muda wa kujiandaa ninakuja”
“Sawa mkuu”
Walinzi wake hao wawili wakatoka na kuufunga mlango. Raisi akashusha pumzi kali huku akionekana kuwa na mashaka sana, hapo ndipo nikagundua kwamba raisi huyu ni muogo sana. Tukasimama kutoka katika vitu tulivyo kalia, Babyanka akaongoza kutoka chumbani huku mimi nikiwa nyuma na raisi mbele yangu. Walinzi wake wakajumuika na sisi kuelekea katika ukumbi maalumu ambao tayari umesha andaliwa vyakula vya kutosha.  Tukiwa tunaingia ukumbini huku, macho yangu yakagongana na K2 alliye nitazama kwa macho makali, ila sikulijali hili. 

Hadi raisi anafika katika sehemu yake aliyo andaliwa kukaa, tukasimama. Kabla raisi hajakaa kwenye kiti hichi nikamzuia, huku macho yangu nikikitazama kiti hichi kwa umakini wa hali ya juu. Walinzi, wazee pamoja na viongozi wengine akiwemo mama yangu, wakabaki kunitazama ni kwa nini nimemzuia raisi kukaa kwneye kiti hichi. Taratibu nichuchumaa chini na kukisogeza kitambaa cha meza iliyopo karibu na kiti hichi, macho yakanitoka baada ya kukuta bomu la kutegwa ambapo raisi akikaa tuu kwenye kiti hichi na kuutingisha waya mwenbaba ulio fungwa kwenye bomu hilo, basi linakwenda kulipuka naye na huo ndio unakuwa mwisho wa maisha yake.

                         AISIIIII……….U KILL ME 34

Sikutaka kumuonyesha raisi huyu ni kitu gani ambacho kinaendelea katika eneo hili zaidi ya kumngong’oneza na kumuambia kwamba sehemu hii sio salama. Jambo hili likamstua sana raisi huyu feki nikamuona sura yake jinsi inavyo badilika kwa woga, moja kwa moja nina amini kwamba ndani ya umbumbii huu kuna watu ambao wamepanga kumuangamiza raisi na kuna muunganiko mkubwa sana hata wa watu ambao tupo katika usalama wa kumlinda raisi tunahusika.
 
“Sasa inakuwaje?”
“Hakuna cha kufanya zaidi ya wewe kuondoka katika eneo hili”
“Sasa si tuwatangazie watu?”
“Hapana”
“Babyanka ondoka na raisi, natafuta jinsi ya kuliondoa hili bomu”
“Sawa”
“Mpeleke chumbani kwake”
“Sawa”
Babyanka akaondoka na raisi pamoja na walinzi  wengine sikuwa na jinsi zaidi ya kuchuchumaa tena na kuliangalia bomu hilo jinsi lilivyo tengwa. Mlinzi mwingine akajumuika na mimi, alipo liona bumo mwili mzima ukawa unamtetemeka Watu ukumbini hawakujua ni kutu gani kinacho endelea na wala hatukuhitaji kuweza kuwatangazia kwamba kuna jambo baya, kwa maana inaweza kusababisha mvurugano ndani ya ukumbi kila mtu akiwa anajaribu kuyaokoa maisha yake.
 
Taratibu nikaanza kulitegua bomu hili kwa umakini wa hali  ya juu, nikaanza kukiachanisha kijiwaya hichi pamoja na bomu, baada ya kufanikiwa kufanya hivyo, nikalitoa bomu hili kwenye kiti kisha nikaliweka chini huku kajasho kakinimwagika.
Mlinzi mwengine akalifunika bumu kwa koti kisha akatoka nalo ukumbini, moja kwa moja nikaelekea katika chumba ambacho Babyanka amempeleka raisi. Nikagonga mlango nikaruhusiwa kuingia ndani, nikamkuta raisi fake akiwa amesimama pembeni ya dirisha huku mwili mzima akimwagikwa na jasho, japo ndani ya chumba hichi kuna air condition ila jasho halikukata kumtoka.
 
“Muheshimiwa tumemaliza unaweza sasa kwenda kujumuika na wazee hao”
“Kweli bomu  mumelitoa?”
“Ndio muheshimiwa tumelito ahakuna tena kizui”
“Nisije nikaenda nikafa mie”
“Hauwezi kufa muheshimiwa, kila kitu kipo  salama”
“Ohoo Yesu wangu nisaidie”
Alizungumza huku akijifuta jasho na kitambaa chake, tukatoka naye huku tuimarisha ulinzi, nikakivua kiti chake nyuma kidogo akakaa huku akishusha pumzi nyingi.
Mc akaanza kuongoza shuhuli hii, ambayo wazee wakaanza kutoa mauoni yao wengine wakimuombea raisi na kumpa Baraka nyingi pasipo kuweza kufahamu kwamba huyu sio raisi alisi.
Shere ikamalizika saa tano usiku, nikamuachia Babyanka jukumu la kumlinda raisi akiungana na viongozi  wengine huku mimi nikielekea nyumbani nikiwa na mama. Tukafika nyumbani na mama, moja kwa moja nikaelekea chumbani kwangu na kukukushanya nguo zangu nilizo kuja nazo na kuziweka kwenye begi, nikatoka sebleni na kumkuta mama akiwa amejikalia kwenye sofa akinisubiria kwa ajili ya mazungumzo machache aliyo hitaji kuzungumza na mimi.
 
“Yudia amekwenda wapi?”
“Hivi sikukuambia?”
“Hukuniambia nini?”
“Yudia ni muiongoni mwa watu ambao walifanikisha nyaraka zako kuibiwa na yeye ndio aliye kuwa anaongoza mipango yote ya kutaka kukuua akishirikiana na meya”
“Weeeeee……!!”
“Ndio mama sikuhitaji kukuambia kwa mara ya kwanza kugopa kukupa presha zisizo na msingi”
“Sasa si anaweza kuja kunifanyizia humu ndani nikiwa peke yangu?”
“Hawezi kufanya hivyo nakuhakikishia katika hilo”
“Dany mwangu mimi ninaogopa kama vipi nikaishi kwa baba yako mkubwa”
“Utakuwa huru katika hilo?”
“Itanibidi kuwa huru katika hilo hadi hali itulie, wewe mwenyewe si umejionea mambo yanayovyo teoke”
“Sawa kwa hiyo nikupeleke kwa baba mkubwa”
 
“Ndio kulala mwenyewe kwenye hili jumba mimi wala siwezi kabisa”
Sikuwa na kipingamizi na ombi la mama kwa maana hali ya usalama juu yake bado haijakuwa vizuri. Nikaondoka naya ne kueleke kwenye gari, tukaondoka nyumbani kwetu na kueleke kwa baba mkubwa. Nikamfikisha hadi getini, akashuka na kuminya batani ya kengele iliyopo geti likafunguliwa na mlinzi akafungua geti na mama akaingia ndani, alipo funga geti na mimi nikawasha gari na kuondoka katika eneo hili. Safari ya kurudi katika hoteli ya Mkonge ikaanza, sikuchukua muda mwingi nikafanikiwa kufika katika hoteli hii.
Nikaelekea chumbani kwa raisi na kumkuta akizungumza na Babyanka. Nikajumuika nao, usiku mzima hatukulala hadi ikatimu alfajiri na mapema tukamuacha raisi ajiandae na safari ya kurudi Dar es Salaam. Nikaeleka sehemu maalumu ya kupata chakula nikiwa na Babyanka, muhufumu akatufwata kwa ajili ya kuhitaji kutuhudumia, kila mtu akaagiza anacho hitaji kupata kwa asubuhi hii. 
 
“Dany”
“Mmmm”
“Wewe ni mzuri?”
“Ahaa acha hizo”
“Kweli Dany wewe ni mzuri kuanzi sura hadi umbo ila sujajua roho yako kama ni nzuri”
“Mwnaume huwa asifiwi uzuir”
“Ahaa nani kuakuambia”
Kabla sijazungumza chochote nikamuona K2 akija katika sehemu niliyo kaa na Babyanka, nikamtazama hadi alipo fika, akasimama pembeni yangu .
“Dany nakuhitaji kwa mazungumzo”
Ikanibidi  kunyanyuka na kuanza kumfwata anapo elekea, tukafika kwenye moja ya bustani, akasimama na kunigeukia.
“Zungumza”
“Kwa nini unanifikiria vibaya?”
“Nina kufkiria vibaya kuhusiana na nini?”
“Wewe umeniona jana nikiwa na Lukas ukaanza kunitukana na kuniseme vibaya”
“Hembu tambua ya kwamba hapa unazungumza na mtu mzima mwenye akili zake na sio mtoto mdogo kama unavyo fikiria. Na kama ni swala la mapenzi mimi na wewe limesha kwisha itabaki kuwa ni mtu na bosi wake, na ikiwezekana pia ninaweza kuhama kitengo”
 
“Dany tambua ya kwamba ninakupenda sana”
“Eheee acha upuuzi, hivi kwangu unahitaji nini, kwangu unataka nini. Kama ni mbo** hata Luka anayo isitoshe Luka huyu huyo niu mtu ambaye alitugeuka mimi na Latifa na sasa hivi unataka kufanya nini”
Nilizungumza kwa ukali ulio mfanya K2 kuwa mnyonge sana, hakudhubutu kuonyesha ukali wake wowo japo ni mkali inapo kuja swala la kazi.
“Tena nikuambie kutu kimoja, koma kunifwatalia ukiendelea kufanya hivyo basi nitahakikisha unanifahamu mimi vizuri sawa”
“Dany sipo tayari kukuacha, sipo tayari kukutenga nahitaji penzi lako, ndio maana ninaamua kufanya chochote kwa ajili yako”
“Koma unafanya vitu vipi kwa ajili yangu, kunipa milioni zako ndio unaseme kwamba umefanya kila kitu kwa ajili yangu. Sikiliza usinione kwamba ninaishi kwenye chumba kimoja ukahisi kwamba sina pesa, nina imani kwamba mshahara wangu unaufahamu, pia kwetu tuna pesa nyingi tu so ninakuomba uwe na heshima katika hili”
 
Nilipo maliza kuzungumza maneno hayo nikaondoka na kumuacha K2 akiwa analengwa lengwa na machozi, nikarudi kwenye meza alipo Babyanka, nikamkuta akiendelea kupata kifungua kinywa.
“Vipi mbona umerudi umenuna?”
“Huyo ndio bosi wangu wa kitengo”
“Umesha pangiwa kazi nini?”
“Bora ingekuwa hivyo”
“Ila”
“Ahaaa tuachane nayo hayo mambo, tunywe chai fasta tuondokoje”
“ Mimi nimesha maliza ni wewe”
Nikaanza kunywa chai haraka haraka, ndani ya dakika tano nikawa nimesha maliza kunywa chai. Nikasimmaa na moja kwa moja tukaeleka chumbanu kwa raisi na kumkuta amesha maliza kujiandaa na kupata kifungua kinywa.
“Muheshimiwa tunatakiwa kuondoka”
“Hakuna tabu”
 
Tukatoka na raisi huku walinzi wake tukiwa tupo makini sana, ila mimi na Babyanka ndio tupo makini sana kwa maana kati yetu wapo ambao wapo kinyume na raisi, akafunguliwa mlango wa gari na mlinzi wake, akaingia na sisi tukaingia kwenye gari zetu huku begi langu la nguo nikiliweka sitii ya nyuma. Safari ikaanza ya kueleke Dar Salaam. Gari ya raisi ipo mbele yetu huku mbele kabisa ya gari ya raisi kukiwa na gari si chini ya nne pamoja na pikipiki mbili za polisi usalama.
Japo ni safari ndefu ya masaa kadhaa ila inatuhitaji umakini wa hali ya juu kwa maana bado hatufahamu nani ni mbaya na nani ni mzuri ndani ya walinzi wa raisi wabaya wanao tumiwa na viongozi wengine wapo tena wengi sana.
Tukafika maeneo ya Segera, askari polisi wanao ogoza kwa pikipiki tulio toka nao Tanga wakageuza na kurudi Tanga, wakachukua askari wengine wawili wa usalama barabarani ambao tutakwenda nao hadi Chalinze na hapo Chalinze watabadilka wengine ambao tunatwenda nao hadi Dar es Salaam.
 
“Mmmmm”
Niliguna huki nikiendelea kuendesha gari hili tulio panda mimi na Babyanka.
“Una guna nini?”   
“Tuwe macho sana na hawa maaskari tulio pewa hapa”
“Kwa nini?”
“Siwaamini, nimejikuta nikiwa na wasiwasi nao”
“Usijali hakuna wanakacho weza kukifanya”
“Sawa”
Tukaendelea kutembea kwa mwendo  wa kasi huku gari pamoja na pikipiki hizo zilito tanguliwa ytukiwa katika mwendo mmoja sawa wa spidi mia na ishirini. Pikipiki hizo zimejaliwa uwezo mkubwa ambao unaweza kuendana sawa na baadhi ya magari yaliyopo hapa katika msafara kasoro gari letu ndio lina uwezo mkubwa sana wa kukimbia kwa kasi. Kadri muda unavyo zidi kwenda ndivyo jinsi ninavyo jikuta nikipata wasiwasi mkubwa sana huku mwili wangu ukisisimka.
“Babyanka kunatatizo”
“Tatizo gani?”
“Sijui ila hii safari kuna tatizo, mwili wangu unasisimka”
“Mmmm, sasa inakuwaje?”
“Ngoja nizipite hizi gari”
“Tambua unavunja sheria”
“Sheria siwezi kuvunja, kwa kuyaokoa maisha ya huyu jamaa”
 
“Dany usifanye hivyo please unaweza sababisha matatizo”
Hata kabla sijazungumza kitu, kwenye kona ya kushuka kwenye daraja la Wami, tukakuta lori kubwa la mafuta likiwa limeifunga njia, kitendo kilocho zifanya gari za mbele kuanza kufunga bereki za gafla, nyingine zikagongana gongana.  Kwa umakini mkubwa, nikazikwepa gari hizo huku gari langu nikiliweka upande wa pili wa barabara nikijitahidi kufunga breki. Gari za mbele zikalivaa lori hilo na kusababisha ajali moja mbaya. Hata kabla hatujakaa sawa milio ya risasi ikaanza kusikika ikirindima eneo hili. Kila mmoja akawa amechanganyikiwa kivyake, nikamuona dereva wa gari la raisi akijitahidi kurudi nyuma ili kugeuza, ila akashindwa kufanya hivyo kwani nyuma gari lake limebanwa na magari mengine. Askari walio kuwa wakiendesha pikipiki, nikawaona wakiwa nao nimiongoni wa washambulijia wa msafara wa raisi. 
 
Kabla sijashuka tayari Babyanka akawa ameshuka na kuanza kujibu mashambulizi hayo ya risasi, nami nikashuka na kuanza kufatua risasi kwa watu hao. Nimewai kufanya kazi nyingi za kutisha na kuogopesha ila hii ambushi tukiyo kutana nayo hapa, inaniogopesha sana.
“Byanka”
“Ndio”
“Tudili na raisi”
“Powaaa”
Nilizungumza kwa sauti ya juu kwa maana kelele ya milio ya risasi iliendelea kurindima, walinzi wengine wa raisi wakaendelea kuangushwa chini kwa kupigwa risasi kitu kilicho zidi kuniogopesha kwani kadri muda unavyo zidi kwenda nvyo wanavyo zidi kufa. Nikamuona naye K2 akipambana vya kutosha kuhakikisha raisi hafi, japo wezetu wanakufa.
 
“Byanka nilinde”
Nilizungumza hivyo huku nikishusha pumzi nyingi kwani ninahitaji kwenda kumtoa raisi kwenye gari aliloipo na kuondoka naye. Biyanka akaanza kufyatua risasi mfululizo, na kuwafanya washambuliaji kutulia kidogo, ikawa nafasi kwangu kukimbia hadi gari la raisi lilipo, kwa ishara nikamuomba afungue mlango wa gari lake kwa manaa pasipo yeye kuufungua kwa ndani mimi wa nje siwezi kuufungu. Raisi akafanya hivyo, japo ni jambo la hatari ila hakuna njia nyingine ya kufanya zaidi ya kufanya hivyo. Raisi akashuka huku kichwa akiwa amekiinamisha chini, nikaupitisha mkono wangu wa kulia kiunoni mwake, kitendo cha kugeuka na kumtazama K2 aliyopo upende wetu nyuma ya gari la raisi, nikakutana na uso wa bastola yake akiwa ameninyooshea mimi na raisi huku sura yake akiwa ameikunja akidhamiria kufanya hicho anacho kihitaji kukifanya kwa wakati huu.
                                                                                          ITAENDELEA

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts